Sifa na kuabudu

John Lema 2010

                            sala ya toba

"Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.

sikiliza wapo radio live

kronolojia ya biblia

Miaka ya matukio mbali mbali katika Biblia.


Dibaji.


Kronologia ni mtiririko wa mambo yaliyotokea zamani, katika historia. Kwa sababu Biblia hajaandikwa katika mpangilio wa kikronologia, vivyo hivyo uhakika kamili haupo katika mipangilio ya matukio haya kwa usahihi kamili. Mfano tukiangulia wakati wa wafalme ni vigumu kupata uhakika wa utawala sababu wakati mwingi wafalme walitawala hata wawili au watatu, baba na mwana. Kijana aliweza kutawala ingawa baba alikuwepo bado anaishi.


Wataalamu wa historia wamechunguza wakati wa Biblia. Wamefaulu kupata na kuelewa mambo mengine yanayotusaidia katika kujua kuhusu matukio mbali mbali katika Biblia, lakini mambo mengine bado, hayajachunguzwa. Katika Biblia kuna vipengele vingine vinavyoweza kupata mwelekezo juu ya matukio. Wataalamu wa historia wameichunguza Biblia na historia na wanaelewa kwamba Sulemani alitawala miaka ya 972-932 kabla ya Kristo. (K.K.) Utawala wake uliendelea kwa miaka 40. (1Fal 11:42) Ufalme wa Israeli uligawanyika mara baada ya utawala wa Sulemani, kama mwaka wa 932 K.K.


Sulemani alianza kujenga Hekalu katika mwaka wa nne wa utawala wake, yaani mwaka wa 969/968 K.K. Kujenga kulianza mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kuliondoka Misri. (1Fal 6:1) Wana wa Israeli waliondoka Misri mwaka wa 1448 K.K. (968 + 480 = 1448) Waisraeli walikaa Misri miaka 430. (Kut 12:40) Wakati huo mateso yalichukua miaka 400. (MDO 7:6) Waliingia Misri mwaka wa 1878 K.K. (1448 + 430 = 1878) Kuingi Misri ni wakati ule Yakobo alipoingia na familia yake. Wakati huo Yusufu alikuwa amepandishwa cheo katika nyumba ya Farao. Baadaye alipoteza kazi yake ya utawala kwa sababu Misri ilipata Farao mwingine. Baadaye mateso yalianza na Waisraeli walikuwa watumwa katika nchi ya Misri.


GAL 3:16,17 inatueleza kuhusu ahadi iliyopewa Ibrahimu, (MWA 22:18) na pia Yakobo alivyohakikishiwa kuhusu ahadi hiyo. (MWA 46:2-4) Yakobo alihakikishiwa ahadi hiyo alipoingia Misri, katika mwaka wa 1878. Baada ya miaka 430 Yakobo alipoingia Misri, sheria ilitolewa kwa Waisraeli. Ilitolewa 1448/1447. Wakati huo wana wa Israeli walikuwa wameanza safari yao kuelekea nchi ya ahadi. Wakati wa Waamuzi wana wa Israeli walikuwa wamekaa katika nchi yao miaka 300. (AMU 11:26)


Hapa tunakwenda kuona jinsi mambo yalivyoendelea.
Pia tutaona historia kidogo ingawa hatuna uhakika na mipangilio ya miaka. Inatubidi kuchunguza kwa makini kuhusu mambo haya: "Hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua." (1KOR 8:2) "Tunafahamu kwa sehemu". (1KOR 13:9) Hivyo inatubidi kufanya uchunguzi kwa makini sana.
Mipangilio ya miaka katika Biblia baada ya kuumbwa kwa Adamu
(B.A. = Baada ya Adamu)
(K.K. = Kabla ya Kristo)

MWANZO.

Tangu mwanzo hadi 1807 K.K. (Kabla ya Kristo)

 

000

Kuumbwa kwa Adamu. Aliishi miaka 930. Alifariki mwaka 930 baada ya kuumbwa kwake. (MWA 1:27-5:5)

Kaini na Habili walizaliwa. Baadaye Kaini alimwua Habili. Inawezekana watoto wengine pia walikuwa wamezaliwa.

Kabla ya gharika watu wote na wanyama walikula majani ya miche (MWA 1:29,30). Baadaye walikula pia nyama. (MWA 9:3)

 

130 B.A.

Sethi alizaliwa. Aliishi miaka 912. Alifariki mwaka wa 1042. B.A. (MWA 5:3-8)

 

235 B.A.

Enoshi alizaliwa. Aliishi miaka 905. Alifariki mwaka wa 1140. B.A. (MWA 5:6-11) Hapo ndipo watu walianza kuliitia jina la Bwana. (MWA 4:26)

 

325 B.A.

Kenani alizaliwa. Aliishi miaka 910. Alifariki mwaka wa 1235. B.A. (MWA 5:9-14)

 

395 B.A.

Mahalaleli alizaliwa. Aliishi miaka 895. Alikufa 1290. B.A. (MWA 5:12-17)

 

460 B.A.

Yaredi alizaliwa. Aliishi miaka 962. Alikufa mwaka wa 1422 B.A. (MWA 5:15-20)

 

622 B.A.

Henoko alizaliwa. Aliishi miaka 365. Alipotembea pamoja na Mungu miaka 300, hakuwepo tena kwani Mungu alimchukua katika mwaka wa 987 B.A. (MWA 5:18-24)

 

687 B.A.

Methusela alizaliwa. Aliishi miaka 969. Aliishi miaka mingi zaidi duniani. Alikufa mwaka ule wa gharika 1656 B.A. (MWA 5:21-27)

 

874 B.A.

Lameki alizaliwa. Aliishi miaka 777. Alifariki mwaka 1651 B.A. (MWA 5:25-31)

 

930 B.A.

Adamu alifariki. Akiwa na miaka 930. (MWA 5:5)

 

987 B.A.

Henoko alichukuliwa na Mungu. Akiwa na miaka 365. (MWA 5:22-24)

 

1042 B.A.

Sethi alifariki akiwa na miaka 912. (MWA 5:8)

 

1056 B.A.

Nuhu alizaliwa. Aliishi miaka 950. Alifariki mwaka wa 2006 B.A. (MWA 5:28-9:29)

 

1235 B.A. Kenani alifariki akiwa na miaka 910. (MWA 5:14)

 

1290 B.A.

Mahalaleli alifariki akiwa na miaka 895. (MWA 5:17)

 

1422 B.A.

Yaredi alifariki akiwa na miaka 962. (MWA 5:20)

 

1558 B.A.

 

Shemu alizaliwa. Aliishi miaka 600. Alifariki mwaka wa 2158 B.A. (MWA 5:32-11:11)

 

1651 B.A.

Lameki alifariki akiwa na miaka 777. (MWA 5:31)

 

1656 B.A.

Gharika. Ilichukua mwaka mmoja na siku kumi. (MWA 6:7-8:19) Matokeo ya gharika yameonekana huko Tigri (= Hidekeli) na mkondo wa mto Frati.

 

1658 B.A.

Arfaksadi alizaliwa. Aliishi miaka 438. Alikufa 2096 B.A. (MWA 10:22, 11:10-13)

 

1693 B.A.

Sela alizaliwa. Aliishi miaka 433. Alikufa 2126 B.A. (MWA 10:24, 11:12-15)

 

1723 B.A.

Eberi alizaliwa. Aliishi miaka 464. Alikufa mwaka wa 2187 B.A. (MWA 11:14-17)

 

1757 B.A.

Pelegi alizaliwa. Aliishi miaka 239. Alikufa 1996 B.A. (MWA 11:16-19) Wakati wa Pelegi dunia iligawanyika (MWA 10:25)

 

1787 B.A.

Reu alizaliwa. Aliishi miaka 239. Alikufa 2026 B.A. (MWA 11:18-21)

 

1819 B.A.

Serugi alizaliwa. Aliishi miaka 230. Alikufa 2049 B.A. (MWA 11:20-23)

 

1849 B.A.

Nahori babu ya Abramu (=Ibrahimu) alizaliwa. Aliishi miaka 148, alifariki 1997 B.A. (MWA 11:22-25)

 

1878 B.A.

Tera baba ya Abramu (=Ibrahimu) alizaliwa. Aliishi miaka 205. Alifariki 2083 B.A. (MWA 11:24-32)

 

1948 B.A.

Abramu alizaliwa. Aliishi miaka 175. Alifariki 2123 B.A. = 1993 K.K (MWA 11:26-25:8)

 

 

Tangu hapo miaka kabla ya Kristo: (K.K.)

 

2168 K.K. (Kabla ya Kristo)

Abramu alizaliwa Uru wa Wakaldayo. (MWA 11:26) Tera, baba yake alikuwa na miaka 70.

Wakati wa Abramu Nuhu aliishi miaka 58, na Shemu miaka 210. (Shemu alifariki miaka 35 baada ja kifo cha Ibrahimu = Abramu).

 

Inawezekana kwamba Shemu ndiye Melkizedeki. (MWA 14:18-20)

Baada ya kuzaliwa kwa Abramu, Arfaksadi aliishi miaka 148, Sela aliishi miaka 178, na Eberi miaka 239, na Pelegi miaka 48, na Reu 78, na Serugi miaka 101, na Nahori miaka 49, na Tera 135, baada ya kuzaliwa kwa Abramu. Hivyo vizazi vilivyoishi ni 11 kwa wakati mmoja.

 

2158 K.K.

Sarai alizaliwa. Sarai pia alikuwa binti wa Tera (MWA 20:12). Abramu alimzidi Sara miaka kumi. (MWA 17:17)

 

2118 K.K.

Tera, Abramu na Lutu waliondoka kutoka nchi ya Uru wa Wakaldayo mpaka Harani. (MWA 11:31)

 

2110 K.K.

Nuhu alifariki akiwa na miaka 950.

 

2093 K.K.

Abramu na Lutu walitoka Harani baada ya kukaa huko miaka 24. (MWA 12)

Tera alibaki huko na alikufa baada ya miaka 60 huko. (MWA 12:1-5)

 

2092 K.K.

Abramu aliondoka kwenda Misri akae huko kwa kipindi cha njaa. (MWA 12:10-13:1)

 

2090 K.K.

Abramu na Lutu walitengana. (MWA 13:5-12)

 

2085 K.K.

Vita katika Bonde la Sidimu. Lutu pamoja na jamaa yake walichukuliwa mateka. Abramu alipigana na ndiye aliyeshinda vita na Abramu alishinda, na akamrudisha Lutu. Baadaye Abramu alikutana na Melkisedeki (Shemu?) (MWA 14)

 

2084 K.K.

Bwana alimtokea Abramu. (MWA 15)

 

2082 K.K.

Ishmaeli alizaliwa. (MWA 16)

 

2069 K.K.

Abramu alipewa jina Ibrahimu na Sarai akaitwa Sara. (MWA 17:5,15)

Tohara. (MWA 17:10,23-27)

Mungu aliangamiza Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu kwa moto na kiberiti. (MWA 19, KUM 29:23)

 

2068 K.K.

Isaka alizaliwa. (MWA 22:1-3) Ibrahimu alikuwa na miaka 100 na Sara miaka 90 Isaka alipozaliwa. (MWA 21:5, 17:17)

 

2050 K.K.

Ibrahimu alimtoa Isaka dhabihu. (MWA 22:1-19)

 

2033 K.K.

Tera baba yao Ibrahimu na Saara alifariki. (MWA 11:32)

 

2031 K.K.

Sara alifariki huko Hebroni akiwa na miaka 127, miaka miwili baada ya kifo cha baba yake. (MWA 23:1,2)

 

2028 K.K.

Isaka alimwoa binti wa Bethueli Rebeka. (MWA 22:20-23, MWA 24)

 

2008 K.K.

Mapacha Esau na Yakobo walizaliwa. (MWA 25:20-26)

 

1993 K.K.

Ibrahimu alifariki. (MWA 25:8) Esau na Yakobo walikuwa na miaka 15.

 

1968 K.K.

Esau alioa binti wa Wahiti Yudithi na Basemathi akiwa na miaka 40. (MWA 26:34)

 

1958 K.K.

Shemu (Melkisedeki?) mwana wa Nuhu alifariki akiwa na miaka 600. Ilitokea miaka 35 baada ya kifo cha Ibrahimu.

 

 

1945 K.K.

Ishmaeli alikuwa na miaka 137 wakati wa kifo chake. (MWA 25:17)

 

1931 K.K.

Yakobo alikwenda kwa Labani, mjomba wake, akiwa na miaka 77. (MWA 28:10-29:13)

 

1924 K.K.

Yakobo aliwaoa binamu zake Lea na Raheli akiwa na miaka 84. (MWA 29:17-28)

 

1917 K.K.

Yusufu alizaliwa. (MWA 30:22-24)

 

1911 K.K.

Yakobo na jamaa yake walitoka kwa Labani kurudi nchi ya Kanani. (MWA 31-35) Inawezekana mama yake alikuwa amekwisha kufariki na baba yake Isaka alikuwa na miaka 157.

 

1905 K.K.

Benyamini alizaliwa.

Raheli alifariki. (MWA 35:17-19)

 

1900 K.K.

Yusufu aliingia Misri akiwa kama mtumwa kwa Potifa akiwa na miaka 17. (MWA 37: 28,36)

Potifa alikuwa farao Sesostris II (1903-1887) mfanyakazi wa ndani na mkuu wa aliyeangalia usalama.

 

1891 K.K.

Yusufu alifungwa. (MWA 39:20)

 

1888 K.K.

Isaka alifariki akiwa na miaka 180. (MWA 35:28,29)

 

1887 K.K.

Yusufu alipelekwa mbele ya farao Sesostris III (Farao alitawala 1887-1849) (MWA 41:14)

 

1887-1880 K.K.

Ilikuwa miaka ya mavuno (MWA 41:47)

 

1880-1873 K.K.

Ilikuwa miaka ya njaa. (MWA 41:54)

 

1879 K.K.

Ndugu zake Yusufu walikwenda Misri mara ya kwanza. (MWA 42)

 

1878 K.K.

Yakobo alikwenda Misri. Alikutana na Yusufu baada ya kutengana miaka 22. Yakobo aliishi miaka 17 baadaye. (MWA 46)

 

1861 K.K.

Yakobo alifariki akiwa na miaka 147. (MWA 47:28, 49:33)

 

1849 K.K.

Yusufu alipoteza kazi na mamlaka yake kwa sababu farao Sesostris III alifariki na farao Amenemhet III alianza kutawala.

Hapo wana wa Israeli walianza kuteswa na mateso yalichukua miaka 400. (MDO 7:6)

Nayo yaliendelea mpaka mwaka wa 1448 K.K., wakati huo wana wa Israeli walitoka Misri.

 

1807 K.K.

Yusufu alifariki akiwa na miaka 110. (MWA 50:26)

Mwisho wa kitabu cha MWANZO.

 

Tangu mwaka wa 1807 K.K. hadi mwaka wa 1558 K.K. ilikuwa katikati ya MWANZO na KUTOKA na ilikuwa miaka 250. Biblia haisemi mambo yaliyotokeo hapo katikati. Wakati huo wana wa Israeli waliongezeka huko Misri. Waliishi kwenye jimbo la Gosheni.

Jamii ya kifalme Babeli wa kwanza ilitawala. (1894-1595) Hammurabi, mwanasheria maarufu, alikuwa mfalme (1792-1750 K.K.).

 

Kwenye mwaka wa 1730 kabila la Hyksos liliwatawala Wamisri. Lilikuwa na magari ya farasi ya kivita na hivyo Wamisri hawakuweza kitu. Kabila la Hyksos lilitawala Misri miaka 150. Kabila la Hyksos lilitoka kaskazini na lilikuwa jamaa ya Shemu. Huko Misri, katika mji wa Thebe farao Sekenenre (1600 K.K.) alipigana na kabila la Hyksos lakini aliuawa katika mapigano. Inawezekana aliuawa wakati wa vita. Fuvu la kichwa chake kilichojeruhiwa liko katika jumba la makumbusho huko Kairo. Kijana wake farao Ahmose (aliyetawala 1580-1558 K.K.) pamoja na ndugu yake Kamose walifaulu na kuwafukuza wa Hyksos toka Misri.

 

Farao Amenhotepi I (alitawala 1558-1525 K.K.) aliyemfuatia farao Ahmose, alianza kuwatesa sana wana wa Israeli. Aliogopa kwamba Waisraeli watakapopata nguvu zaidi watawatawala Wamisri na kuwaweka chini ya utawala wao, kama watu wa Hyksos walivyofanya kabla.

 

1558-1447 K.K.

 

Misri Farao Thotmesi IV alitawala (1425-1405) na baadaye farao Amenhotepi III alitawala (1405-1370). Mke wake malkia Teje.

1408 K.K.

KUMBUKUMBU LA TORATI

 

Kifo cha Haruni na Musa. (HES 20:28, KUM 34:5)

1408-1387 K.K.

KITABU CHA YOSHUA. Ilichukua miaka 21.

1408 K.K.

Chini ya uongozi wa Yoshua wana wa Israeli waliingia nchini Israeli. Kutekwa kwa Yeriko. (YOS 6)

1402 K.K.

Nchi iligawanywa kati ya makabila ya Israeli. (YOS 13-21)

1401 K.K.

Hema ya kukutania ilisimimishwa Shilo. (YOS 18:1)

1400 K.K.

Makabila ya Reubeni, Gadi na upande wa pili wa kabila la Manase walirudi mashariki ya Yordani. (YOS 22)

1387 K.K.

Yoshua alifariki akiwa na miaka 110. (YOS 24:29)

Kumalizika kwa kitabu cha YOSHUA.

 

1387-1070 K.K.

KITABU CHA WAAMUZI. Ilichukua miaka 317.

Waisraeli walianza kumsahau Mungu polepole. (AMU 3:12-14)

Farao Amenhotepi IV, yaani Ekhnaton, alitawala nchi ya Misri (1370-1352). Mama malkia Teje. Mke Nefertiti.

1368 K.K.

Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia aliwatesa wana wa Israeli. (AMU 3:8)

1360 K.K.

Kijana wa ndugu yake Kalebu, Othnieli aliwapa uhuru Waisraeli. (AMU 3:10) Othnieli akiwa mwamuzi. Amani miaka 40.

Waamuzi walitawala sehemu mbali mbali za Israeli, na wachache kwa wakati moja.

Ndiyo maana miaka inalaliana na hata hivyo hatuna uhakika na miaka kamili. (AMU 3:10)

1320 K.K.

Egloni mfalme wa Moabu aliwatesa wana wa Israeli.

Na aliteka mji wa Mitende, yaani Yeriko. (AMU 3:12-14)

1302 K.K.

Ehudi Mbenyamini mwenye mkono wa kushoto, aliwapa uhuru Waisraeli, na alimwua mfalme Egloni. (AMU 3:15-30) Ehudi akiwa mwamuzi na baada yake Shamgari. Wakati wa amani ulichukua miaka 80. (AMU 3:31)

1222 K.K.

Mfalme aliyetawala kaskazini mwa Palestina mfalme wa Kanaani Yabini pamoja na mkuu wa jeshi Sisera, waliwatesa wana wa Israeli. (AMU 4:1-3)

1202 K.K.

Baraka aliondoka kwenda kupigana na Sisera baada ya kuambiwa na hakimu wa kike nabii Debora. Israeli ilipata uhuru. (AMU 4:4-24) Wimbo wa Debora. (AMU 5) Amani ilikuwepo miaka 40. (AMU 5:31)

1162 K.K.

Wamidiani waliwatesa Waisraeli. (AMU 6:1-6)

Gideoni, yaani Yerubaali, aliwashinda Wamidiani akiwa na wanajeshi 300. (AMU 6:11-7:25)

Abimeleki, mwana wa Gideoni, alikuwa mfalme. (AMU 9)

Tola alikuwa mwamuzi miaka 23. (AMU 10:1,2)

Yairi alikuwa mwamuzi miaka 22. (AMU 10:3-5)

Wana wa Israeli walimkosea tena Mungu. Waliabudu Baali na Ashtorehti na miungu mingine. Mungu akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamori kwa miaka 18. Waisraeli walimlilia Mungu. (AMU 10:6-18)

1115-1012 K.K.

KITABU CHA KWANZA CHA SAMWELI. Kilichukua miaka 103.

1115 K.K.

Samweli alizaliwa. (1SAM 1)

1112 K.K.

Yeftha aliwashinda maadui wa Israeli. Akawa mwamuzi Israeli kwa miaka 6. (AMU 11:1-12:7)

Ibzani wa Bethlehemu alikuwa mwamuzi kwa miaka 7. (AMU 12:8-10)

Eloni alikuwa mwamuzi kwa miaka 10. (AMU 12:11-12)

Abdoni Mpirathoni alikuwa mwamuzi kwa miaka 8. (AMU 12:13-15)

1077 K.K.

Wafilisti waliwashinda Waisraeli na kuiba Sanduko la Agano. (1SAM 4)

Kuhani Eli alifariki. (1SAM 4)

Samsoni na Delila. (AMU 16:4-31) Samsoni mwamuzi kwa miaka 20. (AMU 13-16)

Sura za mwisho za KITABU CHA WAAMUZI (AMU 17-21) mambo yake yalitokea kabla ya sura za mwanzo.

1070 K.K.

Mwisho wa KITABU CHA WAAMUZI. Ilichukua miaka 317.

KITABU CHA RUTHU kilianza wakati wa KITABU CHA WAAMUZI. (RUT 1:1)

1056 K.K.

Waisraeli waliwashinda Wafilisti waliokuwa wamewatesa kwa miaka 20. (1SAM 7)

1052 K.K.

Sauli alifanywa kuwa mfalme. (1SAM 10)

1042 K.K.

Daudi alizaliwa.

(Dada na ndugu za Daudi 1NYA 2:13-16 na 2SAM 17:25)

1026 K.K.

Daudi alipakwa mafuta kuwa mfalme. (1SAM 16)

1024 K.K.

Daudi na Goliathi. (1SAM 17)

Sauli alianza kumchukia Daudi. Daudi anaoa binti wa Sauli Mikali. (1SAM 18:15-27)

1017 K.K.

Samweli alikufa.(1SAM 25:1)

1012 K.K.

Wana wa Sauli Yonathani, Abinadabu na Malkishua waliuawa na Wafilisti. (1SAM 31:2)

Sauli alijaribu kujiua. (1Sm 31:4, 1NYA 10)

KITABU CHA KWANZA CHA SAMWELI kilimalizika.

1012-972 K.K.

KITABU CHA PILI CHA SAMWELI. Kilichukua miaka 40.

KITABU CHA KWANZA CHA MAMBO YA NYAKATI Kilichukua miaka 40. (Miaka inahesabiwa tangu sura ya 10)

Mwamaleki kijana alimwua Sauli, aliyeumia wakati alipojaribu kujiua. (2SAM 1:5-10)

Daudi alifanywa mfalme wa Yuda. (2SAM 2:4)

Ishboshethi mwana wa Sauli akawa mfalme juu ya sehemu ingine ya Israeli. (2SAM 2:8-10)

1010 K.K.

Ishboshethi aliuawa. Daudi aliwaadhibu wauaji. (SAM 4)

1005 K.K.

Daudi aliwekwa kuwa mfalme juu ya Israeli yote. Yerusalemu ikawa mji mkuu. (2SAM 5:3, 1NYA 11:1-3)

980 K.K.

Absalomu mwana wa Daudi alijaribu kuchukua utawala kwa njia ya vurugu.(2SAM 15-18)

973 K.K.

Rehoboamu, mwana wa Sulemani alizaliwa. (2NYA 12:13)

972 K.K.

Sulemani alikuwa mfalme. (1FAL 1, 1NYA 29:28)

Daudi alikufa. (1FAL 2:10, 1NYA 29:26-28)

KITABU CHA PILI CHA SAMWELI kilimalizika.

KITABU CHA KWANZA CHA MAMBO YA NYAKATI kilimalizika.

Mungu alitokea Sulemani. (1FAL 3:5-14)

972-853 K.K.

KITABU CHA KWANZA CHA WAFALME. Kilichukua miaka 119.

972-538 K.K.

 

KITABU CHA PILI CHA MAMBO YA NYAKATI.

Kilichukua miaka 434.

 

968 K.K.

Sulemani alianza kujenga Hekalu katika mwaka wa 480 baada ya Israeli kutoka Misri. (968+480=1448 = mwaka wa Israeli kuondoka Misri) (1FAL 6, 2NYA 2)

 

961 K.K.

Hekalu lilikamilika. (1FAL 6:38) Ufunguzi. (1FAL 8, 2NYA 6)

 

960 K.K.

Sulemani alianza kujenga nyumba yake. (1FAL 7:1)

 

947 K.K.

Nyumba ya Sulemani ilikamilika. (1FAL 7, 2NYA 8:1)

Bwana alimtokea Sulemani tena mara ya pili.(1FAL 9:1-9, 2NYA 7:11-22)

 

Malkia wa Sheba alienda kumsalimia Sulemani. (1FAL 10, 2NYA 9)

Sulemani alimwacha Mungu. (1FAL 11:1-11)

KITABU CHA MHUBIRI. Kinaeleza juu ya mawazo ya Sulemani ya kipotofu.

 

932 K.K.

Sulemani alifariki. (1FAL 11:43, 2NYA 9:30-31)

 

Utawala uligawanyika:

Israeli ya Kaskazini, na Israeli ya Kusini, yaani Yuda.

(1FAL 12, 2NYA 10)

 

Ni vigumu kujua miaka kamili ya utawala wa wafalme wa Israeli ya kaskazini na Yuda pia, kwani mara nyingi mtoto alianza utawala hata kabla ya kifo cha baba. Hivyo hatuna uhakika na miaka.

 

931-722 K.K.

Wafalme wa Israeli ya Kaskazini:

 

Yeroboamu I, (931-910 K.K.) alikuwa mfalme Israeli ya kaskazini miaka 22. Alifanya mabaya. (1FAL 12:20-14:21) Manabii wakati wa Yeroboamu: Mtu wa Mungu (Yeddo?) (1FAL 13:1-32). Ahia. (1FAL 14:2-18).

 

Nadabu, (910-909 K.K.) mwana wa Yeroboamu, alikuwa mfalme miaka 2. Alifanya mabaya. (1FAL 14:20, 15:25-28)

 

Baasha, (909-886 K.K.) Mwisakari, alimwua Nadabu, akawa mfalme miaka 24. Alifanya mabaya. (1FAL 15:27-16:6) Nabii alikuwa Yehu.

 

Ela, (886-885 K.K.) mwana wa Baasha, alitawala miaka 2. Alifanya mabaya. (1FAL 16:6-10,13,14) Nabii alikuwa Yehu.

 

Zimri, (885 K.K.) alikuwa mfalme siku saba. Alimwua Ela. Aliua jamaa yote ya Baasha. Alifanya mabaya. Alijiunguza na moto hadi akafa. (1FAL 16:9-20)

 

Omri, (885-874 K.K.) alitawala miaka 12. Alianzisha Samaria. Alifanya mabaya zaidi ya wale waliotangulia. (1FAL 16:16-28)

 

Ahabu, (874-853 K.K.) mwana wa Omri, miaka 22. Mke wake Yezebeli. Ahabu aliabudu Baali. Alifanya mabaya. (1FAL 16:28-22:40) Wakati wake, nabii Eliya alitabiri.

 

Ahazia, (853-852 K.K.) mwana wa Ahabu, miaka 2. Alifanya mabaya. (1FAL 22:51-53)

 

Yoramu, (852-841 K.K.) mwana wa Ahabu, miaka 12. Alifanya mabaya. Manabii Mikaya mwana wa Imla na Elisha walikuwa manabii wakati wa Yoramu. (2FAL 3:1-, 6:26-7:20, 8:28-, 29, 9:15-24)

 

Yehu, (841-814 K.K.) alitawala miaka 28. Aliteketeza jamaa ya Ahabu. Akafutilia mbali kuabudu Baali. Nabii alikuwa Elisha. (2FAL 9-10)

 

Yehoahazi, (814-798 K.K.) mwana wa Yehu, miaka 17. Alifanya mabaya. (2FAL 13:1-9)

Yehoashi, (Yoashi) (798-782 K.K.) mwana wa Yehoahazi, miaka 16. Alipigana na mfalme wa Yuda Amazia na alimshinda. Alifanya mabaya. (2FAL 13:9-25, 14:8-16)

 

Yeroboamu II, (782-753 K.K.) mwana wa Yehoashi , alitawala miaka 41. Alifanya mabaya. (2FAL 14:16, 23-29) Manabii walikuwa Yona, Amosi na Hosea.

 

Zekaria, (753-752 K.K.) mwana wa Yeroboamu alitawala nusu mwaka. Alifanya mabaya. (2FAL 15:8-11) Nabii alikuwa Hosea.

 

Shalumu, (752 K.K.) mwezi 1. Alimwua Zekaria. (2FAL 15:10-15) Nabii alikuwa Hosea.

 

Menahemu, (752-742 K.K.) miaka 10. Alimwua Shalumu. Alifanya mabaya. (2FAL 15:14-22) Nabii alikuwa Hosea.

 

Pekahia, (742-740 K.K.) mwana wa Menahemu, miaka 2. Alifanya mabaya. (2FAL 15:23-26) Nabii alikuwa Hosea.

 

Peka, (740-732 K.K.) alitawala miaka 20. Alimwua Pekahia. Alifanya mabaya. (2FAL 15:25-30) Nabii alikuwa Hosea.

 

Hoshea (732-723/722 K.K.) alikuwa mtawala wa mwisho wa Israeli ya kaskazini. Alitawala miaka 9. Alimwua Peka. Alifanya mabaya. Alichukuliwa mateka Ashuru. (2FAL 15:30, 17:1-6) Nabii alikuwa Hosea.

 

722 K.K.

Kumalizika kwa Waisraeli walihamia Ashuru.

 

931-586 K.K.

Wafalme wa Israeli ya Kusini, yaani Yuda:

 

931 K.K.

Rehoboamu, (931-914) mwana wa Sulemani, alikuwa mfalme wa Yuda miaka 17. Alifanya mabaya. (1FAL 12:1-24, 14:21-31, 2NYA 10-12) Nabii alikuwa Shemaya. (1FAL 12

(1FAL 12:22-24)

 

925 K.K.

Farao Shishaki alitawala Yerusalemu na aliwaibia. (1FAL 14:25,26)

 

Abiya, (913-911) mwana wa Rehoboamu alitawala miaka 3. Alifanya mabaya. (1Kn 15:1-8, 2Ak 13:1-14:1) Nabii alikuwa Iddo.

 

Asa, (911-870) mwana wa Abiya alitawala miaka 41. Alifanya mema. Manabii walikuwa Asaria na Hanani. (1FAL 15:8-24, 2Ak 14-16)

 

Yehoshafati, (870-848) mwana wa Asa, alitawala miaka 25. Mama yake alikuwa Azuba. Alifanya amani na Israeli. Alifanya mema. (1FAL 22:41-51)

 

Yehoramu, (848-841) mwana wa Yehoshafati alitawala miaka 8. Mkewe binti wa Ahabu. Alifanya mabaya. (1FAL 22:51, 2FAL 8:16-24) Nabii alikuwa Obadia.

 

Ahazia, (841) mwana wa Yehoramu mwaka 1. Yehu mfalme wa Israeli alimwua. Ahazia alifanya mabaya. (2FAL 8:25-29, 9:16-29)

 

Athalia, (841-835) mamaye Ahazia alitawala miaka 6. Alikuwa mtawala mbaya sana. (2FAL 11:1-20)

 

Yoashi, (835-796) mwana wa Ahazia alitawala miaka 40. Alifanya mema. (2FAL 12:1-21) Manabii walikuwa Yoeli na Zekaria.

 

Amazia, (796-767) mwana wa Yoashi alitawala miaka 29. Alifanya mema. (2FAL 14:1-20) Nabii alikuwa Zekaria.

 

Azaria, yaani Uzia, (767-740) mwana wa Amazia alitawala miaka 52. Alifanya mema. Aliugua muda mrefu, hakuweza kutawala mwishoni. (2FAL 4:21,22,15:1-7) Nabii alikuwa Isaya.

 

Yothamu, (750/740-735) mwana wa Azaria alitawala miaka 16. Alifanya mema. (2FAL 15:32-38) Manabii walikuwa Isaya na Mika.

 

Ahazi, (732-716) mwana wa Yothamu miaka 16. Hakufanya mazuri. (2FAL 15:38-16:20) Manabii walikuwa Isaya na Mika.

 

722 K.K.

Israeli ya Kaskazini ilihamishwa Ashuru. Israeli ya Kaskazini haikuwepo tena. (2FAL 17)

 

Hezekia, (716-687 K.K.) mwana wa Ahazi alitawala miaka 29. Alifanya mazuri. Aliugua lakini aliongezewa maisha miaka 15. (2FAL 18:1-20:21) Manabii walikuwa Isaya na Mika.

 

Manase, (687-643 K.K.) mwana wa Hezekia alitawala miaka 55. Alifanya mabaya. Baadaya alinyenye kea. (2FAL 21:1-18) Nabii alikuwa Isaya.

 

Amoni, (643-641 B.K.) mwana wa Manase alitawala miaka 2. Alifanya mabaya. (2FAL 21:18-26)

 

Yosia, (641-609 K.K.) mwana wa Amoni alitawala miaka 31. Alifanya mema. Aliimarisha ibada. Ulikuwa wakati wa uamusho Yuda. Farao-neko alimwua. (2FAL 22:1-23:30) Manabii walikuwa Nahumu, Habakuki, Sefania, Yeremia na Hulda walitabiri wakati wa Yosia.

 

Yehoahazi, (609 K.K.) mwana wa Yosia alitawala miezi 3 tu. Alifanya mabaya. Farao-neko alimweka kifungoni na akampeleka Misri. (2FAL 23:30-34) Manabii walikuwa Yeremia na Habakuki.

 

Yehojakimu, (= Eliakimu) (609-598 K.K.) mwana wa Yosia, ndugu wa Yehoahazi alitawala miaka 11. Alifanya mabaya. (2FAL 23:34-24:6) Nabii alikuwa Yeremia.

 

605-562 K.K.

Nebukadreza alitawala Babeli.

 

604 K.K.

Danieli pamoja na wengine wa jamii ya kifalme walihamishiwa katika uhamisho wa lazima Babeli. (DAN 1:1-6)

 

Yekonia, (598/597 K.K.) mwana wa Yehoyakimu alitawala miezi 3 tu. Alifanya mabaya. Nebukadreza aliteka Yerusalemu na kuchukua vitu vya Hekalu na sehemu kubwa ya watu wa Yerusalemu akawapeleka Babeli. (2FAL 24:6-15) Nabii Yeremia.

 

Ezekieli alipelekwa Babeli. Alitabiri miaka 593-570 K.K.

