Sifa na kuabudu

John Lema 2010

    swahilisifa
                                                                                                                  

                                              sala ya toba

“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha  yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu  Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana  Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa  kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako  nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina  la Yesu Kristo. Amina.

happy new year

                                                  

praise power radio  tanzania-mlima wa moto

sikiliza wapo radio live

wapo radio live

click hapa

 http://tunein.com/radio/WAPO-Radio-981-FM-s205284/

 

NAMNA YA KUOMBA

- Hatua na vipengele muhimu katika kuomba -

 

MKARIBISHE ROHO MTAKATIFU. *Rum 8:26-27 *Yoh 14:16-17

Yesu alisema Roho Mtakatifu ni msaidizi wetu. Atatusaidia na kutufundisha yote, kwa maana pasipo yeye, sisi hatuwezi neno lolote. Na sisi peke yetu hatujui kuomba ipasavyo, bali yeye (Roho) ajua kutuombea kwa Mungu kama vile Mungu apendavyo. Hivyo kabla ya kuanza maombi au kusoma neno au ibada au safari au mitihani au kikao n.k. jifunze kujikabidhi kwa Roho Mtakatifu, uombe msaada wake, akupe ufanisi/ubora katika yote yakupasayo kufanya.

Tambua Utu wake, Uungu na Uweza wake.

Jikabidhi katika Nguvu ya Uongozi wake.

Tii kila Uongozi anaokupa.

 

FANYA TOBA NA UTAKASO. *Isa 59:1-2, Yoh 9:31, 1Yoh 1:8-9,7

Sikio la Bwana si zito kusikia wala mkono wake si mfupi kushindwa kututendea mambo tumwombayo, bali maovu yetu ndiyo yanatufarakanisha na Mungu wetu. Mungu hawasikii wenye dhambi. Hivyo chukua muda wa kutafakari na kuungama dhambi zako mbele za Mungu na kuzitubu kwa kumaanisha kuziacha. Mungu ni mwaminifu kutusamehe na kututakasa na uchafu wote. (Isa 1:18). Lakini, kabla hujafanya toba yako binfsi;

(i) - Kwanza, samehe wote waliokukosea, hata kama hawajaja

kukuomba msamaha. Usipowasamehe waliokukosea, na Mungu

hataweza kukusamehe wewe. (Math 6:12,14-15)

(ii) - Ndipo nawe ufanye toba yako binafsi. Na Mungu atakusamehe kabisa.

Hata kama ni nyekundu sana, zitakuwa nyeupe sana. (Isa 1:18, Isa 43:25)

3. MSIFU, MUABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Zab 147 na Zab 148

Msifu Bwana kwa Matendo yake makuu, mwabudu Bwana kwa uzuri wake na kwa sifa zake. Mwadhimishe Mungu kwa Tabia zake, wema wake, fadhili zake na baraka zake mbalimbali anazotutendea. Sifa yako ikifika vizuri mbele za Mungu, ndipo atakuwa tayari kukupa haja za moyo wako. Haja zetu zimefichwa nyuma ya mgomgo wa sifa. Ndio maana Neno linasema;

‘Nawe utajifurahisha kwa Bwana (kwa kumsifu, kumwabudu na kumshukuru), naye atakupa

haja za moyo wako’ (Zab37:4).

Yesu anatuonyesha mfano; angalia sentensi yake ya kwanza katika kuomba kwake imekuwa “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.” (Math 6:9). Anaanza maombi kwa kumsifu Mungu. Msifu Mungu kwa kuimba na kwa kunena/kusema/kuelezea. Mungu anataka kusifiwa na kutukuzwa. Ukifanya sifa nzuri, ya kuufurahisha moyo wake, atakupa hata na vile ambavyo hukutegemea/hukuomba.

4. MWELEZE MUNGU MAHITAJI NA HOJA ZAKO. *Wafilipi 4:6-7,19 Isa 43:26

Mweleze Mungu zile hoja zilizokusukumwa kwenda kumwomba. Nenda mbele za Mungu kama ‘kuhani’ (1Pet 2:9). Kwa unyenyekevu na heshima. Lakini kabla ya kumweleza mahitaji yako binafsi;

(i) Kwanza fanya ‘maombezi’ – ombea watu wengine; (1Tim 2:1-4)

Viongozi mbalimbali na wenye mamlaka, watumishi wa Mungu, marafiki zako, wenye shida, ndugu zako, nchi yako, shule yako, shirika lenu, ofisi yenu, chama chenu, n.k. Usianze kujiombea mwenyewe tuu, zoea kuwatanguliza wengine.

(ii) Kisha fanya ‘maombi yako’– ombea haja za moyo wako. (Math 7:7-11)

Mweleze Mungu haja zako. Ongea na Mungu kwa uwazi na ukweli. Japo anazijua haja zetu, lakini ameagiza kuwa tumwombe ndipo atafanya.‘aombaye hupokea’ yaani; asiyeomba, hapati. Mungu anasema tumpelekee hoja zenye nguvu (Isa 41:21). Omba vitu vizuri na mambo makubwa ili upewe (pray for good things and big things)

5. FANYA MAOMBI YA VITA VYA ROHONI. *Efe 6:10-13 *2Kor 10:3-5

Baada ya kumwendea Mungu na kumweleza mahitaji yako, sasa simama kama ‘mfalme’, kwasababu wewe ni ‘mfalme’ (Ufu 5:8), tumia mamlaka yako ya kifalme, ongea na hali/hitaji ulilokuwa unaliombea, na kwa mamlaka, amuru iwe kama vile ulivyoomba/unavyotamani. Ndio maana Bwana Yesu alipokabidhiwa mamlaka yote na Mungu, naye akatukabidhi sisi (kanisa lake) “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui. Wala hakuna kitakachowadhuru” (Luk 10:19, Yer 1:10, Yak 4:7). Tuma neno lenye mamlaka katika hali/jambo ulilokuwa unaliombea, Amuru iwe vile ulivyokuwa unamwomba Mungu iwe. Kemea kila roho ya shetani inayoweza kuwa inasababisha tatizo katika swala lako.

6. OMBEA ULINZI JUU YA ULIYOYAOMBEA. *Math 6:13a

Baada ya kupiga vita vya kiroho, weka ulinzi katika yale uliyoyaombea, ili shetani na mapepo yake wasiweze kuirudia hali/jambo/mtu yule uliyemkomboa kwa maombi ya vita. Yesu alisema shetani akifukuzwa mahali, haendi mbali, anasubiri kuona kama atapata upenyo wa kuparudia mahali pale alipokuwa kwanza. (Math 12:43-45). Kwahiyo, usipoweka ulinzi, kuna uwezekano wa adui kurudi na kuliharibu zaidi lile jambo uliloliombea na kulipata.

Kumbuka, unapoomba vizuri, unapokea papo hapo (katika ulimwengu wa roho), lakini udhihirisho wake katika ulimwengu wa mwili, unaweza kuchukua muda fulani. Hivyo katika muda huo wa kusubiri, shetani anaweza akapita na kuzuia au kuharibu kile unachokisubiri kidhihirike katika ulimwengu wa mwili. Ndio maana Yesu alitufundisha kuombea ulinzi, “tuokoe na yule mwovu” (Math 6:13a). Weka ulinzi juu ya mambo yako yote. Jengea wigo wa moto wa mbinguni (2Fal 6:16-17), Yafunike kwa damu ya Yesu na agiza malaika walinzi walinde mambo yako masaa yote. Omba hivyo kila siku. (Zab 34:7, Zab 91:9-11, Ebr 1:13-14)

MSIFU, MWABUDU NA KUMSHUKURU MUNGU. *Math 6:13b

Yesu alianza maombi kwa kumsifu Mungu na kumtukuza. Na akamaliza maombi yake kwa kumtukuza Mungu tena. Akasema “kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu ni zako, sasa na hata milele” akamaliza. Kwahiyo nawe kwa kumaliza maombi yako, msifu na kumshukuru Mungu tena, kwa ukuu wake, uaminifu wake, na ahadi zake juu yetu.Ndipo ufunge maombi yako.

MUHIMU: TUMIA MAANDIKO KATIKA KUOMBA *Kol 3:16

-Katika kuomba kwako, mara zote tumia maandiko kumkumbusha Mungu ahadi zake .(Isa 43:26). Mungu analiangalia neno lake ili alitimize. Sababu pekee itakayomfanya Mungu akupe alichoomba, ni ili kulitimiza neno lake. Hivyo, baada ya kumweleza unachohitaji (kwa ajili yako au kwa ajili ya mtu unayemwombea) mpe Mungu andiko/neno lake linalokupa wewe uhalali wa kuomba hicho kitu mbele zake na kupewa.

-Hata unapompinga na kumkemea shetani, baada ya kutoa amri yako dhidi yake, shetani atasubiri kusikia andiko/neno linalomnyima yeye uhalali wa kushika alichoshika. Ndio maana Yesu alimshinda shetani kwa neno la Mungu. Alisema “imeandikwa” na shetani akashindwa. “Nao wakmshinda (shetani) kwa damu ya Yesu na kwa Neno” (Ufu 12:11)

 MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA VIZURI  KWA MUDA MREFU

1. CHAGUA MAHALI PAZURI PA UTULIVU. *Mk 1:35

ili uweze kuomba kwa utulivu na kwa umakini, chagua au tafuta mahali pazuri

patakapokupa utulivu katika kuomba (concentration in prayer). Ndio maana Mungu

alipenda kuongea na Musa juu ya mlima. (Kut 24:12-18). Hata Yesu alizoea kwenda

kuombea mlimani, mahali palipo mbali na vurugu za watu, alipenda kwenda mlimani.

(Math 14:22-23). Tafuta mahali patulivu; chumbani, kanisani, mlimani (Math 6:5-6)

2. CHAGUA MUDA MZURI. *Mhu 3:1,7

Ili uweze kuomba kwa umakini mzuri, chagua muda mzuri ambao akili yako ma mwili

wako viko fresh. Usilazimishe kuomba hata kama akili yako au mwili wako umechoka sana. Kila jambo lina wakati wake. Kama umechoka sana, huo si muda wa kuomba, bali wa kupumzika. Usilazimishe ratiba. ni bora upumzike ili baadaye uweze kuomba vizuri baadaye. Usije ukajikuta unamkemea Yesu badala shetani. Penda kuomba wakati una nguvu ya akili na mwili, ili uwe makini kuongea na Mungu kwa akili timamu. Ndio maana Yesu alipenda kuamka alfajiri sana kwenda kuomba mlimani. (Mk 1:35, Luka 4:42)

3. OMBA KATIKA ROHO (NENA KWA LUGHA). *Efe 6:18, Rum 8:26-27

Mbinu nyingine nzuri ya kuomba kwa muda mrefu na kwa ufanisi, ni kuomba kwa Roho; yaani kuomba kwa kunena kwa lugha. Tunapoomba kwa akili za kibinadamu, Mungu anasikia pia, lakini maombi yako yanakuwa na mipaka / limited kwasababu akili ya mtu haijui kila kitu. Bali Roho wa Mungu anajua kila kitu. Naye hutupa kipawa cha kuomba kwa lugha ya mbinguni iliyo bora zaidi.(Yuda 1:20, Mk 16:17, 1Kor 14:1-4, 15-16,7)

4. OMBA KWA KUFUNGA WAKATI MWINGINE. *Math 6:16-18

Kufunga kula kunasaidia kudhoofisha mwili, ili roho iwe makini zaidi kuongea na Mungu kwa kina zaidi. Mwili huu siku zote haupendi kufanya mambo ya Mungu. Na mwili ukiwa umeshiba, unakuwa na uchovu na uzito wa kufanya mambo ya kiroho. Mbinu mojawapo ya kuudhibiti, ni kuunyima/kuupunguzia posho yake ya chakula. Mwili ukidhoofika kiasi, roho yako inapata nguvu na upenyo mzuri zaidi (Zab 35:13). Mashujaa wote wa imani walifunga na kuomba. Ndio maana Yesu anasema ‘mfungapo’ akimaanisha ratiba ya kufunga, ipo. Inasaidia.

5. OMBA NA RAFIKI (PRAYER PARTNER). *Mhu 4:9-10

Neno la Mungu linasema, ni heri wawili kuliko mmoja. Kuna faida ya kuomba pamoja na rafiki yako. Kwanza, mnapokuwa wawili au watatu, inaleta hamasa na ari ya kuomba zaidi. Si rahisi kujisikia mvivu unapokuwa na waombaji wenzako. Pili; nguvu ya kiroho inaongezeka. Neno linasema, mwombaji mmoja anafukuza adui elfu moja, bali wakiwa wawili, wanafukuza (sio elfu mbili) bali elfu kumi! Shangaa! (Kumb 32:20) Hiyo ni kanuni ya mbinguni/kanuni ya Ki-Mungu. Kadri mnavyoongezeka, nguvu ya Mungu huongezeka.

Kwahiyo, wakati mwingine, omba na rafiki yako, unayemwamini, unayeweza kumshirikisha mambo yako ya binafsi. Mashujaa wengi wa imani, walikuwa na marafiki wa kiroho. (Prayer Partners). Kwa Mfano:- Math 17:1-9

Musa - alikuwa na Joshua, Haruni na Huri

Eliya - alikuwa na Elisha

Daniel - alikuwa na Shadrack, Meshack na Abednego.

Yesu - alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana.

Paul - alikuwa na Barnaba, Timotheo na Tito.

Wewe Je? Uko na nani katika urafiki wa kiroho?

 

Kama huna rafiki wa karibu wa kuomba naye, usikurupuke kujichaglia. Tulia umwombe Mungu akupe mtu atakayekuwa wa msaada kwako. Mtu mtakayefungamanishwa naye katika roho, hata kama mmetengana kijiografia, lakini katika roho, mko na umoja mzuri wa imani. (Math 18:18-19)

6. OMBA KATIKA MKAO UNAOKUPA UHURU NA NGUVU ZAIDI.

Katika kuomba kwa muda mrefu, mkao uliouzoea utakusaidia kwenda mwendo mrefu. Yakupasa kujua nguvu yako na udhaifu wako (strong point and weak point). Wakati wa kuomba, epuka mikao inayokuchosha haraka na tumia mikao inayokua nguvu zaidi. Kwa Mfano:- Ukiwa umechoka, usipende kuomba kwa kupiga magoti au kwa kuegemea kitandani. Ni bora uombe ukiwa umesimama au unatembea tembea, ili kuepuka usingizi na uchovu. Waombaji hodari wanaujua mikao inayowasaidia kuomba maombi marefu. Wengine hawana mikao maalum, bali wakiwa katika maombi, huwa wanabadilisha-badilisha mikao ili wasichoke. Hiyo ni mbinu nzuri pia.

Mifano ya Mashujaa wa imani;

Ibrahim – aliomba kwa kusimama (Mwa 18:22)

Daniel - aliomba kwa kupiga magoti (Dan 6:10)

Paul - aliomba kwa kupiga magoti (Efe 3:14)

Yesu - aliomba kwa kulala chini (Math 26:38-39)

Eliya - aliomba kwa kukaa chini na

kuweka kichwa kati ya miguu (1Fal 18:42)

Mimi - huwa napenda kuomba kwa kutembea tembea

Naweza kumaliza kilomita nyingi chumbani kwangu

Nikitembea huku nikiomba.

Wewe Je? Unaujua mkao wa nguvu? Kama hujui, Tafuta kujua.

 

OMBA NA MUZIKI LAINI KWA KUMWABUDU MUNGU.

Muziki wa kiroho, na wataratibu, unaweza kukutengenezea mazingira mazuri sana ya kuomba kwa muda mrefu. Muziki wa kuabudu, unavuta uwepo wa Mungu kwa namna ya pekee. Neno linasema, waimbaji na wanamuziki walipoimba na muziki ukapigwa, nao wakawa kama mtu mmoja, utukufu wa Mungu ukashuka na kulijaza lile hekalu hata makuhani hawakuweza tena kuhudumu (2Nyak 5:12-14). Kule mbinguni, kila malaika wa sifa, ana kinubi (zeze/gitaa). Elisha hakutoa unabii, mpaka mpiga kinubi alipopiga kwa ustadi, ndipo mkono wa Bwana (Roho wa Mungu) alipokija juu yake, naye akatabiri.

Najaribu kukuonyesha, kuna connection kati ya muziki wa kiroho na utukufu wa Mungu. Kwahiyo, ukiweza kuomba huku umeweka kanda au CD ya nyimbo za kiroho za taratibu, utapata (experience) hamasa ya kiroho (motivation) na utasikia una nguvu ya kuomba kwa muda mrefu. Kama unaweza, tengeneza kanda au CD maalum yenye nyimbo nzuri unazozipenda wewe, ili uwe unaipiga wakati wa maombi. Utajikuta unaweza kuomba kwa muda mrefu na kwa bubujiko zuri zaidi

Mwl. Mgisa Mtebe,Bsc Economics

Mzumbe University,+255 713 497 654

mgisamtebe@yahoo.com

I

Emmanuel.tv

Changing Lives, Changing Nations, Changing the World

Watch Now

 

 

Online World Prophecies

Problem communicating with Vimeo: Please wait a few minutes before trying again.

 

 

 

SOMO: TABIA NA MAHUSIANO

Mafundisho

Na Mr.Gammariel Chiduo

TABIA 6 ZA LAZIMA KATIKA KUJENGA USHIRIKA AU MAHUSIANO MAZURI

NA MUNGU, MKE /MUME, JAMII AU WATU WOTE

UTANGULIZI

· Mwanadamu sio kisiwa, lazima akutane na ashirikiane na watu wengine /au na Mungu

· (Mwanzo 1:26) Mungu anajifunua kwetu katika ushirika "NA TUFANYE MTU…"

· Kuumbwa kwetu ni katika kutimiza takwa la USHIRIKA.

· Umeubwa kwa ajili ya wengine

Mungu amekuumba hivyo ulivyo kwa ajili ya wengine

Ndio maana tuko tofauti sana. Mungu hajacopy na kupaste.

Tofauti zetu huleta hitaji la USHIRIKA na kushirikiana

Utajikuta chochote unachofanya ni kwa ajili ya watu wengine. Mfano:

- Unavaa kwa ajili ya watu, ili watu watakapokuona waone umependeza. Kioo kitakusaidia. Kama ni kwaajili yako vaa suti, ukalale au kaa chumbani.

- Uhai wako ni kwa ajili ya watu. Ukitaka kujinyonga utashtakiwa. Jaribu kuwaambia kuwa uhai ni wangu, sasa nataka kuutoa kama watakuelewa.

· Utajikuta unalazimika kujenga ushirika na wengine maana unawahitaji, na wanakuhitaji sana, hivyo hivyo ulivyo wewe ni wa thamani sana!!

· Umoja ni jambo muhimu sana katika maisha yetu ya wokovu (Yoh 17:20-24) Yesu anatuombea tuwe na umoja.

· Umoja ni kati ya vitu vinavyopigwa vita sana na shetani – ndiko kuliko na siri ya nguvu na ushindi.

· (Mithali 30:27) Nzige hawana mfalme, lakini huenda makundi makundi.

· Biblia inasema " Mmoja hufukuza elfu, wawili makumi elfu!"

· Wakutanikapo wawili au watatu mimi nipo hapo katikati yao.

· Ukiwa na tabia 6 utajenga mahusiano mazuri

· Tabia hizi ni kama CEMENT za kuunganisha matofali ili kujenga nyumba

· Zikikosekana ni sawa na kupanga matofali bila cement.

· Ziko tabia 6 za lazima zinazotumika kote kote, kwenye ushirika na Mungu, Mke au Mume na hata kwa watu wote:-

1. Tabia ya UADILIFU na UTAKATIFU

· Ili kujenga ushirika na uhusiano mzuri UADILIFU na UTAKATIFU ni tabia za lazima.

· Kwenda sambamba na mnayowaza na kusema kwa pamoja.

· Kama kuna ahadi inabidi kutimiza ahadi

· Kutawafanya kuaminiana na kuimarisha umoja na uhusiano wenu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU

(1Petro 1:15) Bali kama aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote.

v Utakatifu ndio tulioitiwa.

v Dhambi ndiyo iliyotutenga na Mungu

v Kutakaswa na kudumu katika utakatifu kutadumisha uhusiano wetu na Mungu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME

>> Uadilifu hujenga na kukuza mahusiano

>> Uovu na kusalitiana kwenye ndoa hata kama ni kwa siri, huvunja na kuua ushirika wenu. Ni kubomoa nyumba yenu kwa mikono yenu wenyewe. Mmejiloga wenyewe. Msitafute mchawi.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE

v Watu hupenda mtu mwadilifu

v Humwamini mtu wa jinsi hiyo kwa kila kitu.

2. Tabia ya UKWELI na UWAZI

· Tabia ya kuficha ukweli na uongo vinavunja Ushirika na urafiki.

· Weka vitu vyote kwenye karatasi nyeupe mbele za watu wavielewe wavione.

· Kama mmoja ana vitu asivyopenda kwa mwingine mawasiliano lazima yafanyike tena kwa heshima na taratibu ili kulinda umoja, kuliko kuweka moyoni

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU

>> Ukweli utampendeza Mungu

>> Kuwa wazi mbele za Mungu kutaongeza kupendwa na Mungu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME

>> Mume au mke huchukizwa sana na vitu vinavyotendeka chini chini visivyoeleweka.

