Sifa na kuabudu

John Lema 2010

Testimonials

Quotes Bi Getrude Hamphrey, amekaa ndani ya ndoa kwa miaka saba bila kupata mtoto, ?Nilidharauliwa na watoto wadogo, hata ndugu zangu wa karibu, wengi walinicheka na kuniona sifai, nilimshika Mungu kwa maana niliamini ipo siku atanipa mtoto kama aliweza kwa Hana, Sara ataweza kwangu pia, na adui zangu watauona utukufu wake? alisema Getrude akiwa amembeba mtoto wake Glory, Mungu amempa haja ya moyo wake. Hii inapendeza sana, kwa wale wasioweza kuzaa au kupata watoto wasihangaike wa waganga kwani YESU anaweza yote. Usimuache Mungu, haijalishi ni muda gani hujaona majibu yako acha kusudi la Mungu litimie ili watu wauone utukufu wake. Quotes
getrude humphrey
aliyepata mtoto

Quotes USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU UTANGULIZI: Ndugu yangu kuna shuhuda nyingi sana zinazoanguka duniani, lakini wachache wanaozingatia kwa vile watoaji si wa dini zao au si wa madhehebu yao wala hawajulikani makanisani. Sasa ninakuomba ewe msomaji, tafuta mahali pa utulivu, mwombe Mungu na kusoma ushuhuda huu ili upokee kile ambacho Bwana amekuletea leo. Msichana Nyisaki Chaula alionyeshwa na Bwana ushuhuda huu akiwa na umri wa miaka 16 mara baada ya kuhitimu elimu ya msingi. Ushuhuda huu alionyeshwa akiwa ameokoka na si kwamba alikufa bali aliona maono. Maono haya alionyeshwa kati ya tarehe 30 ? 31/12/1991; yaani kwa siku mbili tofauti. Msichana huyu hivi sasa ameolewa na Mwinjilistii Lemsy Mheni pale Uyole Mbeya kwa lengo la kukuza huduma yao. Kabila lake ni Mkinga wa Makete, Msichana huyu anapatikana Uyole njia panda ya Malawi ? Zambia na Dar es Salaam pembeni mwa kituo cha mafuta ya magari pale Uyole, Bwana awatangulie katika usomaji. Quotes
nyisaki chaula
USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU

Quotes SURA YA 1 KUITWA: Ilikuwa ni mwezi wa 12/1991 tulipochaguliwa vijana 10 kuombea Mkutano wa Kiroho ambao ulikuwa ukifanyika pale Uyole. Siku moja baada ya maombi ya usiku, nilala pamoja na dada zangu. Siku hiyo nilala usingizi mzito ambao sijapata kuona. Usiku nilishangaa kukuta usingizi umetoweka kabisa, hivyo nikabaki nikiwa macho, ndipo nikasikia sauti ikiita ‚??Nyisaki‚?? nikasikia lakini sikuitikia, ikaita mara ya pili pia sikuitika. Hata mara ya tatu ndipo nikaitika kisha nikasikia ile sauti ikisema ‚??Nimekuchagua kuwa mtumishi wangu‚?? ndipo nikatambua kuwa ni sauti ya Bwana, nikasema ‚??Bwana mimi ni motto mdogo tena hata chuo chochote sijaenda nitawezaje kuifanya kazi hiyo? Bwana akaniambia mkumbuke Yeremia mtumishi wangu nilimchagua angali bado mdogo (Yeremia 1:5) Quotes
chaula
USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU

Quotes Mama Lucy alieleza jinsi watoto wake watatu ambao nao walikumbwa na ugonjwa huo wa kuchanganyikiwa na mara baada ya maombi walifunguka na kuwa wazima. Mtoto wake wa kwanza alikuwa Gerald Peter Songoro (22). Huyu alikaa ndani ya nyumba kwa muda wa miaka miwili bila kutoka nje ya nyumba, bila kuoga na bila kuongea, bila kunyoa nywele, wala ndevu huku akiwa hajifahamu mahali alipo. Jambo hili lilisababisha awe ananuka na kuwa na ndevu nyingi sana kama za waarabu na nywele nyingi zisizonyolewa kwa muda wa miaka miwili na za kutisha. Sasa hivi Gerald anatembea barabarani vizuri na amemaliza Bible School mjini Arusha. Anakula, anaoga na anatembea vizuri baada ya kuombewa. Mtoto wa pili wa mama Lucy ni Alphonce Peter Songoro (20) Huyu naye alichanganyikiwa akawa kichaa kwa muda wa miaka minne. Midomo yake pia katika kipindi hicho ilianza kuoza na kupinda. Quotes
mwanafamilia
waliokuwa vichaa