 

Sedekia, (=Matania) (597-586 K.K.) ndugu ya baba yake Yekonia alitawala miaka 11. Alifanya mabaya. (2FAL 24:17-25:7) Nabii Yeremia.

 

588 K.K.

Nebukadreza alianza kuizunguka Yerusalemu. (2FAL 25:1)

 

586 K.K.

Yerusalemu ilitekwa. Mji na Hekalu viliteketezwa. Sedekia na watu na sehemu kubwa walipelekwa Babeli. (2FAL 25:2-4)

 

582 K.K.

Sehemu ya mwisho ya wafungwa walihamishiwa Babeli.

 

560-480 K.K.

Budha (Bara-Hindi)

 

551-478 K.K.

Konfutse (Uchina)

 

539 K.K.

Koreshi alitawala Babeli. Utawala wa Babeli uliharibika. (2NYA 36:21-) Uajemi ikawa utawala wa dunia nzima mpya.

 

538 K.K.

Wayahudi kama 50.000 walirudi Yerusalemu kufuatia wito wa Zerubabeli. (2NYA 36:22,23)

 

537 K.K.

Msingi wa Hekalu ulijengwa. Kazi ilisimamishwa.

 

536 K.K.

Maono ya mwisho wa kitabu cha Danieli.

 

520 K.K.

Ujenzi wa Hekalu ulianza tena. Manabii walikuwa Hagai na Zekaria.

 

516 K.K.

Zerubabeli alifungua Hekalu.

 

486-465 K.K.

Ahasuero (Kserkses I) alikuwa mtawala wa Uajemi.

Kitabu cha ESTA. (Kilichukua miaka 21)

 

485-425 K.K.

Myunani Herodotos mwandishi wa historia.

 

480 K.K.

Esta akawa malkia.

 

470-399 K.K.

Myunani Sokrates mfilosofia.

 

457 K.K.

Ezra aliingia Yerusalemu pamoja na Wayahudi 2000.

 

445 K.K.

Nehemia alienda kutengeneza kuta za Yerusalemu. Nabii alikuwa Malakia.

 

428-348 K.K. Platon.

 

384-322 K.K. Aristoteles.

Vitabu vya Agano la Kale:

 

Miaka kabla ya Kristo (K.K.)

 

MWANZO. Tangu mwanzo hadi mwaka wa 1807 K.K.

KUTOKA 1558-1447 K.K. (Kilichukua miaka 111)

MAMBO YA WALAWI 1446. K.K.

HESABU 1446-1408 K.K. (Kilichukua miaka 38)

KUMBUKUMBU LA TORATI 1408.K.K.

YOSHUA 1408-1387. K.K. (Kilichukua miaka 21)

WAAMUZI 1387-1070. K.K. (Kilichukua miaka 317)

RUTHU yanatokea wakati wa Waamuzi. (RUT 1:1)

1. SAMWELI. 1115-1012 K.K. (Kilichukua miaka 103)

2. SAMWELI. 1012-972 K.K. (Kilichukua miaka 40)

1. WAFALME. 972-853 K.K. (Kilichukua miaka 119)

2. WAFALME. 853-562 K.K. (Kilichukua miaka 291)

1. MAMBO YA NYAKATI. (Tangu 1NYA 10) 1012-972 K.K. (Kilichukua miaka 40)

2. MAMBO YA NYAKATI. 972-538 K.K. (Kilichukua miaka 434)

EZRA. 538-457 K.K. (Kilichukua miaka 81)

NEHEMIA. 445-432 K.K. (Kilichukua miaka 13)

ESTA. 486-465 K.K. (Kilichukua miaka 21)

AYUBU. Wakati wa Ibrahimu (2168-1993 K.K.)

ZABURI. 1450-500 K.K.

MITHALI. Wakati wa utawala wa Sulemani 972-932 K.K. Na pia baada ya Sulemani.

MHUBIRI. Wakati wa mwisho wa maisha ya Sulemani 935 K.K.

WIMBO ULIO BORA. Wakati wa mwanzo wa utawala wa Sulemani 970 K.K.

ISAYA 739-701. K.K. (au labda hadi mwaka 680 K.K.)

YEREMIA. 627-586 K.K.

MAOMBOLEZO. 586 K.K.

EZEKIELI alizaliwa 623 K.K. Alipelekwa Babeli 598, alitabiri 593-570 K.K.

DANIELI alizaliwa 622 K.K. Alipelekwa Babeli 604, alitabiri Babeli mpaka mwaka wa 536. K.K.

HOSEA aliishi miaka ya 770-700 K.K. Alikuwa nabii miaka ya 750-722 K.K.

YOELI aliishi Yuda katikati miaka ya 800 na 700 K.K.

AMOSI alitabiri Kusini mwa Israeli 765-750 K.K.

OBADIA muda wa kazi haujulikani. Labda mwaka wa 850 au 586 K.K.

YONA aliishi katikati miaka ya 800 na 700 K.K.

MIKA alitabiri 730-680 K.K.

NAHUMU, HABAKUKI na SEFANIA walitabiri wakati wa Yosia 640-609 K.K.

HAGAI na ZEKARIA miaka 520 K.K.

MALAKI kama miaka 425 K.K. Nabii wa mwisho wa Agano la Kale.

 

Miaka 400 ilipita kati ya Agano la Kale na Agano Jipya.

Persia ilitawala baada ya Babyloni na 330 K.K. Ugiriki iliimarika.

Mwaka wa 100 Wayahudi walijaribiwa kuwageuza wawe Wagiriki kwa lazima.

Wayahudi walipambana na Wagiriki lakini Wayahudi hawakufanikiwa.

Septuaginta (jina la Agano la Kale tafsiri ya Kigirigi) ilikamilika mwaka wa 150 K.K.

Polepole Warumi walipata nguvu na mwaka wa 63 K.K. Waisraeli walichukuliwa chini ya utawala wa Rumi.

 

Miaka ya utawala duniani:

 

Babeli 604-539 K.K.

Uajemi 539-332 K.K.

Ugiriki, yaani Uyunani 332-320 K.K.

Misri 320-198 K.K.

Siria 198-165 K.K.

Wamakabi na Wahasmoni 165-63 K.K. (Israeli)

Warumi waliteka Israeli 63 K.K.

 

37-4 K.K. Herode mkuu mfalme wa Palestina.

 

19 K.K. Ujenzi wa Hekalu la Yerusalemu ulianzishwa.

 

 

Agano la Kale lilimalizika.

 

Wakati wa Agano Jipya ulianza.

 

Matukio ya Agano Jipya:

 

5 K.K. Yesu alizaliwa.

8 B.K. (= baada ya Kristo) Yesu aliingia katika Hekalu Yerusalemu akiwa na miaka 12.

26 B.K. Yohana mbatizaji alianza kuhubiri.

26-30 B.K. Kazi ya Yesu.

31 B.K. Kifo cha Anania na Safira.

33 B.K. Kifo cha Stefano.

33/34 B.K. Sauli yaani Paulo alibadilika.

34-42 B.K. Paulo Uarabuni, Dameski, Yerusalemu na Tarso.

42 B.K. Paulo aliwekwa kuwa mchungaji wa kanisa la Antiokia.

44 B.K. Mtume Yakobo alikufa kifo cha mfia dini, Petro alitoka gerezani ki-miujiiza.

45-48 B.K. Safari ya kwanza ya Paulo ya kimisheni.

50-53 B.K. Safari ya pili ya Paulo ya kimisheni.

54-58 B.K. Safari ya tatu ya Paulo ya kimisheni.

58-60 B.K. Paulo aliwekwa kifungoni Kaisaria.

61-63 B.K. Paulo alifungwa Rumi.

67 B.K. Paulo na Petro waliuawa.

98 B.K. Mtume Yohana alifariki.

100 B.K. Wakati wa Mitume ulikwisha.

590-1517 B.K. Ukatoliki uliendelea.

570-632 B.K. Muhamedi

1517- B.K. Kanisa la kiprotestanti lilianza.

1900 B.K. Uamsho wa Pentekoste ulianza.

 

Vitabu vya Agano Jipya:

 

Mwaka wa vimeandikwa:

 

MATHAYO 50 B.K.

MARKO 64-68 B.K.

LUKA 58 B.K.

YOHANA 90 ? B.K.

MATENDO 63 B.K.

WARUMI 57/58 B.K.

1. WAKORINTHO 54/55 B.K.

2. WAKORINTHO 57 B.K.

WAGALATIA 53 B.K.

WAEFESO 61/62 B.K.

WAFILIPI 62 B.K.

WAKOLOSAI 62 B.K.

1. WATHESALONIKE 50 B.K.

2. WATHESALONIKE 52 B.K.

1. TIMOTHEO 63-67 B.K.

2. TIMOTHEO 67 B.K.

TITO 63-67 B.K.

FILEMONI 62 B.K.

WAEBRANIA kabla ya 70 B.K.

YAKOBO 45-50 B.K.

1. PETRO 65 B.K.

2. PETRO 67 B.K.

1. YOHANA 85-90 B.K.

2. YOHANA 85-90 B.K.

3. YOHANA 85-90 B.K.

YUDA 66/67 B.K.

UFUNUO 95 B.K.

 

 

KUTOKA. Ilichukua miaka 111.

 

1558 K.K.

Farao Amenhotepi I (1558-1525) alichukua utawala. (KUT 1:8)

 

1531 K.K.

Haruni alizaliwa.

 

1529 K.K.

Farao Amenhotepi I alitoa amri: "Watoto wa Waisraeli wote wakiume watupwe mtoni, mto Nile." (KUT 1:22)

 

1528 K.K.

Musa alizaliwa. Binti wa farao Amenhotepi I (jina lake Hatsepsuti) alimchukua mtoto Musa. (KUT 2)

 

1525 K.K.

Farao Amenhotepi I alifariki na farao Thotmesi I (1525-1508) alichukua utawala. Musa alikuwa na miaka 3.

 

1508 K.K.

Farao Thotmesi I alifariki na farao Thotmesi II (1508-1504) alichukua utawala. Musa alikuwa na miaka 20.

 

1504 K.K.

Farao Thotmesi II alifariki. Musa alikataa kuwa farao. (EBR 11:24) Hatsepsuti, mama yake wa kambo alichukua utawala (1504-1492).

Wakati huo alizaliwa Thotmesi III, mtoto wa dada au wa kaka yake Hatsepsuti.

 

1497 K.K.

Yoshua alizaliwa.

 

1487 K.K.

Musa alianza kuwatetea Waebrania waliokuwa watumwa Misri. Musa alikuwa kinyume cha Wamisri.

Farao Hatsepsuti akaogopa kwamba Musa, atakapokuwa mfalme, angehamisha utawala kutoka Misri kwenda kwa Waebrania yaani wa Waisraeli.

Ili mambo hayo yasifanyike, Hapsepsuti alitoa amri Musa auawe.

Musa akakimbia mpaka Midiani. (KUT 2:11-15)

 

1482 K.K.

Farao Thotmesi III (1482-1450) alichukua utawala.

 

1450 K.K.

Farao Amenhotepi II (1450-1425) alichukua utawala.

 

1448 K.K.

Musa mbele ya kijiti cha moto. (KUT 3)

Musa alirudi Misri.

Mapigo.

Waisraeli walitoka Misri. (KUT 3-12)

 

1448-1408 K.K.

Safari ya wana wa Israeli kutoka Misri jangwani kwenda nchi ya ahadi.

 

1447 K.K.

Kujengwa kwa Hema ya kukutania. (KUT 25-40)

Mwisho wa KUTOKA.

MAMBO YA WALAWI.

 

1446-1408 K.K.

HESABU. Ilichukua miaka 38.

 

 

Maana ya majina ya Biblia

 

 

A

Abramu = Baba aliyeinuliwa

Adamu = Mwanadamu. Wanadamu. Mwekundu

Agabo = Kupenda

Agagi = Mwenye fitina

Agripa = Farasi mwitu

Ahabu = Ndugu ya baba

Ahasuero = Mtawala. Mfalme

Ai = Maporomoko

Akani = Ajali. Msababishji wa ajali

Akila = Tai

Amori = Wa-mlima

Amosi = Aliyesumbuliwa. Mbeba mzigo. Mwenye nguvu.

Anania = Yehova ni mwenye neema

Anasi = Mungu ni wahuruma

Andrea = Mwanamume

Apolo = Miungu wa Waapolonia

Areopago = Vilima vya (mungu) Aresi

Arkipo = Mtawala wa farasi

Asa = Daktari. Mponyaji

Asafu = Mkusanyaji

Asheri = Heri. Mwenye heri

Athene = Mji wa (mungu) Athene

Augusto = Anayestahili sifa

Ayubu = Anayechukiwa. Mwenyekutubu

 

B

Babeli = Anayeingiza kwenye vurugu. Mvurugaji

Balaamu = Mgeni

Balaki = Mwangamizaji

Barnaba = Kijana wa faraja

Bartholomayo = Mwana wa Talmai

Bartimayo = Mwana wa Timayo

Bath-sheba = Binti wa kiapo. Binti wa saba

Beelzebuli = Bwana wa inzi

Beer-sheba = Kisima ya kiapo. Kisima ya saba

Belshaza = Mfalme alindwa (mungu) Beel

Belteshaza = Beel (mungu) alinda uhai wake

Benyamini = Mwana wa furaha (yaani mwana wa mkono wa kulia)

Bethania = Kijiji cha maskini

Betheli = Nyumba ya Mungu

Bethfage = Sehemu ya kutunza mizabibu mabichi

Bethsaida = Eneo la kuvua samaki

Bethzatha = Nyumba ya upole

Betlehemu = Nyumba ya mikate

Boanerge = Wana wa ngurumo

Bonde la Akori = Ajali

 

D

Dani = Hakimu

Danieli = Mungu ni hakimu wangu

Dario = Mtawala. Anayechipusha

Daudi = Anayependwa

Debora = Nyuki

Dekapoli = Mji wa kumi

Delila = Anayependa kujipendekeza

Dema = Mwanaume wa watu

 

E

Eben-ezeri = Jiwe la msaada

Edeni = Uzuri

Edomu = Nyekundu

Efeso = Anayetamaniwa. Anayetakwa

Efraimu = Tunda lenye sehemu mbili. Mwenye matunda

Eli = Mungu wangu

Elimeleki = Mungu ni mfalme

Elimu = Miti ya mitende. Mikaratusi

Elisabeti = Mungu wa kiapo. Mungu ni kiapo

Elisha = Mungu ni wokovu

Eliya = Yehova ni Mungu

Emau = Vizima moto

Epafra = Kwa mungu jike wa Afrodite

Erasto = Anayependwa

Esau = Mwenye nywele

Esta = Nyota. Mungu wa kike

Ezekieli = Mungu ni mwenye nguvu. Mungu anatia nguvu

Ezra = Msaada

 

F

Farao = Nyumba kubwa

Feliki = Mwenye furaha

Festo = Mwenye sherehe

Filadelfia = Upendo wa ndugu

Filemoni = Mwenye upendo. Mkarimu

Filipo = Rafiki wa farasi. Anayependa farasi

Filisti = Kutoka

Foinike = Nchi ya mitende

 

G

Gabrieli = Mtu wa Mungu

Gadi = Furaha. Bahati

Galilaya = Eneo. Sehemu

Gamalieli = Zawadi ya Mungu. Mungu anatoa thawabu

Gathi = Kinu ya kukamulia zabibu

Gaza = Nguvu. Ushujaa

Gehazi = Bonde la maono

Genesareti = Bustani za watawala

Gershoni = Aliyefukuzwa. Mgeni

Gethsemane = Chombo cha kukamulia mafuta

Gideoni = Anayepiga hadi kufa.

Gileadi = Nguvu. Ngumu

Gilgali = Duara

Golgotha = Fuvu

Gomora = Gharika

 

H

Habakuki = Kumbatia

Habili = Uvumi wa upepo. Mbuga

Hagai = Penye sherehe

Hajiri = Kimbia. Uhamaji. Safari

Hamu = Moto. Vuguvugu. Giza. Nyeusi

Hana = Aliyerehemiwa

Har-Magedoni = Mlima wa Har-Magedoni

Harani = Njia. Mtaa

Haruni = Aliyeangaza. Anayeangaa

Hawa = Uhai

Hebroni = Umoja

Henoko = Aliyeolewa. Kuweka wakfu

Hermoni = Patakatifu

Herode = Shujaa. Mungu nusu

Herodia = Shujaa

Hezekia = Mungu ni nguvu yangu

Hidekeli = Tigris = Mkali na anayekwenda kasi. Panapootesha mtende

Horebu = Pakavu. Pasipo na kitu

Hosana = Wokovu. Atoaye afya. Anayetoa maendeleo.

Hosea = Wokovu

Huri = Shimo. Mweupe. Amezaliwa kwa uhuru.

 

I

Ibrahimu = Baba wa wengi

Imanueli = Mungu pamoja nasi

Isakari = Yeye anatoa ajira. Ananipa mshahara

Isaya = Yahwe anaokoa. Yahwe ni wokovu

Ishmaeli = Mungu anasikia maombi

Iskariote = Mwanamume wa Kerioti. Mtumia kisu

Israeli = Mungu anapigana. Anapigana na Mungu

 

K

Kadeshi = Patakatifu. Palipowekwa wakfu

Kaini = Aliyepatikana. Mkuki.

Kaisaria = Wa kaisari

Kalebu = Mbwa

Kana = Bomba la tawi

Kapernaumu = Kijiji cha Nahumu

Karmeli = Bustani (ya Mungu)

Kayafa = Bonde dogo. Anayetafsiri ishara

Kefa = Mwamba

Kenkrea = Mji wa mtama

Kerithi = Iliyokatwa

Kishi = Upinde

Kishoni = Iliyojipinda. Iliyo na mapindo

Kolosai = Mji wa sanamu

Kornelio = Mwenye pembe

Krispo = Nywele zenye mawimbi

 

L

Labani = Mweupe

Laodikia = Utawala wa watu

Lawi = Umoja. Nia moja

Lazaro = Eleasar = Mungu ni msaada. Mungu amesaidia

Lea = Aliyechoka. Mwenye nguvu. Malkia wa nyumba

Lebanoni = Mweupe

Luka = Mwanga. Kuangaza

Lutu = Shera. Pazia

 

M

Magdalene = Anayetoka Magdala

Malaki = Malaika wangu. Mpeleka ujumbe

Mamra = Mafuta. Unene

Manase = Yeye (Mungu) amenifanya kusahau

Mariamu = Uchungu. Ubishi

Martha = Malkia

Mathayo = Zawadi ya Yehova

Melkizedeki = Mfalme wa busara

Methusela = Mtu wa mkuki

Midiani = Hukumu. Mapambano

Mika, Mikaya = Nani kama Yehova

Mikaeli = Nani anayelingana na Yehova

Miriamu = Uchungu. Ubishi

Mlima wa Mizeituni = Kinu cha kukamulia zabibu

Moabu = Kutoka kwa baba (baba wa mama)

Moleki = Mfalme

Mordekai = (Miungu) kwa Marduki. Kutoka Marduki

Moria = Mungu anajitokeza. Aliyeonwa na Mungu

Musa = Anayevutwa juu

 

N

Naamani = Uzuri. Anayependeza

Nadabu = Anayejitoa. Mzuri

Naftali = Mapambano. Vita vyangu

Nahumu = Anayeleta faraja

Naini = Mzuri. Kupendeza

Naomi = Uzuri wangu. Anayenipendeza. Mzuri

Nathanaeli = Mungu ametoa

Nathani = Yeye (Mungu) ametoa

Nazareti = Mwenye matawi mengi. Mtawala wakike

Nebukadneza = Nabu (mungu) anayelinda mipaka

Nehemia = Yehova anafariji

Nikodemo = Mshindi wa mtaifa

Nile = Mto. Gharika. Mkondo

Nuhu = Mapumziko

 

O

Obadia = Mtumishi wa Yehova

Onesimo = Mwenye faida. Anayesababisha baraka

 

P

Paulo = Mdogo

Penina = Ushanga

Penueli = Uso wa Mungu

Pergamo = Maisha ya ndoa

Petro = Jiwe. Mwamba

Pilato = Aliyejiandaa kwa mkuki

Potifa = Mkuu wa walinzi

Potifera = Zawadi ya Ra (mungu wa jua)

Prisila = Priska mdogo

Priska = Mzee. Anayestahili heshima

Publio = Wa-watu

 

R

Rabi = Bwana wangu

Raboni = Bwana wangu (mkuu kuzidi Rabi)

Rahabu = Paana

Raheli = Kondoo jike

Rebeka = Mtego. Anayejipendekeza

Reubeni = Yeye (Bwana) ameona unyonge wangu. Angalieni kijana

Rumi = Mji wa vilima saba

Ruthu = Urafiki

 

S

Safira = Mzuri. Anayependeza

Salemu = Mpole. Tengamaa

Samaria = Ulinzi. Eneo la ulinzi

Samsoni = Mwenye nguvu. Mwenye mwanga

Samweli = Aliyesikilizwa na Mungu.

Sanbalati = Sin (mungu) amemfanya awe na uhai

Sara = Anayetawala. Malkia

Sarai = Ukoo wa kifalme

Sarepta = Mahali pa usafisho

Sauli = Aliyeombwa

Sayuni = Ngome. Maangamizi. Mahame

Sefania = Yehova anaficha. Yehova ameficha

Sefari = Anaunguza. Juu. Aliyeinuliwa

Senakeribu = Sin (mungu) ameongeza hesabu za wandugu

Sethi = Aliyewekwa sehemu ya pili. Kulipizwa

Sharoni = Tambarare

Shekemu = Mabega. Mgongo

Shemu = Jina

Shushani = Ua

Sidoni = Aliyezungukwa na ngome. Kuvua samaki

Sikari = Mlevi

Sila = Amepatwa kwa maombi

Siloamu = Aliyetumwa

Silwano = Mungu wa msituni

Simeoni = Kusikiliza maombi

Simoni = Kusikiliza maombi

Sinai = Kichaka chenye miiba

Sintike = Mwenye furaha. Msaidizi

Sipora = Ndege (mdogo)

Sirti = Mchanga

Skewa = Kushoto

Smirna = Manemane. Mateso

Sodoma = Iliyounguzwa (chomwa). Sehemu yenye chokaa

Stefana = Aliyevikwa taji.

Stefano = Taji

Sulemani = Mpole

 

T

Tabitha = Swala

Tabori = Mlima

Tarshishi = Jiwe la thamani. Lulu

Tera = Swala wa mlimani

Tertio = Wa-tatu

Tertulo = Wa-tatu

Theofilo = Rafiki ya Mungu

Tikiko = Mwenye furaha

Timayo = Aliyeheshimiwa. Mwenye heshima

Timotheo = Anayeheshimu Mungu

Tiro = Mwamba

Tobia = Yehova ni mzuri

Tomaso = Pacha

Trofimo = Anayekuzwa

 

U

Urimu na Thumimu = Ukamiliki na nuru

Uru = Nuru. Miali (ya moto)

Uyahudi = Nchi ya Mwayahudi

 

W V

Waebrania = Wanatoka pande zingine. Wavuka mpaka. Wageni

Wafilisti = Wanaotoka

Vashti = (Mwanamke) mzuri

 

Y

Yafethi = Yeye anapanua

Yairo = Yeye anaangaza

Yakobo = Anayeshika kisigino. Msaliti

Yeftha = Yeye (Mungu) anafungua

Yeremia = Mungu ni mkuu. Mungu anainua.

Yeriko = Mji wa manukato. Mji wa mwezi mpya

Yeroboamu = Mataifa watakuwa wengi. Taifa litapigana.

Yerusalemu = Msingi wa amani. Nyumba ya amani.

Yesu = Yoshua = Mungu anaokoa. Mungu ni wokovu

Yezebeli = Ambaye hajaolewa. Kuinua

Yezreeli = Mungu anapanda

Yoabu = Yehowa ni baba

Yoashi = Bwana anatoa. Bwana anakuja (kusaidia)

Yoeli = Bwana ni Mungu

Yohana = Yehova ni wa huruma

Yona = Njiwa

Yonathani = Yehova ametoa

Yordani = Unawaanguka. Unawatelemka

Yoshua = Yesu = Yehova anaokoa. Yehova ni wokovu

Yuda = Yeye (Bwana) ashukuriwe. Anayeshukuriwa

Yusufu = (Bwana) anaongeza. Anafukuza

 

Z

Zabuloni = Makao. Pakuishi. Nyumbani

Zakaria = Yehova amekumbuka

Zebedayo = Zawadi ya Mungu. Mungu ni zawadi

Zekaria = Yehova amekumbuka

Zena = Zawadi ya Zeus (miungu)

 

UTAKASO - SOMO 1

Somo la “UTAKASO”au kwa kiingereza “SANCTIFICATION” na kiyunani,”HAGIASMOS” ni moja kati ya mafundisho ya msingi sana katika Kanisa la Mungu.Kukosa mafundisho haya katika Kanisa la Mungu,kunawafanya watu waliookoka,waonekane “SUB-STANDARD”,yaani wenye viwango vya chini; vinavyowafanya wasitambulike au kudhihirika vizuri kwa ulimwengu,kwamba kweli wameokoka.Mtu ambaye ameokoka,lakini hajatakaswa;ni vigumu kuwa nuru ya ulimwengu.Biblia inasema kwamba,nuru ya ulimwengu ni kama mji ulioko juu yam lima.Hauwezi kusitirika au kufichika.Kila mmoja atauona mji huo.Mtu aliyeokoka ambaye hajatakaswa,taa yake imewekwa chini ya pishi,na siyo juu ya kiango;na hivyo haiwezi kuwaangaza wote waliomo nyumbani.Mtu aliyeokoka ambaye hajatakaswa,hawezi kuangaza kwa matendo mema mbele ya watu mpaka watu hao waone tofauti kubwa iliyopo,kati ya mtu aliyeokoka na yule ambaye hajaokoka (Mathayo 5:14-16).Nuru inayoangaza,huvuta wadudu kutoka mbali.Maisha ya watu waliookoka,yanapaswa kuuangaza ulimwengu kiasi cha kuwafanya watu ambao hawajaokoka,wavutwe kwa Yesu hata kabla ya kuhubiriwa Neno la Mungu.(1Petro 3:1).Hali hii haiwezekani kuonekana bila UTAKASO.Watu waliookoka pia wanapaswa kuwa chumvi ya dunia (Mathayo 5:13).Mtu yeyote katika dunia anapenda chumvi.Mtu hata akipika mboga nzuri kiasi gani bila chumvi ataona bado kuna upungufu mkubwa.Watu ambao hawajaokoka,wanatakiwa wajione kuwa na upungufu mkubwa wanapojilinganisha na watu na watu waliookoka.Watatamani maisha ya wokovu.Waitamani chumvi.Hali hii haiwezekani kutokea ikiwa watu waliopo wameokoka lakini hawajatakaswa.Maisha yao hayawezi kuutamanisha ulimwengu kiasi hicho.Ni kwa sababu hii,shetani ameweka giza nene katika Kanisa la Mungu ulimwenguni kote,hususan Tanzania na kuhakikisha watu wengi waliookoka wanabaki gizani.Kwa kutokujua lolote kuhusu mafundisho ya utakaso.Matokeo yake wengi waliookoka wamekuwa siyo nuru ya ulimwengu.Watu wengine waliookoka wamefikiri,na wengine kufundisha kwamba, mtu anatakaswa na kuwezeshwa kuishi maisha ya utakatifu;pale anapojazwa au kubatizwa kwa Roho Mtakatifu.Hii sio kibiblia.Ubatizo wa Roho Mtakatifu,haufanyi mtu kuwa na uwezo wa kuishi maisha ya utakatifu.Ubatizo wa Roho Mtakatifu,unamfanya mtu aliyeokoka awe shahidi aliyevikwa “uwezo utakao juu”,unaomuwesha kujizalisha mwenyewe kwa wingi au kuwaleta watu wengi kwa Yesu anapowahubiria (Luka 24:47-49;Matendo 1:8). Mika 3:8 ”Bali mimi,hakika NIMEJAA NGUVU kwa roho ya BWANA;NIMEJAA hukumu na UWEZO; nimhubiri Yakobo kosa lake,na Israeli dhambi yake”Makusudi ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu,ni zaidi ya kumwezesha mtu kunena kwa lugha mpya.Lugha mpya ni ishara ya kwanza itakayoonekana kwake,lakini uthibisho halisi wa kujazwa au  kubatizwa kwa Roho Mtakatifu ni kuwa na uwezo wa kuwaleta watu wengi kwa Yesu.Wanafunzi wa Yesu kabla ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu,hawakuwa na matokeo ya kuridhirisha katika ushuhudiaji au kuhubiri;lakini baada ya kupata uwezo utokao juu,maelfu ya watu walikuja kwa Yesu kutokana na huduma yao.Ukimsikia mtu huyo anasema amejazwa Roho Mtakatifu miaka kumi iliyopita,lakini hajamleta mtu yeyote kwa Yesu au ameleta watu wawili au watatu kwa Yesu;huu siyo Ubatizo wa Roho Mtakatifu .Ni kuridhika na shaba badala ya dhahabu kama Rehoboamu(2Nyakati 12:9-10).Mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu,anaposhuhudia,anasema kwa Roho Mtakatifu.Roho anasema pamoja naye kwa hekima ya pekee,yenye uwezo wa kuwavuta watu wengi hadi watubu na kumkubali Yesu  Matendo 6:5,10

Kwa hiyo,sasa umefahamu kwamba Ubatizo wa Roho Mtakatifu siyo kwa ajili ya kumtakasa mtu au kumuwezesha kuishi katika utakatifu hali kwa ajili ya kumpa nguvu na uwezo wa kuhubiri na kupata matokeo makubwa.Watu wengine waliookoka wamefikiri,na wengine kufundisha kwamba mtu anapookolewa,wakati huohuo anatakaswa pia.Hii tena siyo sahihi.

 

1.        KUOKOKA NA KUTAKASWA NI MAMBO MAWILI TOFAUTI

Ni mafundisho yasiyo sahihi kudhani kwamba mtu anapookolewa,wakati huo huo anatakaswa pia.Kuzaliwa mara ya pili au kuokoka,na kutakaswa au kupokea utakaso;ni mambo mawili tofauti kabisa.Kuzaliwa mara ya pili au kuokoka,ni kwa watu wasiomjua Yesu kama Bwana na Mwokozi wao au Mataifa;lakini Utakaso,ni kwa watu waliokwisha kuokolewa tayari.Mtu anaweza akawa ameokoka,lakini bado akawa anaishi katika maisha yaliyo mbali na utakaso .Hasira,wivu,chuki,kusengenya,kugombana na kugombania ukubwa,kiburi,majivuno,kutokusamehe,kinyongo,kupenda dunia n.k; bado vinaweza kuonekana kwa mtu aliyeokoka ambaye hajatakaswa.Watu wa namna hii,wanakuwa siyo nuru ya ulimwengu.Mataifa wakiwaangalia watu wa namna hii,wanaweza kuona kwamba hawajaokoka.Hata mtu ambaye ameokoka lakini bado ana hali ya namna hii,anaweza kuijiwa na mashaka  na kuwaza,”Hivi mimi nimeokoka kweli au ninajidanganya:”Mashaka ya namna hii yakiruhusiwa kujijenga ndani ya mtu wa namna hii,anaweza kurudi nyuma kabisa na kuacha Wokovu.Ilivyo ni kwamba mtu wa namna hii,Yesu aliomba Utakaso kwa watu waliokuwa wameokoka tayari.Hakuomba Utakaso kwa watu ambao hawajaokoka(Yohana 17:14-19).Utakaso ni kwa ajili ya Kanisa yaani watu ambao wameokolewa tayari na siyo kwa ajili ya mataifa au watu ambao hawajaokolewa(Waefeso 5:25-27).

 

MIFANO YA KIBIBLIA YA WATU WALIOKUWA WAMEOKOLEWA LAKINI HAWAJATAKASWA.

1.        Wanafunzi wa Yesu:

Wanafunzi kumi na wawili wa Yesu,walikuwa wameokolewa tayari.Mambo yafuatayo yanathibitisha kwamba walikuwa wameokoka:-

·          Waliacha vyote na kumfuata Yesu,walikuwa wameokolewa tayari.Mathayo 4:18-22

·          Petro alimkiri Yesu kuwa ni Kristo na Mwana wa Mungu aliye hai,Mathayo 16:15-17.

·          Yesu alithibitisha kuwa wameacha vyote na kumfuata na akasema wataurithi uzima wa milele katika ulimwengu mpya – Mathayo 19:27-29.

·          Wao pamoja na wengine,jumla yao iliyofikia sabini,walikuwa wamefunuliwa Neno la Kristo na wakalikubali,majina yao yalikuwa yameandikwa mbinguni na walikuwa manakemea pepo kwa jina la Yesu na pepo wanatii.Luka 10:17-24.

·          Baada ya kulipokea Neno,Yesu anasema,ulimwengu kama Yesu asivyokuwa wa ulimwengu wa ulimwengu – Yohana 17:14

 

PAMOJA NA JINSI WALIVYOKUWA WAMEOKOKA,BADO WALIKUWA NA TABIA ZIFUATAZO:-

·          Petro hakuwa na mawazo yaliyo ya Mungu bali ya wanadamu,na aliweza kumsahihisha Yesu Kristo na kujaribu kumfundisha na kumwelekeza.Hakuwa tayari kuongozwa na Neno  la Kristo mia kwa mia Mathayo 16:21-23.

·          Katikati yao,kulikuwa na mgawanyiko,walikuwa wanagombana wao kwa wao na kushindana,wakigombania ukubwa;na walimjibu Yesu kwa namna isiyo ya unyenyekevu Luka 22:24-26;Mathayo 20:20-22,25-28;Marko 9:30-37.

·          Walikuwa na hasira ,wakikasirikiana wao kwa wao –Mathayo 20:24.

·          Walikuwa na wivu,na walijiona kuwa wao ni wao tu.Yeyote aliyeokoka ambaye hakufuatana nao,walimhesabu si kitu.Hakukuwa na upendo kati ya wanafunzi wote wa Yesu Marko 9:38-39; Luka 9:49-50

 

*******************************************************************************************

UTAKASO - SOMO 2

Leo tena tunaendelea na mfululizo wa masomo yetu ambayo yanahusu UTAKASO.Tunaendelea kuziangalia tabia za wanafunzi wa Yesu, na Kanisa la Wakorintho.Ambao tayari walikuwa wameokolewa lakini bado kutakaswa.Basi sasa tuendelee na kipengere cha tano kati ya vipengere saba katika kuziangalia tabia za wanafunzi wa Yesu ambao bado walikuwa hawajatakaswa japo walikuwa wameokolewa.Pamoja na tabia hizo za kuwa na Hasira,ugomvi,kuyawaza yasiyo ya Mungu,wivu na kujiona wao ni wao tu lakini bado walikuwa na tabia hizi zifuatazo:-

·          Walikuwa na roho ya chuki,hasira,kisasi na kutokuvumilia maudhi.Kutokana na roho hii,walitamani kuomba moto ushuke kutoka mbinguni uwaangamize Wasamaria ambao walikataa kumkaribisha Yesu Luka 9:51-56

·          Walikuwa na tama na kujipenda,wakitaka vizuri vyote view vyao,na walichukia kuona vizuri viko kwa wengine.”Umimi”ulikuuwa bado unawatawala Mathayo 26:6-13.