>>Mfano: Jamaa mmoja alimsave mpenzi wa nje kwenye simu yake kama Battery Low! Na mlio akauchagulia. Kila ikiita mke wake akiona Battery Low anaizima na kuiweka kwenye chaji. Uongo wa jinsi hii huharibu mahusiano kabisa, huna utakalojitetea mke au mume akakuamini tena.

>> Ukiwa mkweli na muwazi kwa mwezi wako utadumisha uhusiano wenu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE

>> Mtu mkweli na muwazi hupendwa na watu wote.

3. Tabia ya KUBADILIKA

· Ukikubali kuwa hujakamilika, kwenye ushirika jipange KUBADILIKA

· Kama kuna kitu hakijaenda vizuri angalia kama inakupasa UBADILIKE.

· Badala ya kulaumiana jifunze kukubali KUBADILIKA.

· Tabia ya kubadilika hukuweka uende sawa na sambamba na kukubalika.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU

v Mungu anatarajia mabadiliko makubwa unapoendelea kumjua.

v Maana ya kukua kiroho ni kuongezeka na kubadilika kuelekea ukamilifu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME

>> Badilika unapogundua umekosea.

>> Badilika unapogundua mwenzako habadiliki.

>>Tumelelewa kwenye mazingira tofauti. Mila tofauti. Desturi tofauti.

>>Lipo jambo ambalo likitendeka kwa mwingine ni furaha, na kwa mwingine ni kero. Mfano: Kubanja. Ukiona kunamkera mwenzako BADILIKA anza kuona si tendo zuri.

>> Kubadilika kutawafanya mzidi kufanana na kuongeza utulivu kwenye ndoa.

>>Badilika unapoona misimamo yako haijengi.

(Epuka misimamo mikali, mimi nimeshasema basi… Siongei tena…n.k.)

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE

>> Mungu anatarajia mabadiliko makubwa unapoendelea kumjua.

>> Maana ya kukua kiroho ni kuongezeka na kubadilika kuelekea ukamilifu.

4. Tabia ya KUSAMEHE NA KUTUBU

· Kukiri kosa na kuomba msamaha kunawashinda wengi

· Au kusamehe baada ya kuomba msamaha ni kazi ngumu kwa wengi

· Tabia ya kusamehe na kutubu ili usamehewe hujenga mahusiano kwa upya

· Ukijizoeza kutubu kutakufanya urekebishe makosa uliyofanya

· Kutubu na kusamehe kunahitaji unyenyekevu wa hali ya juu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU

>> Kutubu hurejesha uhusiano wako na Mungu kwa upya.

>>Kuwasamehe wengine huimarisha uhusiano wako na Mungu na kuondoa kila kunyanzi moyoni.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME

>> Kosa linapotendeka, msamaha huhitajika kutoka pande zote mbili.

>>Kutokukiri makosa huharibu uhusiano kati ya mke na mume

>>Hata kama huoni kosa, na mwenzako analiona ni vema kuomba msamaha ili kurejesha uhusiano mzuri uliokuwepo, unaweza kugundua baadaye kuwa ulikuwa unakosea.

>>Makosa yasiwe sababu ya kuwafarakanisha na kuharibu uhusiano wenu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE

>> Tabia ya kusamehe na kuomba msamaha kwa watu wote ni ya msingi katika kujenga mahusiano mazuri na watu.

>> Kutubu na kusamehe kunasaidia kuliweka wazi kosa na kuanzisha jitihada za kutolirudia badala ya kujenga ukuta wa kujilinda kwamba hujakosea, ni bahati mbaya

5. Tabia ya HESHIMA na NIDHAMU

· Ukitaka kuvunja kabisa uhusiano na mtu, onyesha unamdharau

· Kila mtu anapenda kuheshimiwa

· Dharau huharibu na kuvunja kabisa umoja na ushirika

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU

>> Mungu anapenda kuheshimiwa

>>Mungu atazidi kukupenda unapoonyesha nidhamu na heshima kwake

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE/MUME

(1Petro 3:7) Mpe mke heshima…kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

>> Heshima si kwa mume peke yake. Tunza heshima ya mke pia.

>>Kuheshimiana kunajenga umoja na mahusiano.

>>Tabia hii ya kuheshimiana hulinda na kuimarisha uhusiano wenu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA JAMII/WATU WOTE

>>Ukiwaheshimu watu wote wakubwa kwa wadogo, utajijengea uhusiano mzuri na watu wote.

6. Tabia ya KUTOA /KUJITOA

· Tatizo kubwa la msingi au SUMU ya ushirika ni UBINAFSI.

· Ubinafsi ni uchawi unaologa na kuusambaratisha umoja na ushirikiano

· Kwenye mahusiano au ushirika usisubiri wewe tu upewe, tafuta nafasi ya kutoa

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MUNGU

>>Yeye alimtoa Kristo.

>>Mungu ametupa vyote tulivyonavyo, sisi ni mawakili tu.

>>Unatazamiwa ujitoe zaidi na umtolee zaidi kuonyesha kiasi gani unampenda.

(Mwanzo 22:15-18) IBRAHIM AKIMTOA ISAKA

Ibrahimu anamtoa Isaka, yuko tayari kumchinja Mungu akasema "Nimeapa kwa nafsi yangu, kwa kuwa umetenda neno hili; wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, 17katika kukubariki nitakubariki, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao, 18na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

KWENYE UHUSIANO WAKO NA MKE /MUME

( ) Msinyimane

>>Wote wawili uhusiano utadumu na kuongezeka zaidi kama kila upande unazingatia kutoa.

>> Zawadi ndogo ndogo na kubwa kutoka kila upande husherehesha uhusiano wenu.

KWENYE JAMII NA WATU WOTE

Utapendwa na watu, utajipatia marafiki wengi ukiwa mtoaji

(Mhubiri ) Mali ikiongezeka, walao nao huongezeka

(Luka ) Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa kwa kipimo cha kujaa na kusukwa sukwa

SUMMARY

TABIA 6 ZA LAZIMA KATIKA KUJENGA USHIRIKA

1. TABIA YA UADILIFU NA UTAKATIFU

2. TABIA YA UKWELI NA UWAZI

3. TABIA YA KUBADILIKA

4. TABIA YA KUSAMEHE NA KUTUBU

5. TABIA YA HESHIMA NA NIDHAMU

6. TABIA YA KUTOA NA KUJITOA

Tabia hizi hata kama unazo, ongeza viwango vyake, utajenga ushirika na mahusiano mazuri.

 MR Gamariel Chiduo

TAG Head Office

Bishop Moses Kulola

Moses Kulola, born in June 1928, in a family of ten children and five are still alive, registered for my first school in 1939 called Ligsha Sukuma a mission school and after Ligwisha, I enrolled for the institute of Archtchture in 1949. I was baptised in 1950 in the AIM Church Makongoro.
Married to Elizabeth with 10 offsprings where seven are still alive.Begun missionary work in 1950 eventhough i was called upon in 1949 just after my baptism.

In 1959 i was enrolled on government work which i did to preach the gospel in towns and villages being a government employee. My great service to my country came to an end in 1962, where i compeletely dedicated my power, body and soul. In 1964 i enrolled in the theological college and 1966 i qualified with a diploma.

I didnt just stop there with education as i continued with correspondenced studies which accredited to my so many certificates accross the world.
ServiceI worked for two years as Pastor before becoming a Pentacostal believer that is 1961 to 1962, worked in TACR church 1966 till 1991 where i begun decided to started the Evangelistic assemblies of God.EAGT has succeded to growth at a great pace in tanzania, Zambia, Malawi and tantamounting to a total of 4000 churches in a range of big and small and I Moses Kulola being the bishop of the four thousand churches, Assistant Bishop Mwaisabira.

Running four thousand churches has never been a simple that is why the division has been done of 34 counties of operation and five zones for simplifying work and every county and Zone has its own Overseer.

 

Biography of Rev. Roy Durman

Roy With Trophy Crutches Roy Durman was born in Guernsey, Channel Islands, U.K., where he accepted the Lord Jesus Christ as his Lord and Saviour. He was called to ministry and served the Lord in various Pastoral levels for a number of years.

Called to Evangelism

While serving as a Pastor in a New Zealand Church, Brother Roy received from the Lord, in a vision and words of knowledge, a specific word of his call to WORLD EVANGELISM through a ministry of signs and wonders. After waiting on God's timing for 20 years, he received word to commence.

Launching out into world crusades, Roy founded ROY DURMAN EVANGELISTIC WORLD OUTREACH INC., the ministry being interdenominational and transdenominational in outreach. He has now been in Christian service for many years, and continues to minister in world crusades with the same strength and enablement of the Holy Spirit as when he was much younger.

Ministry Outreach

The scope of this ministry has encompassed MASS CRUSADES in South, East, West and Central Africa, South and Central America, South East Asia, The Middle East, the North American continent, and Europe. IN MINISTERING THE GOSPEL, ROY HAS VISITED AT LEAST 62 COUNTRIES AROUND THE GLOBE, 88 AREAS OF THE WORLD, INCLUDING ISLANDS.

Crusade Aftermath

Crusade aftermath has produced conclusive evidence of the many outstanding miracles, which have taken place (in the Name of Jesus) in multitudes who have been healed of countless physical conditions, including blindness, deaf mutes, polio, cancer, … and many other incurable diseases too numerous to mention. Even the dead have been resurrected back to life! AS MANY AS 200,000 HAVE COME UNDER THE SOUND OF THE GOSPEL IN A SINGLE SERVICE. THOUSANDS HAVE FLOCKED TO CHRIST DURING THE CRUSADES, for which Roy ascribes TOTAL PRAISE AND HONOUR TO THE LORD JESUS CHRIST.

Activity of the Holy Spirit

Due to the activity of the Holy Spirit manifested in every crusade, he guarantees that people will see the POWER of the Holy Spirit healing people on the crusade platform, as well as in the crowd, as people dare to believe that God is able to do exceedingly abundantly above all we can ask or think. In every crusade conducted over the years, evidence of the dynamic power of Jesus Christ, the Son of God, has been manifested unto the glory of HIS great Name. HE alone is the Saviour and Miracle Worker.Roy Durman in Dar Es Salaam Crusade, Tanzania 

EVANGELISTIC WORLD OUTREACH

Rev. Roy Durman and his wife Georgette live in the Vancouver area of British Columbia in Canada and travel to the nations with a powerful anointing to bring souls to eternal salvation in Jesus Christ, to heal the blind, the deaf, the lame, and many other diseases, to set Satan's captives at liberty, through the power of Jesus' Name.

"For I am not ashamed of the gospel of Christ: for it is the power of God unto salvation to every one that believes; to the Jew first, and also to the Gentile." [Romans 1:16]

"And Jesus said unto them, 'I AM the bread of life: he that comes to me shall never hunger; and he that believes on me shall never thirst. … him that comes to me I will in no wise cast out. … And this is the will of him that sent me, that every one who sees the Son, and believes on him, may have everlasting life: and I will raise him up at the last day.'" [John 6:35, 37, & 40]

Brother Roy's adventures in ministry include being imprisoned in Egypt, stoned in India, sentenced to death in two countries by witch doctors, captured by guerillas in Uganda, Mafia bomb threats in Columbia, and through a timely word of warning from the Lord, he escaped being killed in an airplane crash. In excellent health, Roy continues in ministry with his wife Georgette, a woman who was specially set apart by God to be his companion and partner in life.

Sermons by Rev. Roy Durman

This page offers a selection of excellent sermons that were printed in Rev. Roy Durman's publications. They offer much wisdom that can be extremely valuable to all believers, particularly those who want to have a more intimate relationship with God and be equipped to spread the Good News of the Jesus Christ, with signs following. To access Brother Roy's sermons, click on the links below:

Home
Return to HOME

na mwl christopher mwakasege

 Je! Umewahi kujiuliza kwa nini wakati mwingine nguvu za Mungu zinakushukia kwa uwingi halafu baada ya muda zinapungua au zinaondoka – unabaki hali kama vile hujawahi kushukiwa hata siku moja? Inawezakana umewahi kujiuliza swali hili na inawezekana hujawahi kujiuliza. Na pia inawezekana hali hii tunayoiuliza hapa juu haijawahi kukutokea. Kumbuka kuwa nguvu za Mungu zinaweza kupungua ndani yako – kwa sababu mbalimbali – ambazo ni pamoja na kutozitumia kwa kiwango kilichokusudiwa. Unakumbuka Yesu alipoulilia mji wa Yerusalemu? Alisema; “Laiti ungalijua, hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani!” (Luka 19:42). Alichokuwa anataka wajue ni kwamba ndani yake kulikuwa na nguvu au upako wa Roho Mtakatifu uletao amani. Lakini tunaona wazi ya kuwa Yerusalemu hawakutumia upako huu na amani ya Mungu ikaondoka pia. Tatizo la Yerusalemu lilikuwa ni kwa sababu hakutambua majira ya ‘kujiliwa’ kwake. Kwa lugha nyingine Yerusalemu ‘ulijiliwa’ au ulitembelewa na nguvu za Mungu ziletazo amani – lakini hawakutambua! Na kwa sababu hawakutambua hilo, kwa hiyo hata nguvu za Mungu hawakuzitambua wala kuzitumia. – Kilichotokea ni kwamba nguvu hizo (1Wakorintho 1:18,24) ziliondoka wasiweze kuzitumia.

 

Tunaona pia katika Yohana 1:11 ya kuwa “ Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.” Yesu anaweza kuja kwako. Nguvu zake (ambazo ndizo nguvu za Roho Mtakatifu) zinaweza kuja kwako – usipozipokea itakuwa vigumu kuzitumia kwa kiwango kinachotakiwa. Maana katika mstari unaofuata wa 12, Yohana anaendelea kusema hivi: “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika …..” Ili uweze kuzipokea na kuzitumia nguvu za Mungu ipasavyo ni vizuri ujue Mungu amezituma nguvu zake kwetu kwa ajili ya nini. Zipo sababu nyingi katika biblia, lakini sisi tunataka tukupe angalau chache wakati huu ili ziwe changamoto kwako.

 

Sababu ya Kwanza: TUWE MASHAHIDI WAKE

Ili tuonekane na kujulikana ya kuwa sisi tu wanafunzi wa Yesu – tunachohitajika kufanya ni kupendana (Yohana 13:35). Huu ni upendo ambao watu wasiomjua huyu Mungu wetu  wanatakiwa wauone kwetu. Wakiona tunavyopendana, basi watajua ya kuwa sisi tu wanafunzi wa Yesu. Unapofanya sala ya toba na kumkaribisha Yesu katika maisha yako – unaokoka. Unaweza ukawa umeokoka lakini usiwe ‘mwanafunzi’ wa Kristo – kwa tafsiri ya Yesu juu ya nani ni mwanafunzi wake. Ikiwa umeokoka na huonyeshi upendo wa Kristo kwa waliookoka wenzako unapoteza hadhi ya kuwa mwanafunzi wa Kristo. Inapofika hali ya kuwa ‘shahidi’ inabidi upokee nguvu za Roho Mtakatifu. Yesu alisema katika kitabu cha Matendo ya Mitume 1:8 ya kuwa: “ Lakini mtapokea nguvu,; akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” Kazi ya shahidi ni kusimama upande wa anayeshitaki au anayeshitakiwa kumtetea huyo ambaye ameamua kuwa shahidi upande wake – akisema na kwa kuonyesha vithibitisho ili kusisitiza kuwa anachokitetea ndicho sahihi. Katika mazingira ya Bwana Yesu, sisi tunakuwa mashahidi kwa kusema na kuonyesha au kuthibisha kwa vitendo ya kuwa yote ambayo Yesu Kristo amesema na yamefanyika juu yake ndivyo yalivyo, na ndiyo kweli inayotakiwa kufuatwa na kila anayemtafuta Mungu wa kweli. Nguvu za Roho Mtakatifu zinatufanya tuweze kusimama katika nafasi ya kuwa mashahidi wa Kristo.

 

Sababu ya Pili: Kushinda Dhambi

Ndiyo! Kushinda dhambi. Unaweza kuishinda dhambi. Katika Mwanzo 4:7 tunaambiwa inatupasa au ni lazima tuishinde dhambi. Mungu hawezi kusema tuishinde dhambi kama hakuna mbinu ya sisi kuishinda dhambi. Pia, katika Warumi tunaambiwa ya kuwa dhambi haitatutawala. Lakini ni lazima tujue ya kuwa hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuishinda dhambi kwa nguvu zake mwenyewe. Kila mtu lazima ajue kuzitumainia nguvu za Mungu tunazozipata katika Roho Mtakatifu kwa sababu ya Kristo kufa msalabani kwa ajili yetu. Ndiyo maana imeandikwa hivi katika 1 Wakorintho 1:18,23,24: “ Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookokolewa ni nguvu ya Mungu …… sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.” Hiki ndicho kinachotokea unapookoka; Kristo anaingia ndani yako kwa uwezo wa Roho Mtakatifu- anakuwa nguvu ya Mungu inayokuwezesha kushinda dhambi. Kwa hiyo kama iko dhambi inayokusumbua – tubu, halafu omba Mungu akuongezee nguvu za Roho wake ili upate kushinda dhambi.

 

Sababu ya Tatu: Kuwa Tajiri

Jambo mojawapo lililotokea kwa mwanadamu dhambi ilipoingia ni kuishi maisha ya umaskini na kupungukiwa. Dhambi pia iliweka matabaka ya matajiri na maskini. Toka mwanzo na hata sasa na siku zote Mungu hapendi watu wake wawe maskini (kwa jinsi ya mwili) Katika 2 Wakorintho 8:9 tunasoma ya kuwa: “ Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” Kwa hiyo ni mapenzi ya Mungu tuwe matajiri. Njia ambayo Mungu anatumia kutuwezesha tuwe matajiri ni kwa kutupa nguvu zake. Kwa maana imeandikwa katika kitabu cha Kumbukumbu ya Torati 8:18 ya kuwa: “Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” Tunasoma hapa ya kuwa tunaweza kuomba tupate msaada wa nguvu za Mungu ili tupate utajiri halali ndani ya Kristo.

 

Sababu ya Nne: Kushinda hila za shetani

Tunasoma katika kitabu cha Waefeso 6:10,11 ya kuwa: “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani” Haitoshi kupokea nguvu za Roho Mtakatifu bila kuwa hodari katika kuzitumia ili upate “kuweza kuzipinga hila za shetani” Ili uwe hodari katika mchezo fulani lazima ufanye mazoezi ya kutosha ili kujifunza mbinu za kukusaidia kushinda upinzani katika mashindano. Pia, katika mambo ya rohoni ni vivyo hivyo. Ili uwe hodari katika uweza wa nguvu za Mungu – haitoshi tu kuzipokea kwa kujazwa Roho Mtakatifu. Bali ni muhimu kufanya ‘mazoezi’ sawa na neno la Mungu ili uwe hodari. Hii ndiyo maana unaweza ukajawa nguvu za Mungu na bado shetani akakushinda na hila zake. Kwa nini? Kwa sababu hujazwa hodari katika kuzitumia. Hii ni sawa na mtu kuwa na silaha yenye nguvu vitani lakini kwa sababu hajui kuitumia ipasavyo anajikuta ameshindwa vita! Nguvu za Roho Mtakatifu zipo pia kwa ajili ya kutusaidia kumshinda shetani na hila zake dhidi ya maisha yetu. Lakini ni muhimu tujue kuzitumia sawa na neno la Mungu – tuwe hodari katika uweza wa nguvu zake. La sivyo tutakuwa tunashindwa na shetani wakati tunazo nguvu za kumshinda ndani yetu.

 

Sababu ya Tano: Kudumu katika maombi

Kila mtu aliyeokoka ndani yake anahamu ya kufanya maombi – kuzungumza na Mungu. Lakini karibu kila mtu anajua ya kuwa kila akiomba anatamani angeweza kuomba vizuri zaidi, kuliko anavyoomba wakati huo.

Jambo hili la kuwa na upungufu katika maombi lisikushangaze. Biblia inatuambia; “…. Hatujui kuomba jinsi itupasavyo ….” (Warumi 8:26). Kazi ya Roho Mtakatifu ni kutusaidia udhaifu huu tulionao wa kuomba – ili kwa nguvu zake tuweze kuomba utupasavyo, na pia tuweze kuwaombea “watakatifu kama apendavyo Mungu” (Warumi 8:27). uzuri wa maombi si tu kwamba ni sababu ya Mungu kutupa Roho wake ili kwa msaada wa nguvu zake tuweze kuomba itupasavyo; bali maombi pia ni njia au mlango wa nguvu za Mungu kuongezeka katika maisha yetu. Ndiyo maana mara nyingi ukikaa katika maombi muda mrefu zaidi – nguvu za Mungu zinaongezeka. Lengo la nguvu hizi kuongezeka ni ili uendelee kuomba kama impendezavyo Mungu hadi upate unachoomba. Kwa mfano, kama nguvu za Mungu ni kidogo ndani yako – hasa wakati umo taabuni au katika majaribu – ni rahisi sana ‘kuzimia’ au kukata tamaa. Imeandikwa hivi: “Ukizimia siku ya taabu, nguvu zako ni chache” (Mithali 24:10) “Bali vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka, bali waowamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia” (Isaya 40:30,31) Nguvu za Mungu ndani yako zitakusaidia usizimie wala usichoke wala usikate tamaa iwe ni wakati wa raha au wakati wa taabu. Ukiona unachoka au unakata tamaa maana yake una nguvu kidogo au zimepungua – kwa hiyo omba Mungu akuongezee nguvu zake ili usichoke wala kuzimia wala kukata tamaa.