Quotes VICHAA WANNE WA FAMILIA MOJA WAFUNGULIWA * Yeye mwenyewe alichanganyikiwa kwa miaka 16 * Mtoto mmoja alijifungia miaka 2 pasipo kutoka nje wala kuongea na mtu yeyote * Mwingine naye alitokwa na damu mfululizo kwa miezi miwili * Wote hao sasa wako huru kwa msaada wa JINA LA YESU! Katika familia moja ya watu wanne MUNGU ametenda muujiza wa uponyaji ugonjwa wa kichaa. Hali hiyo ya ukichaa katika familia hiyo ilionekana kuwa ni tatizo sugu na kwamba ni la kurithishana kizazi hata kizazi katika familia hiyo Quotes
familia
vichaa waliofunguliwa

Quotes Ushuhuda Aliyekuwa jambazi wa muda mrefu na kushiriki matukio ya wizi wa kutumia silaha, Bw. Obote Mwakasege amejisalimisha kwa Bwana Yesu na kuokoka na hivi sasa ni Mchungaji anaihubiri Injili ya wokovu. Akitoa ushuhuda wa maisha yake katika Mkutano wa Mwakasege alisema, maisha ya sasa ya wokovu ni mazuri kwani yamemtoa katika vifungo mbalimbali na kumuweka huru dhidi ya dhambi. Alisema akiwa na umri mdogo alianza kujihusisha na vitendo vya uvutaji bangi na sigara, hatua iliyomfanya ajifunze vitu mbalimbali vikiwemo ujambazi wa kutumia silaha. Akiwa katika hali ya kuendelea na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kushauriwa kuacha vitendo hivyo, baba yake alimtenga katika familia. Aidha Bw. Obote alieleza kwamba amepata kwenda jela mara kwa mara na amechoka na maisha hayo yasiyo na faida. Siku moja katika pita pita yake alikutana na habari za Yesu zilizomfanya kubadilika na kuamua kuokoka na hivi sasa ni mhubiri wa Injili. Quotes
obote mwakasege
aliyekua jambazi

.


Realtime Clock

Gospel Teachings and One To One Enterviews

WAPO RADIO

                                                                                                                                              Ratiba ya vipindi:

0715 - 0800hrs Patapata

0800 - 0845hrs Yasemavyo Magazeti

0845 - 1000hrs Zilizotufikia

1000 - 1200hrs Meza ya Busara

1200 - 1205hrs Habari kwa Ufupi

1800 - 1830hrs DW Idhaa ya Kiswahili

1830 - 1900hrs Duru za Michezo

1900 - 2000hrs Yaliyotokea

tafuta andiko ndani ya Biblia hapa

Enter a verse or keywords
(John 3:16, love, sword of the spirit)

tafuta katika biblia

Search the BibleBibleGateway.com

videos mpya

1739 views - 0 comments
1389 views - 0 comments
1343 views - 0 comments
2005 views - 0 comments

hali ya hewa

Subscribe To Our Site

mtumie rafiki yako

webs

nyimbo za injili-videos

neno la siku ya leo

jiunge nasi

wageni

..


john lema

shuhuda

 • "Bi Getrude Hamphrey, amekaa ndani ya ndoa kwa miaka saba bila kupata mtoto, ?Nilidharauliwa na watoto wadogo, hata ndugu zangu wa karibu, wengi walinicheka na kuniona sifai, nil..."
  getrude humphrey
  aliyepata mtoto
 • "USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU UTANGULIZI: Ndugu yangu kuna shuhuda nyingi sana zinazoanguka duniani, lakini wachache wanaozingatia kwa vile watoaji si wa dini zao au si ..."
  nyisaki chaula
  USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU

Google Translator

mahubiri

comment box

Facebook Fanpage Box

Recent Prayer Requests

 • maisha yangu

  naomba maombi yenu kuhusu mimi na familia yangu ,mungu atulinde siku zote za maisha yetu,kwani tuko kwenye majaribu mazito
 • kupata watoto

  namomba mungu anisaidie niweze kupata watoto wazuri,wakike na wakime.

,

 

 

 

 

Recent Podcasts

.