·          Ilikuwa mzigo kwao kumsamehe aliyewakosea Mathayo 18:21-35

1.        KANISA LA KORINTHO

Watu katika Kanisa la Mungu lililokuwa Korintho,walikuwa wameokoka.Roho wa Mungu alikuwa anakaa ndani yao,na kila mmoja alikuwa hekalu la Mungu 1Wakorintho 3:16-17.

PAMOJA NA JINSI WALIVYOKUWA WAMEOKOKA,BADO WALIKUWA NA TABIA ZIFUATAZO:-

·          Walikuwa na faraka yaani matengano na magawanyiko,yaliyoleta makundi kadhaa katika Kanisa hilo hilo mojaHawakuwa na nia moja wala shauri moja na tena walikuwa na fitina kati yao 1Wakorintho 1:10-11

·          Wengine walikuwa wanasema ni wa Paulo,wengine wa Apolo,wengine wa Kefa au Petro,wengine wa Kristo,na kulikuwa na chuki kati ya kundi moja na kundi jingine 1Wakorintho 1:12-13

·          Walijawa na husuda au wivu na fitina na hata kulikuwa na ugomvi kati ya wale waliojiita wa Paulo na  wale waliojiita wa Apolo 1Wakorintho 3:3-5

·          Walikuwa wanashtakiana mahakamani wao kwa wao mbele ya watu wasiookolewa.Hawakuwa tayari kudhulumiwa,na hivyo walitumia nguvu ili kuvipata vile walivyodhulumiwa;hata ikabidi kupelekana kwa watu wasioamini ama vyombo vya dola mfano Polisi tena asiyeamini kama tunavyojua leo 1Wakorintho 6:1-8.

·          Wanawake walikuwa wakorofi,wabishi na hawakuwa wakiwatii na kuwanyenyekea waume zao 1Wakorintho 14:34-35.

·          Walikuwa hawataki kuwasikia Viongozi wao na kuwatii angalia maandiko haya.Hadi wanamtaabisha mtumishi wa Mungu na kusema nao kwa maneno makali.1Wakorintho 4:18-21; 9:1-2

·          Wanawake walikuwa wanavaa mavazi ya kidunia,yasiyo ya unyenyekevu,wakishindana na kujionyesha kwa dhahabu na lulu,wakipamba nywele kama mataifa na wakikosa adabu 1Wakorintho 4:17;1Timotheo 2:9-12

YATOKANAYO

Mpaka hapa,tumeona ambavyo inavyowezekana kabisa mtu kuwa ameokoka,lakiniakawa bado anafanya mambo mengi,ambayo hayamtofautishi na mataifa.Siyo kwamba hajaokoka,la hasha,ameokoka;ila HAJATAKASWA.Mtu wa namna hii anaweza akawa hapendi kuwa na hasira,lakini akakuta anashindwa kuizuia hasira.Anatubu,lakini anajikuta anaendelea kuwa na hasira kali baada ya kuudhiwa kwa mambo madogo madogo tu.Kwa mfano,mtu wa namna hii anaweza kutoka ofisini akiwa amepanga jinsi ambavyo akifika nyumbani kwake atakavyofurahi pamoja na mkewe na watoto kwa miujiza mikubwa ambayo Yesu amemtendea mfano kupandishwa cheo,kuongezewa mshahara,ama alitoka nyumbani hana fedha na akawa amepata fedha kwa njia ya ajabu sana.Labda amepata safari ya kikazi n.k sasa akawa amenunua bidhaa mbalimbali kama mkate ,maziwa ,nyama,mayai,ama vizawadi zawadi kwa familia yake,lakini matokeo yake inakuwa tofauti.labda alipofika nyumbani,akamkosa mkewe ama amejifungia ndani amelala ama anafua na akachelewa kufungua mlango.Labda alikuwa anaoga n,k sasa tayari mambo yameharibika mwanamume amekasirika kwa kugonga mlango kwa muda bila kufunguliwa na akaanza kutoa maneno ya ugomvi.”unaniacha nagonga mlango kama vile nimepanga wakati hii ni nyumba yangu ,yaani wewe mwanamke umekuwa na kiburi kiasi hicho wala hujali …..”Na maneno mengi mfano wa hayo.Tayari plan yote ya furaha imebadilika.wakati mwingine anaweza hata kutupa vyote alivyovileta chini na hata kununiana siku nzima.Baadaye sasa baba huyu anaikumbuka plan yake ya furaha na familia yake.Moyoni anahuzunika sana na kuanza kumlaumu shetani na kusikitika moyoni na hata ataanza kutubu na hata kushangaa yale anayoyafanya ambayo hayapendi kufanya.Warumi 7:19 “Kwa maana lile jema nilipendalo,silitendi;bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo”katika hali ya namna hii,mtu aliyeokoka ambaye hajapata mafundisho ya Utakaso,au aliyepotoshwa kwa kufundishwa kwamba alipookolewa alitakaswa pia wakati ule ule;atakuwa anajishangaa na kuona hajui alifanyalo kama kweli ameokoka.Warumi 7:15 “Maana sijui nifanyalo;kwa sababu lile nilipendalo,silitendi;bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda”

 

************************************************************************************************************

 

UTAKASO - SOMO 3

Leo tena tunaendelea na mfululizo wa masomo yetu ambayo yanahusu UTAKASO.Basi sasa,ni makusudi ya somo hili kujifunza juu ya tatizo linalokuwepo kwa mtu aliyeokoka ambaye hajatakaswa na njia ya kuliondoa tatizo hilo.Ni maombi yangu kuwa utajifunza yote yanayofuata kwa nia ya kuifahamu kweli,na ukiwa na nia hiyo,kweli hii itakuweka huruYohana 8:32.Huenda somo hili ni “Elimu mpya”kwako,na hujawahi kuisikia habari zake.Hili lisikufanye utoke katika nia ya kuifahamu kweli hata kama ni mpya kwako,bali uwe na shauku zaidi ya kujifunza maana ya elimu hii mpya;kama walivyokuwa Waepikureo na Wastoiko nyakati za Mtume Paulo Matendo 17:17-20.”…tutapenda kujua,basi,maana ya mambo haya..” Elimu mpya ikiwa katika kweli ya Neno la Mungu,inaweza ikatushangaza kama wakati wa Yesu,kutokana tu na sisi kuwa gizani juu ya kweli yote;lakini tukifungua mioyo yetu na kuipokea,inaweza ikawa chanzo kikubwa cha baraka kwetu Marko 1:27-28.Hivyo basi,twende pamoja tukijifunza,na kwa kuwa wewe ni motto wa Mungu;mafuta ya Roho Mungu yaliyo ndani yako yatakufundisha juu ya kweli ya somo hili,na kukuthibitishia kuwa siyo mafundisho ya upotevu 1Yohana 2:26-27.

KIINI CHA TATIZO

Tuendelee sasa na somo letu.Kwa nini basi mtu ambaye ameokoka awe bado na tabia mbalimbali,kama zile za wanafunzi wa Yesu,na wanafunzi waliokuwa katika Kanisa la Korintho?Jibu ni kwamba”Dhambi ikaayo ndani ya mtu”,haiwi imeharibiwa kabisa mtu anapokuwa ameokoka,kabla ya kutakaswa.Dhambi hii ikaayo ndani ya mtu,ndiyo kiini cha tatizo.Warumi 7:16-17”Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda,naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu”

Mtu yeyote,anazaliwa akiwa na asili ya dhambi ikaayo ndani yake tangu tumboni mwa mamaye.Kutokana na dhambi ya Adamu,kila aliye uzao wa Adamu,anazaliwa akiwa na asili ya dhambi Zaburi 51:5;58:3;Ayubu 25:4;14:4;15:14;Maombolezo 5:7;Mathayo 3:7;Warumi 5:12.

ASILI HII YA DHAMBI ITOKANAYO NA DHAMBI YA ADAMU,INAPEWA MAJINA 11 KATIKA BIBLIA:-

1.        Dhambi ikaayo ndani ya mtu Warumi 7:17,20

2.        Utu wa kale au utu wa zamani Warumi 6:6;Waefeso 4:22-23;Wakolosai 3:9-10

3.        Mwili wa dhambi Warumi 6:6

4.        Mwili wa nyama Wakolosai 2:11

5.        Mwili wa Mauti Warumi 7:24

6.        Nia ya mwili Warumi 8:6

7.        Mwili Warumi 8:8-9,12-13;Wagalatia 5:17 Kuna majina mawili tofauti katika lugha ya Kiyunani yanayotafsiriwa Kiswahili “Mwili” (a) “SOMA” – Mwili wa mtu unaoonekana,jingo ambalo linatunza Roho.(b)”SARX”asili ya mwili wa Adamu ambayo ni ya kufanya dhambi,siyo ya utakatifu.Katika mistari hii,”Mwili” ni “SARX”:-

8.        Uchafu 2Wakorintho 7:1

9.        Uadui juu ya Mungu ulio ndani ya mtu Warumi 8:7

10.     Sheria ya dhambi na mauti Warumi 8:2

11.     Upinzani wa Roho ulioko ndani ya mtu Wagalatia 5:17

 Wakati wa kuokoka,asili hii ya dhambi inayoitwa utu wa kale au mwili wa dhambi,unasulubishwa tu lakini wakati wa kutaka unabatilishwa au kuharibiwa kabisa ili tusitumikie dhambi tena Warumi 6:6.Kumbuka kwamba mtu anaweza kusulubishwa lakini akawa bado kufa mpaka avunjwe miguu kwanza Yohana 19:31-32.Hapa,tunaona tofauti ya kusulubishwa na kuharibiwa.Pamoja na asili ya dhambi,mtu pia ana dhambi za kutenda,kwa mfano kuvuta sigara,kunywa pombe,wizi,ibada ya sanamu,uchawi,uasherati au uzinzi,kuua n.k.Dhambi hizi za kutenda ndizo ambazo zinazoharibiwa kabisa wakati wa kuokoka,na mtu akawa huru kutoka katika kuzitenda.Dhambi nyingine kama hasira,wivu,chuki,kujipenda binafsi kuliko unavyowapenda wengine,mawazo machafu n.k;zinatoka ndani sana ya mtu kwenye mzizi wa dhambi.Tungeweza kusema,wakati wa kuokolewa,shina,matawi na majani ya mti wa dhambi,yanakatwa kabisa na kuharibiwa,lakini mzizi wa mti huo unakuwa haujang’olewa.Mzizi wa dhambi,unasulubishwa tu wakati wa kuokolewa.Wakati wa kutakaswa,ndipo mzizi huu wa dhambi,unapoharibiwa kabisa.

Mtu aliyeokoka ambaye hajatakaswa,Roho yake inapenda kumpendeza Mungu katika mambo yote,Lakini mzizi huu wa dhambi unaoitwa Uadui juu ya Mungu ulioko ndani ya mtu,au upinzani wa Roho ulioko ndani ya mtu;unamzuia kuyafanya yale anayotaka kuyafanya.Ni kama jinsi ambavyo jiwe linaporushwa juu,linavyozuiwa kwenda juu zaidi,na hatimaye kurudishwa chini na nguvu ya uvutano.Mtu wa namna hii,hata kama ameokoka miaka 70 iliyopita,anaitwa mtu mwenye tabia ya mwilini,mwanadamu anayeenenda kwa jinsi ya kibinadamu,motto mchanga katika Kristo 1Wakorintho 3:1-4.Wakati wote anavutwa kutenda matendo yanayoonyesha tabia ya mwili wa dhambi na siyo matendo yanayoonyesha tabia ya rohoni.Hawezi kumpenda Mungu kwa moyo wake wote na Roho yake yote.

OPERESHENI YA KUHARIBU DHAMBI IKAAYO NDANI YA MTU

Safari yote ya kiroho ni safari ya imani.Mwanadamu anayeshindwa,kwa imani anamwendea Mungu akiamini kazi iliyofanywa na Yesu msalabani na Mungu mwenyewe anampa uwezo wa kushinda.Sasa basi,mtu aliyeshindwa na dhambi na kuishi nje ya mpango wa Mungu,SAFARI YA KWANZA,anamwendea Mungu na kumwomba msamaha wa dhambi;na Mungu mwenyewe anampa WOKOVU ulioletwa kwetu na Mwokozi Yesu alipomwaga damu yake msalabani kwa ajili yetu.Mtu huyu baada ya kuokoka anatakiwa amwendee Mungu SAFARI YA PILI na kumwomba amtakase au ampe UTAKASO.Mungu anapomtakasa,anamfanyia operesheni ya kuiharibu kabisa dhambi ikaayo ndani mwake.Operesheni hii tunayofanyiwa kwa IMANI,inapewa majina matatu katika Biblia:-

·          KUTAHIRIWA MOYO – Kumbukumbu 30:6;Warumi 2:29;Wakolosai 2:11

·          KUTAKASWA Yohana 17:17-19;1Wathesalonike 4:3;5:23

·          KUKAMILISHWA AU KUFANYWA TIMILIFU 1Yohana 4:17-18;2Wakorintho 13:9

Baada ya operesheni hii,ndipo mtu anapokuwa na MOYO SAFI au MOYO MWEUPE Mathayo 5:8;Zaburi 24:3-4 na KUWEZESHWA kuishi maisha ya Utakatifu kama Baba alivyo Mtakatifu na pia katika Ukamilifu kama Baba alivyo Mkamilifu Mathayo 5:48;1Petro 1:15-16.

UTAKATIFU MAANA YAKE NINI?

Neno “Utakatifu”linatajwa sana katika Kanisa la Mungu,lakini ni wachache wanaofahamu maana yake.Sasa,bila kufahamu maana yake tutawezaje kufahamu kwamba tunaishi katika Utakatifu?Hii ni hatari,maana Biblia inasema katika Waebrania 12:14,kwamba;Hakuna mtu atakayemwona BWANA asipokuwa na Utakatifu.Sasa basi,Utakatifu maana yake ni nini?

UTAKATIFU ni kuwa kama YESU KRISTO katika MOYO,NIA,TABIA,MAWAZO Na MATENDO.Utakatifu ni Hotuba ya Yesu alipokuwa mlimani  Mathayo sura ya 5,6 na 7.ikidhihirika na kushuhudiwa kwa mtu aliyeokoka.Utakatifu siyo suala la kufanya matendo ya nje tu yanayoonyesha tabia ya Kristo.Mungu anaangalia yale ambayo wanadamu hawawezi kuyajua.Je,unaposema au unapofanya jambo,una NIA ipi au UNAWAZA NINI?Ulivyo nje ndivyo ulivyo moyoni?

 

 

 

UTAKASO - SOMO 4

Tunaendelea kulichambua kwa kujifunza somo letu la UTAKASO .Basi hebu tutafakari mambo muhimu yafuatayo:-

 

1.        Mtu anaweza akawa anazungumza na mtu,kwa kinywa laini kuliko siagi;na maneno yake yakawa mororo kuliko mafuta,bali moyoni mwake kukawa na vita,na maneno hayo yakawa ni upanga.Wanadamu wakimwangalia mtu wa namna hii usoni,watamuona kuwa ni mtakatifu,lakini Mungu atamuona ni mnafiki,maana yeye anaangalia moyoni na mawazoni akiisoma nia ya mtu na kuvipima vyote hivi pamoja na matendo ya nje(Zaburi 55:21).

2.        Mtu kwa nje,anaweza kuonekana anaomboleza,huku amevaa nguo za kufiwa na kujionyesha kwamba yuko katika matanga au msiba;lakini akiwa na mawazo na nia nyingine ndani mwake.Watu watamwona hivyo,hata kumpa mahitaji yake;lakini Mungu atamwona kuwa ni mwongo kabisa.Angalia mfano huu

        (2 Samweli 14 :2-8)

3.        Mtu anaweza akafanya jambo jema kwa watu,na watu wakamuona kuwa ni mwema,kumbe Mungu anayemuangalia moyoni,anaona NIA ya mtu yule anapolitenda jambo lile kuwa ni mbaya.Huenda anatafuta sifa,kuonekana,anatafuta kupata maslahi Fulani n.kYesu hakuwa hivyo.Aliwaponya watu kadhaa na akawaambia wasimwambie mtu yeyote habari za uponyaji wao(Marko 7:31-36;1:40-44)

Unaona basi,Utakatifu siyo kufanya matendo Fulani tu.Utakatifu ni jinsi ulivyo.Ulivyo katika matendo,ndivyo ulivyo katika nia,mawazo,tabia na moyo wako.

Mtu anaweza akawa hajaongea na msichana au mvulana kwa kuogopa kuonekana kahaba au muhuni au hakuweka  nywele zake dawa,lakini akawa anatamani moyoni mwake kuweka dawa kwenye nywele au anaweza akawa hakuvaa heleni,bangili au mikufu,lakini moyoni,akawa hakuvaa kwa sababu hana fedha,au ili watu wasimuelewe vibaya,au kwa sababu wanakataza kuonekana ukiongea na mvulana au msichana au wanakatazwa vitu hivyo shuleni anakosoma au wanakataza kanisani mwake anapoabudu ama mume wake,mke wake,baba yake ,mwalimu wake  hapendi ama mila za kwao hazimruhusu lakini kwa ridhaa yake angependa kuvivaa vitu hivyo ama angependa aongee na hata kupanga kwenda kufanya uzinzi na uasherati kinyume na mapenzi ya Mungu.Mungu anapomwangalia mtu wa namna hii,anamwona kuwa ameweka nywele zake dawa, na kuvaa mapambo yote hayo,ama kufanya uzinzi na uasherati, ingawa kwa nje hayaonekani kwa macho.

KUTAMANI MOYONI JAMBO LOLOTE,KUNAHESABIWA NA MUNGU KWAMBA NI SAWA KABISA NA KULITENDA JAMBO HILO(MATHAYO 5:28).MBELE ZA MUNGU,KUHALIFU MOYONI AU KUKOSEA MOYONI NI CHUKIZO KWAKE NA SIYO UKAMILIFU.NI DHAMBI(MITHALI 11:20)

 

Jambo jingine ni kwamba,mtu hawezi kusema ana tatizo moyoni halafu kwa nje asionekane hana tatizo! Yaliyo moyoni,huzaa matunda nje pia(Marko 7:23).

 

Ni makosa pia kusema kwamba Mungu anaangalia ndani ya mtu na haangalii nje.Mungu anaangalia kotekote.Yesu Kristo anasema katika Mathayo 23:26,”…Safisha kwanza ndani ya kikombe,ili nje yake nayo ipate kuwa safi.”

 

Mungu anaangalia vyote-matendo,moyo,nia,tabia na mawazo.Unaweza ukatenda jambo Fulani zuri mara kadhaa,lakini siyo tabia yako.Hili pia ni chukizo.

Natumaini sasa kwamba umeelewa maana halisi ya Utakatifu,na tena umetambua kuwa watu wengi katika Kanisa la Mungu,hawaelewi maana halisi ya Utakatifu.

Tumeona kuwa Utakatifu ni zaidi ya kutenda tu jambo Fulani bali matendo hayana budi kuoana na mawazo,nia,moyo na tabia.Sasa kama ni hivi,mtu atafanyaje?kwa sehemu,mtu anaweza kufanya matendo Fulani ya haki aliyojifunza,lakini mtu atawezaje kujibadili tabia na kujisafisha moyoni na mawazoni,na kuhakikisha wakati wote kuwa nia yake ni safi?Jibu ni kwamba mwanadamu mwenyewe hawezi.Kinachotakiwa,ni mtu aliyeokoka ambaye hajatakaswa,kujiona kuwa ni ole wake kuwa na hali hii ya kimaskini(Warumi 7:24) Kisha amwendee Mungu awezaye kumbadilisha moyoni,mawazoni,katika nia na tabia kwa kumtakasa au kumpa utakaso au kwa kumtahiri moyo.Ni Mungu mwenye uwezo wa kutufanyia tohara hii ya moyo.Sisi hatuwezi!(1Wathesalonike 5:23-24;Waebrania 13:12)

MAOMBI ALIYOTUOMBEA YESU ILI TUTAKASWE.

Yesu Kristo katika Yohana 17:17-20 aliwaombea wanafunzi wake ili watakaswe.Sio wanafunzi wake pekee bali alituombea sisi sote tuliookolewa ili tutakaswe.Sasa jambo hili haliji tu lenyewe AUTOMATIC baada ya mtu kuokolewa,La hasha.Lazima mtu kwanza aliamini nay eye binafsi kuliomba mwenyewe.Kumbuka kwamba Yesu alimwombea kila mwanadamu asamehewe kwa kuwa hajui alitendalo(Luka 23:34).Lakini je,wote wameshasamehewa na kuokolewa?Jibu ni hapana.Ni lazima mtu afanye sehemu yake ya kumsikia mhubiri wa Injili,kuiamini Injili na kisha kuliitia Jina la Bwana akimuomba amsamehe na kumuokoa.Hapo ndipo atakapookolewa(Warumi 10:13-14).Biblia hiyo hiyo pia inasema kwamba Yesu aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukua magonjwa yetu na kwa kupigwa kwake,tuliponywa(Mathayo 8:14-17;1Petro 2:24).Lakini je,wote wamepona?Hakuna wagonjwa katikati yetu?Jibu ni kwamba,wagonjwa wako kwa maelfu yao hata katika Kanisa la Mungu.Ni kwa nini basi?Ni lazima mtu awe na imani katika kazi hiyo iliyomalizwa msalabani, Yesu aliposema “IMEKWISHA”,na inatupasa kukumbuka kuwa Imani,chanzo chake ni kusikia,na kusikia huja kwa Neno la Kristo(Warumi 10:17).Hebu angalia tena jambo lingine hapa.Kama tujuavyo kuwa mtu hawezi kupokea Nguvu ya Roho Mtakatifu,pamoja na ya kuwa ni ahadi ya Baba na tayari Roho Mtakatifu ameshakuja duniani lakini hata hivyo utaweza kuona kuwa mtu hapokei Roho Mtakatifu mara tu anapoamini AUTOMATIC Bali ni mpaka kwanza asikie na kufundishwa habari zake (Matendo 19:1-2)

Vivyo hivyo na UTAKASO.Ingawa Utakaso kwa watu waliookoka,ni kazi iliyomalizika msalabani(Waebrania 13:12);Ili mtu atakaswe,inampasa kusikia kwanza na kufundishwa juu ya UTAKASO,na kasha afanye sehemu yake ili atakaswe,baada ya kuamini mafundisho hayo.

Wanafunzi wa Yesu,walifanya sehemu yao na walitakaswa.Tunaona katika Matendo 1:13-15 wakidumu kwa moyo mmoja yaani kwa shauri moja na nia moja(1Wakorintho 1:10)Siyo kama zamani tena walipokuwa na chuki,kukasirikiana na kugombea ukubwa n.kPetro aliposimama kati ya hao ndugu 120,kila mmoja mwingine alikaa kimya(Matendo 1:15;Matendo 2:14)Isingewezekana kuwa hivyo kabla ya kutakaswa.

SEHEMU YAKO YA KUFANYA ILI UTAKASWE          

1.        Ufahamu kwamba hatupati utakaso kwa kuwekewa mikono na mtu au kuombewa na mtu au kuombewa na mtu.Ni juu    yako mwenyewe kumwomba Mungu akutakase kama jinsi ambavyo ilivyokuwa juu yako mwenyewe kutubu dhambi zako mwenyewe na kupokea wokovu.

2.        Ujione maskini wa roho,mhitaji na mwenye upungufu mkubwa.Uwe na njaa na kiu ya haki ukitamani kutoka moyoni kuishi maisha ya Utakatifu kama alivyo Yesu Kristo(Mathayo 5:3,6)Mungu atampa Utakaso yeye atakayejiona kuwa ni mkavu na mtupu(Isaya 44:3).Ukijiona kuwa ni tajiri umejitajirisha na kwamba huna haja ya Utakaso maana ulikwisha takaswa ulipookoka,Mungu atakuacha ujidanganye katika hali yako ya uvuguvugu na baadaye atakutapika(Ufunuo 3:16-17).Ujione waziwazi kwamba wewe siyo nuru ya ulimwengu,na kwa sababu hiyo,umewazuia watu wengi kuingia katika ufalme wa Mungu,kwa sababu maisha yako hayawatamanishi kama wanavyotamani CHUMVI.

3.        Uwe na nia hasa ya kuacha yote yaliyo kinyume na Utakatifu katika matendo,mawazo,moyo,nia na tabia kuanzia leo na umwambie Mungu kuwa;umekusudia kuishi maisha ya utakatifu yatakayokufanya kuwa nuru ya ulimwengu na chumvi ya dunia,mara tu anapokutakasa au kukutahiri moyo wako leo.

4.        Chukua muda mara moja umlilie Mungu na kumwomba Utakaso mpaka upokee.Unapoingia katika maombi hayo,amini kwamba hali yoyote uliyo nayo,Mungu anaweza kuibadilisha kama kweli huitaki.Fahamu kwamba:-

·          Ni KUSUDI la Mungu,wote waliookolewa watakaswe (Waebrania 13:12;Waefeso 5:25-27)

·          Ni MAPENZI ya Mungu,waliookolewa wote watakaswe (1Wathesalonike 4:3;Waebrania 10:10)

Ni AHADI ya Mungu,waliookolewa wote watakaswe (1Wathesalonike 5:23-24)

MASOMO YANAENDELEA

 Semina ya Roho Mtakatifu

 
 

SOMO LA 1:ROHO MTAKATIFU,MUNGU PAMOJA NASI

Leo,tunapoanza mfululizo wetu wa masomo katika Semina hii ya Roho Mtakatifu,ni muhimu katika Utangulizi kumfahamu

huyu Roho Mtakatifu ni nani,Baadaye,hatua kwa hatua,ndipo tutaangalia kwa kina,mapana na marefu,mambo mengine mengi

kuhusiana na Roho Mtakatifu.Tutajifunza somo letu la Utangulizi katika Semina hii

”ROHO MTAKATIFU,MUNGU PAMOJA NASI”,kwa kulitafakari katika vipengere vine vifuatavyo:-

 

 1. ROHO MTAKATIFU,NAFSI ILIYO HAI
 2. MUNGU ROHO MTAKATIFU
 3. ROHO MTAKATIFU,MUNGU PAMOJA NASI
 4. MAFUNDISHO TUNAYOPATA KUTOKANA NA MAJINA,SIFA NA VYEO VYA ROHO MTAKATIFU

1.       ROHO MTAKATIFU,NAFSI ILIYO HAI

Watu wengi wanapowaza juu ya Roho Mtakatifu,wanawaza juu ya “Nguvu ya Roho Mtakatifu”tu,na hivyo kwa

watu  wa jinsi hii,Roho Mtakatifu,ni namna ya nguvu Fulani au kani Fulani ya kuendeshea mambo.Hatuwezi kupata

baraka za kiroho walizozipata watu wa kanisa la kwanza kama tunamwona Roho Mtakatifu,kama aina ya nguvu Fulani

tu,kama nguvu ya uvutanoau nguvu ya umeme au sumaku,au nguvu ya upepo.Kumwona Roho Mtakatifu kama aina

ya nguvu Fulani tu,ni kumdharau Roho Mtakatifu,jambo linalosababishia kuhesabiwa kuwa si kitu,na kukosa baraka

zote(1Samweli 2:30).Roho Mtakatifu,siyo Kani,au Nguvu Fulani tu kama mafundisho potofu yanavyofundisha.Roho Mtakatifu,ni Nafsi ya Tatu ya Mungu.Maana ya nenoNafsi”,ni “yeyote aliye na uwezo wa uwaza,kuhisi,kutenda,kuzungumza,kushiriki katika mazungumzo na wengine,anayefahamu mwenyewe,mwenye

uwezo wa kuamua jambo,na mwenye majina na sifa,matendo na vyeo”.Maandiko yafuatayo,yanadhihirisha

waziwazi kwamba Roho Mtakatifu,ni nafsi iliyo hai:-

§         Matendo 13:2 “..Roho Mtakatifu Akasema,nitengeeni Barnaba na Sauli,kwa kazi ile niliyowaitia

        nguvu au Kani,hawezi kusema!akasema,ni neon linaloweza kutumika kwa Nafsi iliyo hai.Nafsi iliyo hai. Ndiyoinayoweza kusema na kuwa na kazi ya kuwaitia watu,na kutaka kutengewa watu.

§         Waefeso 4:30 “wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu…”yeye anaweza kuhuzunika

         kwa kuwa ni Nafsi.Kama ni namna tu ya Nguvu kama nguvu ya upepo,haiwezi kuhuzunishwa.

§         Wakorintho 3:16-17;6:19:-Katika mistari hii,tunaona maneno,”mnamtambua”,”anakaa kwenu” “huyo Msaidizi””huyo Roho Mtakatifu”,”Atawaongoza”,”Atakayoyasikia”,”Akiisha kuja”,Huyo atahakikisha”,Atayanena”,”Yeye atanitukuza”,”Atatwaa katika yaliyo yangu”.Maneno yote haya

        hayawezi kutumika kuitaja Nguvu Fulani.Nguvu haiwezi kusikia,kunena wala kuwaongoza watu!Vile vile,

        Msaidizi ni Roho Mtakatifu,siyo Mtume Fulani wa Uislamu kama wafundishavyo wengine(Yohana 14:26).

       Huyu Msaidizi,haonekani kwa macho,ni Roho wa kweli,tena wa milele,sifa ambazo haziwezi kuambatana

      na  mtu yeyote(Yohana 14:16-17)

 

 1. MUNGU ROHO MTAKATIFU

Roho Mtakatifu,anatajwa katika maandiko,kwamba ni Mungu (Matendo 5:3-4;1Wakorintho 3:16-17) tulinganishe na (1Wakorintho 6:19).Zifuatazo,ni sifa zinazothibitisha kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu.Hakuna anayeweza kuwa na sifa hizi,ila Mungu peke yake:-

 

a)       Yeye alikuwako tangu zamani zote,yuko hata sasa,na atakuwepo milele.Ni roho wa milele(Waebrania 9:14)

b)       Yuko mahali pote(Zaburi 139:7-10).

c)       Yeye ni Muumbaji –Alituumba sisi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana

(Ayubu 33:4;Zaburi 104:30)

d)       Anajua yote(2Wakorintho 2:10-11;Yohana 16:13)

e)       Yeye ndiye kidole cha Mungu,yaani Nguvu ya Utendaji ya Mungu

(Luka 11:20;Mathayo 12:28)

f)        Biblia,yaani Neno la Mungu,limeletwa kwetu na Roho Mtakatifu

(2Timotheo 3:15-17;2Petro 1:21)

g)       Yeye ,ni Mwangalizi wa kazi yote ya Mungu,Yeye ndiye anayewaita watu na kuwaweka katika ofisi mbalimbali za

         Utumishi wa Mungu na msimamizi wa kazi yote ya Mungu,na pia mtoa karama,Hakuna anayeweza kuwa

          mwangalizi  wa kazi yote ya Mungu,isipokuwa Mungu mwenyewe(Matendo 13:12;20:28;16:6-7)

h)       Roho Mtakatifu ana uwezo wa kufundisha yote.Mwenye uwezo wa kufundisha yote,ni Mungu pekee

        (Yohana 14:17,26)

 1. ROHO MTAKATIFU,MUNGU PAMOJA NASI

Yesu Kristo alipokuja duniani,alikuwa ni Mungu aliyekuja na kuwa nasi(Mathayo 1:23).Alipoondoka Yesu na kupaa mbinguni,baada ya siku kumi,alikuja kwetu Mungu Roho Mtakatifu(Yohana 16:5-7).Siku ile ya Pentekoste,

Roho Mtakatifu ndipo alipokuja,Upepo,moto,ni alama za uwepo wa Mungu mwenye uwezo wote

(Kutoka 14:21;Hesabu11:31;Waebrania 12 :29;Kutoka 18:17-18)Tangu siku hiyo Roho Mtakatifu,

ni Mungu aliyekuja kukaa pamoja nasi.Baada ya siku hiyo,tunapopokea ujazo wa Roho Mtakatifu siku hizi,

hakuna tena kuonekana kwa ndimi za moto au upepo,kwa sababu hizo zilikuwa ishara za kuonyesha kuja

 kwake Mungu Roho Mtakatifu duniani sawasawa na ahadi ya Yesu.Sasa tayari Roho,alikwisha kuja.