 

Sababu ya Sita: Kuondoa woga

Mtume Paulo aliwahi kumwandikia Timotheo maneno muhimu sana ambayo yanasema na watu wengi hata sasa aliposema; “ Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi” (2 Timotheo 1:7) Timotheo asingeandikiwa maneno haya kama hakuwa mwoga! Inaonyesha alikuwa mwoga kuichochea ‘karama ya Mungu’ iliyokuwa ndani yake! (2 Timotheo 1:6) Kama alikuwa mwoga basi hali hii ilifanya utumishi wake ulegee. Hii inawezekana ilitokea kwa sababu aliona na kushuhudia mateso aliyopata Mtume Paulo alipochochea karama ya Mungu iliyokuwa ndani yake. Kwa kuogopa kuteswa na yeye kama Mtume Paulo, aliamua kuacha kuchochea karama ya Mungu iliyokuwa ndani yake. Ndiyo maana Mtume Paulo  alimhimiza aichochee hiyo karama “….maana Mungu hakutupa roho ya woga bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi” Kama unasikia woga wa kumtumikia Mungu kwa sababu moja au nyingine hauko peke yako. Dawa yake ni nguvu za Mungu ziongezeke ndani yake- na woga huo utaondoka! Timotheo alibanwa na woga. Lakini pia Yoshua alipokuwa anakabidhiwa wajibu wa kuongoza wana wa Israeli baada ya Musa kufa – alishikwa na woga! La sivyo Mungu asingemwambia awe na moyo wa ushujaa mara tatu! (Yoshua 1:6,7,9). Yeremia naye alipokuwa anapewa wajibu wa kumtumikia Mungu akiwa bado mtoto – aliingiwa na woga! Lakini Mungu akamwambia – “Usiogope” (Yeremia 1:4-10). Kwa hiyo kama unasikia woga katika kumtumikia Mungu – omba ili Mungu akupe nguvu zake zaidi ili ziondoe woga. Jambo hili liliwahi kumtokea Mtume Petro. Pamoja na kwamba alimpenda Yesu sana na kuahidi kuwa naye kila mahali – bado woga ulimwingia alipoulizwa kama alimjua Yesu wakati Yesu amekamatwa. Lakini  baada ya kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste hatuoni tena woga ukijitokeza ndani yake – bali tunaona ujasiri mwingi.

Mwl Christopher Mwakasege atoa shuhuda juu ya kifo Fanuel Sedekia

Alisema Roho mtakatifu akwambiavyo omba hiyo haina MJADALA ni kuingia kwenye maombi mpaka upate unachokiomba kwa kuwa gharama ya kuingia kwenye maombi ili kupata ulichotakiwa kukipata ni ndogo kuliko gharama ya kukosa kile ulichoambiwa ukipate katika Maombi hayo.
Roho mtakatifu anapokupa mzigo wa kuombea jambo anakupa na muda ukizembea  muda huo ukipita kinakuwa ni kiporo, na kiporo kinaweza kikalika na kipo ambacho hakiliki.  .
“Tulipoenda Israel na Fanuel Sedekia kisha akaanza kuumwa madaktari waliniambia ubongo wake kwa asilimia tisini haufanyi kazi. Lakini walishangaa kwa nini kila mara niko pale Hospitali wakasema kwa nini usikae tu Hotelini kisha ukawa unapiga simu kuulizia hali ya Mgonjwa? Wao hawakujua kwa nini naenda pale kwa kuwa suala la kupiga simu tu sio tatizo ningeweza kurudi Arusha kisha nikawa napiga simu.
Suala hapa ni kuwa nilikuwa naenda kila mara kwa ajili ya kumfanyia maombi, nilikuwa nakaa kandokando ya Bahari ya Galilaya nafanya maombi juu ya Sedikia kwa masaa sita nikitoka hapo nasikia upako wa ajabu sana kIsha napanda Taxi kuelekea Hospitali. Nikifika Hospitali madactari na watu wa ICU walikuwa washanifahamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye chumba cha nguo nabadili nguo kIsha naingia ICU alikolazwa.
Nikifika nambana Mungu kwa maswali Mengi namuuliza Sedekia, hivi unaongea nini na Yesu muda wote huo si urudi? na kisha namuuliza Yesu, hivi Yesu si unafahamu kuwa Sedekia anamke ukimchukua mkewe atamuachia nani? Kisha baada ya maneno hayo naweka mkono juu yake. Nilipokuwa nikiweka mkono juu yake ghafla upako wote unakuwa kama umenyonywa.
Baada ya hapo narudi hotelini naanza tena kumuuliza Mungu hivi Mungu kama basi husikii maombi yangu sikia maombi ya watanzania kwa kuwa saa hiyo nilijua watanzania wengi wanamuombea Sedekia.
Inafikia wakati nakata tamaa lakini ndani yangu najisemea Mwakasege haiwezekani jitie moyo kisha nabadili aina ya maombi, kwa kuwa nilikuwa na nguo zake pamoja na passport yake nikawa naviweka kati kisha nikawa naanza maombi ya Yeriko, nikawa niko hotelini usiku nazunguka nguo zake na paspot yake huku nikifanya maombi.
Taratibu Mungu akaanza kuniambia kuwa sedekia harudi, Kipidi hicho mimi na familia yangu tulikuwa tumepanga kwenda kupumzika nchini Uingereza wakati wa skukuu ya Chrismass,  na booking mpaka ya Hotel tulikuwa tumeshafanya, na watoto wote wako nyumbani wakijiuliza tunaendaje kupumzika wakati Sedekia anaumwa? Chrismass ikapita na mwaka mpya pia kisha Sedekia akafariki.
Baada ya kifo hicho sikuchoka nkarudi tena kwa Mungu nikamuuliza kwa nini Mungu umeamua kumchukua Sedekia mikononi mwangu? Mungu alinijibu vitu ambavyo siwezi kuvisema hapa.
Kila siku mimi ni mgeni katika maombi namhitaji ROHO anifundishe kwa upya kwa kuwa sijui vita gani ninakwenda kupambana nayo, Mungu anabaki kuwa Mungu kwa kuwa hufanya atakavyo”


NINI MAANA YA KUMPENDA BWANA?

Kumbukumbu la Torati 6:5 Nawe, mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote na Pia ile Mathayo 22:37 inasema Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote”. Hivyo basi kwa kutumia hiyo mistari miwili tunaona kwamba mtu anatakiwa kumpenda Bwana Mungu wake kwa;

Moyo wake wote, Roho yake yote, Nguvu zake zote, Na akili zake zote.
Lakini pia ukisoma kile kitabu cha 1 Yohana 5:3 Biblia inasema “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba, tuzishike amri zake, wala amri zake si nzito”. Hivyo basi kumpenda Mungu ni kuzishika amri zake. Sasa kuzishika amri za Mungu ni suala linalohitaji Moyo wako, roho yako, nguvu zako na akili zako vyote kwa pamoja vifanye kazi ya kumpenda Mungu kwa maana ya kuzishika amri zake.

*Kumpenda Bwana kwa moyo wako.
Kumpenda Bwana kwa moyo wako ni kwa kuutafakarisha moyo wako amri za Bwana kwa maana ya maagizo yake unayotakiwa kuyashika. Hii ni pamoja na kutumia muda wako siku zote kuliweka neno la kristo kwa wingi ndani yako kwa kulitafakari. Unapolitafakari neno la Bwana ndipo pia unapopata mawazo na njia za Mungu za kukufanikisha kimaisha. Zaburi 27:4.

*Kumpenda Bwana kwa roho yako.
Hapa unatakiwa kuitafakarisha roho yako neno la Bwana ambalo linazungumzia wakati ujao (future yako) ishibishe roho yako ahadi za Mungu ili imani yako iongezeke na uanze kuona mambo ya wakati ujao kana kwamba yapo halisi kwa wakati wa sasa. Hili litakusaidia kuishi kwa Imani, maana siku zote utakuwa unafanya yale yanayompendeza Mungu.

*Kumpenda Bwana kwa nguvu zako zote.
Nguvu ni uwezo alionao mtu katika kufanya kazi fulani. Sasa tumia nguvu zako zote za kimwili za kiufahamu, za kifedha nk katika kutekeleza yale yote ambayo neno la Mungu linakuagiza kila siku unapolitafakari kumbuka nimekuambia katika kulitafakari neno la Bwana utapata mawazo ya Bwana juu yako na ndani ya hayo mawazo kuna mipango na mikakati ya kuitekeleza.

*Kumpenda Bwana kwa akili zako zote.
Vile vile akili ni uwezo wa kiufahamu alionao mtu katika kufanya mambo. Hivyo basi wakati unatumia nguvu kutekeleza maagizo ya Bwana basi hakikisha unatekeleza kwa kutumia akili ili ufanye kitu sahihi, kwa wakati sahihi na kwa usahihi.

 

imani ihamishayo milima

MARKO 11: 20- 24.

20. Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. 21. Haya ni matokeo ya Bwana Yesu kuulaani mtini usitoe matunda tena. Alisema neno tu juu ya huo mti, na kesho yake umenyauka! Petro akakumbuka habari yake,akamwambia, Rabbi, tazama mtini ulio ulaani umekauka. Mtini ulikuwa mlengwa wa imani itendayo kazi. Hapa Petro anaona jinsi Neno la Bwana Yesu lilivyokausha mtini ingawa bado haelewi kilicho tokea. Petro anachokumbuka ni Bwana Yesu kuulaani mtini, na kesho yake kukauka. 22. Yesu akajibu akawaambia, Mwaminini Mungu.

Hili ni Neno kubwa analosema Bwana Yesu. Wakati wanafunzi wanashangaa kukauka kwa mtini, wanaambiwa wa mwamini Mungu, kwani imani isiyomtegemea Mungu ni batili na butu. Kumwamini Mungu ni zaidi ya kumwamini kwa kukiri tu kwa kinywa, ni zaidi ya kuamini moyoni mwako. Imani hii anayoizungumzia Bwana Yesu hapa ni ile ya utendaji, yaani imani inayomfanya Mungu kutenda miujiza. Ni imani inayokufanya kuchukua hatua ukijua kwa hakika Mungu atafanya. Ukitaka kuhamisha milima katika maisha yako, ni lazima umwamini Mungu, na sio uwezo wako wala watu.

23. Amini nawaambia,Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ngo’ka ukatupwe baharini wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia yatakuwa yake.  Maelezo haya ndio yenye siri ya ushindi kwa watoto wa Mungu. Bwana Yesu anatuonyesha sumu iuayo imani, yaani mashaka. Mashaka maana yake ni sawa na kumwambia Mungu kwa vitendo kwamba hauamini kuwa atafanya lile unalomwomba akufanyie. Unaweza kusema kwa mdomo na hata kufikiri kuwa moyoni mwako una mwamini Mungu, lakini kile utakachokifanya ndicho kitakachoonyesha kwa uhakika kama unamwamini Mungu au unaenenda kwa mashaka.

• Jambo la pili hapa ambalo ni la muhimu kuelewa ni kuwa anayehamisha milima katika maisha yako ni Mungu, hivyo katika imani yako unatakuwa kutambua kuwa Mungu atahamisha huu milima ulio mbele yangu ni kuamini kwa vitendo. Na hili hutendeka vipi? Kama nina milima katika maisha yangu, nikamwomba Mungu aihamishe, baada ya maombi hayo, nisiendelee tena kuishi au kuongea kama mtu ambaye bado anakabiliwa na milima, kwani tayari nilikwisha mwamini Mungu kuuondoa huo mlima, na hakika Mungu atauondoa!

24. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu. Hapa tunapewa uthibitisho wa uaminifu wa Mungu katika kujibu maombi yetu tukiamini kwa vitendo. Mashaka ni sumu ya imani kiasi kwamba imetunyima Baraka nyingi toka kwa Mungu. Angalia ahadi hiyo ya Mungu hapo juu, kwamba tukiomba lo lote na kujua kwamba anayetupatia ni Mungu, tutapokea. Mashaka hutuambia kuwa hilo haliwezekani, yaani kuna wakati Mungu atajibu na kuna wakati hatakujibu; kama hivyo ndivyo unavyojisikia wakati unamwomba Mungu ikatae roho hiyo kwani hayo ni mshaka.

Neno la mwisho kuhusu roho ya mashaka:  “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima na aombe dua kwa Mungu awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote, maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama Yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.” (Yakobo 1:5-7)

njia ya kweli na uzima

Kuna sauti nyingi zidanganyazo zikidai kuwa imani au dini yao ndiyo bora kuliko zingine na hata zingine kudai mtume wao ndiyo wa mwisho kuja duniani na anapashwa kufuatwa huyo, na kusababisha hata (wakristo jina) kupoteza muelekeo na kuona labda kuna ukweli ndani na kuiacha ile kweli.kwanza tujiulize je MUNGU baba wa yesu kristo aliyeumba mbingu na dunia anayosifa ipi?na sifa za hao miungu wengine bandia zikoje?sasa kwa nini mtu afikirie kuhusu Yesu huko juu, wakati Muhammad au Confucius (Mwana filosofia Fulani wa china), Buddha, au Charles Taze Russell, au Joseph Smith? Kwani hata hao si njia zote zinaelekea Mbinguni? Kwani si Dini zote ziko sawa? Ukweli ni kwamba Dini zote hazielekei Mbinguni kama jinsi ambavyo njia zote hazielekei kariakoo.

 Yohana 14:   1Yesu akawaambia, ``Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. 2Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. 3Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.'' 5Tomaso akamwuliza, ``Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?'' 6Yesu akawaambia, ``Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.''

   8Filipo akamwambia Yesu, ``Bwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.'' 9 Yesu akamjibu, ``Filipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, `Tuonyeshe Baba'? 10Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote.

Yesu pekee huzungumza kwa mamlaka ya Mungu kwasababu Yesu peke yake alishinda mauti. Muhammad,Confucius (Mwana filosofia Fulani wa china), na wengineo wanaendelea kubadilika kuwa mavumbi makaburini mwao mpaka leo hii, lakini Yesu, kwa nguvu zake, alitoka kaburini siku ya tatu baada ya kufa juu ya msalaba wa warumi uliojaa dhiki. Ni Yesu  pekee mwenye uwezo juu ya mauti, anastahili usikivu wetu. Ni Yesu pekee astahiliye kusikizwa.

Ushahidi unaosimamia kufufuka kwa Yesu Kristo ni wa ushindi mkuu na haupingiki. Mwanzo, palikuwa na mashahidi zaidi ya mia tano waliokuwa wamefufuka kwa Kristo! Hao ni mashahidi wengi waliojionea kwa macho. Sauti mia tano haziwezi kupuuziwa. Pia kunalo jambo la kaburi lililokuwa tupu; maadui zake Yesu wangelikuwa wamesimamisha kwa njia ya rahisi habari zote za ufufuo kwa kuonyesha mwili wake , mwili uliooza kama ushahidi, lakini hawakuwa na mwili wowote wa kuonyesha! Kaburi lilikuwa tupu! Je, pengine mitume walikuwa wameuiba mwili? Ni vigumu. Kwa kuzuia uvumi huu usiokuwa wa kweli,kaburi lake Yesu lilikuwa limelindwa vilivyo na Askari waliokuwa wamejihami. Ukichunguza utaona marafiki wake wa karibu walikuwa wametoroka kwa uoga wa kukamatwa kwake na kusulubishwa, haingelikuwa rahisi kwa wavuvi waliokuwa wamevunjika moyo na kutishika, kupambana ana kwa ana na askari waliofunzwa,na wenye ujuzi. Ukweli wa mambo nikwamba ufufuo wa Yesu hauwezi kubatilishwa!

Tena, Yesu ndiye mwenye mamlaka juu ya mauti astahili kusikilizwa.Yesu alithibitisha nguvu zake juu ya mauti, kwahivyo, twahitaji kusikia kile asemacho. Yesu asema ndiye njia ya pekee ya uzimani (Yohana 14:6). Yeye si njia tu; Yeye si mmoja kati ya njia nyingi, lakini Yesu ndiye njia.

Na Yesu huyu asema hivi, “Njoni kwangu,ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha’’ (Mathayo 11:28). Huu ni Ulimwengu mzito na maisha ni magumu. Wengi wetu tumefanyiwa madhambi, tumejeruhiwa, na tumetishika kivita. Ni kweli? Sasa, unataka nini? Uregesho ama dini tu? Mwokozi aishiye au Mmoja kati ya “Mitume’’ wengi waliokufa? Uhusiano wa maana au Kafara za utupu? Yesu si chaguo tu, Yeye ndiye chaguo!

Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta msamaha (Matendo 10:43). Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta uhusiano wa maana na Mungu (Yohana 10:10). Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta uzima wa milele Mbinguni (Yohana 3:16). Weka imani yako kwa Yesu kama Mwokozi wako-hutajilaumu! Mwamini yeye kwa msamaha wa dhambi zako-hutaaibika.

Kama ungelitaka kuwa na Uhusiano  na Mungu,fuatisha Maombi haya. Kumbuka ya kwamba kwa kuomba Ombi hili au Ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyostahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa Neema yako ya ajabu na kwa msamaha-karama ya uzima wa milele! Amina!’

luka 17

11Yesu alipokuwa akienda Yerusalemu alipitia kati ya Samaria na Galilaya. 12Alipokuwa akikaribia kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma walikutana naye. 13Wakasimama mbali wakaita kwa nguvu, ``Yesu! Bwana! tuonee huruma!'' 14Alipowaona akawaambia, ``Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.'' Na walipokuwa wakienda, wakapona ukoma wao. 15 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Yesu akimsifu Mungu kwa sauti kuu. 16Kwa heshima kubwa akajitupa miguuni kwa Yesu akamshukuru. Yeye alikuwa ni Msamaria .

   17Yesu akauliza, ``Hawakuponywa wote kumi? Wako wapi wale tisa wengine? 18Hakuna hata mmoja aliyekumbuka kurudi kumsifu Mungu isipokuwa huyu mgeni?'' 19Akamwambia, ``Inuka, uende; imani yako imekuponya.'' Ufalme Wa Mungu Utakavyokuja

   20Siku moja, Mafarisayo walipomwuliza Yesu Ufalme wa Mungu utakuja lini, aliwajibu hivi: ``Ufalme wa Mungu hauji kwa kuone kana, 21wala watu hawatasema, `Huu hapa' au `Ule kule' kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.''

   22Kisha akawaambia wanafunzi wake, ``Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona siku yangu moja, mimi Mwana wa Adamu lakini hamtaiona. 23Watu watawaambia, `Yule pale' au, `Huyu hapa!' Msiwa kimbilie. 24Kwa maana kama umeme unavyomulika mbingu kutoka upande mmoja hadi mwingine, ndivyo itakavyokuwa siku ya kuja kwangu, mimi Mwana wa Adamu. 25 Lakini kwanza itanipasa nite seke sana na kukataliwa na watu wa kizazi hiki. 26Kama ilivyokuwa nyakati za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku ya kurudi kwangu, mimi Mwana wa Adamu. 27Wakati wa Nuhu watu walikuwa wakila, wakinywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo mafuriko yakaja yakawaangamiza wote. 28Hata nyakati za Lutu ilikuwa hivyo hivyo. Watu walikuwa wakila, waki nywa, wakifanya biashara, wakilima na kujenga. 29Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, moto ulishuka kutoka mbinguni uka waangamiza wote. 30Ndivyo itakavyokuwa siku ambapo mimi Mwana wa Adamu nitakapotokea kwa utukufu.

   31``Siku hiyo, mtu akiwa darini na vitu vyake vikiwa ndani, asiteremke kuvichukua. Hali kadhalika atakayekuwa shambani asirudi nyumbani kuchukua chochote. 32Kumbukeni yaliyompata mke wa Lutu! 33Mtu yeyote anayejaribu kusalimisha maisha yake atayapoteza; na ye yote atakayekuwa tayari kuyapoteza maisha yake atayaokoa. 34Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 35 Wana wake wawili watakuwa wanatwanga pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.'' [ 36Wanaume wawili watakuwa wanafanyakazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.] 37Wakamwuliza, ``Haya yatatokea wapi Bwana?'' Akawaambia, ``Pale ulipo mzoga, ndipo tai wanapokutanika.'' Mfano Wa Hakimu Dhalimu

je ni vyema?

MCHUNGAJI wa Kanisa la EAGT lillilopo Mtaa wa Ichenjezya, mjini Vwawa, wilayani Mbozi, Mbeya, Simon Kitwike (48), amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukataa kuapa ili atoe ushahidi mahakamani.

Mchungaji huyo, alihukumiwa kifungo hicho na Hakimu Kajanja Nyasige wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi.

Kitwike, aliyevunjiwa nyumba yake mwishoni mwa mwaka jana na kuibiwa mali kadhaa , alifika mahakamani hapo, ili kutoa ushahidi wake, lakini alikataa kuapa kabla ya kutoa ushahidi wake akidai ni dhambi.

Hakimu Nyasige, alimwamuru asome kifungu katika Biblia kinachomtaka asiape mahakamani, ndipo mchungaji huyo alifungua Mathayo 5: 35 na kudai ndicho kinachompa msimamo huo.