 1. MAFUNDISHO TUNAYOPATA KUTOKANA NA MAJINA,SIFA NA VYEO VYA ROHO MTAKATIFU

Kama jinsi kulivyokuwa na baraka za ajabu Yesu alipokuwa duniani,kuna baraka za ajabu zinazoambatana

na kuwepo kwa Mungu Roho Mtakatifu pamoja nasi.Katika masomo yanayofuata tutajifunza kwa undani

juu ya baraka hizo.Hata hivyo,kwa utangulizi,tunapata kufahamu yanayoambatana na kuwepo Roho Mtakatifu

 pamoja nasi kwa kuangalia majina ,sifa na vyeo vyake:-

a)       Roho wa kweli(Yohana 14:17,16:13)-Anakaa na kutenda kazi kipekee pale palipo na kweli,yaani pale Neno la

        Mungu linapohubiriwa na kuzingatiwa bila kulichuja(Wagalatia 1:13-16)

b)       Roho wa Utukufu (1Petro 4:14)-Utukufu wa Mungu hutukalia,Roho Mtakatifu aliwa pamoja nasi.

c)       Roho wa Uzima (Warumi 8:2) Roho Mtakatifu yuko nyuma ya kila muujiza wa uzima unaofanyika kwa Jina la Yesu.Pepo wanatolewa kwa Roho wa Mungu(Mathayo 12:28).Miujiza itajaa kwetu akiwepo Roho wa Mungu kati yetu.

d)       Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19;2Wakorintho 13:14;Luka 11:13;Yohana 14:26) Hukaa palipo na Utakatifu.Uchafu,humfanya kuondoka kwetu(1Samweli 16:14;Zaburi 51:4,10-11)

e)       Roho ya Ushauri na uweza(Isaya 11:1-2) Uweza wa Mungu hutufunika,na ushauri wake hutufanya kuenenda katika ,mapenzi ya Mungu.

f)        Roho ya Hekima na Ufahamu,Roho ya Maarifa na kumcha Bwana(Isaya 11:1-2)Roho Mtakatifu hutupa hekima

       .Hutupa ufahamu katika maandiko,na hivyo haiwi rahisi kupotezwa(1Yohana 2:26-27)Roho Mtakatifu hutupa

       kumcha au kuwa na hofu ya Bwana.Hutupa maarifa katika kutenda kazi za kiroho na hata za kimwili(Kutoka 31:1-5)

g)       Roho ya Neema na kuomba(Zekaria 12:10) Hutuwezesha kuomba kipekee(Warumi 8:26-27)

 

 

************************************************************************************

 

 

SOMO LA 2:ROHO MTAKATIFU,MTOA UTAKATIFU

Katika somo la kwanza katika mfululizo wa masomo haya yanayohusu Roho Mtakatifu,Tulijifunza kwamba Roho Mtakatifu,ni mtakatifu,hivyo anakuwepo na kudumu mahali palipo na utakatifu tu.Tukiwana maisha ya uchafu,yaani dhambi;humfanya Roho Mtakatifu akose makao kwetu,na hivyo hawezi kuwepo kwetu.Kama alikuwepo mwanzo kwetu,huondoka (1Samweli 16:14;

Zaburi 51:4,10-11).Sasa swali linakuja,tunawezaje kuwa watakatifu katika maisha yetu ili Roho Mtakatifu afanye makao

kwetu?Jibu ni kwamba,Roho Mtakatifu ,ndiye huyohuyo anayetoa utakatifu tunaouhitaji.Sasa tunamwangalia Roho

Mtakatifu kama Mtoa Utakatifu,kwa kutafakari kazi yake hiyo katika vipengere vitano:-

 1. ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUPAYE KUZALIWA MARA YA PILI
 2. ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
 3. ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU WALIOZIMIA KIROHO
 4. ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO

5.       ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO

 

 1. ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUPAYE KUZALIWA MARA YA PILI

Hatupaswi kamwe kudanganyika kwamba utakatifu siyo duniani ni mbinguni,Maandiko yanaeleza waziwazi

kwamba watakatifu walioko duniani ndiyo anaopendezwa nao Mungu(Zaburi 16:3).Hatupaswi pia

kudanganyika kwamba tunaweza kufanya dhambi hapa duniani,halafu tukasalimika baada ya kufa,kutokana

na misa ya wafu n.k(1Wakorintho 6:9-10;Waefeso 5:5-7;Wagalatia 6:7;Waebrania 9:27;IYohana 5:16;Kumbukumbu 10:17)  la maana hapa ni kufahamu ni jinsi gani tunavyoweza kuwa na ushindi dhidi ya

dhambi hapa duniani,na kuokoka kutupwa motoni,maana bila shaka tunatakiwa kuokoka tukiwa hapahapa

duniani (Luka 19:8-10);Tito 3:3-4)Tunawezaje kuwa na ushindi dhidi ya dhambi?Ni kwa kuzaliwa mara

ya pili,kwa Roho Mtakatifu(Yohana 3:3-10;Tito 3:3-5)Yesu Kristo,alijaribiwa sawasawa na sisi lakini

hakutenda dhambi(Waebrania 4:14-15)Ni nini siri ya ushindi wake huo?Ni kwa sababu alizaliwa kwa

Roho Mtakatifu,yaani alizaliwa tofauti na kawaida ya kimwili ya mume na mke.Sisi nasi tunapotubu dhambi

zetu kwa kumaanisha kuziacha,tunapata rehema hii kwa imani tu(Mithali 28:13)Tunazaliwa mara ya pili

 katika ulimwengu wa roho,na hivyo kuwa na uwezo wa kushinda dhambi kwa muujiza mkubwa.Katika

hali ya kawaida ya jinsi tulivyozaliwa kimwili,kamwe hatuwezi kushinda dhambi.Ni mpaka tufanyike viumbe

vipya kwa Roho Mtakatifu.Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kuzaliwa mara ya pili,naye atafanya.

 

 1. ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO

Kurudi nyuma na kuacha wokovu kunaitwa pia kufa kiroho(Ufunuo 3:1;Waefeso 2:1).Kwa kila aliyerudi nyuma

na kuacha wokovu,hii ni saa ya kuamka usingizini na kuanza upya(Warumi 13:11-12).Lakini,je,inawezekana

kuanza upya tena katika hali hii?Ndiyo,kwa msaada wa Roho Mtakatifu.Hii ni kazi yake nyingine.Roho Mtakatifu

ndiye aliyemfufua Yesu,alipokufa(Warumi 8:11).Kwa jinsi hiyo hiyo,Roho Mtakatifu anaweza kutufufua kiroho

na kutupa uhai tena wa kiroho(Waefeso 2:1,4-6).Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kufufuliwa kiroho,

naye atafanya.

 

 

 1. ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU

Kabla ya kufa kiroho,hutangulia kuzimia kiroho.Shetani hutupeleka hatua kwa hatua,kama upepo katika tairi

unavyotolewa kidogo kidogo kutokana na pancha ndogo.Tukizimia kiroho,upendo wa kwanza unatoweka.

Ingawa bado hatujafikia hali ya kufanya dhambi za uzinzi,uasherati,ulevi n.k kama mataifa,hata hivyo,mambo

ya rohoni yanakuwa hayana mvuto kwetu kama mwanzo.Kuomba,kushuhudia,kuhudhuria ibada n.k,yanakuwa

mzigo kwetu.Tunaanza kuvutwa zaidi na mambo ya dunia.Katika hali hii tunahitaji nguvu mpya,uzima mpya

(Isaya 40:28-31).Anayefanya kazi hii pia ni Roho Mtakatifu,Roho wa uzima(Warumi 8:2).Pepo wa udhaifu

wanatolewa kwa Roho wa Mungu(Mathayo12:28),na vivyo hivyo udhaifu wetu kiroho unatolewa na

Roho wa Mungu.Je umezimia kiroho,Mwambie Roho Mtakatifu akuzindue,naye atafanya.

 1. ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO

Baada ya kuokolewa,tunahitaji pia kutakaswa.Bila utakaso,tutajikuta bado hatuna ushindi dhidi ya dhambi

za ndani katika mawazo,na moyoni,ingawa tayari tuna ushindi dhidi ya dhambi za kutenda.Dhambi za ndani

,ni kama hasira,wivu,chuki,masengenyo,kugombania ukubwa,kiburi,majivuno,kutokusamehe,kinyongo,

kupenda udunia n.k.Hivi vinaweza vikaonekana kwa watu waliookoka ambao hawajatakaswa:Mawazo

yasiyo ya ki Mungu (Mathayo 16:21-23),kugombania ukubwa (Luka 22:24-26;Mathayo 20:20-22,25-28;

Marko 9:30-37),hasira (Mathayo 20:24)wivu,fitina,ugomvi (Marko 9:38-39;Luka 9:49-50;

1Wakorintho 3:3-5),faraka na matengano(1Wakorintho1:10-13),umimi(Mathayo 28:6-13),

kutokusamehe(Mathayo 18:21-35),chuki,kushindwa kuvumilia maudhi,kushtakiana wapendwa mahakamani

(Luka 9:51-56;1Wakorintho 6:1-8);Warumi 7:15 n.k .Mambo haya huondolewa kwa utakaso.

Ndiyo maana Yesu aliwaombea Utakaso wanafunzi wake waliokuwa tayari wameokoka(Yohana 17:14-19)

Roho Mtakatifu ndiye atupaye Utakaso(1Wakorintho 6:11;1Petro1:2)Je,hujatakaswa,mwambie

Roho Mtakatifu akutakase,yeye ni mwaminifu,atafanya(1Thesalonike 5:23-24)

5.       ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO

Katika Wagalatia 5:22-23,tunajifunza juu ya tunda la Roho.Katika lugha ya asili,yote katika mistari hii

yanamaanisha kwamba Tunda la Roho ni moja tu,Upendo.Hata hivyo,upendo huo unadhihirishwa kwetu

katika tabia na matendo kama furaha,amani,uvumilivu,utu wema,fadhili,imani,upole,na kiasi.Ni pale tu

tunapokuwa na maisha yaliyojaa upendo,ndipo tunapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.

Pasipo upendo,tunakuwa shaba iliayo na upatu uvumao,tunakuwa si kitu.Lolote jingine tunalolifanya linakuwa

halina faida(1Wakorintho 13:3).Hatuwi wanafunzi wa Yesu (Yohana 15:8)Sasa basi ,ni muhimu kufahamu

kwamba upendo ni tunda la Roho,tunalolipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.Tukilipokea tunda hili,na kukua

 kila siku katika upendo (1Wathesalonike 3:12),Kama matunda yanavyokua,ndipo tunapokuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli.Tukiwa na tunda la Roho la upendo,tunakuwa na Furaha ya wokovu ambayo haiwezi kuondoka kwetu

kwa sababu ya majaribu yoyote au kukosekana kwa lolote la kimwili(Yakobo1:2).Tutakuwa na amani ipitayo fahamu

 zote(Wafilipi 4:7)inayotuwezesha kuwa na amani na watu ambao tusingeweza kuwa na amani nao.Tutakuwa na

lengo la kutafuta amani na watu wote wakati wote(Waebrania 12:14)Tutakuwa na uvumilivu wa kipekee katika mateso,makwazo kutoka kwa watu n.k Tutakuwa na utu wema kwa watu wengine hata wale ambao hawajaokoka

(Marko 10:17).Tutakuwa na fadhili yaani hali ya kutaka wakati wote watu wanaotuzunguka wawe na furaha.

Tutakuwa watu tuliojaa imani,tusiotetereka kirahisi.Tutakuwana upole yaani unyenyekevu (Mathayo 11:29;

Wafilipi2:5-8)Na pili tutakuwa na kiasi (self-control)yaani uwezo wa kukataa kufanya lile ambalo Yesu hataki,

kwa gharama yoyote.Je,unataka kuwa na tunda la Roho katika maisha yako?Mwambie Roho Mtakatifu,naye atafanya.

 

********************************************************************************

 

 

SOMO LA 3:ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUSAIDIAYE KUOMBA

 

Kila Mkristo,au mtu aliyeokoka,hana budi kuwa na lengo la kufikia kimo na cheo cha utimilifu wa Kristo katika tabia na Utumishi wa

 Mungu(Waefeso 4:11-15)Kufikia kiwango cha Yesu Kristo katika tabia ni jambo linalowezekana,Kama siyo,tusingetakiwa

kuwa wakamilifu na watakatifu kama Baba wa mbinguni alivyo Mtakatifu(Mathayo 5:48;1`Petro 1:15-16)Neno la Mungu pia,

linatufundisha uwezekano wa kuwa na viwango vya utumishi vya yesu alipokuwa duniani,na hata kuzidi(Yohana 14:12).Hata

hivyo haya yote hayawezekani kama sisi siyo waombaji kama Yesu alikuwa mwombaji namba moja.Alifanya maombi alfajiri na mapema

(Marko 1:35).Alijitenga na shughuli mchana na  kufanya maombi (Luka 5:15-16)Aliomba jioni (Mathayo 14:23)Wakati mwingine

alifanya maombi usiku kucha(Luka 6:12)Je,sisi tunaweza kuwa waombaji kiasi hiki?Kwa nguvu na jitihada zetu hatuwezi.

Tunaweza tu,tukisaidiwa na Roho Mtakatifu.Ndiyo maana tunajifunza somo hili muhimu leo katika mfululizo wa masomo haya

ya Roho Mtakatifu ,na kichwa cha somo la sasa ni ” ROHO MTAKATIFU,ATUSAIDIAYE KUOMBA”,

NA TUTAJIFUNZA SOMO HILI KATIKA VIPENGERE VINNE:-

 1. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
 2. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
 3. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU
 4. ROHO MTAKATIFU,MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
 1. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO

Shetani ndiye adui yetu mkuu.Kazi yake ni kuiba chochote kizuri cha kiroho tulicho nacho,na tena kuchinja au kuua na kuharibu yote 

mema kwetu kiroho na kimwili.Tukiwa peke yetu,kamwe hatuwezi kupambana na shetani na kumshinda.Hatuna budi kuwa na

Mungu katika maisha yetu ili tumshinde ibilisi.Daudi alimshinda Goliathi kwa Jina la Bwana.Hakumshinda kwa nguvu zake.Kwa maana nyingine hatuwezi kuzaa matunda yoyote mema ya kiroho kama hatuko ndani ya Yesu.Usalama wetu na ushindi wetu wa kiroho,unategemeana

sana na sisis kukaa ndani yake Yesu,yaani sisi kuwa na uhusiano au ushirika na Kristo.Pasipo yeye,sisi hatuwezi kufanya neno lolote

.(Yohana 15:4-5).Kukaa ndani ya Yesu,kunafananishwa na tawi lililounganishwa na shina.Kuunganishwa huko ndiyo uhai wa tawi.

Tawi likijitenga na shina,linanyauka na kufa.Sasa basi,tunaunganisha na Mungu  na Mungu tunapokuwa tunawasiliana naye katika maombi.Tukiwa hatuna maisha ya maombi,kimsingi ni kwamba tunakuwa ni tawi lililojenga na shina,na hivyo tunanyauka na hatimaye

kufa kiroho.Hatuwezi kuwa na kitu tusipoomba(Yakobo 4:2)

Tutaingia majaribuni tusipoomba (Mathayo 26:41).Tutapepetwa kama ngano na ibilisi na mazuri yote ya kiroho yataondoshwa,na

imani yetu itatoweka(Luka 22:31-32).Shetani atatumeza na kuturudisha katika ufalme wake(1Petro 5:8).Hatuwezi kuwaleta watu

kwa Yesu,tusipokuwa  waombaji,maana Shetani hatawaachia(Zaburi 2:8).Hatuwezi kuona watu wakifunguliwa katika vifungo vya

shetani vya kimwili(Luka 13:16) na vile vinavyotokana na mambo ya rohoni (Matendo 12:5-17).Kwa ufupi tutachukuliwa na

mafuriko ya Shetani(Zaburi 32:6).

 1. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA

Maandiko yanatufahamisha kwamba makao ya Mungu mbinguni,ni Mahali palipoinuka,na Mlimani kwenye kiti cha enzi

cha Mungu (Isaya 57:15;Kutoka 24:12-13;Ufunuo 7:9-10).Ingawa Mungu wetu yuko mlimani,maandiko yanasema

tukimwomba,yeye husikia huko mbinguni na kutujibu maombi yetu kwa kuyatenda tunayoyataka (1Wafalme 8:32;Zaburi 76:8;102:19).Hata hivyo,hatuna budi kufahamu pia kwamba katika mazingira Fulani Mungu hushuka kutoka mlimani na kuja

 duniani katika hali isiyo ya kawaida.Mungu anaposhuka kwa jinsi hii,hutenda mambo ya kutisha,na ya kushangaza,yasiyo ya

kawaida na hivyo kuwavuta wengi mno kwake(Waamuzi 4:12-16,5:13;Isaya 31:4;Hesabu 11:23-25,31-32).Uamsho hutokea

Mungu anaposhuka,na watu wagumu wa mioyo huvutwa kwa Yesu,walio vuguvugu huwa moto,mambo mengine makubwa ya

kuitikisa jamii kama mamia ya wenye ukimwi kupona kwa mpigo,hutokea,Mungu akishuka.

Hata hivyo kushuka kwa Mungu hutokea baada ya maombi ya kuugua na kulia kwa uchungu mkubwa(Kutoka 2:23-24;3:7-8;

Matendo 7:32-34).Wakati wote Yesu Kristo alimfanya Mungu kushuka katika huduma yake kwa kuwa aliomba kwa kulia sana

na machozi(Waebrania 5:7),na wengine walimuombolezea kwa kilio na uchungu mkubwa(Luka 23:27)Kulia kwa kuugua katika

maombi hushusha majibu ya maombi namna ya kipekee(2Nyakati 34:27;Zaburi 34:17;39:12;51:1-2,17;72:12;12;88:1-2;Isaya 58:9;Yeremia 31:9;Luka 18:7).Sasa basi ni rahisi kuomba maombi kwa kulia na kuugua?jibu ni la,bila msaada wa Roho Mtakatifu,itakuwa kama tunaigiza tu.

 

 1. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU

Tunajifunza mambo mengi zaidi kuhusiana na maombi kwa kuyaangalia maisha ya maombi ya Yesu,na

mafundisho yake kuhusu maombi:-

§          Yesu Kristo alikuwa na wakati wa kuomba pamoja na wanafunzi wake(Luka 9:18),Lakini pia alikuwa na muda mrefu wa

        maombi ya peke yake (Luka 5:16;Marko 6:45-46).Ni muhimu kujiunga na kikosi cha maombi cha Kanisa na kushiriki

        maombi 


ya pamoja na wengine,lakini ni lazima kila mmoja kuwa na muda wa kuomba mwenyewe.

§          Yesu hakukubali kuchukuliwa na huduma za kushauri watu,kuwaombea watu n.k na kuziruhusu zimkoseshe kuomba.

        Alijua bila maombi,huduma hizo zitakuwa hazina nguvu.Aliziacha huduma,akafanya maombi(Luka 5:15-16).Kabla ya

        kuzungumza na  watu,alizungumza na Mungu KWANZA.Alifanya maombi ya alfajiri na mapema sana na baadaye

        alipokutana na watu ilikuwa rahisi mno kwake kuponya ukoma na kutoa pepo.(Marko 1:35-42).

§          Kabla ya Yesu kutembea juu ya maji,na kukomesha upepo,alikuwa na kipindi kirefu cha maombi(Marko 6:46-51).Vipindi virefu vya maombi vinaweza kutupa uwezo wa kuona yasiyowezekana yakiwezekana!

§          Utukufu wa Yesu ulitokana na maombi!(Luka 9:28-29)Hatuna utukufu wa Mungu kwa kuwa siyo waombaji!Mwombaji,

utukufu wake humwogopesha shetani

§          Alipokuwa na huzuni aliomba hakunung’unika tu na kulalamika,na ghafla alipata ujasiri wa kukabili lolote lile

(Mathayo 26:36-39;47-49).Hatuna ujasiri na tumejaa woga kwa kuwa hatuombi

§          Maombi yake yalikuwa ni vita hasa.Alipokuwa akiomba,alitoka jasho(hari)kama matone ya damu(Luka 22:44)

.Maombi ni mapambano dhidi ya shetani anayezuia majibu yetu(Danieli 10:12-13).Ni lazima iwe ni vita.Mwili ni lazima

tuushughulishe kama wapiganaji hasa,tukiwa  katika roho Maombi yenye matokeo makubwa,ni yale ya kutoka jasho!Ni

lazima tumkabili shetani katika vita ya maombi kabla hata hajatushambulia.Katika vita ya siku sita kati ya waisraeli na wamisri,

miaka kadha iliyopita;Waisraeli walishinda Wamisri ingawa walikuwa na ndege nyingi zaidi za kivita kuliko wao,kwa kuwa

walizipiga KABLA hazijaondoka katika vituo vyao.Tusingoje matatizo ndio tuombe!

§          Imani yetu na ya ndugu zetu,inaweza kutokutindika,ikiwa tu tutakuwa waombaji;kinyume cha hapo ni rahisi kumezwa na

        shetani(Luka 22:31-32;1Petro 5:8-9)

§          Maombi ndiyo yanafanya tuutunze utakatifu wetu,na kuwa mbali na dunia.Bila maombi ni rahisi kuvutwa na masumbufu

        ya dunia(Luka 21:34-36)

§          Yesu aliliombea Kanisa(Yohana 17:14-15).Ni muhimu kuliombea kanisa na siyo kujiombea wenyewe tu wakati wote.

Je tunaweza kuyatendea kazi yote haya kwa nguvu zetu?jibu ni la.Kwa nguvu zetu hatuwezi,bila msaada wa Roho Mtakatifu.

 1. ROHO MTAKATIFU MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA

Shetani anafahamu sana umuhimu wa maombi,na hivyo atatuzuia sana kufanya maombi kuliko yote mengine,

ili tubaki kama matawi ambayo hayajaunganishwa na shina.Anajua pasipo Mungu,sisi hatuwezi neon lolote.

Kwa kujifunza tu juu ya maombi,bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi.Tunaweza kuomba sisi hatuwezi

neon lolote.Kwa kujifunza tu juu ya maombi,bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi.Tunaweza kuomba

siku mbili,tatu,halafu basi.Pamoja na wanafunzi wa Yesu kuhimizwa kuomba na Yesu mwenyewe,bado

walishindwa kuwa waombaji(Matahyo 26:37-43).Ndipo hatimaye akawaambia atakuja Msaidizi ambaye

kazi yake mojawapo,ni kutusaidia kuomba(Yohana 16:7;Warumi 8:26-28).Yeye Roho,kwa kuwa

hutuombea kwa kuugua,na tena ni Roho ya neema na kuomba,huweza kutupa msaada wa kutuwezesha

kuomba kwa kuugua na kulia(Zekaria 12:10)Baada ya Roho Mtakatifu kuja na kuwasaidia wanafunzi wa

Yesu,maisha yao ya maombi yalibadilika(Matendo 10:9).Siri ni hii,usitumie nguvu zako kuomba.Kabla ya

 kuingia katika maombi,mwombe Msaidizi akusaidie kuomba.

 

 

 

****************************************************************************************

 

 

 

SOMO 4:   UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

Ili tuweze kuwa mashahidi wa Mungu,tunahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya kuokoka na kutakaswa.Ili tumtendee Mungu

kazi kikamilifu,ni lazima tupokee nguvu ya Roho Mtakatifu (Matendo 1:8;Luka 24:49).Kwa sababu hili,somo hili,ni la muhimu sana

 kwa mtu yeyote anayetaka kuwa mtendakazi mzuri wa Mungu.Tutaligawa somo hili katika vipengere vinne:-

10.     MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

11.     UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU

12.     ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPAUFAHAMU KUHUSU UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

13.     JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU

14.     ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA

15.     UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU

6.        MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

Baada ya mtu kuokolewa,inambidi kubatizwa kwa maji kwa jina la baba,Mwana na Roho Mtakatifu(Mathayo 28:19).Hata hivyo,huo siyo ubatizo wa mwisho.Baada ya mtu kutakaswa,anahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu(Mathayo 3:11)Ubatizo wa maji,unamfanya mtu azamishwe ndani ya  maji na kuzungukwa na maji pande zote.Vivyo hivyo,Ubatizo wa Roho Mtakatifu unamfanya mtu aliyeokoka,kuzamishwa ndani ya Roho Mtakatifu na kuzungukwa na Roho Mtakatifu pande zake zote.Roho Mtakatifu,anakuwa msaidizi wake(Yohana 15:26).Ubatizo wa maji,tunabatizwa na wanadamu waliopewa Agizo la Mungu lakini Ubatizo wa Roho Mtakatifu,tunabatizwa na Yesu mwenyewe(Mathayo 3:11).

6.        UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU

Neno “mashahidi”katika (Matendo 1:8),linatokana na neno la lugha ya Kiyunani “Martus” ambalo linatafsiriwa katika Kiingereza,” Martyr” ambalo maana yake ni “Mtu anayekuwa tayari kuteswa sana au hata kuuawa kwa sababu ya imani yake,pamoja na hayo,

 

hawezi kuiacha imani yake”.Bila ubatizo wa Roho Mtakatifu,hatuwezi kuwa mashahidi kama walivyokuwa Stefano na Antipa

(Matendo 22:20;Ufunuo 2:13).Kabla ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu,Petro alisema asingemkana Yesu hata ikibidi kuuawa,

lakini kinyume chake alimkana mara tatu,na yeye pamoja na wanafunzi wenzake walipoyaona mateso yanakuja,walimwacha na

kumkimbia Yesu (Mathayo 26:31-35,56) Lakini baada ya ubatizo walikuwa na ujasiri mkubwa. Matendo 4:13

7.        ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPA UFAHAMU KUHUSU UBATIZO WA ROHO

        MTAKATIFU

§          Maji (Yohana 7:37-39)Hakuna maisha bila ya maji.Mwanadamu ni asilimia 60%maji.Kuharisha na kutapika sana

humfanya mtu kupoteza maji mengi na huweza kusababisha mtu  kupoteza uhai.Vilevile sisi tunaosema tumeokoka,

hatuwezi kabisakuwa na maisha ya kiroho yaliyo hai yenye nguvu,bila Ubatizo wa Roho Mtakatifu.Ni lazima tunyweshwe

 Roho(1Wakorintho 12:13)Jambo jingine,maji ni muhimu katika usafi wa miili yetu hutuondolea kunuka n.k Roho Mtakatifu hutumulikia dhambi au uchafu wowote.

§          Moto (Mathayo 3:11).Kuwepo kwa moto ni alama ya uwepo wa Mungu (Kutoka 3:1-5;Matendo 2:2-3).Moto vilevile,unangarisha madini kama dhahabu na fedha(Malaki 3:2-3).Ubatizo wa Roho Mtakatifu hufanya uwepo wa

        Mungu uwe dhahiri kwa mtu na pia humng’arisha mtu na kuwa mtumishi wa Mungu anayeng’aa .Siyo hayo tu,moto

        huleta mwanga.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutupa mwanga mkubwa wa maandiko yaani Biblia na kutupa mwanga wa

        uzuri wa mbinguni na ubaya wa Jehenam.Ukiwa na mwanga huo hakutakuwa na gharama kubwa yoyote ya kukufanya

        ushindwe kufanya mapenzi ya Mungu.Moto pia huleta nguvu ya kuendesha,magari,treni,Ndege n.k vifaa vyote hivyo

        huendeshwa kutokana na moto unaotokea baada ya cheche za umeme kuunguza mafuta.Kazi ya Mungu inaendeshwa

        kwa nguvu ya moto,ubatizo wa Roho Mtakatifu na kwa moto.Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu,moto unawake

        ndani yake na hawezi kuacha kushuhudia au kuhubiri na kufundisha(Yeremia 20:9;Isaya 62:1;Matendo4:20).Mtu

        aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu,maneno yake huwa moto unaoteketeza kila ugumu wa mioyo ya watu kwa kuwa

       Roho Mtakatifu hushuhudia pamoja naye na hivyo matokeo yake ya utumishi wake huwa makubwa.Ni nguvu kwa ajili

       ya Utumishi (Yeremia 5:14;Yohana 15:26-27;16:6-8;Mika 3:8).

§          Upepo (Yohana 3:8)Upepo wakati wote unatembea,na uko mahali pote.Roho Mtakatifu hakufanya kazi wakati wa mitume tu,hata sasa anatembea na yuko kwetu tayari,ni wajibu wetu kumpokea tu.Upepo huvuma upendako.Ni vigumu kuubadilisha

        mkondo wa upepo tunavyotaka sisi,jahazi hufuata mkondo wa upepo.Ni muhimu kutakaswa kwanza kabla ya Ubatizo huu.Utakaso humfanya mtu kuwa mtii mno katika yote na Roho Mtakatifu ni mshirika wa wale wamtiio(Matendo 5:32)Upepo pia hutuletea hewa safi inayotuburudisha wakati wa joto,moshi n.k Mazingira yoyote magumu tukiyakabili katika utumishi wa Mungu,Roho Mtakatifu huwa hewa safi kwetu inayorekebisha mazingira.

§          Mafuta (Luka 4:16-21)Roho Mtakatifu hututia mafuta  au kutuweka katika utumishi wa Mungu (1Samweli 16:13;Kutoka 30:30;1Wafalme 19:16;Yohana 2:27)Rais kabla hajaapishwahuitwa Rais mteule na hana mamlaka sana wakati huo kisheria.Kuapishwa kwa leo ndiyo kutiwa mafuta kwa zamani.Bila ubatizo huu,mamlaka yetu huwa hafifu.Mafuta

        yanalainisha na kuzuia msuguano.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutupa hekima ya kuvuta roho za watu(Mithali 11:30)

        mafuta  huufanya mwili uwe laini.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hulainisha ukavu wa maombi yetu (Warumi 8:26)

§          Mvua (Zaburi 72:6;Hosea 6:3)Nchi haiwezi kutoa matunda bila mvua.Mtu aliyeokoka hawezi kuwa na matunda mengi bila mvua yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu(Yohana 15:16)

§          Mvinyo(Waefeso 5:18;Matendo 2:12-13) mvinyo kwa walevi unasahaulisha shida.Ubatizo wa Roho Mtakatifu,

        humwezesha mtu kudharau majaribu na kuondoa wasiwasi na kubabaishwa na mambo madogomadogo tu.Mvinyo kwa walevi,pia

       unawapa ujasiri wa kufanya lolote lile,aibu,woga vinatoweka.Ubatizo wa Roho Mtakatifu humfanya mtu kuwa jasiri

       kama simba na mtu aliye kuwa mwoga kama Petro,kuwa jasiri(Mithali 28:1;Mathayo 26:31-35,56;Matendo 4:13).

§          Hua (njiwa)- (Yohana 1:32) Ubatizo wa Roho Mtakatifu haufanyiki kwa mtu wa ulimwengu huu yaani ambaye

        hajaokoka.Njiwa hakutua kwenye ulimwengu,alirudi safinani kwa waliookoka(Mwanzo 8:8-9)Roho Mtakatifu ni 

        mweupe,kama hua.Ni Mtakatifu,huja kwa watakatifu waliotakaswa.

§          Muhuri (Waefeso 1:13)Muhuri ni alama ya mamlaka.Bila muhuri barua hupungua mamlaka yake.Ubatizo wa Roho

        Mtakatifu humfanya mtu kuwa na mamlaka ya Yesu kwake na shetani husema “ Yesu namjua na Paulo namfahamu

        (Matendo 19:15)Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni mamlaka au uwezo kutoka juu wa kuzifanya kazi za Yesu.

§          Arabuni (2Wakorintho 1:21-22)Neno arabuni maana yake- Uhakikisho au uthibitisho wa Uimara.Ubatizo wa Roho Mtakatifu,hutufanya kuwa na uthibitisho wa uimara wa Neno la Mungu,hutuongezea imani ya kufanya maajabu.Shetani

        hawezi kumpeperusha huku na kule mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu.

 

8.        JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU

q       Kuokoka au kuzaliwa mara ya pili.Mafuta haya hayatiwi kwa mtu mgeni ambaye jina lake haliko katika kitabu cha Uzima mbinguni (Kutoka 30:31-33)

q       Kutakaswa(Yohana 17:17;1Wathesalonike 5:23)Wanafunzi 120 orofani,walitakaswa kabla ya Ubatizo wa

        Roho Mtakatifu.

q       Kuwa na Imani kama Roho Mtakatifu yuko kwetu tayari na kwamba ni ahadi ya Mungu kwetu(Matendo 2:38-39);Luka 11:10-13)

q       Kuwa  na kiu ya kumtumikia Mungu(Isaya 44:3)

q       Kuomba kwa kufumbua sana kinywa na kutokuruhusu kutumia akili,wala kuwaza kwambatutasema lugha ya 

          mapepo.(Luka 11:10-13;Zaburi 81:10).

9.        ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA

Mtu akibatizwa kwa Roho Mtakatifu,kutakuwa na mambo ya kusikia kwake na ya kuyaona kwake(Mathayo 3:16-17).

Ishara ya kwanza ni kusikia kutoka kwake kabla ya kuona mengine.Atasema au ananena kwa lugha mpya asiyoifahamu

ambayo siyo ya dunia hii(Matendo 2:4;10:44-46;19:6).Ni muhimu mno kwa mtu aliyeokoka kuomba kwa kunena kwa

lugha hii(1Wakorintho 14:2,4-5,15).Hata hivyo hatupaswi kunena kwa lugha mbele ya mataifa wasioelewa kitu.Watadhani

 sisi ni wendawazimu(1Wakorintho14:18-25)Kunena kwa lugha mbele ya mataifa wasiojua kitu nikuwapa mbwa kilicho

kitakatifu na kutupa lulu zetu mbele ya nguruwe matokeo yake watatudhihaki kwa kuwa hawajui maana (Mathayo 7:6).

 

10.     UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU

Moto bila kuchochewa huzimika(Mithali 26:20).Hatuna budi kuwa waombaji na kuomba kwa Roho,yaani kunena kwa lugha katika maombi  mara kwa mara katika maombi yetu binafsi(1Wakorintho 14:14-15;Yuda 1:20)Vile vile hatuna budi kudumu katika usafi kwa Neno(Zaburi 51:4,11;119:11;Yohana 15:3).Hatuna budi pia kujihusisha katika kushuhudia na kuwaleta watu kwa Yesu (Mika 3:8).

Nyimbo:

             Kutakaswa:

 1. I will say “YES” Lord x2, “YES” Lord x2 ,I will say YES Lord

Nitasema “NDIO” X2 , “NDIO” Bwana x2,Nitasema “NDIO”

 

Ubatizo wa Roho Mtakatifu:

      2.   Moto moto moto moto umewaka x 2, siku ile ya Pentekoste moto umewaka x2.

            Moto moto moto moto umewaka x 2, siku ya leo ACL  moto umewaka x2

            Moto moto moto moto umewaka x 2, siku ya leo Rohoni mwangu  moto umewaka x2 

 

Tafuta utakatifu kwani pasipo huo Utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu. Masomo ya Jumapili

 
 

SOMO 1:       UFUNGUO WA KUJIBIWA MAOMBI

Leo tunajifunza somo muhimu sana,ambalo ni dira ya maisha yetu ya

Utakatifu.Kama watu tuliookolewa na ambao tumeamua kuishi maisha ya utakatifu.Yohana 15:7.Mungu wetu anatuagiza kuomba lolote tutakalo naye atatutendea.Kwa msingi huu leo katika ibada yetu tutajifunza somo letu

UFUNGUO WA KUJIBIWA MAOMBI kwa kuligawa katika vipengere viwili vifuatavyo:-

1. KUKAA NDANI YA KRISTO

2.MANENO YA KRISTO KUKAA NDANI YENU

    KUKAA NDANI YA KRISTO

Kukaa ndani ya Kristo maana yake ni nini?1Yohana 3:6.Kutokutenda dhambi.

Kulishika

Neno la Mungu 1Yohana 2:5-6. Kuenenda kama Yesu alivyoenenda hapa duniani.

Kudumu katika mafundisho ya Kristo 2Yohana 1:9;Yohana 15:10 Kujitoa kwa ajili

ya wengine ili nao wakae katika Imani.Kufanya yote haya ndipo tunapoweza kusema

 tunakaa ndani ya Kristo.

MANENO YA KRISTO KUKAA NDANI YENU

Maneno ya Kristo yanakaa ndani yetu kwa njia tano zifuatazo:-

q       Kulisikia Neno la Mungu

q       Kulisoma Neno la Mungu

q       Kulifahamu au kulielewa Neno la Mungu

q       Kulitafakari Neno la Mungu

q       Kulifanya au Kulitenda Neno la Mungu

 Kulisikia Neno la Mungu

Kulisikia Neno la Mungu kunatupa faida nyingi zinazotuwezesha kuyapokea yale tunayoyahitaji

toka kwa YESU KRISTO Warumi 10:17.Imani huja kwetu pale tunaposikia Neno la Kristo.