Baada ya kusoma kifungu hicho, Hakimu Nyasige alimuuliza tena kama atakuwa tayari kuapa, ili atoe ushahidi, lakini mchungaji huyo aliendelea kubaki na msimamo wake wa kukataa kuapa.

Ndipo hakimu huyo alimsomea kifungu cha sheria na 198 (1) kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 kinachokataza mtu kudharau mahakama na kuwa kuendelea kukataa kuapa ni kuvunja sheria na hivyo ametenda kosa la jinai.

Hata hivyo, Hakimu Nyasige aliendelea kumvumilia mchungaji huyo, ili abadili msimamo wake kwa kumwamuru kusoma Biblia hiyo tena Waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi 13:1- 5, shahidi huyo alisoma kifungu hicho, lakini alipoulizwa kama amebadili msimamo wake alijibu kuwa hawezi kubadili msimamo wake.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Nyasige aalimtia hatiani kutokana na kumuamuru kwenda jela miezi sita na atatakiwa kufika mahakamani tena baada ya kumaliza kifungo  ili atoe ushahidi wake kwa kesi ya msingi.

Akizungumza na mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mchungaji Mwandamizi wa kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwakasaka, alisema amesikitishwa na hukumu hiyo na kudai mchungaji wake alielewa vibaya vifungu vya Biblia vinavyozungumzia viapo.

Naye Mchungaji Erasto Makalla wa Kanisa la Pentekoste, alieleza kusikitishwa kwake na hatua hiyo ya mchungaji kupingana na mamlaka ya serikali na akasema kuna haja ya kuwafanyia semina wachungaji ili waelewe taratibu za serikali.

O Lord Your Beautiful (worship video w/ lyrics)

mtafuteni bwana

Kama Abraham alivyokuwa "rafiki Wa Mungu" kwa uvumilivu na utiifu kwa Mungu, wewe pia unaweza kumjua Mungu na kupata rehema zake, amani, na baraka. Kumjua Mungu kwa uvumilivu wa kweli katika kumwamini ni ujuzi muhimu zaidi katika maisha. Ni ajabu namna gani kwamba Mungu hujidhihirisha Mwenyewe kwa wote wanao Mtafuta kwa mioyo yao yote! Ikiwa utageuka kuiacha njia yako na kweli kujitolea kwa Mungu, Roho Wake ataishi ndani yako. Hakuna kitakacho kutenganisha na upendo Wake unapo tumainia ahadi Zake na Kumfuata kwa utiifu. Yeye atakuwa Mungu wako, nawe utakuwa hazina Yake Mwenyewe. Utagundua kwamba alikununua kwa gharama kuu, na anataka kuwa na ushirika nawe—sasa na hata milele. Uliza Mungu akupe ufahamu unapojifunza kurasa hizi za vifungu kutoka Neno la Mungu. Mungu aliongoza watu wamchao kuandika maneno haya na kwa kimiujiza ameyahifadhi katika vizazi vyote kutoka kwa majaribio yote ya Shetani ya kuyakomesha. ______________________________________________________________ Maandiko yanayo husika katika kijitabu hiki yametolewa kutoka Biblia: Sheria (Torah), Zaburi (Zabur), maandiko ya manabii, na Injili (Injil). KUNA MUNGU WA KWELI MMOJA TU — 1 Kumbukumbu La Torati 6:4, 5 BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Isaya 45:18 Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine. 1 Wafalme 8:60 Watu wote wa ulimwengu Wajue ya kuwa BWANA ndiye Mungu; hakuna mwingine. Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. —Isaya 42:8 Isaya 43:10, 11 Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA,. . . mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi. Isaya 45:22 Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine. MUNGU NI WA REHEMA NA NEEMA — 2 Zaburi 103:8, 11 BWANA amejaa huruma na neema, haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, kadiri ileile rehema zake ni kuu kwa Wamchao. Zaburi 103:17, 18 Bali fadhili za BWANA zina Wamchao tangu milele hata milele,...maana, wale walishikao agano lake, na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye. Mika 7:18 Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu,...kwa maana yeye hufurahia rehema. Maombolezo 3:22 Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi. Maombolezo 3:32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Zaburi 18:25 Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili. 1 Mambo Ya Nyakati 16:34 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele. MUNGU ANAKUPENDA — 3 Yeremia 31:3 BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu. Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani, wala Si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Malaki 1:2 Nimewapenda ninyi, asema BWANA. Zaburi 103:13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Isaya 38:17 Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda [ee Mungu] umeniokoa na shimo la uharibifu; kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako. 1 Yohana 4:16, 19 Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Sefania 3:17 BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa furaha kuu, atatulia katika upendo wake. Atakufurahia kwa kuimba. JAMBO KUBWA MUHIMU MAISHANI NI KUMJUA MUNGU — 4 Danieli 11:32 Lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu. Yeremia 9:24 Bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA. Kumbukumbu La Torati 30:19, 20 Nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake na kushikamana naye: kwani hiyo ndiyo uzima wako. Zaburi 119:2 Heri wazitiio shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wote. Zaburi 42:1 Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Kutoka 33:14 Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. KUJITEGEMEA PASIPO MUNGU NI KUANGAMIA — 5 2 Mambo Ya Nyakati 15:2 BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi. Yeremia 17:9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mithali 16:25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; lakini mwisho wake ni njia za mauti. 2 Petro 2:4, 9 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu. Basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu. 1 Samweli 12:15 Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu. Yohana 15:6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatu. pa motoni yakateketea. KUMJUA MUNGU NI LAZIMA TUMTAFUTE — 6 Yeremia 29:13 Nanyi mtanitafuta, na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Mithali 2:4, 5 Ukiutafuta kama fedha, . . . ndipo utakapo . . . pata kumjua Mungu. Mathayo 7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Mithali 8:17 Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Maombolezo 3:25 BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, kwa hiyo nafsi imtafutayo. Matendo 17:26, 27 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja. ...Ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. MUNGU ANATUTAKA TWENDE KWAKE — 7 2 Mambo Ya Nyakati 30:9 Kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye mwenye neema, na mwenye rehema, wala hatawageuzia mbali uso wake, mkimrudia. Zaburi 86:5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao. Yakobo 4:8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Zaburi 145:18 BWANA yu karibu na wote Wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu. Isaya 1:18 Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Mathayo 11:28, 29 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Yohana 6:37 Wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. MUNGU NI MTAKATIFU — 8 Kutoka 15:11 . . . Ni nani aliye kama wewe, Ee BWANA, . . . mtukufu katika utakatifu. 1 Samweli 2:2 Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; kwa maana hakuna ye yote ila wewe. Ayubu 34:10 Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu; wala Mwenyezi kuf anya uovu. Isaya 6:3 Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake. Isaya 57:15 Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu. Zaburi 145:17 BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote. Marko 10:18 Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. Ufunuo 15:4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu. WATU WA MUNGU NI LAZIMA WAISHI MAISHA MATAKATIFU — 9 Yakobo 2:19, 20 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? 1 Yohana 2:4; 3:10 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; bali humpenda mtu afuatiaye wema. —Mithali 15:9 Waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. —1 Petro 1:15 Amosi 5:14 Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo BWANA, Mungu wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo. MAMBO MUNGU ANAYOAMURU — 10 Mika 6:8 Na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako! Mambo Ya Walawi 19:2 Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu. Luka 10:27 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. Marko 10:19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usi danganye, Waheshimu baba yako na mama yako. Warumi 12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Yoshua 1:8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Marko 11:22 Mwaminini Mungu. MAMBO MUNGU ANAYOCHUKIA — 11 Mithali 6:16-19 Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; moyo uwazao mawazo mabaya; miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; shahidi wa uongo asemaye uongo; naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu. Isaya 61:8 Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wivi na uovu. Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. Malaki 2:15, 16 Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA. Zekaria 8:17 Wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA. WATU HUPUNGUKIWA NA MATAKWA YA MUNGU — 12 Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. —Yohana 5:42 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. —Yakobo 2:10 Isaya 6:5 Ndipo niliposema, Ole wangu! kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi. Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. —Yakobo 4:17 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, hakuna mwenye haki hata mmoja. —Warumi 3:10 Warumi 3:23 Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. 1 Yohana 3:10 Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. Isaya 53:6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe. Ni nani awezaye kusimama mbele za BWANA, huyu Mungu mtakatifu? —1 Samweli 6:20 KAZI ZETU WENYEWE HAZIWEZI KUMPENDEZA MUNGU — 13 Warumi 10:2, 3 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Isaya 64:6 Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi. Ezekieli 33:13 Nimwambiapo mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo. Warumi 8:8; 3:20 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria. 2 Wakorintho 3:5 Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. DHAMBI HUTUTENGANISHA NA MUNGU — 14 Warumi 5:12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. Yakobo 1:15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ezekieli 18:20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa. Isaya 59:2 Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Mithali 11:19 Haki huelekea uzima; afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe. 2 Mambo Ya Nyakati 24:20 Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za BWANA, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi. 1 Samweli 15:23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, yeye naye amekukataa wewe. GHADHABU YA MUNGU JUU YA DHAMBI — 15 Zaburi 7:11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, naam, Mungu aghadhibikaye kila siku. Nahumu 1:3 BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe. Wakolosai 3:6 Kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu. Warumi 1:18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Warumi 1:29-32 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao. HUKUMU IKO MBELE — 16 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu. —Waebrania 9:27 Ufunuo 20:12, 15 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. Waebrania 10:31 Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai. Mathayo 12:36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la sir likiwa jema au likiwa baya. —Mhubiri 12:14 Mathayo 13:49, 50 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. HATUWEZI KUJIFICHA KUTOKANA NA MUNGU — 17 Mithali 15:3 Macho ya BWANA yako kila mahali; yakimchunguza mbaya na mwema. Zaburi 139:1-4 Ee BWANA, umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, umeelewa na njia zangu zote. Maana hamna neno ulimini mwangu usilolijua kabisa, BWANA. 1 Samweli 16:7 Kwakuwa BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo. Zaburi 94:9 Aliyelitia sikio mahali pake asisikie? Aliyelifanya jicho asione? Yeremia 16:17 Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote; hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone. Waebrania 4:13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. KUGEUKA NA KUTOKA DHAMBINI KUNAHITAJIKA — 18 Ezekieli 18:23 Je! mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi? Luka 13:3 Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Mithali 28:13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. Yoeli 2:12, 13 Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema. Hosea 14:2 Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie BWANA; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema. Ayubu 33:27, 28 Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, mimi nimefanya dhambi, yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, an uhai wangu utautazama mwanga. KUTUBU KUNALETA MSAMAHA — 19 Isaya 55:6, 7 Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu; mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie BWANA, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa. Zaburi 34:18 BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa. Yeremia 36:3 Wapate kurudi, kila mtu akaiache njia yake mbaya; nami nikawasamehe. . . dhambi yao. Zaburi 32:5 Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu. 1 Yohana 1:9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe. Kutubu kunamaanisha kugeuka kutoka dhambini pamoja na kuungama mbele za Mungu. DHABIHU INAYOTAKIKANA KUTUPATANISHA NA MUNGU — 20 (Dhambi ilileta utengano.) Mambo Ya Walawi 17:11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. Waebrania 9:22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo Kutoka 12:5, 13 Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja. ...Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu. Mwanzo 22:8, 13 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. . . . Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. YESU NDIYE MWANA KONDOO ALIYETOLEWA NA MUNGU — 21 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! —Yohana 1:29 Alionewa, lakini alinyenyekea, wala hakufunua kinywa chake; kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, na kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake; naam, hakufunua kinywa chake. —Isaya 53:7 Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi. . . . Basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? —Waebrania 9:12,28, 14 1 Petro 1:18, 19 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. UKOMBOZI NI KWA MAAFIKANO TU NA MUNGU — 22 Warumi 3:24, 25 Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. —Warumi 5:8,9 Hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu. —Wagalatia 2:16 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. —Waefeso 2:8,9 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi. —Matendo 10:43 Matendo 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. KUZALIWA KWA YESU KWATANGAZWA — 23 Luka 1:26-38 ...Malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. ...Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, ...na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.... kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake. Watu tu walioingia Ulimwenguni pasipo uzao wa Mume na Mke walikuwa Adamu na Kristo. Adamu alileta dhambi katika Ulimwengu, lakini Yesu alileta ushindi juu ya dhambi. KWA KWELI YESU NI NANI — 24 Wafilipi 2:6, 8 Ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Yohana 10:30, 36 Mimi na Baba tu umoja. Je! yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu? Yesu Kristo, Neno la Milele, amekuwako daima. Kwa muujiza, Mungu alisababisha atungwe mimba katika tumbo la Mariamu. Kimwili anajulikana kama Mwana wa Mtu, na Kiroho anajulikana kama Mwana wa Mungu. Maandiko yanatumia neno "Mwana" kueleza uhusiano ulioko kati ya Mungu na Neno lake—Yesu Kristo. Waebrania 10:5 Kwa hiyo ajapo . . . Lakini mwili uliniwekea tayari. Na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu. —Warumi 1:4 Yohane 20:28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! KWA KWELI YESU NI NANI — 25 1 Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili. Wakolosai 2:9 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Isaya 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Yohana 8:58 Yesu akawaambia, . . . Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukum tambua. —Yohana 1:10 1 Timotheo 2:5, 6 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote. Wakolosai 1:14, 15 Ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana. BIBLIA (MAANDIKO) NI NENO LA MUNGU — 26 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. —2 Petro 1:21 Luka 1:70, 77 Kama alivyosema tangu mwanzo kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao. Roho ya BWANA ilinena ndani yangu, na neno lake likawa ulimini mwangu. —2 Samweli 23:2 Kumbukumbu La Torati 6:6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako. 2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki. Warumi 15:4 Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini. Mathayo 22:29 Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. Zaburi 138:2 Kwa maana umeikuza ahadi yako, kuliko jina lako lote. YESU NDIYE NENO LA MUNGU — 27 Ufunuo 19:13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. Yohana 1:1, 14 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu. Yesu anamdhihirisha Mungu 2 Wakorintho 4:6 Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Yohana 1:18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Mungu yuanena kuptia kwa Yesu Waebrania 1:1, 2 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yohana 8:38 Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo. NENO LILILOANDIKWA NA LILILO NA UHAI KU LINGAN ISHWA — 28,29 Biblia ni chakula kwa nafsi Ayubu 23:12 Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu. Mathayo 4:4 Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Biblia inaangaza njia yetu Zaburi 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu. Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga. —Zaburi 119:130 Yesu ni mkate kutoka mbinguni Yohana 6:51, 48 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Mimi ndimi chakula cha uzima. Yesu ni nuru ya ulimwengu Yohana 8:12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. Biblia huleta maisha yen ye mazao Zaburi 1:2, 3 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa. Yesu hutoa maisha yen ye mazao Yohana 15:4a, 5 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. MAANDIKO YAELEZA JUU YA YESU KRISTO Yohana 5:39, 46 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. . . . Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Luka 24:27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe. NENO LA MUNGU LA MILELE HALIBADILIKI — 30 Zaburi 119:89, 160 Ee BWANA, neno lako lasimama imara mbinguni hata milele. Jumla ya neno lako ni kweli, na kila hukumu ya haki yako ni ya milele. Isaya 40:8 Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele. Mathayo 5:18 Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Yohana 10:35 Na maandiko hayawezi kutanguka. Mtu asijaribu kubadilisha maneno ya Biblia Kumbukumbu La Torati 12:32 Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze. Mithali 30:6 Usiongeze neno katika maneno yake; asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima. —Ufunuo 22:19 Mithali 13:13a Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu. KIFO CHA YESU KILIKAMILISHA MPANGO WA MUNGU — 31 Yohana 10:17, 18 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Mathayo 26:53, 54 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri? Matendo 3:18 Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo. Matendo 2:23 Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua. Isaya 53:10 Lakini BWANA aliridhika kumchubua; amemhuzunisha; utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi. KIFO CHA YESU KUTANGAZWA NA MASHAHIDI — 32 Marko 15:27, 28 Na pamoja naye walisulibisha wanyang’anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. Basi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi. Mathayo 27:45, 50-51, 54 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. . . . Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. . . . nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka. Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo ya liyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu. Yohana 19:32-37 Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. ...Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na...watamtazama yeye waliyemchoma. YESU ALISHINDA KIFO — 33 Matendo 2:24, 32 Ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. Waebrania 2:14, 15 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 1 Wakorintho 15:55, 57 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Ufunuo 1:18 Na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. 2 Timotheo 1:10 Na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili. YATUPASA TUFANYEJE NA YESU? — 34 Ufunuo 3:20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauWa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. —Warumi 4:5 Yohana 20:22; 16:24 Pokeeni Roho Mtakatifu...ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Mathayo 10:37, 16:24, 25 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; ...Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Wagalatia 3:29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. KUPITIA KWA YESU TUNA UZIMA MPYA — 35 1 Yohana 5:11, 12 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Wagalatia 2:20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu. Warumi 8:2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. 2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! yamekuwa mapya. 1 Petro 1:23; 2:2 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu. MUNGU NI BABA KWA WATU WAKE — 36 Zaburi 68:5 Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. Isaya 64:8, 63:16 Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako. Wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako. Hosea 1:10 Tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai. Mathayo 7:11; 6:9 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?. . . Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje. 2 Wakorintho 6:17b, 18 Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. —Warumi 8:14 KUPITIA KWA YESU TUNAMJUA MUNGU KAMA BABA — 37 Yohana 14:6, 7, 23 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Wagalatia 4:4-7; 3:26 ...Mungu alimtuma Mwanawe...ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu ali mtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 1 Yohana 2:1 Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. YESU HULETA UPENDO, FURAHA, AMANI — 38 1 Yohana 4:16 Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. Waefeso 4:32 Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. —Yohana 13:35 Wagalatia 5:22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani... Walakini nitamfurahia BWANA, nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. —Habakuki 3:18 Zaburi 16:11 Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako ziko furaha tele; na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele. Warumi 5:1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. YESU ATAWAFUFUA WAFUASI WAKE WA KWELI — 39 Warumi 8:11 Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. 1 Wakorintho 6:14 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. Yohana 11:25, 26 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. 1 Wakorintho 15:21-23 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. Yohana 14:19 Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. USIDHARAU WOKOVU HUU MKUU — 40 Waebrania 10:28, 29 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? Yohana 12:48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakuf a katika dhambi zenu. —Yohana 8:24 Luka 12:4, 5 Nami nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda zaidi. Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo. Waebrania 2:3 Sisi je! tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? YESU KRISTO ATATUHUKUMU — 41 Matendo 17:31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu. Yohana 5:22, 23 Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. 2 Wakorintho 5:10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee. kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. Warumi 2:16 Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, kwa Kristo Yesu. 2 Wathesalonike 1:7, 8 Wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu. Luka 19:27 Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu. SIO WOTE WANAOSHUHUDIA KUMFUATA YESU WALIO WA YESU — 42 Tito 1:16 Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana. Warumi 8:9 Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Ezekieli 33:31 Nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao. Mathayo 15:8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Mathayo 7:21-23 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika uf alme wa mbinguni; bali ni yeye af anyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. WAFUASI HALISI WA YESU HUMII — 43 1 Yohana 2:3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Ezekieli 36:27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Waebrania 5:9 Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii. Warumi 6:18 Na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki. Waefeso 2:10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. Warumi 8:10, 13 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. 2 Timotheo 2:19 Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu. ULIMWENGU UNACHUKIA WAFUASI WA YESU — 44 Yohana 15:18, 19 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake, lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Yohana 16:2, 3 Naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. 1 Yohana 3:1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Matendo 14:22 Na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. 2 Timotheo 3:12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. Yohana 16:33 Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. AHADI KWA WANAO DHULUMIWA — 45 Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. —1 Petro 5:7 Isaya 41:10 Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Baba yangu na mama yangu wameniacha, bali BWANA atanikaribisha kwake. —Zaburi 27:10 Waebrania 13:6 Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? 1 Petro 4:14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. Zaburi 91:11; 23:4 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana Wewe upo pamoja nami. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. —Wafilipi 4:13, 19 USHINDI JUU YA DHAMBI NA SHETANI — 46 1 Wakorintho 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. Waebrania 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha flee-ma kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. 2 Timotheo 2:22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 1 Yohana 1:7 Bali tukienenda nuruni, kama yeye ahivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. Warumi 6:11 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Zaburi 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi. MAOMBI YA KWELI NI USHIRIKA NA MUNGU — 47 Zaburi 27:8 Uliposema, Nitafuteni uso Wangu, Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta. Zaburi 62:8 Enyi watu, mtumainini sikuzote, ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu. Yeremia 17:14 Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu. 1 Wathesalonike 5:17, 18 Ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. —Yakobo 1:5 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. —Yohana 15:7 Zaburi 34:4 Nalimtafuta BWANA akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote. Zaburi 66:18; 25:11 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia. Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi. YESU ANAKUJA—UWE TAYARI! — 48 1 Wathesalonike 4:16, 17 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo. 2 Wakorintho 7:1 Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. 1 Yohana 2:28 Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake. Yakobo 5:8, 9 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Ndugu, msinung’unikiane msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. Luka 12:40 Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu. UJAZWE NA ROHO WA MUNGU Mithali 1:23 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; tazama, nitawamwagia roho yangu, na kuwajulisheni maneno yangu. Matendo 2:38 Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Waefeso 5:18-21 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. Wafilipi 2:13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. 1 Wakorintho 3:16; 6:2 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na bakuli akaja, akaniambia, "Njoo, mimi nitakuonyesha adhabu aliyopewa yule mzinzi mkuu, mji ule uliojengwa juu ya maji mengi. Wafalme wa dunia wamefanya uzinzi pamoja naye; na wakazi wa dunia wamelewa divai ya uzinzi wake." Kisha, Roho akanikumba, akaniongoza mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Mwanamke huyo alikuwa amevaa vazi la rangi ya zambarau na nyekundu; alikuwa amejipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu ambacho kilikuwa kimejaa machukizo na mambo machafu yanayoonyesha uzinzi wake. Alikuwa ameandikwa juu ya paji la uso wake jina la fumbo "Babuloni mkuu, mama wa wazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani." Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watu wa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababu ya kumtangaza Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno. Lakini malaika akaniambia, "Kwa nini unashangaa? Mimi nitakuambia maana iliyofichika ya mwanamke huyu na mnyama huyo amchukuaye ambaye ana vichwa saba na pembe kumi. Huyo mnyama uliyemwona alikuwa hai hapo awali, lakini sasa amekufa. Hata hivyo, karibu sana atapanda kutoka shimoni kuzimu, lakini ataangamizwa. Wanaoishi duniani watashangaa; naam, watu wote ambao majina yao hayakupata kuandikwa katika kitabu cha uzima tangu mwanzo wa ulimwengu, watashangaa kumwona huyo mnyama ambaye hapo awali, aliishi, kisha akafa na sasa anatokea tena! "Hapa panahitaji akili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba, na huyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo pia ni wafalme saba. Kati ya hao wafalme saba, watano wamekwisha angamia, mmoja anatawala bado, na yule mwingine bado hajafika; na atakapofika atabaki kwa muda mfupi. Huyo mnyama ambaye alikuwa anaishi hapo awali lakini sasa haishi tena ni mfalme wa nane, naye pia ni miongoni mwa hao saba, na anakwenda zake kuharibiwa. "Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme ambao bado hawajaanza kutawala. Lakini watapewa mamlaka ya kutawala kwa muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. Shabaha ya hawa kumi ni moja, na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote. Watapigana na Mwanakondoo, lakini Mwanakondoo pamoja na wale aliowaita na kuwachagua, ambao ni waaminifu, atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme." Malaika akaniambia pia, "Yale maji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi, ni mataifa, watu wa kila rangi na lugha. Pembe zile kumi ulizoziona na yule mnyama watamchukia huyo mzinzi. Watachukua kila kitu alicho nacho na kumwacha uchi; watakula nyama yake na kumteketeza kwa moto. Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia ya kutekeleza shabaha yake, yaani kwa kukubaliana wao kwa wao na kumpa huyo mnyama mamlaka yao ya kutawala, mpaka hapo neno la Mungu litakapotimia. "Na yule mwanamke uliyemwona ndio ule mji mkuu unaowatawala wafalme wa dunia."