Kwani tunapata Heri Luka 11:28. Ni Baraka tele .Tunaweza kujiuliza kuwa je inanipasa mimi mtu

 niliyeokoka kusikiliza Neno la Kristo kwa muda gani? Marko 8:2;Matendo 20:7-11.Kadiri tunavyokuwa na muda mrefu sana wa kulisikia Neno ndipo Imani yetu Inapoongezeka.Kusikia Neno la Mungu ni kuijaza Imani katika roho zetu.Tunaweza kusikia Neno kwa njia nyingi na hapa tutaziangalia baadhi ya njia hizo:-

ü       Tunapowahi Ibada na kuhakikisha hakuna kitu kinachotupita katika ibada mojawapo ya wiki kama ni maombi,kusifu,kuabudu,kutoa zaka na sadaka,kufunga,kushuhudia,kualika wengine hapo tunakuwa tumelisikia Neno la Mungu na kulitendea kazi ipasavyo.Tunapohudhuria ibada zote kama ni Alhamisi kwenye kuchambua Biblia,Maombi,Mkesha wa maombi Ijumaa,Jumamosi Jumuiya za makanisa ya Nyumbani,Jumapili –Tunapowahi tokea saa tatu asubuhi n.k tujue pia kuwa tutasikia Neno mfano kwenye madarasa ya biblia Jumapili ama Neno kutoka madhebahuni yote hayo na mengine mengi Mfano kwenye semina n.k tujue tutapata hazina kubwa sana ya Neno la Mungu kwa kusikia watumishi mbalimbali wakitufundisha.

ü       Kusikiliza kaseti mbalimbali za mahubiri ya watumishi wa Mungu wakati tuwapo majumbani kwetu,Tunaweza kuziazima ama kuzinunua kwenye maduka mbalimbali yanayouza kanda za mafundisho mbalimbali.

            Kulisoma Neno la Mungu

 Ziko faida na baraka tele tunapolisoma Neno la Mungu.Tunahimizwa kulisoma Neno wakati wote kwa kujitahidi sana  1Timotheo  4:13;Ufunuo 1:3;Isaya 34:16;Yeremia 51:61;Matendo 8:28;Waefeso 3:4 Haitoshi tu kulisikia Neno.Lazima tutenge muda wetu na kuweza kulisoma kwa kuzisoma Biblia zetu.Tukifanya hivyo tujue kuwa tutaongeza kiwango chetu cha kujibiwa maombi yetu.Mtu awaye yote ambaye bado hajui kusoma na kuandika lazima achukue hatua ya kusoma na hapa tuna madarasa ya kuwafundisha watu kusoma na kuandika.Ni muhimu kuchukua hatua ya Imani.Vinginevyo lazima tujue kuwa tunazikosa baraka nyingi sana.Tuwe kama TOWASHI.

 Kulifahamu au kulielewa Neno la Mungu  

Kulisoma Neno lazima kuambatane na kulifahamu au kulielewa Neno la Mungu.Mathayo 24:15.Tunawezaje kulifahamu au kulielewa Neno la Mungu.Matendo 8:30-31;Nehemia 8:7-8.Lazima tuketi chini ya waalimu waliobobea katika maandiko na sio kuketi chini ya waalimu vipofu.Towashi aliketi chini na kufundishwa na kuelewa na Mwalimu wake Philipo.Je wewe uko tayari?

 Kulitafakari Neno la Mungu

Tulitafakari Neno la Mungu ni kuyaangalia yale ambayo tuliyoyasikia,kuyasoma na kuyaelewa na kuona yanahusianaje na maisha yetu?Lazima tujiulize Je kuna onyo,Je kuna dhambi yoyote ya kutubu na kuacha,Je kuna Neno la faraja au la kunitia moyo?Je kuna mahali Neno limetuonyesha utupu wetu?ama kutusahihisha,au kuna mafunuo mapya.Ni ufahamu upi na kwa pamoja unayajumuisha yote kwa pamoja na kuyaleta mbele za Mungu katika shukrani na maombi.Huku ndiko kulitafakari Neno na kuna faida nyingi sana katika kufanya hivyo.Yoshua 1:8;Mithali 16:20 na Zaburi 27:4-5.(Njia ya mbinguni,tukitaka mema.

 Kulifanya au Kulitenda Neno la Mungu

Kulisikia,kulisoma,kulielewa,kulitafakari lazima viambatane na kulifanya au kulitenda Neno la Mungu.Hiki ndicho kilele cha baraka zetu katika kujibiwa maombi.2 Mambo ya Nyakati 11:1-4.Mtu anayelisikia Neno la Mungu na kulitenda.Mathayo 7:24 -27;Yakobo 1:22-25 Ezekiel 33:30-32. Je kuna awaye yote ambaye baada ya ujumbe huu atakuwa kama hawa Ezekiel 33:30-32

 Tusimame.

 JE UMEUBEBA UFUNGUO WAKO?BASI SUBIRI MAJIBU YA MAOMBI YAKO YANAKUJA.FANYA YAKUPASAYO KUFANYA NA BWANA ATAKUBARIKI.

 SOMO 2:       WAJIBU WA WATOTO WA MUNGU

Unapokuwa umeokolewa na kuamua kumfuata Yesu ,Tunaelekezwa kukaa mahali ambapo hatimaye tutaukulia wokovu.Mahali hapa tulipoingia leo kama ni mara yetu ya kwanza ama umekuja tena na tena basi amua leo kupangangania mahali hapa bila kuwaza tena kuondoka ili upate kuukulia wokovu na hatimaye umwone Yesu katika jina la Yesu.Sasa baada ya uamuzi huo inakupasa kuambatana na wale ambao lengo lao ni kumwona Yesu.Au kuingia mbinguni.Rafiki yako atakuwa yule ambaye mtapatana,katika kila eneo Amosi 3:3 Yesu kristo anatuambia kuwa tutakuwa rafiki zake pale ambapo tutatenda anayotuambia Yohana 15:14.Kwa msingi huo yako mengi sana ambayo tunaelekezwa kutenda mara baada ya kuokolewa.Tumekuja mahali hapa huenda ikawa umezoea mahali penye watu wengi na hapa unaona tuko wachache,hupaswi kabisa kuogopa elewa kuwa uko mahali pa salama katika jina la Yesu.Kumbukumbu 7:7,tutayaangalia leo maandiko ili kuyaangalia machache kati ya yale aliyotuangiza Yesu.Tito 3:1.Kwa msingi huo tutalichambua somo letu Wajibu wa watoto wa Mungu kwa kuviangalia vipengere vitatu vifuatavyo:

 1. Wajibu wa watoto wa Mungu
 2. Baraka za watoto wa Mungu waaminifu
 3. Yatupasayo kufanya.

 

1.                                           WAJIBU WA WATOTO WA MUNGU

Sisi kama watoto wa Mungu tunapaswa kuelewa wajibu wetu mara baada ya kuokoka.2 Wakorintho 6:18; Yohana  1:12.

q       Kuepuka matengano 1 Wakorintho 1:10 Tunapaswa kupendana kama watoto wa baba mmoja.

q       Lazima tuwe na nia moja.Wafilipi 2:16;Waebrania 10:25;Warumi 12:10 Lazima kumwona ndugu yako kwamba  ni  wa thamani ama bora kuliko wewe.Na kuhakikisha kuwa mara zote tunakusanyika pamoja kama kundi moja huku tukimtazamia mwokozi.Tunapaswa kuwatanguliza wenzako katika kila jambo(yaani kumpenda ndugu kuliko nafsi yako)yeye naye atafanya kama wewe pale utakapoanza.Kuwatanguliza wengine katika maombi.

q       Tunapaswa kufahamiana vema.Katika shida zetu raha zetu ,kufahamiana katika shughuli zenu ili  tuombeane.tufahamiane tabia zetu,kazi zetu mienendo yetu ili tuwe nuruni.

q       Pia tunapaswa kuonyana kwa upendo ili pale ambapo yapo yanayotuzingira kwa mfano dhambi mbalimbali ambazo bado tunaendelea nazo ama kwa kujua ama kwa kutokujua basi tuweze  kuombeana ili  tuwekwe huru.Waebrania 3:13-18;4:1-2.Petro alifurahia sana wala hakukwazika pale ambapo alikemewa na Paulo pamoja na kuwa Petro alikuwa Mtume ambaye alimwona Yesu na kukaa naye lakini Paulo hakuwahi kukaa na Yesu.

q       Tunapaswa kuwapenda adui zetu  na kuwaombea.Mathayo 5: 44-47 tujue kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawapalia makaa na hatimaye wakawa marafiki zetu.

q       Tunapaswa kuwa watii. kwa Mungu wetu  na kwa viongozi wetu ama wale wanaotuongoza  katika lolote lile.Mfano wanakwaya,wakinamama,wanamaombi n.k lazima tuwatii wale waliowekwa kutuongoza ili wafanye kazi zao kwa furaha kwani wanakesha kwa ajili yetu.1Petro 1:14-16 .Yesu alikuwa mtii hata mauti. Huyu ndiye kielelezo chetu pamoja ya kuwa alikuwa Mungu.

q       Tutafute kwa bidii kuwa watakatifu kama lengo letu ni kumwona Mungu.Waebrania 12:14 Hatupaswi katika kanisa letu kuwa na vikundi na mijadala ambayo ni kinyume cha mtu mtakatifu ambaye wakati wote atatafuta kwa bidii kumwona Mungu.Katika tabia,mwenendo,usemi n.k Lazima tuwe kama wanafunzi wa Yesu ambao walijulikana hata kwa usemi.Ndio maana Petro alipomkana Yesu aliambiwa hata usemi wako wakutambulisha1Timotheo 4:12-16 tukielezwa kuwa tunapaswa kufanya jambo Fulani hatutaanza kupinga na kujadili bali tutafanya kwa utii bila kusitasita.Mfano kushuhudia,kualika,kutoa report,kusoma Biblia zetu ,kuomba,kuvaa kiblia, n.k(Kumbukumbu 22:5,1Wakorintho 11:1-13).Lazima tuenende kama Kristo alivyoenenda. 1Yohana 2:6;Malaki 3:8-12  Tunapoelekezwa kutoa zaka na sadaka lazima tujue ni kwa ajili ya baraka zetu na hatuna budi kutoa na kuwa mbali na laana.Tunapoelekezwa umuhimu wa kuwahi malangoni au katika nyumba ya Bwana ili kuomba ama kumgojea Bwana n.k.Sisi kama malimbuko matakatifu tunapowahi au kufanya lolote tujue hata wale watakaokuja watatuiga sisi kama wazaliwa wa kwanza.Tukichelewa ibada na wao watachelewa.Lazima kuzishika amri na kushindana na ulimwengu.Kwenda katika sherehe ambazo ni kinyume na Biblia ni kutokutii.Mfano Ubatizo wa watoto wadogo,Ubarikio,kuangalia TV kwenye program ambazo hazimbariki Bwana ama kucheza michezo mbalimbali ambayo tungeweza kuwa na muda mzuri wa kuomba,kualika,kushuhudia n.kmfano bao,karata,ligi,n.k.Lazima tujue kuwa muda wetu una thamani sana na kama wanafunzi wa Yesu tumekombolelewa kwa thamani kubwa sana.Kunywa pombe,masengenyo  uongo,wivu,hasira,ugomvi,wizi,uzinzi,ulawiti,ushoga,uasherati, husuda .nk.Mithali 23:29-35;Zaburi 140:3;141:3-4;`

q       Hatupaswi kujichanganya  na Mataifa na kuiuiga mwenendo wao bali wao wauige mwenendo wetu.Zaburi 106:35 kama kuvuta sigara,pombe,kuwa na kiburi,tama mbaya Isaya 55:2;Mithali 6:17-19  tunapaswa kuwa mbali na ulimwengu. Na kutend a haki.1Yohana 5:3-4;1 Yohana 2:29

q       Tunapaswa kuwa thabiti katika Imani hadi mwisho.Waebrania 3:14 lazima tuwe vielelezo katika kuvaa ,kusema ,kutenda,kuishi .Ili wale wanaokuja waiige imani yetu bila kwazo lolote.Tunapopatwa na matatizo yoyote yaleTunapaswa kumng’ang’ania Yesu na sio mwanadamu.Tunaweza kuteswa hata kufukuzwa kazi lakini kwa gharama yoyote tusikubali kuiacha imani. Waebrania 6:11 tuzidishe bidii katika kutembeleana,kuangaliana sisi kwa sisi,tuombeane na kuwa na mzigo wa kuwakumbuka wengine katika maombi.mfano viongozi wetu,tujitoe kwa mali zetu na kuwa watoaji.tufanye chagizo ama chakula n.k

q       Tuwe waaminifu katika kila eneo.uaminifu katika fedha,mali xza wengine,uaminifu katika Kristo kama watakatifu waliotutangulia.Tuuge mfano wa akina Epafra,Titiko,Timotheo n.k Wakolosai 1:2;1-7;Waebrania 12:14;Wagalatia 5:22-25;Waefeso 6:21;Wakorintho 4:17.

q       Tunapaswa kuilinda Imani yetu.Kama Antipa Ufunuo 2:13

q       Tuwe tayari kuonywa na kuishindania Imani  2Yohana 1:8;Waebrania 3:14

q       Tuwe waaminifu katika mali za watu 2Nyakati 34:9-12;Nehemia 13:12-13;2Wafalme 12:14-15; Lawi 19:13 ;Mithali 19:29 Kama tumeweka nadhiri ama ahadi katika lolote tufanye bidii kuiondoa.

q       Tusiogope kuwa tuko wachache  bali tunapaswa kumtukuza Mungu kwani analo kusudi lake kwetu hatimaye sisi nasi tutaongezeka na kuwa jeshi kubwa..Tujenge imani hiyo na tutashinda.tunganganie hapa tujifunze na tule na kushiba NENO Yoshua 1:8-9;1 Petro 5:2-5

 

 

2.BARAKA ZINAZOAMBATANA NA WATOTO WA MUNGU  WAAMINIFU

               

Ø       Tutawekwa juu ya vitu vyake vyote.Yaani tutatawala pamoja na Yesu. Luka 12:41-44

Ø       Tutapokea thawabu sawasawa na matendo yetu.Tunapowatunza watumishi wa Mungu ama kuwahudumia wengine tujue tutapokea thawabu ya haki.Tujue tunamhudumia Yesu.Mathayo 10:41;Mathayo 25:36-40 Mkumbuke mwanamke wa Sarempta.1Wafalme 17:7-16;2Wafalme 4:8-17.

Ø       Yesu ametuandalia makao kule juu mbinguni na anatuita Rafiki zake.. Yohana 14:1-3

Ø       Tunapokuwa watoto wa Mungu ,Mungu anataabika nasi na hapendi kutuona tuna huzuni yoyote yeye hushughulika nasi.Yeremia 31:20;Isaya 30:17;Zaburi 103:3;34:19

 

3.YATUPASAYO KUFANYA

 

Tunapaswa kuhakikisha iwapo majina yetu yameandikwa mbinguni katika kitabu kile cha uzima.Kama bado tunapaswa kutubu kwa kumaanisha na kuhakikisha kuwa tumeokolewa leo kabla ya kuondoka hapa kwani wakati uliokubalika ni sasa.na tufanyike watoto wa Mungu.Mithali 28:13;Warumi 10:9,13;Ufunuo 3:20;Yohana 1:12;

ü       Tuchochee tulichopewa kwa bidii Warumi 12:11

ü       Tunapaswa kuhudhuria kila kusanyiko bila kukosa

ü       Kudumu katika maombi

ü       Kuishindania Imani bila kugeuka nyuma kama mkewe Lutu.

 

Tusimame wote na kumshukuru Mungu kwa yale yote tuliojifunza na kama yako ya kurekebisha ndio wakati mzuri wa kuyatendea kazi mafundisho bila kumwangalia mwingine

 

 

SOMO:3

 

PASIPO NA MWILI WANGU NITAMWONA MUNGU

 

Baada ya kuokolewa ,tujue tuko kwenye mashindano.Sio njia rahisi kuingia mbinguni kama wengine wanavyodhani bali lazima tufahamu kuwa tutakutana na vikwazo vingi.Tunapaswa kutia bidii ili tuingie mbinguni.Waebrania 4:11.Hakuna namna nyingine lazima tumshinde shetani na mbinu zake.Sasa lazima tuzifahamu mbinu za Ibilisi mapema.

Mbinu kadhaa anazozitumia shetani ni kutuletea Magonjwa,kutokufanikiwa,maudhi n.k

Ndio maana Bwana Yesu alisema Ombeni msiingie majaribuni.Kumbuka Petro alimkana Yesu mara tatu,Yuda vile vile alimsaliti Yesu kwa tamaa ya pesa.Lazima tuwe macho,na kutia bidii na kumshinda shetani.

Kwa msingi huo leo kwa makusudi kabisa tutaiangalia mbinu hii kubwa ya shetani katika kuwaaangusha watu wa Mungu.

Shetani anajua sana kuwa watu wengi wana mateso mbalimbali na watu wengi wanapokuwa wako katika mateso inakuwa rahisi sana kumkufuru Mungu na hata kuyakana matakatifu yake.Ayubu alikuwa Mtakatifu,mcha Mungu na hakuwepo mtu kama yeye Duniani pia alikuwa Tajiri mwenye unyenyekevu wa hali ya juu sana.Ayubu 1:8-12.Wengi wetu tunapokuwa katika hali ya kufanikiwa  ni rahisi sana kusema HALELUYA.Lakini shetani akianza kutuletea magonjwa ,mateso,maudhi,vitisho,kutengwa,kuudhiwa,vita,maombolezo n.k ni rahisi sana kukufuru na kumwona Mungu kama hayupo.Hata wengine tunaanza kuhisi labda tumefanya dhambi ndiyo yametupata haya na haya.Kweli tunaweza kufanya dhambi na kupata magonjwa ,mateso n.k lakini sio kila wakati ni dhambi.AYUBU 1:6-22.Hapa ayubu ambaye anatajwa kuwa Mtakatifu hapa tunaona jinsi ambavyo mali zake zote pamoja na watoto zilivyoteketea..AYUBU 2:2-7.Lakini bado shetani hakumwacha yeye utaona pamoja na vyote hivyo lakini bado yeye mwenyewe aliugua sana hadi kukaribia kufa. Hata hivyo bado Ayubu hakumwazia Mungu kwa upumbavu. Pamoja na mateso hayo lakini bado shetani haoni kwamba ilitosha na Mungu anamwelezea mtumishi wake jinsi ambavyo alivyokwenda mbele zake pasipo kumwazia Mungu wake mabaya ,lakini shetani bado analeta mashtaka mengine juu ya Ayubu na kumwambia Mungu kuwa huenda ikawa Ayubu hamchi Mungu bure.AYUBU 2:3 Lakini  utaweza kuona kuwa Ayubu aliishinda tena mitego ya ibilisi na kusimama imara.Hapa Ayubu hakuwa mtenda dhambi bali hapa alikuwa anashindana na adui.

Sisi nasi tunapokuwa tumeokolewa tunapaswa kuishi maishi ya utakatifu hatupaswi kufanya dhambi tena.Na pamoja na kukaa katika maisha ya usafi na utakatifu lakini lazima tufahamu kuwa bado kutakuwa na matatizo mbalimbali ambayo tutapaswa bado kukabiliana nayo.lazima tufahamu kuwa mjaribu anatujaribu.kama alimjaribu Yesu,Ayubu,sembuse sisi?Luka 1:5-7 angalia mstari ule wa sita.(and they were both righteous before God,walking in all the commandments and ordinances of the Lord blameless)Sio wakati wote tunapopata majaribu  ama mahangaiko yanatokana na dhambi.bali tunapaswa kuelewa kuwa shetani yuko kazini kama mjaribu.Ni juu yetu kushindana naye hadi atukimbie.Kumbuka kuwa maumivu mbalimbali ama mateso ya kila namna yanaweza kutufanya tukamkufuru Mungu.Lazima tuwe makini .haya yalitokea kwa Ayubu lakini yeye hakudhubutu kamwe kumkufuru Mungu.Japo yanaweza yakatupata kama yaliyompata Ayubu,Wanaweza kutokea watu kama mkewe Ayubu kutuvunja moyo ili tuikane Imani,ama wakatuona tumechanganyikiwa,tunanuka,tumekonda,tumefilisika,hata marafiki zetu wakaweza kutukimbia hiyo sio ajabu.walifanya pia kwa Ayubu. AYUBU 3:24-26;4:15;6:1-3,6-7;7:4-5,13-16;17:7;19:13-20.Ayubu alishughulikiwa ipasavyo.Leo tungesema ni UKIMWI.Alikuwa na uchungu sana ,maumivu makali sana,mapepo,majipu kila mahali,hofu,mashaka,ndoto mbaya,umauti.kunuka na kuoza,kuharisha,kutapika,majonzi,kudhihakiwa ,kudharauliwa n.k.

Ndio maana Ayubu akasema AYUBU 19:26-29 Na baada ya ngozi …PASIPO NA MWILI WANGU NITAMWONA MUNGU..Hata kama shetani atatuhangaisha kiasi gani lakini lazima tujue kuwa siku moja nitamwona Bwana.Mwili huu unapita ndugu yangu ni kama mana inayoharibika ama kunyauka utabaki katika udongo lakini ROHO ZETU ndizo zitakwenda kumwona Mungu zitamrudia aliyeziumba.Tukae katika imani ili hatimaye tukutane na Mungu

Iko miili ya mbinguni na miili ya duniani.Tunaweza  kuishi mbinguni kwa Mungu kwa kuishi kwa Imani na maisha ya Utakatifu.Sisis ni wasafiri tunaelekea mbinguni na hapa ni wapitaji tu.Tuishi kama wasafiri na wapitaji katika dunia hii.1Wakorintho 15:40-44 miili hii ya mbinguni ni miili mizuri sana haina makovu wala hakuna haja ya kujichumbua ama kwenda saloon hii imejitosheleza.Tutavikwa miili mipya na kupewa jina jipya .Miujiza yote hatimaye itapita,utajiri,umaskini kila kitu kitapita.Hatupaswi kubabaiswa na shetani kwani hata tukifa kufa kwetu ni faida kama tukifa katika Bwana.WAFILIPI 1:21.Pasipo miili hii tutamwona Bwana.Tumwangalie Ayubu alivyomgangania Bwana na hatimaye akarudishiwa mara dufu.Sisi nasi tukikaa na kudumu katika imani Mungu wetu ataturudishia mara dufu kama kwa mtumishi wake Ayubu katika jina la Yesu.AYUBU 42:10-17;Daniel 3:17-18.Tukatae katakata kuitumikia sanamu na kila kitu cha mfano wa hayo machukizo .Bora tumn’gan’gania Yesu.

Tusimame:

Mshukuru Mungu kwa yale yote uliyojifunza na chukua hatua ya kufanya kwa kuhakikisha kuwa tunamngangania Yesu kwa gharama yoyote ile.

 

Somo 4:

 

WAIONAYO NJIA ILE NI WACHACHE

Mathayo 7: 13-14

 

Siku inakuja ambapo watu wote watabaguliwa na kutengwa makundi makundi.Kondoo na Mbuzi.Lazima tuelewe kuwa sio wote Wakristo ambao wanakwenda kanisani achilia mbali watu wa dini zingine ama wapagani lakini hata wale wanaolitaja jina la Bwana ambao wataingia katika Ufalme wa Mungu.Tunapaswa kufahamu kuwa Juya litachambuliwa na samaki watatengwa na matakataka yote ya baharini kama vile kaa ama konokono n.k,Zitajulikana Ngano na magugu kwani kama ilivyo ndivyo ambavyo siku hiyo ya kutisha inakuja.Basi kwa mifano hiyo ni vema leo tuendelee kujifunza masomo ya utakatifu  ili tuzidi kujifunza iwapo tupo katika njia iliyo njema au la.Bwana atusaidie ili tuzidi kutafuta na kukaa katika njia ile iendayo mbinguni.tutaligawa somo letu katika vipengere vifuatavyo:

 

1.        WAIONAYO NJIA ILE NI WACHACHE

2.        KUANDAMANA NA  MKUTANO KUTENDA UOVU

3.        KUSITASITA KATIKA NJIA MBILI

4.        JINSI YA KUFANYA

 

1. WAIONAYO NJIA ILE NI WACHACHE

Njia iendayo katika mateso ya moto ni pana sana na waingiao ni wengi sana.Si wote waimbao kwaya,kushika biblia n.k waendao mbinguni.Mathayo 7:21 wengi wenye majina makubwa makubwa hata wengine ni wachungaji,mapadre n.k watakwenda njia ile pana.Ni wachache sana waendao mbinguni.Hatupaswi kuridhika tu kuhudhuria ibada kama hii kwani hata shetani anaingia kanisani.Ayubu 1:6 .Si swala la kumwabudu Mungu mmoja kwani pia mashetani hufanya hayohayo tena kwa kutetemeka.Yakobo 2:19.Moto wa milele uliubwa kwa ajili ya shetani na malaika zake na Mungu hakukusudia kabisa kumwachilia mwanadamu aende huko.Lakini wengi wanakwenda huko kwa kukosa maarifa ama kufuata tu mkumbo.Mtu anakuja kanisani kwa lengo tu Fulani mfano kuwafuata wazazi kutafuta misaada ama fedha,wachumba ,kazi ,chakula n.kna ukimpima katika mizani ya utakatifu utakuta hayupo yupo duniani kabisa.Lazima tufahamu kuwa kuna maisha baada ya hapa duniani na hatutaishi hapa duniani milele na milele.Hapa sisi wote ni wasafiri na wapitaji.Mathayo 25:41.Tuwe macho tusije tukaaibika kama wale wasio na matumaini.Tusifuate tu mkumbo jiulize endapo kweli umeokoka.

2. KUANDAMANA NA  MKUTANO KUTENDA UOVU

Kutoka 23:2 hatupaswi kabisa kufuata mambo yanayofanywa na mataifa au watu wote kwa sababu ndiyo kawaida ya ulimwengu huu ama utamaduni wa eneo hilo.Mfano kuna watu huoa mke zaidi ya mmoja,kunywa pombe,kutembeleana mvulana na msichana majumbani,kucheza dansi,miziki ya kidunia na kusema ni sanaa tu,kufanya uasherati  eti ni kawaida watu kujuana kabla ya ndoa,Kusema uongo,mizaha,utanina kusema aah huyu ni mtani wangu n.kNa wengine hujifariji na kusema hivi kweli Mungu yeye hana huruma kweli ataangamiza watu wote?Mungu hashushi viwango.Ufunuo 21:27.Hakuna chochote kile kinyonge kitakachoingia kule mbinguni.Mungu ni Nuru wala giza halitaonekana ndani yake.Waebrania 12:14.Wengi wetu hata sasa tumedanganyika na hata kujifariji na kufanya kama wengine wafanyavyo.Tumefanya kanisa letu kama desturi na mazoea ya wengine,kwa sababu makanisa mengi wanafanya hivyo sisi nasi tunaona ni sawa.Hatushuhudii tena,hatuombi tena,wengi wetu hatuoni tena maana ya kuja na biblia na madaftari ya kuandika kwani tumelizoea neon na kubeba tena vitu hivyo ni aibu na hata makanisa mengi ya walioendelea hawafanyi hivyo na sisis tunaiga.Tujue Munguwetu hatatuhurumia kwani Neno limekufundisha tena na tena yatupasayo kufanya lakini sisi kwa kiburi chetu tumeamua kulizoea neno na kuwa kama wengine wafanyavyo.Mwanzo 4:19,23.Lameck alijisifia kuoa mke zaidi ya mmoja lakini toka mwanzo Mungu hakukusudia kuwa mwanadamu afanye hivyo.Mungu atatuharibu sawasawa na nyakati za Sodoma na Gomora ama wakati wa Nuhu.Nyakati za Nuhu wengi walimfuata Lameck na Mungu akawaangamiza wote.Mwanzo 7:6-12.Mwanzo 19:1-26.Ssi nasi tuangalie tusiambatane na watendao uovu na kudhani ni salama.

3. KUSITASITA KATIKA NJIA MBILI

Yakobo 1:8 Hatupaswi kusitasita bali kuishi kwa Imani.tusiwaangalie wale wasitao na wenye mawazo mawili bali sisi tusonge mbele na kumwamini Mungu.Waebrania 10:37-39;1Wafalme 18:21 2Wafalme 17:33,41.Watu wa nyakati hizo walikuwa wanamwabudu Mungu huku wakiziabudu sanamu zao.Hata leo watu wengi hufanya hayo hayo.Hufanya mambo yao na huku wakiwa pia wakimwabudu Mungu aliye hai na Mungu hataki michanganyo.Ufunuo 3:15-16.

 

4. JINSI YA KUFANYA

Mithali 28:13 Tunapaswa kutubu,na kuishi maisha ya utakatifu maisha yanayompendeza Mungu.Yohana 15:5;Wafilipi 4:13;Luka 1:77;Yakobo 2:3 lazima tugundue kuwa hatuwezi kwa nguvu zetu ni kwa kuwezeshwa.Wengi wetu tunachanganya changanya masomo.Tuwe moto na sio baridi.Tujiulize iwapo wote waliopo duniani wameokoka na kama bado sisi tunafanya nini kama watu waliookoka.Lazima tuwe na huruma,tusije mahali hapa peke yetu,tusiyaangalie mamboyetu wenyewe bali tuyaangalie mambo ya wengine na kuhakikisha kanisa letu linakua na kuongezeka.Na wakati huo huo tujiangalie ili sisi wenyewe tusije tukawa kibao bali tukaze mwendo na kuziangalia nafsi zetu tusije tukakengeuka na kurudi nyuma bali tunapaswa kukaza mwendo.Mwenye sikio na asikie.

     Somo:5                       ROHO YA ASI

Tunaishi siku za mwisho na siku hizi za mwisho yuko Roho anayetenda kazi kubwa katika nyakati hizi za mwisho aitwaye ASI. 2Thesalonike 2:1-8 .Tunaligawa somo letu katika vipengere vinne vifuatavyo:       

1.      Roho ya Asi

2.      Maana ya Uasi

3.      Uasi dhambi kuu

4.      Jinsi ya kuwa mbali na uasi.

 1. Roho ya Asi

Jina jingine la Asi ni Roho ya mpinga Kristo.Yeye ndiye mkuu wa uasi.Mwana wa kuasi.Mwana wa ibilisi.baba ya Uasi chapa ya ibilisi na kazi yake kuu ni kumwasi Kristo ama kumpinga Kristo.Zamani malaika mkuu aliitwa Lucifaer(nyota ya Alfajiri) Isaya  14:12-15;Ezekiel 28:14-15. Lucifer aliumbwa na kutiwa mafuta kuwa Kerubi ili awe juu ya malaika wengine.Yeye ndiye alikuwa mwenye kuimba sifa na akaona bora ampindue Mungu.Alitaka kumzidi hata Mungu.Huyo ndiye chanzo chenyewe cha kuasi.Mikael akapewa jukumu la kupigana na yule Joka la zamani.Ibilisi na shetani huyu hakumshinda.Huo ndio uasi au uhaini alioufanya mbinguni.Na alipotupwa  Ufunuo 12:7-9 .Sasa akawaendea Adamu na Hawa na kuwashawishi Adamu na Eva ili wamwasi Mungu.Nao watupwe nje ya bustani ya Edeni.Na kweli walipotupwa nje alisababisha kuharibika kwa kizazi chote cha Adamu.Waefeso 5:6;2:1-2 Huyo mpinga Kristo yupo lakini hajafunuliwa bado na kazi yake kubwa ni kuhakikisha wana wa Israel hawapati nafasi ya kuwa pamoja na Mungu bali wote wawe waasi.Japo nia ya Mungu ni kuwaokoa waIsrael wote.

 

Kufunuliwa kwake hadharani ni mpaka kunyakuliwa kwa kanisa.Hivyo sasa hivi Roho ya kuasi itakuwepo sana kwa viwango vya juu katika dunia.Pia watu waliookolewa Roho hii itawavaa sana.Ni msingi kuelewa kuwa watu waliookolewa wanakuwa ni wana wa kutii.1Petro 1:14.Mtoto wa kutii.Uasi umebadilishwa na kuwa jambo la kawaida kwani Hofu ya Mungu haipo tena miongoni mwetu.Hata hivyo tunapaswa kuchagua la kushika.Tumepewa kufanya kwa hiari .Tunapaswa kuchagua mema na mabaya.Kumbukumbu 30:15,19 Chagueni hivi leo ni nani wa kumtumikia?(I have set before thee this day Life and Good ,and Death and Evil )Utashangaa sana kuona roho hii ya uasi inatawala sana kwa watu.Inawezekana kabisa kuona waliokuwa wanatuongoza na hata kusimamisha katika imani labda ni watumishi wa Mungu yaani wachungaji,maaskofu,wainjilist,wazee wa kanisa,wanakwaya,waombaji,wahudumiaji katika makundi mbalimbali n.k

Waalimu wetu waliotusimamisha katika imani roho hii pia ikiwavaa.(Ant-Christ).Na upendo wa wengi utapoa.Kwa sababu ya kuongezeka maasi.Dalili ya uasi lazima tuzifahamu mapema na madhara yake ili tujue jinsi ya kufanya tukiiona hali hiyo kwetu.

2.      Maana ya Uasi

Kiblia ni kufanya lolote kati ya haya.Kumbukumbu 9:23-24.Kutolisadiki Neno la Mungu.Watu hivi sasa hawasadiki kuja kwa Yesu,moto wa milele ama kwa ujumla maneno ya Mungu ambayo kabla alikuwa anayasadiki.Wengi huchagua tu maneno ya kuwafariji ama baadhi na mengine hawayasadiki tena.Zaburi 119:6 lazima tujue kuwa roho hii iko kazini.Yakobo 2:10;2 Wakorintho 2:7;Daniel 9:5

Kutokufuata maagizo ya Mungu.Tunapaswa kuhubiri na kufundisha injili.Kutoa zaka,kubatizwa n.k Kuna kazi sana hivi sasa ya kuwasimamisha wengine katika utakatifu.sasa ni kama mzigo watu wanapenda tu kuhubiriwa baraka tu na sio kweli ya neno la Mungu.Lazima tumtumikie Mungu katika lolote  lakini sasa hivi kutokana na roho hii ya asi ni mzigo mzito sana kumtumikia Mungu katika huduma mbalimbali.Ni shida kufunga,kuomba,kuimba,kumwabudu Mungu ,kusimamia wengine katika kutenda haki,kushuhudia,kualika n.k

Kutokumtii Mungu na kutupa sheria  yake nyuma yao .Nehemia 9:26 Watu sasa hivi hawaoni ni lazima tena kuyatii maagizo ya Mungu na badala yake kazi yao ni masengenyo ama kutaka kuua huduma za wengine.Watu kama hao wataona kuwa ni mzigo sana kuwatii viongozi wanaowaongoza ama kutii Neno la Mungu linalowaogoza na kuwatia katika kweli yote.

Kumpa Mungu mipaka Zaburi 78:17-21 ,40-41 katika kufany ahili au lile sawasawa na Neno.watataka kupindisha na kufanya watakavyo wao.Wanawavunja wengine moyo wa kumtumikia Mungu.Ama kutaka wengine wawasikilize katika udhaifu wao.Mfano wengine wanapokuwa wamerudi nyuma wanataka kuwarudisha wengine nyuma .Mfano akimwona mtu anaumwa ambaye anamtegemea Mungu anamwambia twende kwa waganga wa kienyeji n.k

SOMO LINAENDELEAMitihani ya Kujipima

 
 

MITIHANI YA KUJIPIMA

 

TOFAUTI YA MWANAFUNZI WA YESU NA MAKUTANO

Kuna aina mbili za Watu waliookolewa.Baada ya kuokolewa Yesu Kristo anamtegemea kila mmoja wetu kuwa Mwanafunzi wake.Yaani Mwanafunzi wa Yesu.Nyakati za kanisa la kwanza wengi wa watu ambao walikuwa wanamfuata Yesu hawakuwa wanafunzi wake.Wengi walikuwa makutano.Mkutano wote ulikuwa unamtafuta Yesu lakini si kwa sababu ya mafundisho bali Kwa sababu ya mikate.(kazi,fedha,watoto,scholarship,mitaji,mafanikio mbalimbali n.k)Usikitendee kazi chakula chenye kuharibika,bali chakula kidumucho hata uzima wa milele;ambacho mwana wa Adamu atawapa,kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba,yaani,Mungu….”sasa Maneno haya yanamaanisha kuwa Yesu alipokuwa anawatazama makutano alijua kabisa kuwa hawakuwa na nia ya kujifunza kutoka kwake bali wale na kushiba kwa ajili ya mwili na sio roho.

 Sasa wewe n a mimi Mungu wetu anahitaji sana kutoka kwetu kuwa tutakuwa watu wenye kutamani sana kusikia na kujifunza kutoka kwa Mungu.Kwa sababu hiyo ni vizuri uwe mtu anayependa kujifunza hata kufikia kimo cha utimilifu wa Kristo.Basi sisi lazima tukubali kuitwa wanafunzi wa Yesu.Kama kweli tunahitaji kuwa wanafunzi wa Yesu na sio makutano tutakubali kukaa chini ya waalimu wa Neno la Mungu na kujifunza jinsi ya kuukulia wokovu.

Njia mojawapo ya kuukulia wokovu ni pamoja na kujisomea mwenyewe Neno la Mungu.Na hapa sasa tunaanza kujisomea masomo mbalimbali ambayo baada ya kujifunza kwa kina itakubidi kujipima mwenyewe kwa kufanya mitihani mbalimbali ambayo itakuwa inaletwa kwetu kwa kuandikwa mahali hapa na baada ya kusoma somo na kulielewa vema na sio kutumia uzoefu wako katika wokovu utapaswa kuituma mojakwamoja kwa anwani  hii hapa chini na kwa msaada wa Roho Mtakatifu utasahihishwa na kuelekezwa mambo Fulani Fulani ili uweze kuzidi kuwa mwanafunzi Bora na mwaminifu kwa Kristo Yesu kwani wote tunawajibika kwake.Mungu akusaidie katika kuelewa na kuyatendea kazi yote unayopaswa kufanya bila uasi wowote. Mungu akubariki sana,

roho

Mtu aliyeokoka nafsi yake inatawaliwa na roho. Roho inakuwa imeushika usukani, na kumwongoza huyo mtu. Hivyo huyo mtu atatenda matunda ya roho ambayo ni matendo yanayompendeza Mungu. Roho nayo inayo milango ya fahamu ambayo ni mawasiliano na Mungu, uwezo wa kujulishwa (ituition) na dhamiri (consious).

Mtu ambaye anaongozwa na roho anakuwa na mlango wa fahamu wa mawasiliano na Mungu. Atakuwa na uwezo wa kuwasiliana na Mungu. Hapa ndiyo maana biblia inasema kuwa, Mungu hawezi kusikia mtu mwenye dhambi. Maana mwenye dhambi nafsi yake inaongozwa na mwili na shetani, haongozwi na roho hivyo hana mlango wa fahamu wa mawasiliano na Mungu, maana mlango huu unapatikana kwenye roho tu.

Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi, bali mtu akiwa mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake humsikia huyo (Yohana 9:31).

Mtu wa Mungu hakikisha unaishi maisha matakatifu ili uwe na mawasiliano na Mungu. Ili Mungu unapomuomba akusikie na kujibu.

Mlango mwingine wa fahamu wa roho ni uwezo wa kujulishwa. Mtu anayeongozwa na roho ndiye anayeweza kujulishwa mambo mbalimbali yaliyoko katika ulimwengu wa roho, mambo ambayo hayajulikani kwa mtu yeyote isipokuwa yanajulikana kwa Mungu pekee.

Mungu hafanyi kitu bila kuwajulisha masihi wake. Watu waliookoka wamekuwa wakijikuta wako katika majaribu mbalimbali bila ya Mungu kuwajulisha. Hii imekuwa hivi kwa sababu badala ya kuongozwa na roho, wameruhusu mwili uwaongoze, hivyo wamekuwa wakitenda maovu ambayo yamesababisha Mungu asiwajulishe. Mawasiliano yamekatika.

Hakika BWANA MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake (Amosi 3:7).

Siri ya BWANA iko kwao wamchao, naye atawajulisha agano lake (Zaburi 25:14).

Mlango wa tatu wa fahamu wa roho ni dhamiri. Dhamiri ya roho ni kutenda mapenzi ya Mungu. Dhamiri ndiyo inayoshika usukani iwapo mtu mhusika atakuwa anaongozwa na roho. Dhamiri ni sauti ambayo husikika ndani ya mtu ikimshauri atende mema. Hivyo iwapo ni ndani ya mtu ambaye hajaokoka basi dhamiri hiyo haitafanikiwa japo kuwa itamshawishi kutenda mema. Iwapo ni ndani ya mtu ambaye ameokoka basi dhamiri itafanikiwa kumshawishi mtu ampendeze Mungu. Dhamiri ni sauti ya Mungu, unapokataa kutii dhamiri yako hapo umemkataa Mungu. Sheria ya Mungu imeandikwa ndani yetu ndiyo hiyo dhamiri.

Neno la Mungu linasema,

Basi nasema, enendeni kwa roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili
(Wagalatia 5:16).

Mtu wa Mungu, tuuue mwili kabisa ili usiweze tena kuitawala nafsi na kutuongoza kutenda maovu. Tukubali kuipoteza nafsi ili roho iweze kuitawala nafsi na ndipo tutaweza kuongozwa na roho na kuweza kumpendeza Mungu.

Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu… na kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi, bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki… basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maama kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaongozwa na roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu (Warumi 8:5 – 14).

Mtu wa Mungu iwapo wewe umeamua kwenda mbinguni na bado yanajidhirisha matendo ya mwili ya uasherati, uchawi, ufisadi, ibada ya sanamu, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo yanayofanana na hayo, kama vile, useng’enyaji, ubinafsi, uvutaji sigara na madawa ya kulevya, kutokuwapenda ndugu n.k. Mungu anasema, watendao mambo ya jinsi hii hawataurithi ufalme wa Mungu.

Biblia, watu wa Mungu inasema kuwa, Wanaoongonzwa na roho hao ndiyo wana wa Mungu. Watu wa Mungu, iwapo bado unaongozwa na mwili, tumeona kuwa nia ya mwili ni mauti. Hivyo mtu wa Mungu usiupe nafsi mwili kabisa.

KUZALIWA MARA YA PILI

Baada ya kujifunza hayo ni vizuri nimalizie kwa kuzungumzia kuhusu kuzaliwa mara ya pili Nimeona iwe hivyo kwa sababu maisha matakatifu yanaanza baaya ya mtu kuzaliwa mara ya pili.

Katika nchi ya Tanzania kuzaliwa mara pili kumepotoshwa maana yake halisi, hivyo watu wamepokea tafsiri ambayo siyo. Hii imesababishwa na madhehebu yaliyotangulia kuhubiri injili hapa Tanzania yahakuliezea jambo hili kwa usahihi. Mafundisho potofu kuhusiana na hili yanasema, kuzaliwa mara ya pili ni kubatizwa. Tafsiri hii kama ingekuwa ni safari ya ndege kwenda Ulaya basi ilikuwa imepoteza mwelekeo kwa mbali sana, na kama ilikuwa inaenda Japani basi ingejikuta ipo Australia.

Mafundisho haya yanatakiwa yapingwe kwa nguvu zote bila aibu wala uoga wa aina yoyote, tena yapingwe waziwazi kabisa. Haya mafundisho ndiyo chanzo cha kuwepo wakristo watende dhambi, wasio na uwezo wa kuishi maisha matakatifu; wakristo wa jina lakini hawaishi maisha matakatifu.

Wakristo baada ya kubatizwa wamesahau kuwa bado wanahitaji kuishi maisha matakatifu, hivyo wameridhika na ubatizo na kwa vile wamehakikishiwa kuwa ubatizo ndiyo passport ya kuingia mbinguni, basi, hawana juhudi yoyote ya kuishi maisha matakatifu. Matendo yao ni ya kipagani wanachojali wao ni ule ubatizo na kufuata taritibu za dhehebu.

Biblia inasema,

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa (Marko 16:16).

Biblia inasema, Ili uokoke kuna mambo mawili kuamini na kubatizwa. Kitu ambacho mtu anatakiwa akifanye kwanza ni kuamini. Baada ya kuamini ndipo ubatizwe. Kwa hiyo tendo la kuamini ni kitu tofauti kabisa na kubatizwa. Kuamini ni kuamini na kubatizwa ni kubatizwa, kila tendo lina maana yake na umuhimu wake tofauti.

Kosa lililofanyika hapa kubatizwa kumeinuliwa juu hadi kukafunika na kumeza kuamini. Hivyo kuamini hakupo bali kupo kubatizwa. Kuamini kutoweshwa watu wanajiunga na ukristo bila ya kumwamini Yesu. Kuamini kunatajwa lakini si kwa hadhi yake; si kwa maana yake; si kwa msisitizo unaostahili. Hivyo kutokana na hili, kitu cha muhimu kimekuwa ni kubatizwa. Hivyo watu wamekuwa wakibatizwa hata bila ya kuamini. Asilimia tisini ya wakristo wa Tanzania hawajamwamini Yesu bali wamebatizwa na kujiunga na dini ya ukristo.

Nikisema hivi wengi hunipinga na kusema kuwa mtazamo wangu huo hauko sahihi. Lakini mimi ninasema kuwa, Ndiyo ilivyo ukubali usikubali. Na hii ni hali kusikitisha sana, tunahitajika kufanya kazi ya kuwafundisha watu ili walijue hili. Idadi kubwa ya wakristo wa Tanzania ni wapagani waliojiunga na ukristo na hawana tofauti na wapagani. Dhambi wanazifanya sambamba na wapagani; ushirikina wanaufanya sambamba na wapagani; maofisini wanaongoza katika kutokutenda haki.

Unaweza kujiunga na ukristo lakini ukawa hujamwamini Yesu. Kuamini ni kupokea badiliko rohoni lakini kujiunga na dini bila kuamini hakuwezi kuleta badiliko rohoni.

Biblia inasema,

Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka (Warumi 10:9).

Unapomwamini Yesu unamkaribisha moyoni mwako ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Anayatawala maisha yako.

Tendo la kumwamini Yesu limekuwa likionekana kama ni tendo la kuigiza tu. Hii imekuwa hivyo kwa sababu, mtu aliyemwamini Yesu na yule hajamwamini Yesu hawana tofauti yoyote ile. Hakuna badiliko lolote lililotokea linalowatofautisha. Amemwamini Yesu lakini bado mtenda dhambi kama alivyokuwa kabla ya kuamini. Limekuwa ni igizo lakini si kitu halisi.

Baada ya Adamu kutenda dhambi, roho ya mwanadamu ilikufa. Hivyo tangu hapo wanadamu waliendelea kuzaliwa mwili lakini roho zao zikiwa zimekufa japokuwa tunatembea.

Roho ndiyo huenda mbinguni siyo mwili, hivyo ili mtu aende mbinguni ni lazima roho iliyokufa ihuishwe iwe hati. Roho zilizokufa hutupwa Jehanamu. Yesu alikuja kuihuisha roho ili wewe uweze kwenda mbinguni.

…………wa roho, hutokea badiliko la kiungu ambapo roho iliyokuwa imekufa huhuishwa na kuwa hai. Hapo hapo hutokea badiliko lingine upande wa mwili. Mwili nao hufa.

Na hao walio wa KristoYesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tama zake (Wagalatia 5:24).

Hii ndiyo maana ya kumwamini Yesu. Unapomwamini Yesu hutokea badiliko la roho kuhuishwa. Ilikuwa imekufa na sasa imekuwa hao. Huyu mtu kabla ya kumwamini Yesu, roho yake ilikuwa imekufa mwili ulikuwa hao hivyo alikuwa anaongozwa na mwili, lakini sasa amemwamini Yesu, roho yake iko hai na mwili umekufa hivyo sasa anaongozwa na roho. Kwa vile anaongozwa na roho hawezi kutenda dhambi maana roho itamwongoza kutenda mema. Mtu huyu ndiye anatakiwa kubatizwa. Huwezi kubatiza mtu ambaye hajahuishwa roho yake, ukibatiza mtu ambaye hajahuishwa roho yake, ukibatiza watu ambao roho zao hazijahuishwa bado zimekufa, bado wanaongozwa na mwili, hata baada ya kubatizwa hawataweza kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Kitu kibaya zaidi hawataingia mbinguni maana inayoingia mbinguni ni roho siyo mwili, sasa wamekuwa roho zao zimekufa bado.

Biblia inasema,

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli (Yohana 4:24)

Agano la kale Mungu aliabudiwa kwa mwili, lakini tangu Yesu kuja Mungu anaabudiwa katika roho. Kuabudu katika mwili kulishindwa kuwawezesha watu waishi maisha matakatifu kwa sababu roho zao zilikuwa zimekufa. Hivyo Yesu alikuja ili kuhuisha roho zetu. Mungu ni Roho hivyo pia anahitaji aabudiwe katika roho. Mtu ambaye rohoyake imekufa hawezi kumwabudu Mungu. Ili mtu amwabudu Mungu ni lazima kwanza kabisa roho ihuishwe. Hapa ina maana kwamba mtu ambaye hajahuishwa, roho yake humwabudu Mungu katika mwili. Mwili hauwezi kumwabudu Mungu ambaye ni roho. Mtu ambaye bado roho yake haijahuishwa yaani bado imekufa ukimbatiza bado roho yake itakuwa imekufa, maana tendo la ubatizo halihuishi roho, bali kumwamini Yesu na kumpokea awe Mwokozi wako ndiko huhuisha roho. Hivyo, roho huhuishwa hata bila kubatizwa. Mtu huyu aliyebatizwa bila kumwamini Yesu na kumpokea awe mwokozi wake, kwa vile roho yake bado imekufa, atakapomwabudu Mungu, atakuwa anamwabudu Mungu katika mwili.

Mwili ni udongo utarudi kwenye udongo, huo ndiyo mwisho wa mwili. Mwili hauendi mbinguni hata kama mwili utamwabudu Mungu.

Roho inayokwenda mbinguni ndiyo inamwabudu Mungu.

Biblia inasema,

Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli; kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu (Yohana 4:23).

Mungu anawatafuta watu wamwabudu katika roho siyo wamwabudu katika mwili. Wakristo wengi katika nchi ya Tanzania wamekuwa hawalijui hili wanamwabudu Mungu katika mwili, watashangaa siku hiyo maana hawatakuwa wameandikwa katika kitabu cha uzima. Mtu anaandikwa katika kitabu cha uzima baada ya roho yake kuhuishwa. Hapo ndipo anakuwa raia wa mbinguni. Mbinguni zitaingia roho zilizo hai, roho zilizokufa zitatupwa Jehanamu. Huku ndiko kuzaliwa mara ya pili. Mara ya kwanza ulizaliwa katika mwili kama raisa wa dunia na sasa unazaliwa roho kama raia wa mbinguni.

Mara ya kwanza ulizaliwa na mama yako katika mwili na sasa unzaliwa roho. Kuzaliwa mara ya pili ndipo huku kuhuishwa roho. Roho ilikuwa imekufa sasa imezaliwa upya imekuwa hai. Kubatizwa siyo kuzaliwa mara ya pili. Yesu alikuwa mtakatifu hakuhitaji kuzaliwa mara ya pili, kama kubatizwa ni kuzaliwa mara ya pili basi Yesu asiingehitaji kubatizwa, maana tayari alikuwa mtakatifu.

Kubatizwa ni tendo la kutangaza yaliyotokea ndani yako. Unalitangaza badiliko ulilolipata ndani yako. Tangazo hilo ni kwamba, ulikuwa umekufa na sasa umefufuka na Yesu. Unapozamishwa ndani ya maji unatangaza kuwa ulikuwa umekufa na unapotolewa kwenye maji unatangaza kuwa sasa umefufuka. Yesu alihitaji kulitangaza tukio hili pia kuwa, Yeye yu hai. Hapo hapo Mungu akalithibitisha jambo hilo kwa kumtuma Roho Mtakatifu kwa mfano wa hua, hapohapo pia sauti ikasikika mbinguni ikisema,

Ikawa watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, Mpendwa wangu; nimependekezwa nawe (Luka 3:18-20).

Pale msalabani Yesu alimwambia yule mmoja wa wahalifu waliosulibiwa pamoja naye,

Na mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa alimtukana, akasema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini yule wa pili alimjibu, akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lolote lisilofaa. Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amini, nakwambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi (Luka 23:39-43).

Huyu aliingia mbinguni bila ubatizo, bali alimwamini Yesu na kumpokea, hivyo roho yake ilizaliwa mara ya pili pale msalabani. Hakutangaza tukio lililotukia ndani yake kwa sababu muda wa kufanya hivyo haukupatikana. Kutokatangaza hakungemzuia kuingia mbinguni (yaani kutokubatizwa).

Siyo kwamba ninadharau ubatizo kuwa si wa muhimu, hapana, lakini ninafundishwa hili jambo liwe wazi ili Shetani asilitumie kupoteza watu wa Mungu. Mimi mwenyewe nimebatizwa kwa maji mengi. Yohana alitaka kukataa kumbatiza Yesu kwa ile Yohana alimjua Yesu kwamba ni Mtakatifu tayari, hivyo hastahili kubatizwa. Lakini Yesu alisema,

Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akasema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali (Mathayo 3:13-15).

Huwezi kudharau ubatizo. Mungu anataka tutangaze tukio lililotukukia ndani yetu. Kuna mambo mengi ambayo Mungu anataka tuyafanye baada ya kumpokea Yesu. Kuna mengine pengine tunaweza kushindwa kuyafanya kutokana na muda, kutokuyafanya hayo hakuwezi kutuzuia kwenda mbinguni, maadamu tutakuwa tumehuishwa roho zetu.

Huyu mtu yule wa msalabani hakubatizwa, kutokubatizwa hakungemzuia kwenda mbinguni, lakini iwapo kungekuwa na muda angebatizwa. Ni hivyo hivyo hata katika mambo mengine ya kujazwa Roho Mtakatifu. Mtu aliyempokea Yesu anatakiwa ajazwe Roho Mtakatifu, lakini iwapo muda huo haukupatikana hawezi kutokwenda mbinguni kwa sababu hakujazwa Roho Mtakatifu. Ila kwa mtu ambaye atajaliwa maisha baada ya kumpokea Yesu ni jambo la muhimu kujazwa Roho Mtakatifu ili awe na nguvu za kiroho.

Wakristo wameshindwa kutoa huduma za kuwaleta watu kwa Yesu walio katika dakika za mwisho za kifo, kwa kuwa wanafikiria watawabatiza namna gain? Hivyo badala ya kuwaongoza wampokee Yesu peke yake inatosha kuingia mbinguni hata kama watakuwa hawajabatizwa. Watu wa Mungu jambo hili hebu tusaidiane kuliweka sawa na Mungu atakubariki sana.

Huku kuzaliwa mara ya pili ndiko kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako na ndiko KUOKOKA. Kuokoka ndiko mwanzo wa kuabudu. Huwezi kumwabudu Mungu wakati hujaokoka. Neno kuokoka ndilo limezoeleka kutumika katika jamii yetu. Kuokoka ndiyo mwanzo wa uhusiano na Mungu.

Unajua kwa nini wakristo wengi hawajui neno la Mungu? Hata wakifundishwa hawaliewi? Hawa wakristo hawajaokoka, hivyo roho zao bado zimekufa. Neno la Mungu ni roho, kwa vile ni roho, linapopokelewa ndani ya mtu linatakiwa lipokelewe na roho. Neno la Mungu likipokelewa na mwili haliwezi kueleweka na huyo mtu. Neno la Mungu hueleweka tu linapoingia ndani ya mtu ambaye roho yake imehuishwa. Neno la Mungu ni roho ni Chakula cha roho. Kujifunza neno la Mungu mtu ambaye roho yake imekufa, yeye ni mwili, hapo ina maana kuwa mwili unaupa chakula cha roho. Mwili chakula chake ni ugali, samaki, mkate, nyama, n.k.

Mtu mwenye elimu ya juu sana ya kidunia kama hajaokoka pia hawezi kulielewa neno la Mungu. Elimu na akili yake ya kimwili haviwezi kulielewa neno la Mungu. Ni hivyo hivyo kwa mtu asiyeokoka lakini amesoma sana elimu ya biblia, bado hatakuwa ameweza kulifahamu neno la Mungu, hata kama takuwa na PHD ya Biblia. Atajua kuwa kuna Roho Mtakatifu lakini hatakubali kuwa, Mtu anaweza kujazwa Roho Mtakatifu; atajua kuwa Yesu aliponya, lakini hatakubali kuwa, sasa bado anaponya; n.k.

Watu wa Mungu, Mungu anandaa kanisa kwa unyakuo, hebu turudi kwenye kweli ya neno la Mungu. Si wakati wa kushabikia mafundisho ya dini au dhehebu, ni wakati wa kujipigania roho yako wewe mwenyewe. Hebu tuishi maisha matakatifu ili tustahili kumlaki Bwana Yesu mawinguni.

Posted in MAFUNDISHO |

MAISHA YA USHINDI

Wakristo waliookoka hufikiri kuokoka ndiyo mwisho wa vita. Mtu ambaye hajaoka huyo ni mali ya shetani tayari. Baada ya mtu kuokoka huo ndiyo mwanzo wa vita, kuokoka ni kutangaza vita kati yako na shetani. Hivyo pamoja na kuokoka unatakiwa uishinde hiyo vita.

Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kwamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za baba yangu, na mbele ya malaika zake (Ufunuo 3:15).

Kama nilivyotangulia kusema kuwa, vita vya kiroho vinapiganiwa kwenye nafsi, kati ya mwili na roho au kati ya shetani na Mungu, kwamba nani aushike usukani kumwongoza huyu mtu atende mapenzi ya Mungu au atende mapenzi ya shetani. Hivyo hapa kitu cha muhimu ni kutenda matendo ya nani, je, ya Shetani au ya Mungu? Ukitenda matendo ya shetani hapo unakuwa umeshindwa vita hii na ukitenda matendo anayotaka Mungu hapo utakuwa umeshinda vita.

Wakristo wameokoka lakini, baadaye wakashindwa vita. Roho waovu wamo ndani yao wakiwatumikisha. Wanawatumikisha katika mambo ambayo wao wanaona kuwa hiyo ni tabia yao. Tabia ya kiburi, hasira, chuki, kutokuwapenda ndugu, wivu, uzushi, husuda, faraka, useng’enyaji, ufisadi, n.k.

Mtu wa Mungu hutakiwi kumtumikia pepo wa aina yoyote ile hata kama huyo pepo anajidhihirisha kwako kama tabia. Unatakiwa upigane na roho waovu wa aina yoyote ile na uwashinde. Usiruhusu pepo yeyote yule akae ndani yako.

Mungu anataka kukubariki kiroho na kimwili. Lakini miungu iliyomo ndani yako inamzuia Mungu asikubariki. Chimbueni udongo wa mashamba yenu. Kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki (Hosea 10:12). Sasa hivi kanisa tunaenda kuingia katika utukufu mkuu wa mwisho wa nyumba ya Mungu ulionenwa na nabii Hagai, kuwa, Mungu anaenda kulibariki kanisa lake kiroho na kimwili.

Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba utukufu, asema BWANA wa majeshi. Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi. Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi, na katika mahali hapa nitawapa amani, asema BWANA wa majeshi (Hagai 2:6- 9).

Nabii Hosea anawaandaa watu watayarishe mashamba yao ili utukufu huu ulionenwa na nabii Hagai uje. Hosea anasema chimbueni udongo wa mashamba yenu. Mkulima anapochimbua udongo wa mashamba, hung’oa mizizi na magugu yote na kutupa nje. Mtu wa Mungu hebu chimbua ndani yako ung’oe kila pando lililopandwa na shetani na ulitupe nje.

Mtu ni mwili nafsi na roho. Katika sura zilizopita tuliona kuhusu milango mitano ya fahamu. Hii milango iko kwenye mwili. Pia tumeona jinsi nafsi inavyofanyakazi katika mtu. Tuliona kuwa hapo ndipo kwenye uwanja wa vita yenyewe ya kiroho. Vita vyetu tunapigana na roho waovu wa shetani ambao huingia kwenye nafsi ili watulazimishe kutenda maovu. Tunatakiwa tuwashinde wasiweze kuingia kwenye nafsi na kuitawala. Ili tuweze kuwachimbua hawa roho waovu na kuwatupa nje na kuwashinda, tutaenda kujifunza zaidi kuhusu nafsi.

Nafsi nayo inayo milango ya fahamu ambayo ni kuamua (willing), kujisikia au hisia (imotion) na mawazo. Kama tulivyokwisha kuona huko nyuma kuwa, roho waovu wanaingia ndani ya mtu, huenda hadi kwenye nafsi. Roho waovu wanapoingia kwenye nafsi hutawala milango ya fahamu ya nafsi. Hivyo huutawala uwezo wa kuamua, kujisikia na kuwaza.

Mtu ambaye nafsi yake inatawaliwa na roho waovu, Mungu japokuwa atamshauri huyo mtu asitende dhambi, hata hivyo sauti ya Mungu haiwezi kusikilizwa. Pamoja na Mungu kutokusikilizwa Mungu huwa hachoki kumshawishi mtu asitende dhambi. Mtu japokuwa atatenda dhambi lakini sauti ya Mungu huwa pale kumkataza ingawaje hataitii. Hivyo mtu anapotaka kutenda dhambi husikia sauti mbili ndani yake, moja inamkataza kutenda dhambi ya pili inamlazimisha mtu atende dhambi. Huyu mtu atatenda dhambi kwa sababu nafsi yake itakuwa imetawaliwa na huyo roho ovu kama mtu nafsi yake itakuwa inatawaliwa na malaika wa Mungu, atatii sauti ya Mungu.

Kuamua

Katika kila jambo analolifanya mtu huwa linaamriwa katika nafsi kupitia mlango wa fahamu wa nafsi wa kuamua. Kama nafsi ya mtu imetawaliwa na shetani, shetani huteka uwezo wa kuamua na kuhakikisha kuwa maamuzi ya kumpendeza Mungu hayapati nafasi. Hivyo mtu hulazimika kuwa na maamuzi ya kishetani. Roho waovu walioko ndani ya mtu yule ndiyo watakuwa wanaamua. Mfano. Wewe umekabidhiwa wadhifa wa kutoa haki fulani kwa watu. Roho ya chuki, wivu, ubinafsi, uchoyo, n.k. ndiyo itakuwa inaamua. Utajikuta unakalia haki za watu hutaki kuwapa; utajikuta unataka kuhongwa rushwa ndipo utoe hizo haki. Uko tayari mwenye haki apate hasira ya aina yoyote ile hata kama ni kufa afe tu, roho ya chuki iliyoko ndani yako imeamua ukalie haki yake huyo mtu.

Mahali pengine Mungu anakutaka usiwe na hasira, chuki au usilipe kisasi, wewe umekamatwa na roho ya kutokusamehe. Unapima jambo la kusamehe, huwezi kusamehe jambo kubwa. Ili ujulikane kuwa ndani yako kuna roho ya kusamehe hebu samehe mambo yaliyo makubwa. Mtumishi wa shetani maamuzi yake huamriwa na shetani. Mtu wa Mungu hebu pambanua maamuzi yako iwapo ni ya ki-Mungu au ni yakishetani. Unatakiwa upambanue kuwa unatii sauti ipi? Hili jambo ni wazi kabisa wewe kujua ni nani unayemtumikia. Hivyo mtu wa shetani anajulikana wazi kabisa, hata kama utakuwa umejifunika ukristo. Huwezi kuvuna chungwa kwenye mlimao japo kuwa vinafanana. Maamuzi yako ndiyo hayo yaliyomo ndani yako. Je, kuna roho wa hasira? chuki?, choyo? n.k. hivyo ni dhahiri hata kwa walio na upendo, furaha, amani, n.k.

Mkristo mgomvi, mwenye hasira, mwenye kiburi, mwenye ufisadi, n.k. huyu siyo mkristo wala hana safari ya kwenda mbinguni. Huyu ni mtumishi wa pepo la hasira, kiburi, ufisadi, n.k.

Kujisikia

Ndani ya mtu huwa kuna mvuto unaomvuta kutenda kitu, kujisikia mwili unatamani kutenda jambo fulani; kuwa na shauku au kiu ya kufanya jambo fulani; kuhisi maumivu, n.k.

Shetani anapokuwa ameitawala nafsi hawezi kuruhusu hisia za kimungu, bali hisia zitakazopata kibali ni hisia za kimwili na hisia za shetani pekee.

Mawazo

Shetani akitawala nafsi, mawazo ya mhusika yanatawaliwa na shetani. Mawazo yote atakayokuwa anawaza yatakuwa ya kimwili na ya kishetani. Mtu huyu hawezi kutafakari mambo ya kiMungu. Mawazo yametawaliwa na shetani kutafakari mambo ya Mungu ni bughudha kwake. Mtu huyu hatapenda hata kusikiliza neon la Mungu. Mkristo ambaye hapendi kutafakari mambo ya Mungu au kusikiliza neno la Mungu, basi huyo moja kwa moja mawazo yake yamejaa roho waovu, hivyo hao roho waovu hawataki kusumbuliwa na neno la Mungu.

Neno la Mungu linasema

Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo (2 Korintho 10:4 – 5).

Mawazo ni njia mojawapo ya mawasiliano kati ya mtu na ulimwengu wa roho. Hivyo Mungu huzungumza na mtu kupitia mawazo; shetani naye huzungumza na mtu kupitia mawazo; pamoja na hivyo wewe mwenyewe mawazo yako ya kimwili huzungumza na wewe. Hapo ndipo wazo lolote huanzia na baadaye linaenda kwenye kuamua, liamuliwe kutendeka au lisitendeke na baadaye likiamriwa kufanyika, linaingia katika hisia mtu anaanza kujisikia mwili wake kutenda jambo hilo.

Kuna muda wa kutosha kabisa kupigana na roho waovu, tangu walipoingia ndani yako hadi wanapokufikisha kwenye kutenda dhambi au kutenda maovu. Kwa vile kila tendo analolitenda mtu huanza kama wazo au fikra baada ya hapo ndipo hilo wazo au fikra inaamuliwa kufanyika au kutokufanyika na baadaye ndipo hisia au kujisikia kulitenda hilo jambo hufuatia. Mungu anatuambia kuwa tupigane na hao roho waovu wakati bado wako kwenye hatua ya mawazo au fikra. Tena tuangushe kabisa kila wazo linalojiinua juu ya Mungu.

Roho ovu anayekushambulia utamuona kwenye mawazo yako kwanza, hivyo hapo hapo ujue kuwa tayari umeingiliwa na roho ya kigeni, anza kupigana nayo hapo hapo kabla huyo roho ovu hajafika hatua zingine.

Biblia inasema,

Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana (Yoshua 1:8).

Mawazo ya mtu wa Mungu hayatakiwi kutafakari tafakari za kishetani. Watu wa Mungu tunatakiwa tuyaangushe mawazo na fikra zote za kishetani. Mawazo ya shetani yasipate kibali. Hivyo Mungu anatuagiza mawazo yetu yatafakari neno la Mungu usiku na mchana.

Mtu wa Mungu maeneo ya kupigana na shetani katika nafsi ni mawazo, maamuzi na kujisikia. Hakikisha shetani hapati nafasi. Nabii Hosea anasema tuchimbue udongo wa mashamba yetu. Kwa kudhibiti maamuzi yako, kujisikia kwako na mawazo yako, kwamba roho waovu wote unaowaona wakijidhihirisha uwatupe nje kabisa, uteke nyara kila fikra imtii Mungu, hapo ndipo utaweza kuchimbua udongo wa mashamba yako. Hapo ndipo utaweza kuishi maisha matakatifu na shetani hataweza kukufanya uabudu miungu.

Posted in MAFUNDISHO |

MIUNGU

Wakristo wanafikiri kuwa unapokuwa mkristo huwezi tena kuwa muabudu miungu, Shetani siku zote anatafuta mbinu kila kukicha za kumfanya mwanadamu amkosee Mungu.

Wana wa Israeli japokuwa walikuwa watoto wa Mungu, lakini kuna wakati walijikuta wanaabudu miungu, hivyo hivyo hata wakristo wa leo, kweli ni watoto wa Mungu, lakini wakristo kwa kutokujua neno la Mungu wameabudu miungu.

Wana wa Israeli walifanya yaliyomachukizo mbele za macho ya BWANA, nao wakawatumikia mabaali. Wakamwacha BWANA, Mungu wa baba zao aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakafuata miungu wengine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha BWANA, akaghadhabika (Wamuzi 2:11 – 12).

Wako wakristo leo wamefanya kama haya yaliyokuwa yanafanywa na Waisraeli, wamemwamini Yesu, sawa, lakini wanaabudu miungu. Shetani amebadilisha mbinu, zamani aliwafanya watu waabudu miungu wa sanamu na vitu vingine vilivyokuwa vinaonekana. Hata Mungu wakati wa agano la kale aliabudiwa kwa mwili. Wakati huu wa agano jipya Mungu anaabudiwa kwa imani katika roho. Ni hivyo hivyo hata shetani, miungu wa zamani wakati wa agano la kale waliabudiwa kwa mwili, lakini miungu wa sasa si wakuonekana bali wanaabudiwa kwa imani. Miungu wa sasa siyo sanamu bali ni roho waovu wa shetani.