Zanzibar Muslims, Officials Stop Church Building, Erect Mosque

On an island off the coast of East Africa where the local government limits the ability of Christians to obtain land, officials in one town have colluded with area Muslims to erect a mosque in place of a planned church building.

On the Tanzanian island of Zanzibar, Pastor Paulo Kamole Masegi of the Evangelistic Assemblies of God had purchased land in April 2007 for a church building in Mwanyanya-Mtoni, and by November of that year he had built a house that served as a temporary worship center, he said.

Masegi intended for the house to serve eventually as his family’s home within the church compound, but on Nov. 11, 2007, his congregation began to worship there.

Soon area Muslim residents objected, saying they didn’t like seeing the church in the area, said Pastor Lucian Mgaywa of the Church of God in Tanzania.

“This was the beginning of the church’s tribulations,” Pastor Mgaywa said.

In August 2009, local Muslims began to build a mosque just three feet away from the church plot, Pastor Mgaywa said. In November 2009, Pastor Masegi began building a permanent church structure. Angry Muslims invaded the compound and destroyed the structure’s foundation, the pastors said.

Church leaders reported the destruction to police, who took no action – and also refused to release the crime report for court purposes, Pastor Masegi said. When he would inquire about the case, he said, the station head would inform him that the district police chief had the crime report and therefore it was not available.

“So it’s not possible to take the file to the court, because doing so would amount to defending Christianity,” the station police chief told him, according to Pastor Masegi.

With the district police chief sealing off any possibility of a court hearing, the church was unable to proceed with plans for building a permanent structure. In the meantime, construction of a mosque was well underway. It was completed by the end of December 2009.

The planned church building’s fate appeared to have been sealed earlier this year when Western District Commissioner Ali Mohammed Ali notified Pastor Masegi that he had no right to hold worship in a “residential house.” The Feb. 16 letter from the commissioner to Pastor Masegi forbidding him to convert his house into a worship center confirmed the decision by the district chief of Bububu police station not to prosecute those who destroyed the foundation of the planned church building, he said.

“Now the Christian faithful are feeling targeted even by the government officials,” said Pastor Masegi. “The region is predominantly Muslim, and attempts at evangelizing are always met with brutal resistance.”

Since the prohibition to conduct worship services in his home, both police and area Muslims monitor Pastor Masegi’s movements, he said, and the congregation has no place to worship.

In predominately Sunni Muslim Zanzibar, churches face other hurdles. There are restrictions on getting land to build churches, open preaching is outlawed and there is limited time on national television to air Christian programs. In government schools, religion classes are limited to Islam.

Zanzibar is the informal designation for the island of Unguja in the Indian Ocean. The Zanzibar archipelago united with Tanganyika to form the present day Tanzania in 1964.

Muslim traders from the Persian Gulf had settled in the region early in the 10th century after monsoon winds propelled them through the Gulf of Aden. The 1964 merger left island Muslims uneasy about Christianity, seeing it as a means by which mainland Tanzania might dominate them, and tensions have persisted.

na mwalimu mwakasege

JIHADHARI NA MAFUNUO

    Nafahamu ya kuwa mara tu baada ya kusoma kichwa cha somo hili, ulianza kujiuliza maswali mbali mbali juu ya mafunuo.     
                Jihadhari na Mafunuo! Huu ni ujumbe muhimu uliomo katika somo hili. Si mafunuo yote ni ya Mungu au yanatoka kwa Mungu. Mafunuo maana yake nini? Chanzo cha kuwepo mafunuo ni nini! Utayafahamu kwa njia gani au kwa namna gani mafunuo yasiyokuwa ya Mungu?          
                Haya ni baadhi tu ya maswali mengi yanayojibiwa katika somo hili. Naamini kabisa ya kuwa Roho Mtakatifu aliyekuongoza kulisoma somo hili hivi sasa, atakuwa pamoja nawe katika kukuelewesha kwa undani na ufasaha zaidi mambo niliyoyaandika.    
                Kumbuka hizi ni siku za mwisho na kurudi kwa Bwana Yesu Kristo mara ya pili kuja kulichukua kanisa kumekaribia sana. Bwana na atuwezeshe katika kutafakari  maneno yaliyomo katika somo hili, ili siku ajapo tusiwe watu wa kuaibika mbele zake – bali tuwe watu wa kufurahi na kumsifu milele na milele – Amina! Kila wiki kwa wiki sita mfululizo tutakuwa tunajifunza sehemu ya somo hili. Ni matumaini yangu utakuwa pamoja nami kila wiki!  click link hapo chini


Wiki ya Kwanza: MAFUNUO
Wiki ya Pili:
Mambo matano muhimu unayohitaji kujua juu ya Mafunuo
Wiki ya Tatu: Kwa nini tupime mambo yote?
Wiki ya Nne: Tutapima mambo yote kwa namna gani?
Wiki ya Tano: Hila za ibilisi ndani ya Kanisa
Wiki ya Sita: Tatizo la Wakristo na dawa yake

karibu zaidi siku zote niwe

the ministry of fred obare

"My main reason for living is to bless God with the gifts He has given me, spread His word through music, make a great impact and change the world for the Lord."

Fred's Favorite Scriptures

"For all have sinned and come short of the glory of God" - Romans 3:23

"For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord" - Romans 6:23

" I am the door; anyone who enters in through Me will be saved (will live). He will come in and he will go out (freely), and will find pasture." - John 10:9

" For God so greatly loved and dearly prized the world that He (even) gave up His only begotten (unique) Son, so that whoever believes in (trusts in, clings to, relies on) Him shall not perish (come to destruction, be lost) but have eternal (everlasting) life. - John 3:16

Fred Obare Ministries
P.O. Box 190423| BIRMINGHAM, AL 35219
205-567-8640
www.fredobare.org | mcobare@yahoo.com

Kila amchukiaye ndugu yake ni muuaji-(1 Yohana 3:15)

Usilipize Kisasi! Unasikia? Hata ikiwa umefanyiwa ubaya wa namna gani, Biblia inafundisha na inakusihi usilipize kisasi kwa huyo aliyekufanyia ubaya. Biblia inasema hivi:

"Wapenzi, msijilipizie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu Mimi, Mimi nitalipa, anena Bwana" (Warumi 12:19)


            Kuna hasara zinazoweza kukupata ukiamua kulipa kisasi kwa mambo uliyofanyiwa ambayo hayakupendezi. Ikiwa ni masuala ya kikabila, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kidini, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kifamilia, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kikazi, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya uhusiano wako na majirani zako, usilipe kisasi.Ndiyo! Usilipe kisasi! Kwa nini? Kwa sababu "imeandikwa kisasi ni juu yangu Mimi; Mimi nitalipa, anena Bwana".
Lakini ikiwa utaona ya kuwa Mungu hawezi kukusaidia na ukaamua kujichukulia madaraka ya kujilipiza kisasi hasara zifuatazo hakika zitakupata!

Hasara ya Kwanza:
UTASHINDWA!

            Katika jambo lolote lile lililokukasirisha - liwe la kidini, au kikabila, au kifamilia, au kikazi, na kadhalika ukiamua kulipa kisasi utashindwa wewe kwa sababu vita hivyo si vya mwili na wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili! Tunasema hivi kwa sababu katika 2 Wakorintho 10:3- 5 imeandikwa hivi:"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi yamwili; maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo".

            Tena katika kitabu cha Waefeso 6:12 imeandikwa hivi: "Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho".
            Uwanja wa mapambano uliyonayo ni "katika ulimwengu wa roho" na mapambano uliyo nayo "si juu ya damu na nyama" - ingawa unaona ya kuwa ni watu na ni binadamu kama wewe wanaokusonga - lakini fahamu hili ya kuwa wanatumiwa tu na ibilisi!
            Mbinu mojawapo ya shetani anayotumia akitaka kukuangamiza ni kukufanyia kitu kitakachokukasirisha ili uamue kujibu au kushindana kimwili kwa sababu anajua ukishindana "kimwili" au katika mwili utashindwa hakika, maana vita hivyo si vya mwili wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili!

Hasara ya Pili:
MATATIZO HAYATAKWISHA!

            Kumbuka imeandikwa hivi katika kitabu cha Wagalatia 6:7; "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote ampandacho mtu. Ndicho atakachovuna".
            Ikiwa umeamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule aliyekufanyia - ubaya hautakwisha, kwa sababu utavuna ulichopanda.Ndiyo maana imeandikwa hivi:"Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, mabaya 
hayataondoka nyumbani mwake" (Mithali 17:13)

            Ukiamua kulipiza kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nyumbani mwako - Biblia inasema "mabaya hayataondoka nyumbani mwako" Hii ndiyo maana matatizo mengi katika ndoa na katika jamii hayaishi - kwa sababu mtu akifanyiwa ubaya naye analipa kisasi.
            Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nchini mwako ujue hakika mabaya hayataondoka nchini mwako. Hili ndilo lililowapata wenzetu wa nchi za Burundi na Rwanda - kulipizana kisasi - matokeo ni uhasama usiotaka kupotea - pamoja na juhudi zote za kimataifa kutafuta suluhisho.
            Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa kazini kwako - fahamu mabaya hayataondoka kazini kwako. Ikiwa ni shuleni - mabaya hayataondoka hapo shuleni.
            Tena hali ya mwisho inakuwa mbaya zaidi,kila wakati kisasi kinapoendelea kupandwa. Kwa sababu ukiwapa watu ubaya - nawe utapewa ubaya kwa; "kipimo cha kujaa na kushidiliwa, na kusukwa - sukwa - hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile upimacho ndicho mtakachopimiwa (Luka 6:38)
            Kumbuka ubaya haushindwi na ubaya mwingine, bali unashindwa na wema - kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo! Ndiyo maana Warumi 12:21 inasema; "Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema".

Hasara ya Tatu:
UNAMZUIA MUNGU KUKUPIGANIA

            Unaweza ukashangaa, lakini ndivyo ilivyo! Ukiamua kulipa kisasi juu ya tatizo ulilonalo - unamzuia Mungu asikusaidie kulitatua.Mungu hawezi kukusaidia kwa sababu imeandikwa "msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana, imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana".
Neno "ipisheni" limeandikwa kwa sababu kulipa kisasi "kunazuia" ghadhabu ya Mungu isipigane upande wako! Tena si hivyo tu lakini ukilipa kisasi unaingilia kazi ambayo si yako! Ni kazi ya Mungu maana anasema "Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana" Ikiwa kisasi ni juu ya Mungu kulipa, basi huhitaji wewe kulipa. Je, tunakwenda pamoja katika hili?
            Hatua yako ya kulipa kisasi inazuia mkono wa Mungu kukupigania - kwa hiyo ipishe ghadhabu ya Mungu kwa kutokujilipizia kisasi!

Hasara na Nne:
UNAJICHUMIA DHAMBI!
            Unapoamua kulipa kisasi, unajichumia dhambi! Hii ni kwa sababu kulipa kisasi huja kwa njia ya chuki iliyojengeka ndani yako kwa ajili ya mambo mabaya uliyofanyiwa. Huwezi kulipa kisasi bila ya kumchukia huyo unayejilipizia kisasi kwake. Na Biblia inasema hivi:
"Kila amchukiaye ndugu yake ni muuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila muuaji hana uzima wa milele ndani yake" (1 Yohana 3:15).
Umeona hilo! Chuki huzaa kisasi, na huzaa dhambi ya kuua! Na 
Isaya 59:2b inasema; "dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia".
            Kwa hiyo kama umekwisha lipa kisasi au umekusudia moyoni mwako kulipa kisasi ni muhimu utubu ili Mungu akusamehe na mawasiliano yako na Yeye yawe mazuri.

Click picture to listen to a sample of music from each cassette (between 10 - 30 seconds)
All in .wav format 8,000Hz 8 bit mono 8KB/s unless specified.

Volume 3

mpende adui, . . . mwokozi amenituma Tanzania (392KB .wav file)

click

Furahini Katika Bwana - Maasai Vichekesho

kusikiliza shuhuda click link zifuatazo  Remember, you need RealPlayer to play shuhuda. A free edition of this player can be downloaded from here. Karibu - Welcome.

Ushuhuda wa Peter Musabi Kihungu Part I -

Ushuhuda wa Peter Musabi Kihungu Part II

In English
Proton - Bishop Dag Heward-Mills
Coming into the City - Rev.Kwarteng Siaw
Wiping Out The Negative Birth Mark - Rev.Kwarteng Siaw
Fresh Oil For Fresh Moves 1 - Rev. Dr. Robert Ampiah-Kwofie
Fresh Oil For Fresh Moves 2 - Rev. Dr. Robert Ampiah-Kwofie
Fresh Oil For Fresh Moves 3 - Rev. Dr. Robert Ampiah-Kwofie

sikiliza radio za injili hapa

 gonga link chini kusikiliza redio za injili

Kicheko Int Radio

Radio Safina Live

askofu gamanywa-hakuna lisilowezekana

Hii ni huduma ya Kiroho iliyoanzishwa na Askofu Sylvester Gamanywa, mmoja wa maaskofu vijana na shupavu mwenye jicho la kuona mbali na kushiriki katika harakati kadhaa.

Mara nyingi ni mtu wa kuingia katika kila jambo  na kutumia mamlaka yake kutafuta ufumbuzi. Katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa miongoni mwa wahubiri wa kwanza kujitoa katika kuendesha kampeni  ya kuhimiza amani na kuliombea taifa.

Akitumia kituo chake cha Redio ya Kikristo itwayo Wapo F.M, Askofu Gamanywa, aliongoza pia harakati za kuhimiza watu kubadili tabia ili kujikinga na gonjwa la UKIMWI, hapo serikali ikatambua mchango wake na akateuliwa kuwa mmoja wa Makamishina wa Tume ya kupambana na ugonjwa huo Tanzania.

Ingawa alikuwa mhubiri kwa muda mrefu, akimiliki pia Gazeti la Kikristo la Msema Kweli, Askofu Gamanywa alipata mafanikio makubwa katika miaka sita tu iliyopita ambapo uamsho mkubwa umedhihirika katika huduma yake.

Baada ya huduma yake kupanuka alifungua kituo cha miujiza na uponyaji huko Mbezi Beach, jijini kiitwacho BCIC, ambacho mbali ya kuwa ni kituo cha maombi na uponyaji kwa damu ya  Yesu, ni mahali ambapo semina na masomo maalumu yanayolenga kuibadili tabia ya Watanzania hufanyika kwa mafanikio makubwa.

Kwa wakati huu Askofu Gamanywa, anaendesha kampeni  iliyolenga kuokoa kizazi kijacho kwa kupambana na uharibifu wa maadili kwa vijana.

Askofu Silvester Gamanywa ndani ya kumekucha ya ITV from Tangibovu on Vimeo.

kilimanjaro revival choir

sauti ikatoka

                        Kutoka kushoto Mtumishi Lenita Reeves kutoka Maryland, Pastor Brenda McClintock kutoka Missouri na Pastor Catherine Abihudi katika picha ya pamoja kwenye semina iliyofanyika hivi karibuni huko Marekani.

PLEASE PRAY FOR THE CHURCH IN ZANZIBAR

Two church buildings were razed June 28 on the Tanzanian island of Zanzibar after Sunday worship services.

Suspected radical Muslims set the church buildings on fire on the outskirts of Unguja Township, on the island off the coast of East Africa, in what church leaders called the latest incidents of a rising tide of religious intolerance.

"We don't want churches on our street," read a flier dropped at the door of Charles Odilo, who had donated the plot on which the Evangelical Assemblies of God in Tanzania (EAGT) building stood. "Today we are going to burn the church, and if you continue we are going to burn your house  also."

With Christian movements making inroads in the Muslim-dominated area, the EAGT church and a Pentecostal Evangelical Fellowship in Africa (PEFA) church building a few miles away were burned down as a fierce warning, church leaders said.

The PEFA church building was located in the Kibondeni area eight miles from Unguja, and the EAGT structure was in the Fuoni area six miles from Unguja. Samuel Salehe Malanda, pastor of the 30-member PEFA church, said their building doubled as a nursery school on weekdays. "In this church building there were six benches and a blackboard," Malanda said. "The children have no place to do their learning. What are we going to do?"

Construction of the PEFA church building was in the final stage of completion, area church leaders said, when Masoud Jecha, assistant sheikh of Kibondeni, visited it and threatened Malanda. "If you do not stop your construction, we will bring down the building," Jecha told the pastor.Malanda said the church reported the arson attack to police, who have purportedly begun an investigation, and the congregation has also sought the help of the chief leader of the rural government. The church's police report included mention of Muslim extremist suspects bent on stopping the spread of Christianity in Zanzibar.

Church leaders said Odilo, who had donated his plot for the EAGT church building, was living in fear of the Islamic militants burning down his house, as they are known for carrying out their threats.

Pastor Paul Makungu said his EAGT church has 29 adult members and 13 children. He has also filed an arson report with local police, who are investigating suspects including radical Muslims and the chief neighborhood leader.Bishop Obeid Fabian, chairman of an association of congregations known as the Fraternal Churches, said Christians in Zanzibar have received several threats.

"In this latest incident, the threats were spread through pamphlets," he said. "At other times, Muslim youths have hurled stones on church rooftops and insulted Christians."On May 9 Muslim extremists expelled Zanzibar Pentecostal Church worshippers from their rented property at Ungunja Ukuu, on the outskirts of Zanzibar City.

With no help forthcoming, church members have begun gathering for fellowship in their homes, Fabian said. In Zanzibar City on April 17, government officials ordered Christians of the Church of God Zanzibar from their rented government building effective April 19, ostensibly to pave the way for renovations. But two months later, said pastor Lucian Mgayway, no renovation work had begun, and the government has since turned it into a business site. The church had been worshipping in the building since October 2000.

"The churches affected since attacks began in April are at a critical stage," said Fabian. "We as church leaders find it very difficult to bring our church members together who are now dispersed with no place of worship. The church needs financial support to get worship places for members as well security. But this seems not forthcoming."

In predominately Sunni Muslim Zanzibar, churches face other hurdles. There are restrictions on getting land to build churches, open preaching is outlawed and there is limited time on national television to air Christian programs. In government schools, only Islamic Religious knowledge is taught, not Christian Religious Education.Zanzibar is the informal designation for the island of Unguja in the Indian Ocean. The Zanzibar archipelago united with Tanganyika to form the present day Tanzania in 1964.