Hata hivyo miungu inayoonekana bado ipo lakini si kwa jinsi ya sanamu bali ni kwa jinsi ya kitu chochote kile kinapowekwa kuwa cha kwanza, Mungu akawekwa kuwa wa pili.

• Miungu inayoonekana

Kuweka kitu chochote kile kiwe cha kwanza Mungu awe wa pili, hicho kitu kinakuwa miungu kwako. Kitu hicho kinaweza kuwa ni baraka ya kutoka kwa Mungu, kama vile, mume, mke, wazazi, watoto, mali, elimu, n.k. hebu nitoe mifano kadhaa.

Mfano wa kwanza

Dada mmoja alikuwa ni mkristo, ameokoka. Alichelewa sana kuolewa. Siku ya siku ilifika akajikuta ameolewa. Alifurahi sana na alimpenda sana mume wake. Msichana huyo kabla ya kuolewa alikuwa anayo bidii sana ya kwenda kanisani, kujifunza neno la Mungu, na kuomba. Msichana alikuwa anamtafuta sana Mungu kwa bidii. Baada ya kuolewa, kwa kumpenda sana mume wake, msichana akawa anatumia muda wake mwingi kuongea na mume wake, hadi akawa haendi hata kanisani. Hapa mume wake amesimama katikati ya huyo msichana na Mungu. Mume amekuwa wa kwanza, Mungu amekuwa wa pili. Huyu mume amekuwa miungu wa huyo dada.

Mfano wa pili

Watoto ni baraka tumepewa na Mungu. Mungu anataka tuwalee katika uchaji wa Mungu na tabia njema za kiutu. Wakristo wengi leo hii wanawadekeza watoto wao, kiasi kwamba mtoto wake hata kama akifanya jambo baya ambalo si la kiutu ambalo halikubaliki katika jamii, bado yeye mzazi anaona mtoto wake amefanya jambo jema.

Mzazi yuko tayari kutenda dhambi kwa sababu ya mtoto. Mtoto anaishi kwenye jamii, mtoto ni wa Mungu, wewe umepewa umlee, wewe hutaki mtoto awe na tabia njema, hutaki jamii imkosoe mtoto wako mahali amekosea, uko tayari kukumbatia makosa ya mtoto wako, badala ya kusimama na neno la Mungu. Mtoto wako atakuwa mzigo na tatizo la jamii atakayoishi nayo, baada ya kutoka nyumbani kwako. Kwa habari ya mtoto wako uko tayari Mungu kumweka pembeni. Hayo maamuzi yako kwa mtoto si ya kimumgu bali ya kishetani. Wewe shetani amekudanganya kuwa huo ni upendo kwa mtoto wako, huo siyo upendo bali unamwabudu mtoto, hivyo mtoto wako amekuwa miungu kwako.

Mfano wa tatu

Biblia inasema kuwa, Mume atamwacha baba na mama yake na kuungana na mke na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Mwanzo 2:23 – 24

Mungu amesema hivyo na anataka kitu chochote kisiwatenganishe pamoja na hivyo ametaka watu waiheshimu hiyo ndoa. Ndoa na iheshimiwe na watu wote. Waebrania 13:4. Ndoa huunganishwa na Mungu, hivyo ndoa ni mali ya Mungu, kitu au mtu yeyote yule anayeitenganisha au hata anayeshindwa kuiheshimu ndoa anatenda dhambi kubwa kwa Mungu, amemdharau yule aliyeiunganisha.

Watu wanaoambiwa waiheshimu ndoa, si watu wa nje ya ndoa ile tu, bali hata wana ndoa wenyewe mume na mke wanatakiwa waiheshimu. Ndoa si mali ya wanandoa bali ni mali ya Mungu.

Wana ndoa mume au mke anayeruhusu mtoto wake akae katikati ya mume na mke na kuamua kumweka mtoto awe wa muhimu badala ya mume au mtoto awe wa mhimu badala ya mke. Mtoto ameruhusiwa kuidharau ndoa iliyofungwa na Mungu mwenyewe. Wewe uliyemweka mtoto wako kuwa wa muhimu kuliko mume wako au kuliko mke wako, umemfanya mtoto wako kuwa miungu kwako, maana umeamua kwenda kinyume na neno la Mungu kwa ajili ya mtoto. Umekumbatia mtoto ukalitupa neno la Mungu. Wengine wameweka mali, kazi, n.k. mbele kuliko mume au mbele zaidi kuliko mke. Hiyo ni miungu kwako.

Mfano wa nne

Wewe umeiweka kazi mbele kuliko Mungu wako. Kazi imechukua nafasi ya kwanza Mungu amekuwa wa pili. Unatafuta kazi hata kama kwa kutenda dhambi ili mradi upate kazi, unailinda kazi yako kwa kutenda dhambi badala ya kumpa Mungu ulinzi wa kazi yako, unatafuta kupanda cheo kwa kutenda dhambi, umesema kuwa kazi yako haikuruhusu kupata muda wa kwenda kusali.

Kwa sababu ya kazi yako huna muda wa kumwabudu Mungu. Kazi yako umeiweka ya kwanza, Mungu umemweka wa pili. Kazi yako unaiabudu ni miungu kwako. Pamoja na kuabudu kazi, wakristo wengine wameabudu biashara zao wameabudu mali zao, n.k.

• Miungu isiyoonekana

Tabia zote iwe njema au mbaya ni roho. Tabia zote mbaya huwa ni roho waovu na tabia zote nzuri huwa ni malaika. Roho wanakuwa ndani ya mhusika. Mkristo yeyote mwenye tabia yoyote ile mbaya huo ni udhihirisho wa roho waovu (pepo) walioko ndani yake.

Baada ya Yesu kuingia ndani ya mkristo huwafukuza roho waovu (pepo) wote walioko ndani yake. wewe mkristo mwenye tabia mbaya, na unaendelea kuzilea tabia hizo basi, unalea mapepo. Hayo mapepo ni shetani. Hiyo ni miungu yako unaitumikia.

Wakristo wengine wameng’ang’ania tabia na desturi za kimapokeo ya kimila, ukoo na kikabila, ambazo hazitendi mapenzi ya Mungu. Hayo yote kwako wewe ni miungu. Wakristo wanakuwa wabaguzi wa rangi na kabila. Mzungu mkristo aliyeokoka anambagua mwafrika kwa ajili ya rangi. Hilo ni pepo la ubaguzi liko ndani yako, ni miungu wako unayemtumikia. Wakristo wengine wanabagua watu kwa sababu ya ukabila. Wakristo wengi wameshindwa kuoa au kuolewa wanasema hawajapata wenza, kumbe Mungu alishawapa wenza lakini wamewakataa kwa misingi ya ukabila. Unafikiri Mungu anaweza kutii miungu yako ili akupe mwenza kwa misingi ya ukabila iwapo kama wewe amekupangia mwenza wa kabila lingine?

Mbinguni ni mbingu ya Mungu. Amewaandalia watoto wake wote watakaa kwa furaha na amani bila kubaguana, Mungu hana nafasi ya kuingiza wabaguzi mbinguni. Siyo ubaguzi tu, kuna mila, desturi na tabia nyingi sana zisizokuwa za kiutu, kila ukoo, kabila au Taifa linazo na wakristo nao wanaendelea nazo. Hivyo wanafuata kawaida ya dunia. Mungu amekataa kufuatisha kawaida ya dunia, bali tuishi maisha ya kumpendeza.

Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. Maana wakati wa maisha yenu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya mataifa. Mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi wakiwatukana (Petro 4:2 – 4).

Hii yote ni miungu. Mkristo mwenye kumtumikia roho ovu wa aina yoyote au pepo wa aina yoyote ile. Hiyo roho ovu au huyo pepo ni shetani kama umekubali kumtumikia shetani amekuwa miungu wako. Wakristo wamekuwa wakitumikia miungu ya kiburi, ulafi, wivu, uchoyo, fitina, hasira, chuki, ukabila, ubaguzi wa rangi, uzushi, ubinafsi, kutokusamehe, n.k. Mungu anasema kuwa watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Hawataurithi ufalme wa Mungu kwa sababu wanaabudu miungu.

Mungu aliwaambia wana wa Israeli kuwa kwa sababu ya machukizo, Mungu anaghadhabu, tena hataona huruma na wajapolia kwa sauti kuu hata wasikiliza. Basi, akaniambia, umeyaona haya, mwanadamu? Je! Ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye machukizo wanayoyafanya hapa? Kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha, na, tazama, wanaliweka tawi puani. Kwa sababu hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu, jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza (Ezekieli 8:17 – 18).

Hii ni sawa kabisa na wakati wa sasa hivi, wakristo wengi wana vilio. Wanalia juu ya watoto wao, biashara, kazi ndoa, afya, n.k. wamemwomba Mungu hataki kujibu. Wamefunga na kuomba lakini Mungu amenyamaza kimya. Umemfanya mtoto kuwa miungu, kazi, biashara, n.k. navyo umevifanya miungu, Mungu hawezi kupigania miungu, Mungu hawezi kulinda miungu. Mungu ameutoa mkono wake, amemruhusu shetani afanye atakavyo, hivyo mapepo hayana kizuizi, yanafanya yatakavyo. Utaomba, utalia, watumishi wa Mungu, mbalimbali wataomba lakini Mungu hatajibu. Hutapata msaada popote pale hadi utakapoacha kuabudu miungu.

Posted in MAFUNDISHO | Leave a Comment »

JINSI ROHO WAOVU WANAVYOINGIA

KWA MTU ALIYEOKOKA

Baada ya mtu kuokoka, Yesu huwafukuza roho waovu wote. Lakini hao roho waovu hawaendi moja kwa moja, hurudi na kujaribu kumshambulia yule mtu ili kama watashinda basi waingie na kuendelea kumtumikisha huyo mtu. Hebu nilielezee jambo hili kwa njia ya picha.

Pepo akiisha ingia namna hiyo atakuwa anapata nafasi siku moja moja anakuongoza kutenda dhambi. Hata ukitubu hiyo dhambi pepo atakuwa bado amekushinda siku nyingine tena atakuongoza kutenda dhambi. Dawa ya roho ovu akiishaingia kwenye nafsi siyo kutubu. Watu wengi wa Mungu walioshambuliwa na kushindwa na roho waovu, wamekuwa wakitubu ili waweze kuwashinda hawa roho waovu waliowavamia, lakini hawajaweza kufanikiwa, badala yake wamekuwa wakristo wa kutenda dhambi na kutubu.

MTU AMBAYE HAJAOKOKA

MWILI NAFSI ROHO

Uasherati, Upendo
Uchafu, Furaha
Ufisadi, Amani
Ibada ya sanamu Uvumilivu
Uchawi, Utu wema
Hasira, Fadhili
Uzinzi, n.k
Wivu
n.k.

Picha hii inaonyesha mtu ambaye hajaokoa jinsi matendo ya mwili (roho waovu) yalivyoingia ndani ya nafsi na kuitawala.

MTU ALIYEKOKA

MWILI NAFSI ROHO

Uasherati, Upendo
Uchafu, Furaha
Ufisadi, Amani
Ibada ya sanamu Uvumilivu
Uchawi, Utu wema
Hasira, Fadhili
Uzinzi, n.k
Wivu
n.k.

Baada ya Yesu kuingia ndani ya mtu aliyeokoka, huwafukuza roho waovu wote watoke kwenye nafsi. Yesu huwaleta malaika zake kwenye nafsi ili waongoze na kuitawala nafsi.

MTU ALIYEOKOKA NA KUSHINDWA VITA

MWILI NAFSI ROHO

Uasherati, Upendo
Uchafu, Furaha
Ufisadi, Amani
Ibada ya sanamu Uvumilivu
Uchawi, Utu wema
Hasira, Fadhili
n.k.
wivu Uzinzi
n.k

Aliokoka roho waovu wakafukuzwa wote na Yesu. Yesu akaleta malaika kwenye nafsi. Mtu huyu alishambuliwa na roho ya uzinzi ambayo ilimshinda, hivyo imerudi kwenye nafsi. Sasa nafsi pamoja na kuwa malaika roho ya uzinzi nayo imeruhusiwa na mhusika hivyo ipo. Siku moja moja nayo itakuwa inpata nafsi inaushika usukani na kumwendesha huyu mtu.

Dawa ya hawa roho waovu waliokushinda siyo kutubu. Kutubu ni vizuri, unasamehewa hiyo dhambi uliyoitenda, lakini lile pepo la uzinzi, litakuwa bado limeushika usukani. Hivyo hapo kunahitajika kazi mbili zifanyike. Kwanza ni kutubu na kazi ya pili ni kufukuza huyo pepo atoke kwenye nafsi. Hapo yanahitajika maombi makali, ikiwezekana funga na kuomba. Mfukuze huyu pepo hadi usimwone tena kwenye nafsi, hapo ndipo utakuwa umemshinda. Bila hivyo huyo pepo ataendelea kukutumikisha.

Wakristo wanatumikishwa na roho waovu hasira, chuki, fitina, uchoyo, useng’enyaji, ubinafsi, umimi, uzushi, unyanyasaji, ulafi, na miungu wengine wengi ambao sikuwataja. Watendao mambo ya jinsi hii hawataurithi ufalme wa Mungu. Wakristo wa jinsi hii wao wanasema kuwa, hizi ni tabia zao. Hizi siyo tabia bali ni roho waovu wako ndani ya mhusika wanamlazimisha kutenda hayo. Hivyo umekuwa mtumishi wa roho waovu.

Posted in MAFUNDISHO |

MASHAMBULIZI KUTOKA ROHO WAOVU

Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake, nao hawakushinda, wala mahala pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na shetani, audanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye… kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari. Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu (Ufunuo 12:7 – 12).

Shetani hayuko hapa duniani kucheza. Yuko kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kwa hali na mali wewe usiingie mbinguni. Yeye anayo kazi moja tu, ya kupigana na wewe na akushinde. Yeye halali. Akikushindwa leo kesho anatafuta mbinu nyingine. Hivyo yako mashambulizi makali ya shetani, roho waovu mapepo na majini.

Mtu wa Mungu huwezi kuyashinda mashambulizi ya shetani bila kujifunza mbinu zake anazozitumia na huwezi kumshinda bila ya wewe kujifunza upiganaji. Wakristo wengi wameshindwa vita hii japokuwa bado wanaenda kanisani.

Baada ya mtu kuokoka, hupata passport ya kwenda mbinguni. Sambamba na passport hiyo Mungu humpa nguvu, uweza na mamlaka ya kumwezesha kupigana na shetani na kumshinda. Hivyo mkristo anatakiwa ajipiganie yeye mwenyewe na ashinde. Yesu ameshakupa passport ya kwenda mbinguni, hivyo ipiganie hiyo nafasi ili shetani asikumyang’anye, usipojipigania utaikosa mbingu.

Lakini pamoja na hayo, kuwa na nguvu, uweza na mamlaka, bila ya kuwa na ujuzi wa hali ya juu wa kuvitumia ni kazi bure kuwa navyo. Hili ndilo tatizo la wakristo, wanazo nguvu, uweza na mamlaka lakini hawajui mbinu ya kuvitumia. Ni sawa na raia asiyepitia mafunzo ya kijeshi, umpe mzinga, ndege ya kivita, n.k akapigane vita.

Shetani hushambulia kupitia njia kuu mbili. Njia ya kwanza ni kupitia roho waovu walioko ndani ya wazazi, na mababu zetu. Baada tu ya mtu kuzaliwa roho waovu walioko ndani ya wazazi na mababu huingia ndani ya mtu. Hii ni njia ya mapokeo, tunapokezana kutoka kwa wazazi. Wazazi walipokea kutoka kwa mababu. Hawa roho waovu tumeishi nao muda mrefu, hivyo wametutumikisha sana, sasa tumezoea kutumikishwa nao, maana wamekuwa nasi tangu kuzaliwa. Roho waovu hawa hata mtu baada ya kuokoka huendelea kumfuatafuata tu. Ni lazima wakufuate maana wamekuwa ni rafiki wa ukoo na familia yenu. Kama hutajua jinsi ya kupigana na hawa roho waovu wa mapokeo ni razima wakushinde tu. Hawa roho waovu wa mapokeo unaweza kuwashinda kwa kujifunza laana na kuivunja. Bila kuijifunza laana na kuivunja ni lazima wakushinde. (soma kitabu changu kiitwacho, ULIIVUNJA LAANA ULIPO AMINI?

Njia kuu ya pili ya shetani kushambulia ni kwa majeshi yake ya pepo yaliyoko katika ulimwengu wa roho yanayofanya mashambulizi ya kila siku mchana na usiku. Haya mashambulizi ni ya kawaida mashambulizi haya unayashinda kwa maombi ya kawaida lakini yawe yenye nguvu. Nikisema maombi ya kawaida nina maana ya kuwa, maombi ambayo siyo kuvunja laana.

Katika kitabu hiki tunaenda kujifunza mbinu anazozitumia shetani kutushambulia kupitia njia hii ya pili yaani mashambulizi ya kawaida. Sambamba na kujifunza mbinu za ushambuliaji anazotumia shetani, huwezi ukamshinda, bila ya wewe kuwa na mbinu madhubuti. Hivyo tutajifunza pia mbinu madhubuti za kumshinda. Nimetangulia kusema kuwa, utamshinda kwa maombi. Katika kitabu hiki sitazungumzia kuhusu maombi hayo bali tunaenda kujifunza mbinu za kumshinda shetani. Baada ya kuzijua mbinu hizo ndipo utaomba na kumshinda. Ukiomba bila kujua mbinu huwezi ukamshinda, ni sawa na kipofu kupigana na mtu mwenye macho, kipofu hataweza kushinda. (kama unataka kujifunza uombaji wenye nguvu, soma vitabu vyangu, MSINGI WA MAOMBI, KUNENA KWA LUGHA, NGUVU YA UFUNGAJI, UNAYO MAMLAKA.

• Mapigano ya mwili na roho

Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na roho na roho kushindana na mwili, kwa maana hizi zinapigana, hata hamwezi kufanya mnayotaka (Wagalatia 5:17).

Mtu ana mwili, nafsi na roho, mwili ni udongo. Mungu alifinyanga udongo akaupulizia pumzi ya uhai. Baada ya mtu kufa mwili hurudia hali yake ya udongo. Pumzi ya uhai ndiyo roho. Roho hii imetoka kwa Mungu, inayo tabia ya uMungu. Hii roho ndiyo mwanadamu mwenyewe atakayeishi milele, aidha mbinguni au Jehanamu kutegemeana na mtu mwenyewe alivyo hapa duniani.

Roho inayo tabia ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, kwa vile inajua kuwa isipompendeza Mungu itatupwa Jehanamu hivyo inajitahidi kumpendeza Mungu. Matendo ya roho yanaitwa tunda la roho.

Lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna sheria
(Wagalatia 5:22 – 23)

Mwili unataka kuifaidi dunia, maana unajua kuwa uko hapa duniani kwa muda tu na utarudi katika udongo. Roho hata kama itaenda mbinguni au jehanamu mwisho wa mwili hautabadilika. Hivyo mwili unataka kufanya matendo ya dunia hii ambayo hayampendezi Mungu, mwili hauna juhudi yoyote katika kuifanikisha roho iende mbinguni. Hivyo mwili unataka kufanya mambo yake, na roho nayo inataka ifanye mambo yake, hivyo mwili na roho vinapigana ili kila mmoja anayotaka ndiyo yafanyike.

Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu (Wagalatia 5:19 – 20).

Hivyo mwili unataka matendo ya mwili ndiyo yafanyike, roho inataka ifanye matendo ya roho. Katika kupigana huko anayeshinda ndiye mambo yake yanatendeka.

Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi roho ya mwanadamu ilikufa japo kuwa tunatembea. Hivyo mtu akabaki mwili na nafsi. Watu wakaendelea kuzaliwa wakiwa mwili na nafsi huku roho zao zimekufa. Baada ya mtu kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yake, hapo hapo hutokea badiliko la kiungu katika ulimwengu wa roho. Roho huhuishwa na kuwa hai, wakati huo huo mwili hufa japo kuwa tunatembea. Badiliko hili au tukio hili ndiyo huitwa kuokoka. Huku ndiko kuzaliwa mara ya pili, mara ya kwanza ulizaliwa mwili na mama yako na mara ya pili umezaliwa roho na Yesu. Hapo ndipo jina la mhusika huandikwa kwenye kitabu cha Uzima wa milele.

Na hao walio katika Kristo wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake (Wagalatia 5:24).

Roho na mwili vinapopigana katika mtu ambaye hajaokoka, roho lazima ishindwe maana imekufa. Hivyo mtu ambaye hajaokoka ni lazima atende matendo ya mwili, atake asitake. Roho na mwili vinapopigana katika mtu ambaye ameokoka mwili lazima ushindwe maana utakuwa umekufa. Hivyo mtu aliyeokoka atatenda matendo ya roho, ambayo ni tunda la roho.

Uwanja wa mapambano
(Msitari wa mbele katika vita)

Nafsi ndiyo sehemu ya ufahamu wa mwanadamu; sehemu ya uwezo wa kujitambua, ndiyo akili (mind). Baada ya udongo kupuliziwa pumzi ya uhai ndipo nafsi ilitokea, kikawa kiumbe hai kinachojitambua. Mwanadamu ataingia mbinguni na ufahamu wake akijitambua. Ni hivyo hivyo hata watu watakaotupwa Jehanamu watatupwa na ufahamu wao, watakuwa wanajitambua.

Kazi ya nafsi katika mtu ni nini? Ili niweze kulijibu swali hili vizuri, hebu nimfananishe mtu na gari. Gari lina kiungo kimoja kiitwacho usukani. Usukani katika gari ni chombo ambacho kinageuza gari mwelekeo, gari liende kushoto, kulia, mbele, n.k.

Nafsi nayo katika mtu inafanya kazi hiyo hiyo. Mtu anafanya mambo mengi sana; anasema mengi, anafikiri mengi; n.k yote haya yanawezeshwa kufanyika na nafsi. Hii ndiyo kazi ya nafsi kuwezesha mambo yote yatendeke anayoyatenda mtu.

Usukani kwenye gari, japo kuwa unaliwezesha gari liende kushoto, kulia, hauwezi kuamua gari liende kushoto, kulia, mbele au vinginevyo. Usukani hauamui gari kukata kona. Anayeamua gari likate kona ni dereva anayeliendesha hilo gari, yeye anakotaka kwenda ndiko gari litakwenda. Na hivyo hivyo hata nafsi. Nafsi haiwezi kuamua kitu gani mtu atende. Tumeona habari ya roho na mwili kupigana. Hawa hupigania nini hasa? Hawa hupigania usukani, nani aushike usukani ili amwongoze mtu kutenda matakwa ya aliyeushika usukani. Hivyo usukani ukishikwa na mwili mtu atalazimika kutenda matendo ya mwili na kama usukani ukishikwa na roho basi mtu atalazimika kutenda tunda la roho.

Mtu ambaye hajaokoka roho yake imekufa hivyo watakapopigana roho na mwili, roho atashindwa. Roho atashindwa kwa sababu amekufa. Mwili atashika usukani, hivyo mtu huyu ataishi maisha ya dhambi. Hata akijiunga kwenye dini na kufuata taratibu zote za dini, hata akipata elimu ya juu ya neno la Mungu na hata akipata wadhifa mkubwa kwenye dini hiyo, yote hayo hayatamsaidia kuishinda dhambi.

Mtu ambaye ameokoka roho na mwili wakipigana, mapigano hayo roho atashinda. Roho ataushika usukani hivyo mhusika atalazimika kutokutenda dhambi.

Uwanja wa vita wa mapambano, ndiyo mstari wa mbele wa mapambano, kwenye vita vyenyewe, kwenye mapigano makali kati ya Mungu na Shetani, wakati wakipigania nani amchukue mtu. Uwanja wa mapambano hayo huwa ni kwenye nafsi. Vita yote ya mtu aende Jehanamu au aende Mbinguni, hupiganiwa ndani ya mtu mwenyewe kwenye nafsi. Wakristo wengi hawalijui hili ndiyo maana wamekuwa wakristo wakushindwa na shetani. Hapa inakuwa ni tofauti na yule mfalme wa uajemi aliyezuia majibu ya maombi ya Danieli. Haya majibu yalikuwa yanatoka mbinguni, shetani akamzuia malaika njiani, Mikaeli alikuja akapigana naye. Hawa walikuwa nje ya Danieli. Kutokana na hili wakristo wengi hata wanapopigana na shetani, maombi yao mapigo wanayaelekeza angani kuelekea mbinguni. Kupigana kwa namna hiyo ni kwa wapiganaji wasio na ujuzi wa kazi ya kuomba, hawana elimu ya kupigana na shetani. Adui yuko mstari wa mbele, hayuko angani, mstari wa mbele ni kwenye nafsi. Mapambano yote yanayohusu maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu, hufanyika kwenye nafsi.

Nchi ya Marekani ilipotaka kuipiga nchi ya Afghanistan ilitafuta rafiki aliyekaribu na Afghanistan ili kiwe kituo cha kuongozea mapambano. Hivyo hivyo Mungu na Shetani wanapopigania kumchukua mtu, huweka vituo vyao karibu na uwanja wa mapambano mwili na roho tayari wako uadui, hivyo shetani huja kushirikiana na mwili kwa sababu nia yao inafanana. Mungu naye huweka kituo chake kwenye roho kwa vile wote nia yao inafanana.

Hii vita hugeuka badala ya mwili na roho kupigana, sasa wanaopigana huwa ni Mungu na Shetani sasa kwenye habari ya matendo ya mwili yaliyo andikwa kwenye Wagalatia 5;19 – 21, badala ya kusomeka matendo ya mwili sasa husomeka, Basi mapepo ya shetani ni uasherati, uchafu, n.k. hivyo hata upande wa Mungu badala ya kusomeka tunda la roho, badala yake inasomeka, Malaika wa Mungu. Nimeweka isomeke hivyo kwa sababu sasa siyo vita ya mwili na roho tena, bali sasa ni vita ya Mungu na Shetani. Hivyo badala ya matendo ya mwili sasa ni mapepo ya shetani, na badala ya tunda la roho sasa ni malaika wa Mungu.

Mungu na Shetani hupigania mtu, anayeshinda anaushika usukani. Kama ni shetani basi mapepo wa shetani huingia kwenye nafsi na kuushika usukani. Na kama aliyeshinda ni Mungu basi malaika wa Mungu huingia kwenye nafsi na kuushika usukani.

Usukani wa gari uko kwenye chumba chenye kiti kipana wanaweza kukaa hata watu watatu japo kuwa dereva aliyeushika usukani atakuwa mmoja tu. Ni hivyo hivyo hata kwenye nafsi ni sehemu ambayo wanaweza kukaa mapepo wengi au malaika wengi, japo kuwa anayeushika usukani anakuwa ni mmoja. Lakini kwa vile wanaokuwemo kwa wakati mmoja ni malaika wengi au mapepo wengi, hivyo hupokezana kuushika usukani leo huyu kesho yule au asubuhi yule, jioni huyu na usiku mwingine anaushika, n.k.

Kama mshindi ni shetani siyo lazima shetani aweke mapepo wake wote ndani ya mtu mmoja. Shetani humwangalia mtu mwenyewe alivyo na kuweka mapepo kadhaa. Mtu akiwekewa mapepo mengi hataziweza kazi zote za mapepo hayo, maana kazi za shetani ni ngumu. Mtu mmoja yeye awe jambazi, mchawi, mgomvi mganga wa kienyeji, shoga, n.k haitakuwa rahisi kwa huyo mtu kuziweza kazi hizo.

Kama mshindi ni Mungu, Mungu huweka malaika zake wote ndani ya mtu mmoja kazi za Mungu ni nyepesi mtu mmoja anaweza kuzimudu zote bila matatizo. Huyo mmoja atakuwa na upendo, furaha amani, utu wema, n.k. na akaziweza.

Mtu ambaye hajaokoka amejaa mapepo kwenye nafsi yake, hivyo mapepo humtumikisha. Mtu anapoamua kuokoka Yesu huingia ndani yake na kuyafukuza mapepo yote. Baada ya kuwafukuza mapepo au roho waovu wote, Yesu huweka malaika wake. Hivyo huyo mtu aliyeokoka kuanzia hapo huanza kuishi maisha matakatifu. Hawezi tena kunywa pombe maana roho iliyokuwa inamwongoza kunywa pombe sasa haiko; hawezi tena kufanya uzinzi, uchoyo, kiburi, ulafi, n.k.

Huyu ndiye mtu wa Mungu anayekwenda mbinguni. Wakristo wa leo wameokoka, wamejazwa Roho Mtakatifu na wananena kwa lugha, lakini bado wana roho waovu wakijidhihirisha. Ni Ukristo gani huu? Ni wokovu gani huu? Mkristo huku ni mzinzi, jambazi, mchoyo, chuki, wivu, mgomvi, hasira, kujikweza, umimi, ubinafsi, kiburi, ubaguzi wa rangi na kabila, n.k kama kweli Yesu aliwafukuza hawa roho waovu ulipookoka na wakatoka ndani yako na malaika wakaingia na kukaa na kuanza kukuongoza, je, imekuwaje tena wewe bado roho waovu wako ndani yako? Wewe unajidanganya kuwa hiyo ni tabia yako! Hiyo siyo tabia bali ni roho waovu. Usifikiri kwenda mbinguni ni kujiunga katika dini na kuwa na bidii ya kwenda kanisani. Kwenda mbinguni ni vita. Vita hiyo haiko kanisani bali iko ndani yako, unatembea nayo, unalala nayo, kila mahali unakokwenda vita unayo ndani yako, unatakiwa uishinde.

Kanisani ni mahali pa kwenda kuongeza ujuzi wa kupigana. Mtu wa Mungu hebu jiulize mara mbili tatu, kuhusiana na wokovu wako, je, kwa nini roho waovu bado wako ndani yako wanakuongoza kutenda mambo yaliyo kinyume na Mungu? Kumbuka watu watendao mambo ya jinsi hiyo roho waovu uliowaruhusu waingie ndani yako, unawapenda wanakutumikisha, hivyo unawatumikia. Umeokoka na kujazwa Roho Mtakatifu lakini bado unatenda dhambi za uzinzi, wizi, rushwa, n.k. kwa nini mkristo aliyeokoka anatenda dhambi?

Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao (Mathayo 18:20).

Neno la Mungu linasema kuwa, watu wawili watatu wakikutana kwa ajili ya Mungu. Mungu naye atakuwa mahali pale ili kulithibitisha jina lake kuwahudumia wote walioko pale, hivyo Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu, malaika wanakuwepo pale. Nguvu, uweza na mamlaka ya Mungu vinakuwa pale.

Watu wanapokuwa wamekusanyika kwa ajili ya Mungu, Mungu anakuwa pale ili kuhakikisha kuwa kila mtu aliyefika pale amehudumiwa, bila ya hata mmoja aliyehudhuria kubaki bila ya kupata huduma. Ingawaje kila mtu hupokea sawasawa na kujitoa kwake. Wengine hupokea kikubwa wengine hupokea kidogo.

Ninamkumbuka mtu mmoja alikuwa mlevi sana wa pombe, mkristo, alikuwa anasali kanisa la Roman Catholic. Alikuwa anapenda kuhudhuria mikutano ya Injili ya hadhara inayohubiriwa na mhubiri Moses Kulola. Mtu huyu alikuwa anayasifu sana mahubiri ya Mhubiri huyu, Mhubiri Moses ana nguvu za Mungu kweli kweli, mimi sitaki kuokoka, lakini nikihudhuria kusikiliza mahubiri yake baada ya mkutano kuisha huwa siwezi kunywa pombe kabisa kwa muda wa miezi miwili, mitatu, ndipo huanza kuwa na hamu ya kunywa pombe tena.

Huyu mtu hakutaka kuokoka, lakini alikuwa anapenda kuhudhuria kwenye kusanyiko la mkutano wa Injili. Mahali hapo Mungu alikuwapo ili awahudumie watu wote waliokuwepo. Hivyo utake usitake ili mradi uko pale lazima utahudumiwa na Mungu, hata kama wewe huzitaki hizo baraka lakini madamu upo pale lazima utaambukizwa hizo baraka. Huyu alikuwa anaambukizwa baraka ambazo alikuwa anakaa nazo mwendo wa miezi mitatu.

Shetani katika utendaji wake naye huiga utendaji kama wa Mungu. Hivyo naye, mahali wawili watatu wamekusanyika kwa ajili ya shetani, shetani naye yuko pale kwa ajili ya kuwahudumia. Hapa ina maana kuwa, shetani, mapepo na roho waovu wanakuwa pale kwa ajili ya kuwahudumia wote watakaokuwa pale.

Roho huhama na kuingia ndani ya watu wakitokea ndani ya watu wengine ambao tayari wanao, aidha roho huhama na kuzagaazagaa wakitafuta watu wawaingie. Utendaji huu wa roho waovu kuhama kutoka mahali na kwenda mahali huitwa uhamisho wa roho (Transference of spirits) kiswahili kizuri ni Uambukizaji wa roho.

Hii ndiyo njia kuu ya pili ambayo shetani huitumia kuwashambulia watu. Hii njia ndiyo hutumika kwa mashambulizi ya kawaida ya kila siku ya shetani. Njia kuu ya kwanza nimesema ni ile ya mapokeo kutoka kwa mababu, ambapo nilisema kuwa roho waovu waliokushambulia kupitia njia hii utawashinda kwa kujifunza kuhusu laana na kuzivunja. Mapepo au roho waovu waliomshambulia mtu kwa njia ya kuambukizwa utawashinda kwa maombi ya kawaida yasiyokuwa ya kuvuja laana. Maombi ya kawaida, lakini yawe ni yenye nguvu.

Kutokana na hili mtu anaweza kuwa na pepo aina moja wengi, lakini wameingia kupitia njia zote mbili, njia ya mapokeo na ile ya kuambukizwa. Utakapopigana nao kwa maombi ya kawaida, wale waliokuja kwa njia ya kuambukizwa watasikia hayo maombi wataondoka, lakini wale waliokuja kwa njia ya mapokeo hawatasikia hayo maombi hivyo hawataondoka. Hawa huondoka kwa kujifunza laana na kuivunja.

Kwa nini hawawezi kuondoka? Hili swali linajibu refu sana, kwa vile somo letu halihusu roho walioingia kwa mtu kwa njia ya mapokeo bali linahusu roho waovu waliomshambulia mtu kwa njia ya mashambulizi ya kawaida, hivyo sitalijibu swali hili bali ukitaka kuelewa soma kitabu changu kinachoitwa, uliivunja laana ulipoamini?