Muslim traders from the Persian Gulf had settled in the region early in the 10th century after monsoon winds propelled them through the Gulf of Aden and Somalia. The 1964 merger left island Muslims uneasy about Christianity, seeing it as a means by which mainland Tanzania might dominate them, and tensions have persisted.

breakthroughassembly

kutazama picha bonyeza hapa : breakthroughassembly photos

umeoshwa kwa damu ya kondoo?

tafakari ya leo

Yohana 15:7
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

mahubiri


mahubiriPlaylistRingtones
john lemaswahilisifa 2010

kwanini unatoa na hubarikiwi?

“Lakini nasema hivi, apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama ilivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana   Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2Wakorintho 9:6,7). utoaji wako uwe si haba (au kidogo) bali uwe kwa ukarimu. Ukitoa kidogo utapata kidogo – bali ukitoa vingi utapata vingi. Ndiyo maana imeandikwa; “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa” (Luka 6:38) Tena, utoaji unatakiwa ufanyike “si kwa huzuni; wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu  “… na wala si kwa unyimivu”.

           Michango mingi iliyomo makanisani siku hizi  wakati mwingine inafanyika kwa kulazimishana. Mtu anatakiwa atoe kwa kupenda kwake toka moyoni mwake – si kwa lazima. Kumlazimisha mtu kutoa ni kwenda kinyume cha utaratibu wa utoaji.  Wakristo wengi wamekosa baraka au mafanikio katika utoaji kwa sababu wanatoa huku wanahuzunika au kulalamika! Wengi wanawanung’unikia viongozi wa makanisa yao kuwa wanatumia fedha au vitu vibaya. Kama una wasiwasi na matumizi ya matoleo yako –basi yaombee kwa Mungu ayalinde yatumike kwa utukufu wake kuliko kulalamika.  Je! umewahi kumsikia mkulima akihuzunika au kulalamika kwa kuwa ameongezewa shamba la kulima na kupanda? Hakuna. Mkulima halalamiki bali anafurahi kwa kuwa amepata eneo kubwa zaidi la kupanda umeongezewa eneo la kupanda ili uvune zaidi. Ni eneo la kukusaidia kutoa zaidi ili upokee zaidi!

           Utoaji ni sawasawa na upandaji. Mtu akipanda anategemea kuvuna pia. Kwa hiyo mtu akitoa anategemea kupokea.Mkulima yo yote akitaka mavuno mazuri toka shambani mwake kati ya vitu anavyoviangalia ni aina ya mbegu na aina ya udongo. Siku zote atapanda kwenye udongo mzuri wenye rutuba.
            Mfanya biashara siku zote anataka aweke mtaji wake katika vitu vitakavyomletea faida kibiashara na siyo hasara. Lakini, inasikitisha kuona kuwa inapofika wakati wa utoaji – wakristo wanatoa tu bila kuangalia kwanza “udongo mzuri” ni upi ili utoaji wao uwaletee matokeo mazuri.

    Biblia inatuambia katika mfano wa mpanzi ya kuwa mbegu zingine“…. Zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia” (Mathayo 4:8 )Je, “udongo mzuri” unaoleta faida nzuri ni upi? Sehemu za kutoa zenye matokeo au mavuno mazuri ni hizi zifuatazo; (1)Katika nyumba ya Mungu – kanisani ili kuendeleza kazi ya Mungu – soma Malaki 3:10-11; na Kumbukumbu ya Torati 8:18. (2)Kuwasaidia watumishi wa Mungu na watakatifu wake kwa vitu/mali ulizo nazo. Soma 1Wafalme 17:10-24 na 2Wakorintho 9:10-13. (3)Kuwasaidia maskini kwa vitu/mali ulizo nazo. Soma 2Wakorintho 9:8-9.

Angalia upandaji wako katika utoaji – je! umepanda kwenye udongo ulio mzuri? Kati ya baraka ambazo zinapatikana kutokana na kuwa mwaminifu katika utoaji wa zaka (fungu la kumi) na dhabihu (matoleo mbalimbali), Mungu alisema hivi; 
           “Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba ….” (Malaki 3:11).
Inawezekana unatoa sadaka, na huoni baraka zozote zinazotokana na kutoa kwako – hebu angalia na jichunguze kama umekuwa mwaminifu katika kutoa ZAKA KAMILI. Kwa mfano kama fungu la kumi la pato lako ni shilingi 1000,000 – toa zaka kamili yaani shilingi 10,000/=. Usitoe pungufu ya hiyo maana haitakuwa zaka kamili
.
Ikiwa umekuwa mwaminifu katika kutoa Zaka kamili na dhabihu halafu huoni matokeo yake basi, tumia mamlaka ya Jina la Yesu Kristo – mfunge na kumkemea ibilisi ambaye ndiye mharibu wa mali yako aondoe mikono yake juu ya mali yako. 
       
Kumbuka Yesu Kristo alisema;“Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalofunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”  (Mathayo 16:19).

bishop yohana masinga

usinipite mwokozi

sinza christian centre

Come & Praise The Lord at Sinza Christian Center from 7pm!
 
Blessings!
Annie

askofu mgullu kilimba

Christian Mission Fellowship (CMF) headquarters (formerly known as VICTORY CHRISTIAN ASSEMBLIES) is located at Sinza area in the city of Dar es Salaam, Tanzania. The church Ministry was founded in 1995, by Bishop Mgullu Kilimba. In the past twelve years this Church has planted 59 new local churches accross the country!

In 2003 a Bible training Centre was started for the Church Planters who after the training were sent to unreached areas. Right now there are about ten church planters in various fields accross the country. The training program has been always undertaken at CMF church headquarters. Plans are underway to shift to the 30-acre College compass once the construction projects at the sitte are complete. Click Bible School for more information.

In 2004 a strategic decision was taken to change Victory Christian Assemblies to a new of CHRISTIAN MISSION FELLOWSHIP, the main reason behind the change was to focus more on Missions.

Every CMF church around the country conducts its services according to their own programs, which include Sunday and mid-week worship services, prayer meetings, and Bible Study groups and outreach activities. Also women and youth have their meeting days. Members alo do meet in various cell groups for discipleship purposes.

Other ministries include practical counselling, missionary activities, ountreach, house-to-house evangelism, school ministries, and ministry to the needy.

cults?au.....

mmasai aliyeokoka

tumeokoka tuwe watakatifu

Mungu hajatuita tuwe manabii, mitume, waalimu, wachungaji na waijilisti tu! Ametuita tuwe watakatifu, suala linaloangaliwa hapa sio huduma uliyonayo, ila Mungu anaangalia utakatifu wako!

Emelda Maboya

safari ya mji mtakatifu na mama rwakatare

luka 1:37-53

37Siku ya mwisho ya sikukuu, ambayo kwa kawaida ndio ili kuwa kilele cha sherehe, Yesu alisimama akasema kwa sauti kuu, ``Mtu ye yote mwenye kiu na aje kwangu anywe. 38Kama Maandiko yasemavyo, ye yote aniaminiye, vijito vya maji yaletayo uzima vitatiririka kutoka moyoni mwake.'' 39Yesu alisema haya kuhusu Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini Yesu wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa bado hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajainuliwa na kutukuzwa.
40Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu walisema, ``Hakika huyu ndiye yule Nabii.'' 41Wengine wakasema, ``Huyu ni Masihi!'' Lakini wengine wakauliza, ``Kwani Masihi kwao ni Gali laya? 42Je, Maandiko hayakusema kuwa Masihi atakuwa mzao wa Daudi na kwamba atazaliwa Bethlehemu, mji alioishi Daudi?'' 43Kwa hiyo kukawa na mgawanyiko kati ya watu kumhusu Yesu. 44Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa.
      Kutokuamini Kwa Viongozi Wa Wayahudi
45Hatimaye wale walinzi wa Hekalu waliokuwa wametumwa kumkamata Yesu, walirudi kwa makuhani wakuu na Mafarisayo. Wakaulizwa, ``Mbona hamkumleta ?''
46Wale walinzi wakajibu, ``Hakuna mtu ambaye amewahi kufundisha kama yeye.'' 47Mafarisayo wakajibu, ``Ameweza kuwa danganya hata ninyi? 48Je, mmewahi kuona kiongozi ye yote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini? 49Lakini huu umati wa watu wasiojua sheria ya Musa,wamelaaniwa.''
50Ndipo Nikodemo, yule aliyemwendea Yesu siku moja, ambaye alikuwa kati yao akauliza, 51``Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?''
52Wakamjibu, ``Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza Maandiko nawe utaona kwamba hakuna nabii anayetokea Galilaya!'' [ 53Kisha wakaondoka, kila mtu akarudi nyumbani kwake.

unajua hili?

    Wapendwa sikuhizi kumezuka mtindo wa Watumishi kuvaa mapete yenye vito mbali mbali(A.K.A pete za bahati), na hilo Nimeona hasa kwa viongozi wetu wakuu ukianzia kwa mkuu mwenyewe,wasaidizi wake, baadhi ya wabunge na wakuu wa mikoa wana pete fulani kubwa kwenye vidole vyao ukiachilia mbali pete za ndoa. Hili pia nimeliona kwa maaskofu wa KKKT na Anglican. Hivi kuna sababu yeyote nyuma ya hizi pete?au kuna ajuae maana na sababu ya kuvaliwa kwa pete hizi?.

       Kwa mtazamo wangu nadhani Hakuna sababu yeyote nyingine, hayo mapete yana uhusiano na imani fulani ya nguvu za giza., isipokuwa tu kwa wale wanaozivaa pasipo kujua.lakini wengi wao huonekana wamezivaa wakiwa wamekusudia na wanajua wanachokifanya.
             Mchungaji Florian Katunzi wa EAGT city center (akiwa anaendesha moja ya ibada ya maombezi kule saba saba) amewajia juu wachungaji wanaovaa pete hizo akidai kuwa wengi wao wanazitumia kwa nguvu za kichawi.kama vile kuleta mvuto,kupata heshima na kadhalika .Alinukuliwa na vyombo vya habari  katika moja ya mikutano yake,Mchungaji huyo kijana anayekuja kwa kasi, amedai kuwa watumishi wengi wanaovaa pete hizo wanazitumia kinyume na maagizo ya Biblia takatifu.

rorya wasalimu amri kwa yesu

 Wazee wakiri sasa usalama utarejea: Katika kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Rorya, mkoani Mara ambao wamekuwa wakipigana mara kwa mara kutokana na wizi wa mifugo.
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) World Outreach Mission, la Arusha imeamua kujitosa huko, ili kuwaonyesha wananchi hao njia sahihi ya kuiendea, ili waachane na mambo yaliyopitwa na wakati na ambayo chanzo chake ni ibilisi.

Njia sahihi iliyoonyeshwa na kanisa hilo, ni kuwahubiria injili ya wokovu wakazi wa vijiji vinavyounda wilaya hiyo, ambapo katika kijiji kimoja cha Raranya, injili hiyo ilipokelewa vema na wakazi wake, jambo lililosababisha takribani wananchi wa kijiji kizima, walioshiriki katika mikutano ya injili kijijini hapo, wajisalimishe kwa Yesu Kristo, akiwemo Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho na mtu mmoja maarufu kwa jina la Daudi, amabye alijulikana kwa mambo mengi lakini sasa anajulikana kwa jina moja tu Mwanafunzi wa Yesu.

Mkutano huo wa injili, ambao ulifanyika kwa siku nane kijijini hapo, kwenye viwanja vya Ruranya Centre, kwa vile ulisababisha wanakijiji wengi kujisalimisha kwa Yesu Kristo, kanisa hilo liliamua kununua kiwanja kijijini hapo, ili kufungua kanisa, litakaloweza kuwatunza kiroho kondoo hao wapya,Katika mikutano hiyo iliyoambatana na ishara na miujiza, mtoto mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 12, ambaye kwa muda wa miezi sita alikuwa amepopooza mwili mzima, aliweza kupata uponyaji, pale alipoweza kusimama kwa miguu yake na kushika vitu mbalimbali.

Kutokana na matendo mengi ya miujiza yaliyofanyika kijijini hapo, mambo hayo yaliwashangaza sana wananchi wa kijiji hicho, wakisema kuwa hawajawahi kuyaona kijijini hapo, licha ya kijiji hicho kutembelewa mara kwa mara na wakaamua kujisalimisha kwa Yesu,Mchungaji wa kanisa hilo, Timothy Wambura alisema; 'Kweli mambo yaliyokuwa yanatokea katika mikutano yetu, yalikuwa ni ya kushangaza sana, maana nguvu za Mungu zilikuwa zikijidhihirisha wazi wazi, kitu ambacho kwangu ni furaha sana na namrudishia Mungu sifa na utukufu, maana ndiye aliyefanya hayo'.

Mchungaji Wambura aliongeza haya; 'Ni kitu cha kumshukuru Mungu sana, hasa katika wilaya hii, maana inasifika kwa mauaji na wizi, lakini naona Bwana ameamua kuingia kazini mwenyewe, kwa kuamua kushughulika na mioyo ya watu wa hapa,Alisema historia ya Rorya, ilikuwa inamuumiza sana kichwa, kwa kuwa na yeye ni mzaliwa wa wilaya hiyo, kutokana na ndugu zake wengi kuwa waathirika wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wilayani hapo, jambo lililomlazimu kupeleka injili wilayani humo.

Kwa upande wao, wazee wa kijiji hicho, walielezea kufurahishwa kwao na mkutano huo, wakasema kuwa wanaamini utakuwa wa baraka kubwa katika maisha yao, maana umewasaidia kuwabadilisha vijana wao kuachana na biashara ya kuzurura ovyo na wizi wa mifugo,Wahubiri katika mikutano hiyo, walikuwa Katibu Mkuu, Idara ya Uinjilisti, mchungaji Wilberforce Mongi, mwangalizi sehemu ya Musoma na Tarime, Constantine Budodi, mwinjilisti Daudi Mgwali na mwinjilisti David Ombeni mwanachuo kutoka chuo cha Uhasibu Arusha na mshirika wa Kanisa la World Outreach Mission. Kila siku, wastani wa zaidi ya watu 100 walikuwa wanaokoka. Zaidi ya Watu wazima 65 walibatizwa ubatizo wa maji mengi.

Naye Mmishenari kutoka WOM ndugu Kisai Leonard ambaye alibaki Raranya kwa takribani siku saba zaidi alisema kuwa, watu wameendelea kuhudhurua katika mafundisho ya neno la Mungu jambo linaloashiria kuwa, wakazi wa Raranya wana kiu na neno la Mungu na Roho wa Mungu ameendelea kuwahudumia katika kipindi hiki cha mafundisho ili waweze kukua kiroho.

MCHUNGAJI WAMBURA

                                       Wito wa Utumishi wa       Mchg TimothyWambura ulianza mwanzoni mwa miaka ya 1979. Katikati ya miaka ya 1990, akiwa mtumishi wa Shirika la World Vision wito wahuduma ulikuja kwa nguvu na mwaka 1997 aliacha kazi na kwenda chuo cha Biblia EAST Nairobi Kenya.  

Mchungaji Wambura anakumbuka siku hizo za wito wa moto, na watu aliowashirikisha kwa awali juu ya wito wake ni Mchungaji Orol Sossy wa Bethel C.C na Engineer Francis Nyansambo. Baada ya hapo mtumishi wa Mungu alienda chuoni na kuhitimu digrii ya kwanza ya Theolojia na baadae Digrii ya pili (Masters) ya Uongozi na kisha Digrii nyingine Masters - Divinity. Kuwepo chuoni kwa muda huo hakukuzuia maono kusimama ama kusubiri. Mwaka 2004, kanisa la TAG World Outreach Mission lilitokeza baada ya kuwepo moyoni kwa kipindi chote hicho toka mwaka 1979 takribani miaka 25. Kwa hakika maono ya Kimungu huwa hayafi na wala hayazimiki. Mchungaji Wambura pamoja na Mke wake Mama Happiness Wambura, wameendelea kuwa baraka sana sio kwa jamii inayozunguka Arusha, bali hata kwa jamii yote ya Tanzania na nje ya Tanzania. Maisha yao na unyekevu wao katika huduma ya Mungu na kuhudumia Watu wote wa rika zote na hali zote ni ishara tosha ya namna ya walivyojitoa kumtumikia Mungu. Familia ya Mchungaji imebarikiwa kuwa na watoto watano, Genya (Mrs Kimicha), Ngugulile, Wambura, Yakobo na Yohana.

"Mpendwa, unakaribishwa katika kanisa WOM na kwa hakika utakutana na YESU anayeokoa"

Vijana wa Kanisa la World Outreach Mission, wapo katika maandalizi ya Mkutano mkubwa wa injili unataorajiwa kufanyika mwezi mapema mwezi huu wa Juni 2010.

    MATUKIO YA KARIBUNI

 • Wiki ya Uinjilisti - Kitaifa/WOM
  June 28, 2010 (8:00 AM)
 • Maombi ya Kufunga - Kitaifa/WOM
  September 20, 2010 (8:00 AM)
 • Siku Kuu ya Vijana - CAs
  October 03, 2010 (8:00 AM)
 • Wiki ya Umisheni - Kitaifa/WOM
  November 01, 2010 (8:00 AM)
 • uharibifu kama huu unapotokea nani wa kulaumiwa?

  Kulingana na Maandiko, hakuna shaka kwamba Shetani anatawala juu ya majeshi ya pepo wabaya ambao wanakaa katika anga la dunia, na wanaomsaidia kutawala ufalme wa giza. Biblia pia inaonyesha kwamba katika hao pepo, wapo wenye kutawala eneo fulani kijiografia (ona Danieli 10:13, 20, 21; Marko 5:9, 10). Maandiko pia yanaonyesha kwamba Wakristo wana mamlaka ya kutoa pepo katika watu wengine, na wana wajibu wa kumpinga Shetani (ona Marko 16:17; Yakobo 4:7; 1Petro 5:8, 9). Lakini je, Wakristo wanaweza kuangusha mapepo walioko juu ya miji? Jibu ni kwamba, hawawezi, na kujaribu kufanya hivyo ni kupoteza muda wao.

  Kwa kuwa tunaweza kutoa pepo katika watu si sababu ya kudhani kwamba tunaweza kuangusha pepo wanaotawala juu ya miji yetu. Ipo mifano mingi sana ya watu kutolewa pepo katika Injili na kitabu cha Matendo, lakini, unaweza kukumbuka mfano hata mmoja wa mtu kuangusha pepo aliyekuwa anatawala mji au eneo la kijiografia katika Injili au Matendo ya Mitume? Huwezi kwa sababu mifano hiyo haipo. Je, unakumbuka fundisho au ushauri hata mmoja katika nyaraka, kuhusu wajibu wetu kuangusha mapepo wabaya kutoka angani? Hakuna. Basi, hatuna msingi wa KiBiblia kuamini kwamba tunaweza au tunapaswa kupambana katika “vita ya kiroho” dhidi ya mapepo wabaya katika anga.Mara nyingi Wakristo hufanya kosa la kupata maana nyingine zaidi ya iliyokusudiwa na Mungu katika vifungu vya Maandiko vinavyotumia lugha ya mfano. Mfano mzuri ni jinsi wengi wanavyoelewa vibaya maneno ya Paulo kuhusu “kuangusha ngome” yafuatayo.

  Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili. (Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangushya ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia (2 Wakor. 10:3-6).

  Kutokana na maneno hayo – “kuangusha ngome” – ambayo ni lugha ya mfano, fundisho zima limejengwa ili kutetea wazo la kufanya “vita ya kiroho” kwa ajili ya “kuangusha ngome” za mapepo katika anga. Lakini ni vizuri tuelewe kwamba Paulo hapo hasemi juu ya mapepo katika anga, bali ngome za imani za uongo ambazo zimo katika mawazo na akili za watu. Paulo anaharibu fikra, si mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho!

  Hili linakuwa wazi zaidi tunaposoma maandiko hayo kulingana na mantiki yake. Paulo alisema hivi: “tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo” (maneno mepesi yameongezwa ili kukazia). Vita ambayo Paulo anaizungumzia kwa lugha ya mfano ni vita dhidi ya mawazo au fikra ambazo ziko kinyume na maarifa ya kweli ya Mungu.

  Kwa kutumia mifano ya kijeshi, Paulo anaeleza kwamba tuko vitani, vita ili kupata mawazo ya watu walioamini kweli za Shetani. Silaha yetu kubwa katika vita hii ni ukweli, na ndiyo sababu tumeagizwa kwenda duniani kote na kuhubiri Injili, tukivamia eneo la adui kwa ujumbe unaoweza kuwaweka mateka huru. Ngome tunazoharibu zimejengwa kwa matofali ya uongo, na kuunganishwa na sementi ya udanganyifu.

  kupenda fedha

       Je mibaraka au mali yatoka wapi? Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 8:18 "Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu zakupata utajiri ili alifanye agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo.                                                                                                                                     

  Yeremia 9:23-24 "Bwana asema hivi mwenye hekima asijisifu kwa hekima yake wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake bali ajisifuye ajisifu kwa sababu hii ya kwamba ananifahamu mimi na kunijua ya kuwa mimi ni Bwana nitendaye wema na hukumu na haki katika nchi maana mimi napendezwa na mambo hayo asema Bwana." Mali yaweza kutupa mfano mbaya juu ya vitu. Imeandiikwa, Luka 12:15 " Yesu akawaambia angalieni, jilindeni na choyo maana uzima wa mtu haumo katika vitu vyake alivyo navyo."

  Si vyema kuweka pesa mbele ya vitu vingine vyote. Imeandikwa, Mathayo 6:24 "Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu na ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu hamwezi kumtumikia Mungu na mali." 1 Timotheo 6:9 "Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi na tamaa nyingi zisizo na maana zenye kudhuru ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu."

  Ni vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Imeandikwa, Marko 10:23-25 "Yesu akatazama kotekote akawaambia wanafunzi wake jinsi itakavyokuwa shida kwa mwenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu ,wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake Yesu akajibu tena akawaambia, wanafunzi wake  jinsi ilivyo shida kwa mwenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."

  Kupenda pesa huleta dhambi. Imeandikwa, 1Timotheo 6:10 "Maana shina moja ya mabaya ya kila namna ni kupenda fedha amabayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi."

  Kutosheka sikuwa na mali au fedha nyingi. Imeandikwa, Wafilipi 4:12-13 "Na jua kudhiliwa tena na jua kufanikiwa katika hali yo yote katika mambo yo yote nimefundishwa kushiba na kuona njaa kuwa na vingi na kupungukiwa na yaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu." Mathayo 6:21 "Kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo utakapokuwapo moyo wako."

  manabii wa uongo

            BWANA Yesu alituonya ya kuwa siku za mwisho kutakuwa na makristo wa uongo na kujifanya wakombozi wa ulimwengu huu. Imeandikwa, Mathayo 24:4-5 "Yesu akajibu akasema angalieni mtu asiwandanganye kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni kristo nao watawadanganya wengi."

  Yesu alisema dalili ya siku za mwisho ni makristo wa uongo. Imeandikwa, Mathayo 24:23-26. "Wakati huo mtu akiwaambia tazama kristo yuko hapa au yuko kule msisadiki maana watatokea makristo wauongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza yamkini hata wateule. Tazama nimekwisha kuwaoya mbele. Basi wakiwaambia yuko jangwani msitoke; yumo nyumbani msisadiki."

  Paulo aliwaonya watu kuhusu mitume wa uongo wasio hubiri Yesu wabibilia. Imeandikwa, 2Wakorintho 11:3-4 "Lakini nachelea kama yule nyoka alivyo mdanganya Hawa kwa hila yake asije akawaharibu fikara zenu mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Maana yeye ajaye akihubiri Y esu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri au mkipokea roho nyingine msiyoipokea au injili nyingine msiyo ikubali mnatenda vema kuvumilia naye."

  Wakristo hao wa uongo wanamtumikia nani? Imeandikwa, 2Wakorintho 11:13-15 "Maana kama watu hao ni mitume wa uongo watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mitume wakristo wala siajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru Basi si neno kubwa watumishi wake wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi yao."

  Kabla ya kuja Yesu  mara ya pili kutakuwa na dhihirisho la makristo wa uongo. Imeandikwa, 2Wathesalonike 2:3-4 "Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana siku ile haiji usipokuja kwanza ukengeufu ,akafunuliwa yule mtu wa kuasi mwana wa uharibifu yule mpingamizi ajiinuae nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa ambaye yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu akijionyesha nafsi yake kanakwamba yeye ndiye Mungu."

  Je? Mwisho wa kristo wauongo utakuwaje na tutawajua vipi? Imeandikwa 2Wathesalonike 2:8-10 " Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake yule ambaye kuja kwake ni mfano wa kutenda kwake shatani kwa uwezo wote na ishara ya ajabu za uongo na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea kwasababu hawakukubali kuipenda ile kweli wapate kuokolewa."

  Jambo la kuhuzunisha ni kwamba wale wanao mfuata yule mpinga kristo wanadhani yakuwa wanaifanya kazi ya Mungu. Imeandikwa, Mathayo 7:22-23 "Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa njina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi ndipo nitawaambia dhahiri sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu."

  injili ya mafanikio ni kibiblia?

   Je wewe ni mchungaji,nabii askofu?umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kanisa lako likue? Sababu ya kweli ndani ya moyo wako ni nini? mashindano,kumtumikia MUNGU,kujipatia kipato kikubwa, kujulikana?imefikia hatua mpaka wachungaji na watumishi wengine wanatumia A.K.A! hii inachefua.

  umeweka nguvu zote katika kuhubiri mafanikio kuliko ufalme wa MUNGU,na kazi aliyotuagiza BWANA YESU ,kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19-20 "basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru ninyi na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari." unapohubiri mafanikio tuu mwanzo mpk mwisho wa ibada Je, unataka kanisa lako likue ili ujisikie umefanikiwa? Je, unataka uheshimiwe na kuwa na ushawishi mkubwa? Je, unataka kuwa na mamlaka juu ya watu? Je, unatazamia kutajirika? Hizo zote ni sababu mbaya za kutaka kanisa lako likue.

  Ukitaka kanisa lako likue ili Mungu atukuzwe kadiri watu wengi wanavyobadilishwa maishani kwa Roho Mtakatifu, basi hiyo ni sababu nzuri kabisa ya kutamani kukua kwa kanisa.Inawezekana ukajidanganya – kufikiri kwamba makusudi yetu ni safi na huku ni ya kimwili kabisa, tena ya kibinafsi.

  Tunawezaje kujua ukweli wa makusudi yetu? Tunawezaje kujua kama kweli tunataka kujenga ufalme wa Mungu au kujenga ufalme wetu binafsi tu?

  Njia moja ni kwa kufuatilia jinsi tunavyoitikia mafanikio ya wachungaji wengine. Kama tunafikiri makusudi yetu ni safi, kama tunafikiri kwamba kweli tunataka ufalme wa Mungu na kanisa Lake likue, lakini tukigundua wivu mioyoni mwetu tunaposikia juu ya kukua kwa makanisa mengine, hiyo inadhihirisha kwamba makusudi yetu si safi. Huonyesha kwamba kweli hatujali sana kukua kwa kanisa, bali tunajali kuhusu kukua kwa kanisa letu. Mbona iwe hivyo? Kwa sababu makusudi yetu yana kiasi fulani cha ubinafsi.

  Pia tunaweza kukagua makusudi yetu kwa kupima itikio letu la ndani tunaposikia kwamba kanisa jipya limeanzishwa katika eneo letu. Tukijisikia kutishika, hiyo ni ishara kwamba tunajali zaidi kuhusu ufalme wetu kuliko ufalme wa Mungu.

  Hata wachungaji wa makanisa makubwa au yanayokua wanaweza kukagua makusudi yao hivyo hivyo. Wanaweza kujiuliza maswali kama haya: “Je, ningekubali kuanzisha makanisa mapya kwa kuwatuma na kuwaachilia kabisa viongozi muhimu na watu wa kanisani kwangu, na kwa njia hiyo kupunguza idadi ya washirika wangu?” Mchungaji anayepinga sana wazo hilo bila shaka anajenga kanisa lake kwa ajili ya utukufu wake. (Kwa upande wa pili, mchungaji mwenye kanisa kubwa anaweza kuanzisha makanisa mapya kwa ajili ya utukufu wake pia, ili aweze kujigamba kuhusu idadi ya makanisa yaliyozaliwa na kanisa lake.) Swali lingine la kujiuliza ni hili: “Je, nina mahusiano na wachungaji wa makanisa madogo au nimejitenga nao, nikijiona kwamba niko juu kuliko wao?” Au hili: “Je, nitakuwa tayari kuwa mchungaji wa watu kumi na mbili hadi ishirini katika kanisa la nyumbani, au hiyo itaniathiri katika ubinafsi wangu?”

  mafanikio au baraka ni nyongeza, pia ni ahadi ya kila aaminiye.

  mwimbaJi mwenye vipawa vingi

  MWANDISHI: Kwanza kabisa nataka kujua wewe ni mwenyeji wa mkoa gani.
  JENNIFER: Swali zuri, mimi ni mwenyeji wa Kigoma,lakini nimezaliwa mkoa wa Singida.
  MWANDISHI: Ni kitu gani ambacho unakikumbuka ulihusiwa na wazazi wako na sasa kinafaida kwako/ hasara.
  JENNIFER: Baba alitusisitiza miaka yote kusoma na sasa naona faida yake.
  JENNIFER: Bahati mbaya sana, mama yangu alifariki nikiwa mdogo, kwa hiyo nililelewa na baba na nilimpenda sana japo na yeye hayupo duniani lakini bado nampenda na kumkumbuka.
  MWANDISHI: Ni kitu gani ulifurahi kukifanya utotoni na unakikumbuka hadi leo.
  JENNIFER: Ni siku wezi walipovamia nyumbani kwetu kisha nikachukua chupa ya soda iliyokuwa chumbani na kutoka nayo sebuleni huku nikipiga kelele za ‘mwizi, mwizi’ na wezi hao wakakimbia. Sijui nilipataje ujasiri wa kufanya hivyo maana sizani kama nina ujasiri huo kwa sasa.
  MWANDISHI: Kwa sasa unaimba muziki wa kumtukuza Mungu, unakumbuka ulianza kuimba ukiwa na umri gani?
  JENNIFER: Nilianza kuimba nikiwa darasa la nne ikiwa ni pamoja na kucheza ngoma kwenye vikundi vya shule, lakini pia nikiwa katika kwaya ya kanisa la Romani Katoliki (RC) Kurasini.  MWANDISHI: lini ulianza kuimba rasmi muziki wa Injili?
  JENNIFER: Japo nilianza utotoni kama nilivyokwisha kuambia, lakini rasmi nilianza mwaka 1995.
  MWANDISHI: Una watoto wangapi?
  JENNIFER: Nina watoto wawili wote wa kiume.
  MWANDISHI: Wanawake wengi wanapoolewa hupenda kutumia majina ya waume zao, je wewe Mgendi ni jina la mumeo au babako?
  JENNIFER: Mgendi ni jina la baba yangu.
  MWANDISHI: Mumeo anaitwa nani?
  JENNIFER: Anaitwa Chaula.
  MWANDISHI: Kwanini hutumii jina la mumeo?
  JENNIFER: Jina hili nalitumia kanisani, mtaani na kwingineno. Ila sijaona umuhimu wa kubadilisha jina, kwani haijalishi naitwa nani, mimi mke bado ni mke wa Chaula tu. Kubwa zaidi ni nyaraka zangu zote muhimu zina jina la baba yangu, hivyo siyo mchakato mdogo kubadilisha jina.
  MWANDISHI: Umefaidikaje na kazi yako ya uimbaji?
  JENNIFER: Nimefanikiwa kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu kupitia uimbaji wangu na nyimbo zangu zinasikilizwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Watu wengi wameinuliwa mioyo yao baadhi na wengine wametubu makosa yao sambamba na kupokea uponyaji kupitia nyimbo hizo, hiyo ni faida kubwa kwangu. Pia nimefanikiwa kusafiri ndani na nje ya nchi na mwisho maisha yangu nayaendesha kupitia uimbaji. Nimeajiriwa shambani mwa Bwana, nakula vya madhabahuni.
  MWANDISHI: Dah! Mbona unanichanganya, umesema umeajiriwa shambani mwa Bwana na unakula vya madhabahuni, lakini nasikia unapiga mzigo sekondari ya Tambaza kama mwalimu?
  JENNIFER: Nikweli niwahi kufundisha mwaka 1998-2000. Awali niliwahi kufundisha  Handeni, Tanga mwaka 1993-1994, na mwaka 2002 nilifanikiwa kufundisha Benjamini Mkapa ambapo nakumbuka nilifundisha kwa muda wa mwezi mmoja.
  MWANDISHI: Kwanini uliacha ualimu?
  JENNIFER: Nilipata nafasi ya kwenda kusomea ukutubi, na nilipomaliza nikaajiriwa Chuo Kikuu Mhimbili ambapo napo nifanya kwa muda wa miaka mitatu ndipo nikaamua kujikita zaidi katika huduma ya uimbaji.
  MWANDISHI: Kuna shabiki wako mmoja katika masuala ya muziki huu wa Injili alitaka kujua, eti ulishawahi kusoma katika shule ya Uchama?
  JENNIFER: Hapana, ila kuna mtoto wa baba mdogo naye anaitwa Jennifer Mgendi ndiye alisoma hapo.
  MWANDISHI: Ulisema mbali na uimbaji unafanya kazi ya sanaa.
  JENNIFER: Kweli.
  MWANDISHI: Ni sanaa gani hiyo?
  JENNIFER: Ni kuhusiana na masuala ya kuandaa filamu zangu za dini.
  MWANDISHI: Inamaana wewe ni mkali wa kuandaa filamu za kiroho?
  JENNIFER: Haswa! Mpaka sasa nimetoa filamu tatu,  Joto la roho, Pigo la faraja na  Teke la mama.
  MWANDISHI: Maswali ninayo mengi sana lakini, naona kwa leo tuishie hapa.                              JENNIFER: Amen, karibu tena siku nyingine ukipata nafasi.

  singles corner

                              karibu ujisajili katika site dada ya swahilisifa. http://uchumba.webs.com/

  site iko ktk matengenezo 

  usiku wa maombezi ulivyokuwa(washington dc)

  Mtumishi wa Mungu Christopher Mwaka sege akiombea umati wa watu waliojitokeza kwa wingi katika maombi maalum ya kuliombea Taifa  la Tanzania na maziwa makuu,shughuli hiyo ilifanyika katika kanisa la Bethel World Outreach Church Silver Spring Md U S A.

  cult!  (nabii wa uongo aja na mpya)

  Nabii wa uongo tito  alipoulizwa kama yeye  ni nabii wa uongo?.tito alijibu:.Ni uongo gani ninaosema wakati kila kitukimeandikwa katika bibliatakatifu?kunywa pombe si dhambi,kwenda disco si dhambi, Dhambi ya ZINAA kwa mwanaume haimuhusu ndio maana mwanaume hanatalaka,Kutumia  mipira ya kiume ni dhambi kubwa sana maana tendo la ndoa si starehe bali ni uumbaji(creation)hivyounapotumia  mpira wa kiume na kutupa inamaana unaua viumbe aliokupa.

  Hapo nabii Tito akisema kuwa kuwa na wanawake wengi si dhambi Mungu anapenda hivyo akatolea mfano katika biblia wa mfalme Suleiman aliyekuwa na wanawake wengi sana lakini bado alikuwa ni kipenzi cha MUNGU.Yeye nabii TITO akasema mwenyewe ana wake wa3.wawili wako hapa DAR,mmoja yuko ARUSHA..na ana mpango wa kuongeza wake mpaka wafike saba na taarifa hizi kashawaambia wake zake,Nabii Tito ana watoto 7 wake kabisa hivyo kuendelea kushikilia msimamo wake wa suala hili katika imani yake.

  karatasi zake anazoziuza shilingi elfu moja..baadhi ya mambo anayozungumzia ni kunywa pombe na kula nguruwe si dhambi,kuoa wanawake wengi na kutoa talaka si dhambi kabisa,mwanaume dhambi ya zinaa haimuhusu kabisa,wababa ni dhambi kutumia mipira ya kiume,ni dhambi mwanamke kusalisha na kumtawala mwanaume..katika vipengele vyote hivi katoa na nukuu ya mistari katika biblia,MUNGU ni binadamu tena mwanaume.

  hakuishia hapo alibainisha mpango wake wa kufungua kanisa,ambapo amesha watembelea wana muziki wa miziki ya kidunia ,pamoja na wacheza filamu mashuhuri tanzania ili kutimiza azma yake.

  amka we usinziaye!

  Neno la Mungu linasema kwamba kurudi kwa Yesu Kristo kunategemea kuhubiriwa kwa “habari njema ya Ufalme … katika Ulimwengu wote” (Mathayo 24:14).kwa hiyo basi, ikiwa tunataka Yesu Kristo arudi haraka,  ni budi kila mtu “kwa wakati wake”, ashike zamu ya utumishi wake ipasavyo, bila kuzembea wala kulegea! Kumbuka Biblia inasema; “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu ….” (Yeremia 48:10). Unataka siku ile Yesu Kristo atakaporudi akuambie nini kama mtumishi wake? … mtumwa (mtumishi) mwaminifu na mwenye akili …” (Mathayo 24:45).  au… mtumwa (mtumishi) … mbaya …” (Mathayo 24:48). “vema, mtumwa (mtumishi) mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako” (Mathayo 25:21). “Wewe mtumwa (mtumishi) mbaya na mlegevu …” (Mathayo 25:26). “Na mtumwa (mtumishi) yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno” (Mathayo 25:30). kumbuka Yesu kristo mwenyewe alisema “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi” (Yohana 9:4). ndugu yangu huitaji kuwa na kanisa kubwa ndio uanze kazi.

  kumbuka moto uliokuwa nao wakati unaokoka!ulikua huoni haya kutembea na biblia kubwa,kusimama kituo chabasi kuwaambia watu HABARI ZA  YESU.leo hii unaenda ibadani hata biblia huna,unaona haya hata kumuambia jirani yako habari za YESU na wokovu wake.umeokoka au uko ktk Dini ya wokovu?umeshawahi kujiuliza sifa ulizonazo zafaa kukuingiza mbinguni?hapa Duniani unapotaka kusafiri nchi ingine kabla ujaenda ubalozini kuomba viza lazima ujichunguze je unakidhi matakwa ya kuomba viza hata kabla hujapeleka maombi yako.je wewe unayesema unasafari ya mbinguni umeshawahi kujihoji unakidhi masharti ya kuingia ktk mji mtakatifu wa MUNGU?(ufunuo 22:15..)15Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji. kumbuka Ufalme wa Mungu hutekwa na wenye nguvu. Humgharimu mtu kuwa na nguvu ili kuuteka ufalme wa MUNGU.

  Wokovu unapatikana kwa gharama, unatunzwa kwa gharama, lakini una raha yake, nayo ni amani ipitayo amani zote.     Mbarikiwe 

  ktk uandaaji wa vipindi

  Mpendwa!swahilisifaTV, iko ktk majaribio na uandaaji wa vipindi vitakavyo kuwa hewani kila siku masaa 24.ilikuboresha vipindi.ushauri au maoni yako yana karibishwa,pia huduma ya redio kwa mtandao iko mbioni kuanza karibuni nyote. kwa live events.

                john lema

   

  exalt his name

  True prayer begins with confessing who God is.

  Before asking the Lord to heal and do signs and wonders and before the place was shaken, the apostles declared, "Sovereign Lord," they said, "you made the heaven and the earth and the sea, and everything in them" (Acts 4:24).

  When Moses approached God's throne, he confessed who God is. The Scripture tells us, "Enter into his gates with thanksgiving, and into his courts with praise: be thankful unto him, and bless his name" (Psalm 100:4).

  True prayer begins by confessing who He is. We confess His glory. We confess His holiness. We confess His majesty.

  When I enter prayer, I always begin by telling God who He is: "Lord, You are God Almighty. You are just. You are pure. You are holy." I begin to magnify His holy name.

  "The heavens declare the glory of God," the psalmist cried (Psalm 19:1). He always began with exaltation.

  How can you approach God and immediately begin telling Him your needs until you tell Him how mighty He is to meet those needs?

  You begin by confessing how mighty He is.

  Prayer begins with declaring the glory of God. You cannot begin true prayer until you declare who God is.

  shule ya biblia

  Emmaus Shule ya Biblia inahudumia watu wote wanaopenda kusoma Biblia kwa njia ya posta. Masomo na mitihani yanatumwa kwa mwanafunzi. Baada ya kujaza anarudisha mtihani kwenye ofisi zetu. Ilianzishwa kwa mara ya kwanza Tanzania mwaka 1960.

  Inafundisha Biblia kwa watu wa aina zote, na waumini wa dini zote. Haifundishi misingi wala mitazamo ya dhehebu lolote, bali ujumbe wa Neno la Mungu jinsi lilivyo.

  Jina EMMAUS linatokana na jina la kijiji kimoja katika Biblia ambako wanafunzi wawili walikuwa wanaelekea walipotokewa na Bwana Yesu alipofufuka, Luka 24:13. Kijiji hicho kiliitwa Emau kwa Kiswahili, na Emmaus kwa Kiingereza. („Emmaus“ ni tofauti kabisa na shirika la EMAU Tanzania ambalo ni kifupisho cha „Elimu ya Malezi ya Ujana“. Ili kuondoa utata, shule hii inatumia jina la Kiingereza, EMMAUS.)

  umuhimu wa fungu la kumi

  Kutoa fungu la kumi ni jambo ambalo wakristo wengi hung’ang’ana nalo. Katika makanisa mengine kutoa fungu la kumi inasisitizwa kupita kiasi. Wakristo wengi pia hukataa kutii agizo la kutoa sadaka kwa Bwana. Kutoa fungu la kumi au sadaka inahitajika kuwa ni kitendo cha furaha na baraka. Lakini sivyo katika makanisa ya sasa.

  Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale? Hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5). Wengine huchukulia ya kuwa fungu la kumi, katika agano la kale ilikuwa kama sehemu ya ushuru uliokuwa ukitolewa kwa ajili ya makuhani na walawi. Agano jipya haiamrishi wala kupendekeza mfumo halali wa kutolea fungu la kumi. Paulo asisitiza kuwa waumini watenge sehemu ya mapato yao kwa ajili ya kusimamia kanisa (wakorintho wa kwanza 16:1-2).