Mungu huhudumia watu wake kwa kupitia watumishi wake mbalimbali, makanisa, mikutano, n.k. ni hivyo hivyo na shetani naye anasambaza mapepo yake ili yawashambulie watu kupitia watumishi wake mbalimbali, wengine wanajijua kuwa ni watumishi wa shetani, wengine wanatumika bila kujijua. Shetani pia anavyo vituo mbalimbali vya kusambazia mapepo yake. Kama vile, vilabu vya pombe, kumbi za starehe, sinema za ngono na za mauaji, magazeti, vitabu, nyumba za kulala wageni, n.k.

Neno la Mungu linasema,

Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki, wala hakusimama katika njia ya wakosaji wala hakuketi barazani pa wenye mizaha (Zaburi 1:1)

Shauri la wasio haki ni kusanyiko lililokusanyika kwa ajili ya shetani. Njia ya wakosaji na baraza la wenye mzaha pia ni mikusanyiko iliyokusanyika kwa ajili ya shetani. Mungu anajua kabisa kusanyiko lolote la watu waliokusanyika kwa ajili ya shetani, shetani, mapepo na roho waovu watakuwa pale, ili kuwahudumia watu wote watakao kuwa pale. Hivyo ndiyo maana Mungu amekukataza usiende katika kusanyiko lililojikusanya kwa ajili ya matendo ya shetani.

Mahali wazinzi wawili watatu wamekusanyika kwa ajili ya uzinzi, pepo la uzinzi liko pale kwa ajili ya kuwahudumia watu wote watakaokuwa pale; mahali wawili watatu wamekusanyika kwa ajili ya ulevi, pepo la ulevi liko pale kwa ajili ya kuwahudumia watu wote watakaokuwa pale. Ni hivyo hivyo hata katika mikusanyiko mingine yote.

Watu baada ya kuokoka Yesu aliingia ndani yao, aliwafukuza mapepo na roho waovu wote. Wakristo kwa uzembe na kutokufahamu neno la Mungu wamekuwa wakiendelea kukaa kwenye mikusanyiko ya kishetani, wameendelea kukaa kwenye mabaraza ya wenye mizaha, wameendelea kusimama kwenye njia za wakosaji, wameendelea kwenda kwenye mashauri ya wasiyo haki. Huko kuna mapepo na roho waovu wanakungoja kukuhudumia. Huko utaambukizwa mapepo.

Mtu mmoja ameokoka, kabla ya kuokoka alikuwa mlevi sana, sasa anasema kuwa, yeye ataendelea kwenda kwenye ile bar aliyokuwa ananywea pombe, anasema anakwenda pale ili akutane na rafiki zake wa zamani ambao bado walevi ili awashuhudie neno la Mungu pale bar. Yeye anasema hatakunywa pombe atakuwa anakunywa soda.

Mimi nakwambia kuwa mkristo wa namna hii ataishia kurudi kunywa pombe tena. Kwenye bar ni kwenye kituo cha shetani cha kusambaza mapepo ya ulevi. Pepo la ulevi liko pale kwa ajili ya kuwahudumia wote watakaokuwepo pale.

Msichana mmoja alikuwa na rafiki yake. Huyu msichana akaokoka. Rafiki yake alikuwa kahaba. Msichana aliyeokoka alikuwa bado anaendelea kuambatana na msichana kahaba katika safari zake za ukahaba, kwa misingi ya kwamba anamsindikiza rafiki yake lakini yeye ameacha ukahaba. Wanapofika kwa hawala wa kahaba yule, msichana mlokole anakaa pembeni kidogo. Kahaba na hawala yake wanaanza kuongea mambo yao ya uzinzi. Wanaongea wanafurahi na kucheka. Huyu mlokole kwa aibu ya kuogopa lawama kwa rafiki yake ili asionekane vibaya, kuwa amedharau maongezi yao, yeye ameamua kuwa asiongee wala asichangie kitu chochote, bali wanapocheka yeye ameaamua kuwa awe anakenua meno pekee. Hivyo wakati mazungumzo yanaendelea yeye yuko kimya, lakini wanapocheka yeye naye mlokole anakenua meno.

Mimi ninasema kuwa huyu msichana hatafika popote baada ya muda ataanza uzinzi, hata kama atakuwa ameshajazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha. Lakini kwa nini ajikute amerudi kwenye uzinzi tena?

Wewe mkristo uliyeokoka na unanena kwa lugha, umejikuta unatenda dhambi tena, umejikuta ni mlevi, umejikuta ni mzinzi, mwizi, jambazi, mseng’enyaji, una wivu, mchoyo, mwasherati, ubinafsi, mshirikina, chuki, n.k umeshambuliwa na shetani na amekushinda, hivyo sasa unamtumikia. Mbinguni huendi maana watendao mambo ya jinsi hii hawataurithi ufalme wa Mungu.

Yesu alifukuza hao pepo uliokuwa nao ulipookoka na walitoka wote. Hapo haikuwa mwisho wa safari. Hapo ndiyo ilikuwa mwanzo wa safari. Biblia inasema, yeye ashindaye. Wewe ulitakiwa undelee kupigana na hawa roho waovu ili wasirudi tena na uendelee kuwashinda. Lakini sasa wamekupiga na wamekushinda. Sasa unawatumikia.

• Mashambulizi kupitia milango ya fahamu

Shetani anapomshambulia mtu, hutupa mishale yake ndani ya mtu huyo kupitia katika milango mitano ya fahamu, yaani kuona, kusikia, kugusa, kuonja na kunusa.
Mishale ya shetani ndiyo hao mapepo huingia ndani ya mtu kupitia hiyo milango ya fahamu.

Kuona

Siku moja nilikuwa na safari asubuhi mapema sana wakati kulikuwa bado giza giza. Niliondoka kwenda kituo cha magari ya abiria. Kutoka nyumbani nilipita njia za mkato. Nilipita kichochoro fulani katikati ya nyumba na nyumba, ghafla niliona mwanamke na mwanamume wakifanya zinaa pale niliudhika sana, nikageuka na kuamua kupita njia nyingine.

Nilikuwa ninakwenda kuhubiri Injili mji wa mbali. Nilifika safari yangu. Usiku wa manane, nilikuwa ninatafakari mambo mbalimbali. Wakati nikitafakari nilistukia ile picha ya tukio la zinaa nililoliona, ikanijia katika fahamu zangu. Niliudhika sana. Ile picha iliendelea kuja mara kadhaa, na iliendelea muda wa siku kadhaa kuja kwenye fahamu zangu.

Mimi siyo kamera ya sinema, niwe nimelichukua hilo tukio. Kwenye tukio hilo la uzinzi kulikuwepo shetani na mapepo yake tayari kuwahudumia wote watakaokuwepo mahali hapo. Hivyo mimi nilipoona tu tukio hilo, wale roho waovu waliingia ndani yangu kupitia macho yangu. Na pale usiku wa manane nilipoiona tena ile picha, hapo ilikuwa ni yule pepo aliyeingia ndani yangu alitafuta jinsi ya kuingia ndani ya nafsi. Nilipoendelea kuiona ile picha kwa muda wa siku kadhaa, ndivyo hivyo hivyo huyo pepo alivyokuwa akiendelea kujitahidi kuingia kwenye nafsi, ili aushike usukani.

Kusikia

Siku moja nilikuwa nasafiri katika nchi ya Uganda nilikuwa kwenye basi. Ndani ya basi kulikuwa zikiimbwa nyimbo kwenye radio. Nyimbo zile sikuzijua tafsiri zake, zilikuwa katika lugha ya makabila ya huko Uganda. Mimi ni msukuma wa Mwanza, Tanzania kabila za Uganda sikuzielewa. Wakati muziki ukiendelea ulikuja wimbo mmoja ambao kwenye kibwagizo chake uliimba kwa lugha ya kiswahili ambayo niliuelewa tafsiri yake. Wimbo ule ulisema habari za baba mmoja mzee mnene sana, anafanya tendo la ngono na msichana binti mdogo umri wa mjukuu wake. Wimbo huu haukunipendezea kuusikiliza. Baadaye wimbo huu uliisha zikafuata nyimbo zingine ambazo zilikuwa zote za kiganda, hivyo sikuelewa tafsiri za nyimbo hizo. Nilifika safari yangu. Baada ya siku chache niliusikia wimbo huo, hicho kibwagizo tena kikiimbwa ndani yangu. Mimi siyo kinasa sauti bali ile roho ya huo wimbo ndiyo ilikuwa imeingia ndani yangu.

Musa alipotuma wajumbe kwenda kuipeleleza nchi ya Kanaani, wajumbe kumi na mbili kila kabila la Israeli mjumbe mmoja mmoja. Kati yao kulikuwa na Yoshua na Kalebu.

Kisha BWANA akanena na Musa. Akamwambia, tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya kanaani, niwapayo wana wa Israeli (Hesabu 13:1 – 2)

Baada ya Musa kuwatuma, walienda wakaipeleleza hiyo nchi wakarudi. Waliporudi walileta habari ya kuwavunja moyo watu, habari ya kuwaogopesha watu. Wana wa Israeli walivunjika moyo na kuogopa kuingia nchi ya Kanaani.

Wakarejea baada ya kupeleleza nchi wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa Wana na Israeli… wakawaletea habari wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi. Wakawaambia wakasema. Tulifika ile nchi uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake. Lakini watu wanaokaa ile nchi ni hodari, na miji yao ina maboma nayo ni makubwa sana, na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko. Kalebu akawauliza watu mbele ya Musa akasema, natupande mara, tukaitamalaki, maana twaweza kushinda bila shaka. Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea Wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, ile nchi tuliyoipita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi (Hesabu 13:25 – 33).

Wana wa Israeli wakasikia habari ambazo ziliwapa hofu. Hofu ni sumu ya imani, hivyo wana wa Israeli wakaingiwa hofu kuu.

Wana wa Israeli wakaingiwa na roho ovu ya hofu iliyokuwa tayari imeingia ndani ya wapelelezi. Baada ya kusikia hayo ilitokea nini?

Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; wakatoka machozi usiku ule kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni, Mkutano wote wakamwambia, ingekuwa heri kama tungelikufa katika Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. Mbona BWANA anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake wetu na watoto watakuwa mateka. Je, afadhali turudi Misri. Wakaambiana, tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri. Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya mkutano wa kusanyiko la Wana wa Israeli (Hesabu 14:1 – 5).

Hapa tayari pepo la hofu lilikuwa limekwisha kuwashambulia Wana wa Israeli kupitia kusikia. Wale wapelelezi walikuwa wameingiwa na hilo pepo la hofu, liliwaingia kupitia kuiona ile nchi, hivyo pepo lilihama na kuwaambukiza mkutano wote wa Wana wa Israeli kupitia kusikia. Tunaona kuwa Yoshua na Kalebu wao lile pepo la hofu halikuwa limewaingia wao walikuwa mashujaa, wao walimwamini Mungu. Walijaribu kuwatoa hofu na kuwatia moyo wa kishujaa, lakini Yoshua na Kalebu walikuwa wamechelewa, maana kwenye nafsi za Waisraeli tayari roho wa hofu alikuwa ameshaingia na kushika usukani na alikuwa ameshaanza kuwaendesha tayari.

Maneno ya Yoshua na Kalebu hayangeweza kuwatoa pepo wa hofu ambao tayari walikuwa wameingia.

Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, walikuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa Wana wa Israeli wakasema, nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wenyeji wa ile nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaongope. Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe (Hesabu 14: – 10).

Wana wa Israeli roho ya hofu ilikuwa imeushika usukani tayari ikiwaendesha. Huyo alikuwa ni shetani mwenyewe ameshawawahi Wana wa Israeli, ameshawashinda. Yoshua na Kalebu juhudi zao za kuwashawishi Wana wa Israeli, ilikuwa ni sawa na kutwanga maji katika kinu. Kwa vile shetani mwenyewe ndiye aliyekuwa ameshika usukani tayari, hivyo shetani aliamrisha Yoshua na Kalebu wapondwe mawe. Yoshua na Kalebu walifikiri kuwa bado wanaongea na watu wa Mungu, kumbe tayari walikuwa wameshakuwa watumishi wa shetani.

Wakristo wako kanisani wanafikiri bado ni watu wa Mungu kumbe tayari wao ni watumishi wa shetani, ndani yao kuna roho waovu ambao ndiyo wanawaongoza. Haiwezekani kabisa mtu wa Mungu anayekwenda mbinguni, hapo hapo bado anaongozwa na roho waovu wa uzinzi, ujambazi, kujikweza, ubinafsi, ulafi, wivu, hasira, kutokutii neno la Mungu, fitina, n.k. wakristo wanaoleta vurugu kanisani hivi ni roho gani inayowaongoza kuleta vurugu hizo? Hao walishashindwa vita vya kiroho mapepo yaliyomo ndani yao ndiyo yameushika usukani, ndiyo tabia zinazojidhihirisha kwa nje, wanasema, hasira ni tabia yangu, Mungu ataitoa polepole. Unajidanganya wewe mwenyewe, hilo ni pepo la hasira unatakiwa ulishinde. Wengine wanasema, ubinafsi, uchoyo, chuki, n.k. hizi ni tabia tu na wala haziwezi kuwazuia kwenda mbinguni. Sasa nakwambia kuwa, watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurirthi Ufalme wa mbinguni kabisa.

Mungu alikasirishwa na Wana wa Israeli akawaua jangwani wote wale wazee wa miaka ishirini kwenda juu kwa sababu walishindwa kumwamini Mungu, isipokuwa Yoshua na Kalebu ambao walikuwa hawakuingiwa yule roho wa hofu. Mungu akasema Yoshua na Kalebu pamoja na watoto walio na umri wa chini ya miaka ishirini, ndiyo watakaoingia. Hawa watoto wao walikuwa hawapo katika mkutano huo, walikuwa bado hawajafikia umri wa kupigana vita, wao hawakuwa wameingiwa na huyo roho wa hofu. Hivyo Yoshua na Kalebu walichofanya, walikwenda kuwakusanya wale watoto na kuwapandikizia roho ya ushujaa iliyokuwemo ndani yao. Watoto wakawa na roho ya ushujaa na waliingia Kanaani bila woga wala hofu na walishinda.

Njia hii ya kusikia, shetani amewashambulia wakristo wengi na akawaweza. Shetani amewashinda wakristo wengi katika maeneo mbalimbali ya maisha yao. Wengi wameingiwa na roho waovu na wakaanza kutumikishwa katika tabia mbovu za kishetani. Wengine Mungu aliwapa maono fulani mazuri ili wafanye shughuli fulani ya maendeleo yao ya maisha. Kabla ya kutekeleza waliamua kuomba ushauri kwa watu, watu waliwavunja moyo, watu waliwapa hofu kuwa hawataweza. Roho ya hofu ilitoka ndani ya washauri na iliwaingia na waliogopa kuifanya shughuli hiyo ambayo Mungu alikuwa amewaonyesha..

Mungu amekuwa akiwapa watu wake mbalimbali maono mengi kwa ajili ya kazi yake na kwa ajili ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya maisha yao. Walishirikisha watu ili wapate ushauri, ushauri umekuwa ukitolewa wa kuwavunja moyo, hivyo wameshindwa kuyatekeleza maono hayo. Maono hayo umepewa na Mungu kwa nini unatafuta ushauri? Je, humwamini Mungu?

Mtu wa Mungu, shetani huwashambulia watu kupitia roho waovu ambao wako ndani ya watu wengine kwa kupitia kusikia. Wale Wana wa Israeli waliwaangalia wale wapelelezi kwa mtazamo wa wengi wape. Hivyo waliangalia idadi wakaona wale wapelelezi kumi ndiyo wawasikilize, wakaona wale wapelelezi wawili ni waongo, Mungu hatendi kwa mitazamo ya watu, ya kwamba, wengi wape. Mungu haongei na wengi bali Mungu hutumia mtu mmoja au watu wachache. Kuna wasichana ambao walipata wachumba, lakini wakatafuta ushauri wa watu, washauri kumi wakasema mchumba hafai, washauri wawili walisema mchumba anafaa. Wao walifuata ushauri wa wengi wape, kumbe kwa wengi wape ndiko Mungu hakuwepo.

Mtu wa Mungu unapokuwa unaongea na mtu yeyote yule hakikisha unapambanua yale anayoyaongea, maana roho waovu wakati wowote wanatafuta kuingia ndani ya watu wengine kutoka kwa watu wengine. Hili ni pamoja na unapokuwa unasikiliza mahubiri kutoka mhubiri yeyote yule. Wakati mhubiri anahubiri Mungu humtumia mhubiri ili awahudumie watu wanaomsikiliza mhubiri na wakati huo huo shetani naye hutaka kumtumia mhubiri huyo huyo ili naye awahudumie wale wanaomsikiliza huyo mhubiri. Hivyo unaposikiliza neno la Mungu usimeze kila kitu, chambua na kupambanua mifupa tupa, minofu kula.

Mhubiri anaweza kuhubiri vizuri sana neno la Mungu lakini akatumia muda mwingi katika mahubiri yake kujisifu jinsi yeye alivyo mhubiri mzuri au akasifu kanisa lake lilivyo zuri. Waumini wakiondoka pale wataondoka na shida zao walizozileta kanisani ili Mungu akutane nazo, zitakuwa bado zipo. Mungu atakuwa hakukutana nazo, kwa sababu mhubiri hakumwinua Yesu bali alijiinua yeye na dini yake, na kwa vile mhubiri au dini yake havikufa msalabani, hivyo vimeshindwa kukutana na shida za watu. Watumishi wa Mungu haipo sababu ya kujisifu sisi wakati tunahubiri, hebu tumhubiri Yesu peke yake. Tumwinue Yesu peke yake.

Mashambulizi kupitia kusikia ndiyo njia inayotumiwa zaidi na shetani. Hata Mungu ndiyo njia kubwa zaidi anayoitumia. Imani huja kwa kusikia.

Kugusa.

Kuombea au kubariki kupitia kugusa, roho huhama kutoka kwa anayeomba kwenda kwa anayeombewa. Je, wewe unazo roho gani ndani yako? Hivyo roho njema na roho waovu wote waliomo ndani ya mwombaji huhamia kwa anayeombewa. Unapomwombea mtu baraka fulani wakati wewe huna hiyo baraka, ujue hakuna kitu kinachoenda kufanyika. Huna upako unaombea mtu upako!

Watumishi wa Mungu ni muhimu kuishi maisha matakatifu ili usiingiwe na roho waovu na ukaanza kuwaambukiza watu wa Mungu wasio na hatia. Unapoweka mkono juu ya mtu ili kumwombea au kumbariki, katika ulimwengu wa roho hutokea kitu halisi. Tendo hilo siyo maagizo tu. Isaka alipozeeka sana alipokuwa karibu na kufa alitaka kumrithisha Esau baraka zote zilizokuwa ndani yake. Yakobo kwa kutumia ujanja akawa amebarikiwa yeye badala ya Esau. Esau alipokuja aliambiwa kuwa baraka zimeisha. Kwa nini zimeisha? Isaka alikuwa anakufa hivyo alikuwa anahamisha baraka zote kabisa, hivyo alikuwa amezihamishia zote kwa Yakobo. Hata kama Isaka angeamua kumwekea mikono Esau halafu akaomba kwa kutumia maneno yale yale aliyoyasema alipokuwa akimwombea Yakobo, hakungefanyika mbaraka wowote ule, lingekuwa igizo lisilo na maana. Roho wa mbaraka alikuwa ameishahamia kwa Yakobo.

Tofauti na Isaka unapomwombea mtu baraka kwa sasa ambapo wewe huhamishi baraka zote kwa sababu bado unaendelea kuishi na bado unahitaji kuwaombea watu wengine, bado hata wewe unazihitaji, kwa jinsi hii zinaondoka badhi na wewe unaendelea kubaki nazo, akija mwingine naye unamwombea, bado unaendelea kubaki nazo zingine. Isaka alikuwa anahamisha zote ndiyo maana ziliisha.

Watu wa Mungu sasa hivi tuko kwenye kipindi ambacho shetani amejifanya malaika wa nuru. Hivyo anao watumishi wake ambao amewaingiza kwenye kazi ya Mungu. Pia anayo makanisa ya Kikristo yanayomtumikia shetani. Ni kipindi cha kujihadhari sana na mambo ya kuwekewa mikono kila unapoona mhubiri amehubiri na kukusisimua. Wakristo wengi kwa kutokufahamu wamejikuta wamebeba roho za kigeni. Sasa hivi siyo kipindi cha kutegemea uombewe na kuwekewa mikono. Ni kipindi unachotakiwa ujifunze neno la Mungu. Neno la Mungu likijaa kwa wingi ndani yako omba lolote nawe utapewa.

Maelezo hayo kuhusu shetani anavyoshambulia kupitia milango ya fahamu yanatosha kukupa mwanga. Sitazungumzia milango ya fahamu kuonja na kunusa.

Mtu wa Mungu roho waovu wanapoingia ndani ya nafsi yako unawaona kabisa. Kama mimi nilivyosikia wimbo kwa siku kadhaa huo wimbo uliendelea kusikika tena ukiimba ndani yangu. Unaona hapa niliusikia. Pia kama nilivyoona tendo la ngono siku kadhaa niliendelea kuiona hiyo picha tena ndani yangu. Huko ndiyo jinsi roho waovu unavyoweza kuwaona. Unapokumbuka kwenye fahamu zako kitu ulichokiona zamani, huko kukumbuka ujue ni ile roho ya kile kitu ulichokiona huko nyuma. Hivyo ndivyo jinsi ya kuwaona hao roho waovu wanavyokushambulia. Mbali na hivyo kule kuwaza kwenye fahamu jambo fulani ikiwa jambo hilo liko kinyume na neno la Mungu, basi fahamu ya kuwa hao ni roho waovu wanakushambulia.

Roho waovu wanapomshambulia mtu, mtu mhusika huwaona na kuwahisi. Hakuna roho ovu yeyote anayeweza kuingia ndani au anayeweza kumshambulia mtu bila ya mhusika kumwona. Baada ya roho waovu kuingia ndani yako, ndipo huanza mashambulizi. Kama ni roho wa dhambi wanaanza kukushawishi au kukutamanisha kutenda dhambi. Ukiona hivyo ujue kuwa umeshaingiliwa na roho ya kigeni ambayo sasa imeanza kupigana na wewe ili ikushinde utende dhambi. Hapo sasa ndipo kipindi cha vita ya kiroho kilipo. Vita vya kiroho unavyo visikia ndicho kipindi hicho sasa. Hapo usingoje hadi uitende hiyo dhambi. Ukishatenda dhambi ina maana umeshashindwa vita, hata ukija kuitubu hiyo dhambi haisaidii kitu. Sawa utakuwa umesamehewa dhambi hiyo, lakini tatizo utakuwa hujalimaliza, maana roho waovu watakuwa bado wako kwenye nafsi na pamoja na kwamba umetubu. Roho waovu hawataondoka kwenye nafsi kwa sababu ya kutubu, roho ovu huyo ataendelea kukupeleka kutenda dhambi, hivyo utakuwa mkristo wa kuendelea kutumikishwa katika hiyo dhambi. Dawa yake ni kupigana naye huyo roho ovu kwa maombi, mara tu unapoanza kumwona roho ovu ameingia ndani yake. Usimlee wala usimdekeze. Ukitamani dhambi fulani, ujue hapo siyo wewe, bali ujue kuwa umeingiliwa na roho wa kigeni, ujue kuwa roho ovu anakushambulia. Hivyo ndivyo jinsi ya kuwaona hawa roho waovu walioingia ndani yako. Hivyo unao muda wa kutosha kabisa wakupigana na roho waovu kabla hawajakushinda na kuanza kuletea madhara kwako. Maombi ya kawaida yakishindwa, funga na kuomba.

• Mashambulizi ya roho waovu kupitia vitabu, picha, gazeti, sinema, n.k

Wakati fulani nilikuwa ninajifunza kuhusu dini za Kikristo mbalimbali za aina ya cults (ukengeufu) kama vile dini ya Kisabato, Mashahidi wa Jehova, Yesu tu (William Marriot Branham), n.k. wakati nilipokuwa najifunza kuhusu dini ya Sabato, nilisoma vitabu vingi sana. Vinavyohusu misingi mbalimbali ya imani hiyo. Baadaye nilianza kusikia sauti ndani yangu, kuwa, iwapo ningefuata torati ya Musa, nikaongezea katika wokovu nilionao ningekuwa mtakatifu wa hali ya juu sana, kuliko kuokoka pekee au msabato pekee. Nikasikia kuwa waliookoka wamekosea kuutupa Usabato na wasabato wamekosea kuutupa wokovu. Hivyo iwapo nitaacha kula samaki wasio na magamba, nguruwe na niiheshimu siku ya Jumamosi, ningempendeza sana Mungu.

Niligundua kuwa hayo tayari yalikuwa ni mashambulizi kutoka kwa shetani. Vita hiyo niliendelea nayo muda wa siku nyingi kidogo, nilikuwa karibu kushindwa, maana nilifikia hatua ya kujiandaa kuanza kutekeleza. Lakini Roho Mtakatifu akaniambia,

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au Sabato (Wakolosai 2:16).

Niliifukuza hiyo roho hadi nikaishinda ikatoka nikawa siisikii tena.

Wakristo wengi wanasoma vitabu bila kuchagua au kupambanua kuwa kitabu hicho kina madhara kwake kiroho. Biblia ni kitabu kimeandikwa na watu waliokuwa wamejaa Roho Mtakatifu ambaye aliwaongoza kukiandika. Hivyo biblia ni kitabu kilicho na uvuvio wa Roho Mtakatifu.

Ukisoma kitabu kinachohusu mambo ya zinaa kinakuwa kimeandikwa na mtu aliyekuwa ana pepo au roho waovu wa zinaa. Hivyo kitabu hicho kinao uvuvio wa pepo la zinaa. Ukiangalia sinema inayohusu zinaa, walioitengeneza walikuwa na roho waovu wa zinaa ndiyo aliowaongoza kutengeneza hiyo sinema. Hao ni watumishi wa roho ya zinaa, hivyo roho ya zinaa anawatumikisha. Sinema hiyo, hivyo inao uvuvio wa roho waovu wa zinaa. Ni hivyo hivyo hata katika kusikiliza nyimbo mbalimbali.

Wakristo wengi shetani amewashambulia kwa njia hii na kuwashinda kabisa, hivyo sasa wanaendelea kumtumikia shetani, huku wakijidanganya kuwa wanabidii ya kwenda kanisani, wanajidanganya kuwa kwa vile bado wananena kwa lugha, wataingia mbinguni. Mbinguni anaingia mkristo aliyeokoka na kushinda vita. Wewe umeokoka sawa, umejazwa Roho Mtakatifu sawa, unanena kwa lugha sawa, lakini umeshindwa vita.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa, kula matunda ya mti na uzima, ulio katika bustani ya Mungu
(Ufunuo 2:17).

Nimefanya utafiti kuhusiana na magazeti. Magazeti yameanzishwa na watu wanayoyamiliki. Lakini ndani ya wanaoyamiliki magazeti hayo, kuna roho fulani ambayo imewatuma waanzishe hayo magazeti. Japo kuwa gazeti linaweza kuwa na habari nyingi mbalimbali, lakini unaweza kugundua hasa mhimili wa habari zinazotolewa au mwelekeo wa gazeti lenyewe. Kama ni gazeti la siasa utalikuta linakumbatia chama fulani au linaonyesha dalili ya chuki kwa baadhi ya vyama fulani.

Nimeona hapa Tanzania kuna magazeti yanayoongozwa na roho waovu wa mauti. Gazeti ambalo kila toleo au katika matoleo mengi, matukio ya vifo vya kikatili ndiyo hupewa kipauwa mbele, tena habari hizo huandikwa kwa vichwa vya habari vikubwa na kuwekwa ukurasa wa mbele. Habari ya tukio la kifo cha kikatili ni habari, siyo vibaya ikiandikwa kwenye gazeti. Lakini ikiandikwa kwenye gazeti ambalo linaongozwa na roho ya siasa, hiyo habari haitapewa kipauwa mbele, wala haitaandikwa kwa kichwa cha habari kikubwa tena itawekwa katika kurasa za ndani siyo ukurasa wa mbele. Kutokana na hili, shetani naye anayo magazeti yake ya kusambazia roho waovu. Habari moja ya uporaji ulioendeshwa kiufundi sana na kufanikiwa, huyo roho ovu wa uporaji huo anasambazwa na gazeti hilo kwa madhumuni ya kwamba, kupitia watu kuisoma habari hiyo huyo pepo au roho ovu aingie ndani ya watu wengine wengi zaidi, ambao nao watakuwa wakiendesha uporaji kwa ufundi wa hali ya juu.

Habari za kuanguka dhambini mtumishi wa Mungu, mhubiri mkubwa, siyo habari nzuri hata kidogo, siyo habari njema katika kambi ya Yesu. Ni habari njema ya furaha, katika kambi ya shetani, ni habari ya ushindi kwa shetani. Mimi ningeisikia habari hiyo wa kwanza, ningefurahi sana, maana ingeishia kwangu na nisingemwambia mtu yeyote zaidi ya mimi kwa kufanya hivyo ningeizuia habari hiyo isimfikie adui, hivyo ningeitetea kambi ya Yesu. Adui akisikia habari hiyo ataitumia kuwa silaha ya kuwashambulia watu wa Mungu. Wengine watakaposikia wataanguka dhambini na wengine watavunjika moyo, watasema kuwa, kama Mhubiri huyu ameanguka dhambini basi hakuna wokovu. Kuna magazeti yenye kupenda kusambaza habari mbaya zinazotukia katika kambi ya Yesu. Yanasambaza habari hizi si kwa faida ya Yesu bali ni kwa faida ya shetani. Haijalishi gazeti hilo linajiita ni la kikristo au vinginevyo, lakini linaweza kuwepo kwa ajili ya kumtumikia shetani, hivyo badala ya kuujenga ufalme wa Mungu, yanajenga ufalme wa shetani, yanaubomoa ufalme wa Mungu.

Posted in MAFUNDISHO | Leave a Comment »

 

MUNGU na mwanadamu

kuishi maisha matakatifu

Baada ya kuwa umempokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wako, unatakiwa mwili wako, ufe. Mwili unapokufa matendo ya mwili yanakufa. Mwili unakuwa hauna uwezo wa kufanya dhambi.

Mkristo hatakiwi kabisa baada ya kuokoka aendelee kutenda dhambi, kwa sababu akiendelea kutenda hawezi kuingia mbinguni.

Mtu wa Mungu uliyeokoka lakini bado unatenda dhambi, unatenda kwa sababu hujausulubisha mwili wako. Hujajitoa kikamilifu kwa Mungu. Hata hivyo wakristo wengi wamejitoa asilimia mia kwa mia kwa Yesu na wameusulubisha mwili wao kikamilifu, lakini ndani yao wanaonekana roho waovu wamo, japokuwa wamezishinda dhambi zinazoonekana kwa macho kwa urahisi. Roho waovu hao ni uchoyo, wivu, kiburi, hasira, chuki fitina, uzushi, ubinafsi, useng’enyanji, umimi, unyanyasaji, n.k.

Roho waovu ni malaika wa shetani. Mtu yeyote anayetoa kibali cha roho waovu kukaa ndani yake, basi ameamua kuwa hekalu la hao roho waovu. Huwezi kuwa hekalu la Mungu na wakati huo huo ukawa hekalu la shetani. Hivyo wewe kama umeruhusu roho waovu wakae ndani yako basi umeamua kuwa hekalu la shetani, japo kuwa bado unajiita mkristo.

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu (Wakorintho 6:19 – 20).

Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo nyinyi (Wakorintho 3:16 – 17).

Kuliharibu hekalu la Mungu, ni kuwaruhusu roho waovu wakae ndani yako. Mungu anasema, ukiliharibu hekalu lake atakuharibu wewe. Mtu wa Mungu vita vyetu na shetani hatuvipigani kwa kujiita wakristo peke yake, bali tunapigana na hawa roho waovu wasiingie ndani yetu. Wewe ukiwaruhusu waingie na wakae ndani yako, ina maana unawapenda, watakutumikisha. Hapo watakuwa wamekushinda hii vita ya kiroho. Roho hawa waovu ni malaika wa shetani, ni mapepo, ni watumishi wa shetani. Wako ndani yako ili kukulazimisha kutenda dhambi, utende kinyume na neno la Mungu, katika maeneo mbalimbali ya maisha yako. Roho waovu ndiyo mizizi ya dhambi, kuendelea kuwa ndani yako ujue kuwa hiyo ndiyo mizizi ya dhambi inayokulazimisha umkosee Mungu. Unahitajika kuichimbua hiyo mizizi, kuing’oa na kuitupa nje kabisa na usiiruhusu irudi tena.

 

.


Realtime Clock

Gospel Teachings and One To One Enterviews

WAPO RADIO

                                                                                                                                              Ratiba ya vipindi:

0715 - 0800hrs Patapata

0800 - 0845hrs Yasemavyo Magazeti

0845 - 1000hrs Zilizotufikia

1000 - 1200hrs Meza ya Busara

1200 - 1205hrs Habari kwa Ufupi

1800 - 1830hrs DW Idhaa ya Kiswahili

1830 - 1900hrs Duru za Michezo

1900 - 2000hrs Yaliyotokea

tafuta andiko ndani ya Biblia hapa

Enter a verse or keywords
(John 3:16, love, sword of the spirit)

tafuta katika biblia

Search the BibleBibleGateway.com

videos mpya

1762 views - 0 comments
1414 views - 0 comments
1365 views - 0 comments
2031 views - 0 comments

hali ya hewa

Subscribe To Our Site

mtumie rafiki yako

webs

nyimbo za injili-videos

neno la siku ya leo

jiunge nasi

wageni

..


john lema

shuhuda

 • "Bi Getrude Hamphrey, amekaa ndani ya ndoa kwa miaka saba bila kupata mtoto, ?Nilidharauliwa na watoto wadogo, hata ndugu zangu wa karibu, wengi walinicheka na kuniona sifai, nil..."
  getrude humphrey
  aliyepata mtoto
 • "USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU UTANGULIZI: Ndugu yangu kuna shuhuda nyingi sana zinazoanguka duniani, lakini wachache wanaozingatia kwa vile watoaji si wa dini zao au si ..."
  nyisaki chaula
  USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU

Google Translator

mahubiri

comment box

Facebook Fanpage Box

Recent Prayer Requests

 • maisha yangu

  naomba maombi yenu kuhusu mimi na familia yangu ,mungu atulinde siku zote za maisha yetu,kwani tuko kwenye majaribu mazito
 • kupata watoto

  namomba mungu anisaidie niweze kupata watoto wazuri,wakike na wakime.

,

 

 

 

 

Recent Podcasts

.