  Agano jipya halielezi kiasi cha pato ambacho ni kitengwe kwa ajili ya kusimamia kanisa. (wakorintho wa kwanza 16:2). Kanisa la kikristo leo limechukua kile kiwango cha fungu la kumi kutoka kwa agano la kale na kukisisitiza kuwa ndicho kiwango cha chini cha mkristo kutoa. ijapokuwa agano jipya haitoi kiwango cha kutoa, inaelezea umuhimu na manufaa ya kutoa. watoe sawa na uwezo wao “kila mtu kulingana na pato lake.” Wakati mwingine ina maana ya kutoa zaidi ya fungu la kumi, na mara nyingine kichache kuliko fungu la kumi. Yote hutegemea uwezo wa mkristo mwenyewe na mahitaji ya kanisa. Kila mkristo sharti aombe na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu juu ya swala hili (Yakobo 1:5). “ kila mtu atoe kile alicho azimia kutoa kutoka ndani ya moyo wake, si kwa manung’uniko wala kulazimishwa, kwa kuwa Mungu hupenda mwenye kutoa kwa moyo mkunjufu” (wakorintho wa pili 9:7).

  Kwa kifupi, fungu la kumi linapelekwa pale mtu anapoendelea kupata huduma za Kiroho. Mwinjilisti anapokuwa amemwongoza sala ya toba yule aliyeukubali wokovu, iwapo aliyeokolewa hayupo karibu na huduma ya yule mwinjilisti, hushauriwa atafute Kanisa lililokaribu naye linalohubiri wokovu, na kuamini juu ya miujiza ya Yesu Kristo, ili aendelee kujifunza Neno la Mungu. Pale anapokuwa anaendelea kuukulia wokovu ndipo mahali pa kutoa fungu la kumi. Mtu binafsi anayekuwa amehubiri injili na kufanya mwingine aokoke, siyo wa kupewa fungu la kumi, fungu la kumi linapelekwa katika huduma ambayo mtu anaendelea kupata huduma za kiroho.

  Maandiko yanasema “Leteni zaka kamili ghalani….” [Malaki 3:10]. Ghala linalotajwa hapa siyo mtu, bali ni katika kusanyiko la watu ambapo wanapata huduma mbalimbali za kiroho. Mahali hapa huhitajika nyenzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha, kwa ajili ya kazi ya Mungu.

  chale,tattoo ni ruksa kwa mkristo?

  Agano la kale liliwaamuru waIsraeli, “Msiikate miili yenu kwa ajili ya wafu wala kuchanja chale juu ya ngozi za miili yenu.Mimi ni Bwana” (mambo ya walawi 19:28). Hata hivyo ijapokuwa waumini kwa sasa hawako chini ya sheria ya agano la kale (warumi 10:4; wagalatia 3:23 – 25; waefeso 2:15), hoja ya kuwa kulikuwa na sheria juu ya chale lazima lituletee maswali agano jipya haisemi lolote juu ya muumini achanjwe chale au asichanjwe.

  Kulingana na swala la chale na kujikata alama mwilini, mtazamo wetu ni uwe; je, twaweza kumuomba Mungu atumie alama hizo kwa utukufu wake? “kwa hivyo mnapokula, mnapokunywa, chochote mfanyacho, kifanyeni kwa utukufu wa Mungu” (wakorintho wa kwanza 10:31). Biblia haituamuru kinyume cha chale na alama za mwili lakini pia haituonyeshi ya kuwa na haja na alama hizo miilini mwetu.

  Jambo lengine ni nidhamu. Biblia inatushauri kuvaa mavazi yetu kwa nidhamu (Timotheo wa kwanza 2:9). Kuvaa ki nidhamu ni kuziba sehemu zote zilizotarajiwa kuzibwa na mavazi. Lengo la nidhamu hii ya ki mavazi si juu ya wewe mwenyewe bali kwa ajili ya wengine wasije wakanaswa na hali yakuvutiwa nawe kiasi cha kukutamani. Chale pia zinaushawishi Fulani kwa hivyo zinakeuka mipaka ya nidhamu hii.

  Kanuni muhimu ya kibiblia ni kutazama jambo kwa mfumo wa imani. Kama hulionei shaka moyoni juu yakuwa linampendeza Mungu basi lifanye. “kwa kuwa lolote ambalo, si la imani ni dhambi” (warumi 14:23). Tunapaswa kufahamu kuwa miili yetu na nafsi zetu pia zimekombolewa na ni mali ya Mungu. Ijapokuwa haelekei moja kwa moja juu ya chale na alama za miili, wakorintho wa kwanza 6:19 -20 inatupatia kanuni moja, “Nini? Hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, ambaye mnaye kutoka kwa Mungu na ninyi si mali yenu wenyewe. Mmenunuliwa kwa thamani kwa hivyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambvyo ni vya Mungu.” Miili yetu sharti iandamane na ukweli kokote tuendako. Kama miili yetu ni mali ya Mungu basi lazima tuwe na ruhusa yake kabla hatujajichanja chale hizo au alama hizo za mwili.

  askofu climate irungu

  Askofu climate irungu wa The Kingdom Church (WCCC)
  Location:
  , SE26 5BS
  Phone:
  01315552290

  preaching at the ceremony - "The biggest enemy is not the devil but your ignorance."

  sikiliza mahubiri yake live.

  katika live streaming hii hapa www.livestream.com/bishopclimateirungu.tv or visit http://www.bishopclimate.org/

  marufuku kukata tamaa!

  Majira ya kunyanyaswa, kukataliwa, kuchoka hayo ndio majira ya kuwa karibu na Mungu, usiondoke wakati wa mapito kwa maana ndipo mlango wako wa kutokea ulipo.

  “Mungu anakupa fursa  ya kutoka kwenye nafasi moja kwenda katika nafasi nyingine, anakuweka katika nafasi ili uiendee fursa ambayo amekupa, kila pingamizi unalopitia katika maisha yako,  ndani ya mapingamizi hayo kuna mbegu za kuiendea fursa yako.

  Tatizo sio tatizo, tatizo ni nini kilicho ndani ya tatizo lako. Mungu hutoa fursa mara moja tu lakini nafasi huja zaidi ya mara mbili ili kuinua kiwango chako”.Unapokua na ndoto, tegemea kupata majaribu na misukosuko, usiogope hautakufa mpaka ndoto yako itimie. Mungu amekusudia yaliyo mema kwako. Shetani amekusudia upate mabaya hivyo simama imara ndoto yako itatimia tu.

  Inabidi uione nguvu iliyomo kwenye msalaba sio kuishia kuziona zile mbao tu! Ukifungua macho na kuiona nguvu ile ya msalaba, utamuona Bwana Yesu!

  “Tusifikirie Kwamba hakuna Mungu kwa sababu ya matatizo yetu, Tuwe na Tumaini, Mungu anaweza kufanya zaidi ya tuwazavyo. Neno la Mungu lina nguvu kwa sababu,  Neno ni Mungu. Amini Neno lake nawe utaishi”Wengine hawataona MAONO yako wewe peke yako unayaona tangu mbali, hivyo kaa vyema na Mungu, MAONO yako yatatimia. Pasipo MAONO haiwezekani kupendeza Mungu. Ni mapenzi ya Mungu kila mtu awe na maono. Katika biashara, familia, huduma. Fikiria kufanya makubwa, utayaona matokeo ukikaa vyema na Mungu.

  download swahilisifa toolbar

  Hi,
  I recently installed the swahilisifa Toolbar and thought you might also find it interesting.
  It has lots of useful features and many people seem to like it (including me!).
  To find out more about this toolbar and download it, go to:
  http://swahilisifa.OurToolbar.com/

  uki download toolbar hiyo itakuwezesha kusikiliza habari mbali mbali toka bbc,voa,radio japan,etc pia kwa kubofya alama ya blue kushoto kwa toolbar utaweza kuingia moja kwa moja ktk site yetu bila kuandika command yeyote.

  JE! TUNAIPOTEZA MAANA YA KUSIFU NA KUABUDU?

   

  Katika kujaribu kuitazama jamii ya wakristo katika siku zetu, nimefika mahali nikajiuliza kwamba huenda, kwa wengi wetu, ile maana ya kibiblia ya kumsifu na kumuabudu Mungu inapotea.

  Ikitajwa kumsifu na kumuabudu Mungu, kwa haraka fikra za wengi wetu hukumbuka ratiba ya ibada za makanisani tunakoabudu. Kama siku ya ibada Kipindi cha Sifa huanza saa 3:00 asubuhi, basi fikra zetu hukumbuka na kukaa hapo. Na huku tukiisubiri kwa shauku kubwa. Kwa bahati mbaya siku na saa hiyo pengine inakuwa mara 1 au 2 tu kati ya siku 7 za wiki. Ni kama tuko Agano la Kale ambapo Mungu hakukaa ndani ya watu.

  Kwa Dar es Salaam, inaposemwa “kusifu na kuabudu,” si ajabu fikra za wengi hurejea haraka Diamond Jubilee, na kumbi nyinginezo, zikiwemo za mahoteli makubwa. Pia inakuja haraka ile picha ya umati ambao hufurika, na majina ya waimbaji maarufu au “mastaa” na “mapromota”. Kwa wengine kusifu na kuabudu humaanisha “kutoa ‘singo’,” “kufyatua albamu” au tamasha la uzinduzi; na kiingilio Sh. 3,000; 10,000, n.k.

  Kuna wengi wanaosubiri kwenda kupata au kuambukizwa faraja katika matamasha, au ile saa ya kusifu na kuabudu kanisani. Muda au tukio hilo likimalizika, basi, wanarudi katika ile hali yao ya siku zote ya ukavu wa mioyo na huzuni. Huku maisha ya wokovu wakiyaona kama mzigo unaotaabisha kuubeba; wenye taabu nyingi na raha chache. Wanaishi katika jangwa la roho nzito. Hali ambayo ni kinyume kabisa na ile Mungu aliyoikusudia katika Agano la Kristo na wanadamu.

  Imeagizwa, “Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.… mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi za rohoni, huku MKIIMBA NA KUMSHANGILIA BWANA MIOYONI MWENU; na KUMSHUKURU Mungu Baba SIKUZOTE kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo …,” Waefeso 5:17-20. Haya aliyoagiza Roho Mtakatifu kupitia kwa Paulo ndiyo hali halisi inayopaswa kuwa mioyoni mwetu SIKUZOTE. Nafahamu ni vigumu. Lakini ndiyo hali Mungu anayotarajia kuiona kwetu. Siyo kwa siku za ibada, tamasha au harusi tu.

  Tatizo letu kuu siyo dhiki au ugumu wa maisha tunayopitia bali zaidi ni kupungukiwa ufahamu sahihi. Maana Paulo aliyeyaandika haya alipitia dhiki nyingi kuliko tunazozipitia wengi wetu. Lakini aliweza kuishi maisha haya anayotuandikia sisi pia. Ametuagiza aliyoyafanya yeye. Wewe una “pumzi,” msifu Mungu. CD hata ikiimba siku nzima nyumbani, hiyo haimaanishi wewe umemsifu Mungu. CD wala mtu mwingine asikuwakilishe.

  Msifu Mungu wewe mwenyewe. “Kila mwenye pumzi amsifu Mungu” -Zaburi 150:6. Imenenwa, “… ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi (Yesu) hataona kiu milele … maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele,” Yohana 4:14. Hatakuwa mkavu wa kushindwa kuimba sifa. Hatosubiri “kufufuliwa” na tamasha wala ibada ya kanisani.

  Comments:

  HTML

  MUHUBIRI ASIYE MIKONO WALA MIGUU

  nick vijicic,

  ni changamoto kwa wale watoao udhuru kwa kazi ya BWANA.ni mtumishi wa MUNGU ahamasishaye umsikiapo.amezunguka sehemu nyingi duniani akihubiri neno la MUNGU.

   

   

  maji ya uponyaji.

  Mtafaruku mkubwa umeibuka katika makanisa mbalimbali nchini kuhusu uhalali wa utumiaji wa maji ya uponyaji (Anointed Water) ambayo yamekuwa yakiingizwa kwa kasi kubwa na watumishi wa kiroho kwa ajili ya kuwahudumia kondoo wao wenye matatizo mbalimbali. Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, mtafaruku wa maji hayo unatokana na baadhi ya wachungaji huwatoza fedha kidogo  kondoo wao kwa madai ya kuwa wanachangia gharama za kuyasafirisha kutoka Israel ama Nigeria. Upekuzi huo umebaini kuwa, kwa miaka ya hivi karibuni, maji mengi yanatolewa bure na mtumishi wa Mungu, Nabii Temitope Balogun Joshua a.k.a TB. Joshua ambaye ni mwangalizi wa The Synagogue Church of All Nations (SCOAN) nchini Nigeria. Hivi karubuni, mchungaji mmoja alitua nchini akiwa na maji hayo kutoka kwa TB Joshua na kuanza kuwauzia waumini wake kwa lugha ya kuchagia kidogo gharama za usafirishaji kutoka Nigeria hali ambayo imetafasiriwa na watu wengine kwamba si sahihi. Mbali na kuwatoza fedha kidogo waumini wake, mchungaji huyo inasemekana ameleta maji ya Kichina (feki) kutokana na kukosa nembo  ya TB Joshua ambaye kanisa lake hujaza watu wazito kutoka nchi mbalimbali. “Maji ya uponyaji yaliyoingizwa nchini na mchungaji (anamtaja jina) ni feki kwa sababu hayana hata picha za Nabii TB Joshua, na amekuwa akiwapulizia waumini wake kwa kuwatoza kiasi kidogo cha fedha kwa kutumia lugha ya kuchangia gharama aliyotumia kuyasafirishia kutoka Nigeria wakati yeye alipewa bure,” alisema mchungaji wa kanisa moja lililopo jijini Dar es Salaam. Kama kawaida yetu baada ya kupata nyeti hizo, gazeti hili lilimsaka kwa udi na uvumba mchungaji anayetumia maji hayo kujitajirisha kiana kupitia huduma hiyo na lilipompata kisha kumuwekea tuhuma zake mezani, aliruka futi mia kwa maelezo kwamba madai hayo si ya kweli.  “Siyo kweli kwamba maji haya ni feki kama inavyodaiwa na baadhi wa wachungaji wenzangu, wakati nayachukua kutoka kwa TB Joshua niliacha kuna mengine yanatengenezwa na yametoka hivi karibuni, kwa mantiki hiyo kusema haya ni ya Kichina wanakosea. “Kuhusu suala ya kuwatoza fedha waumini wangu na watu ninao wahudumia hili nalo si kweli, isipokuwa huwa wanachangia kiasi kidogo cha pesa kama kurudisha gharama ya pesa nilizotumia wakati wa kuzisafirisha,” alisema mchungaji huyo mwenye mwili mnene kidogo na kijipara cha mbali. Mchungaji huyo aliongeza kuwa ili kuthibitisha kuwa maji hayo si feki tayari ameshaongea na TB Joshua kuja nchini kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa maji hayo na kukata kilimi cha watu wanaompakazia maneno ya kizushi yenye lengo la kuua huduma yake ambayo ameihangaikia kwa muda mrefu. Wakati mchungaji huyo akipangua tuhuma hizo, kuna baadhi ya watumishi wa Mungu ambao wamekuwa wakipinga huduma hiyo ya maji na kusema kuwa, kufanya hivyo ni sawa na kuyaabudu. Mmoja wa watumishi hao ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga huduma za wenzake hasa wanaotumia maji, vitambaa, funguo za gari, sabuni na nguo kuwaombea waumini alisema kuwa, leo hii Watanzania wamekuwa kama vile wamerongwa kwani wamekuwa wanaangalia ni kanisa lipi linatenda miujiza na kukimbilia huko. Mchungaji huyo mwenye sifa za kutumia muda mwingi kuhubiri habari za kuponda huduma za wenzake alisema kuwa Watanzania wasipojihadhari na mlipuko wa miujiza unaofanywa na watumishi wenzake watajikuta mwisho wa siku wanaangukia motoni.  

  Comments:

  HTML

  Luka 10:18-19,

  Akawaambia nalimuona shetani,akianguka kutoka mbinguni kama umeme, Tazama  nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui, wala hakuna atakayewazuru’.

  mchungaji abiud misholi.

  Isaya 40:3-5.

  ‘Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye nyikani,itengenezeni njia kuu kwa Mungu wetu . Kila bonde litainuliwa na kila mlima na kilima kitashushwa , palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa na utukufu wa  BWANA  utafunuliwa na wote wenye mwili watauona pamoja kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya’.

   

   Mch.Abiud Misholi.                                                                                                               ILI TUJIFUNZE KUMTEGEMEA MUNGU KWA ASILIMIA MIA MOJA.wakati mwingine Mungu hutujaribu ili tujifunze kumtegemea, nakumbuka wakati mke wangu ni mjamzito na alipofikisha muda wa kujifungua sikuwa na pesa hata kidogo katika akiba yangu, hivyo ilipofika wakati anaumwa uchungu nikuwa na kiasi cha shilingi mia na hamsini (150) katika akiba yangu , pesa ambayo nisingeweza kumhudumia kwa kitu chochote. Ndipo nilipoamua kumzalisha mwenyewe japo kuwa sikuwa na ujuzi wowote wa ukunga.Wakati mwingine watu hupita katika wakati mgumu ili kuweza kupimwa imani zao kwa Mungu.Mfano; Wakati naanzisha huduma yangu kijijini nilikuwa na waumini wanne tu yaani mimi na mke wangu, na mzee wa kanisa na na mke wake, jambo la kusikitisha ilikuwa ni katika kipindi cha sadaka ambapo wote tulikuwa hatuna kitu basi ilikuwa kama mchezo wa kuigiza.Wakati wa kuinuliwa ukifika umefika bwana, nakumbuka mara ya kwanza kupanda ndege nilikuwa naenda nchini  Kenya sasa wakati nimepata tiketi kwanza niliinusa....nikakuta harufu ya ndege, sasa nikapanda na wakati inaanza kupaa.... wakati huo nikiwa kimya naomba Mungu na kumwambia BABA NAIWEKA MIKONONI MWAKO ROHO YANGU huku nawaza cheupe wangu simuoni tena, kwakweli hali ilikuwa inatisha lakini nikakumbuka kuwa nilimuomba Mungu siku moja nipande ndege, hapohapo nikapata nguvu mpya.

  Ambaye hakulala na njaa hawezi kujua ni sehemu gani chakula kipo’.Hivyo usipopitia matatizo huwezi kujua ni kwa namna gani unaweza kuwafariji wanaopitia matatizo.

  2wakoritho1:3-5,

  Na ahimidiwe Mungu bab wa BWANA wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja, atufarijie katika dhiki zetu zote ili nasi tunapate kuwafariji wale walio katika dhiki ya namna zote, kwa faraja hizo tunazofarijiwa na Mungu. Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo’.

   

  Comments:

  HTML

  mwimbaji wa nyimbo za injili

  Ushasikia kwamba muziki wa gospel(injili) siku hizi unatamba sana nchini Tanzania.Mmojawapo ya wasanii wa muziki huo wa injili wanaotamba ni Jennifer Mgendi(pichani).Mbali na kuwa muimbaji wa nyimbo za injili, Jennifer pia ni mtunzi mzuri wa hadithi za filamu.Baadhi ya filamu alizowahi kutunga ni kama ile ya Pigo la Faraja na Joto la Roho.

  Mgendi alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki wa injili mwaka 1995 na albam yake ya kwanza iliitwa ‘Nini?’. Baada ya hapo alitoka tena na albamu zake zilizokwenda kwa majina ‘Ukarimu wake’, ‘Yesu Nakupenda’,'Nikiona Fahari’ na ya hivi karibuni zaidi inayoitwa Mchimba Mashimo.

   

  MJUE DR EGON FALK-WA NEW LIFE OUTREACH TANZANIA

  Dr Egon Falk – Dr Egon Falk

  MP3 search on MP3hunting

    huduma yake imewagusa wengi hasa wale wasiofikiwa(vijijini),nafikiri watumishi ni wakati wa kuamka sio kung´ang´ania mijini tu.huduma zetu zilenge kuwafikia wale waishio vijinini ambao ni wengi kuliko wakazi wa miji mikuu.

    Wakolosai 3:15-17 (Swahili New Testament)15Ruhusuni amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena muwe na shukrani. 16Neno la Kristo lidumu ndani yenu kwa wingi, mki fundisha na na kuonyana katika hekima yote; na huku mkiimba zab uri, nyimbo na tenzi za rohoni na mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu. 17Na lo lote mtakalofanya, ikiwa kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.

  wateule sasa kuweni macho

   

  Anaitwa nabii Tito (Nabii wa pombe- a prophet of beer) ni nabii anayehubiri watu kunywa pombe akitumia maandiko matakatifu ya Biblia na kudai kuwa Biblia inaruhusu kunywa pombe.Hufanya mahubiri yake maeneo ya posta mpya hapa jijini Dar es Salaam.
  Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi tosha kwa magonjwa mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara. Dini yake aliyoianzisha inarushu watu kuoa wake wengi,kuvuta sigara na kunywa pombe.Huyu ndiye nabii Tito (a prophet of beer)

  TAMBUA MAJIRA NA NYAKATI

  BAADHI ya wataalamu wa Biblia wamesema kwa jinsi ya ajabu wanyama mbali mbali waliokuwa na maana kubwa kinabii ambao walishatoweka katika ardhi ya nchi takatifu ya Israeli nao wamerejea tena, jambo ambalo linaonyesha kutimia unabii wa Biblia, baada ya Mungu kuwarejesha tena kwao (Israeli) Wayahudi. "Jambo ambalo ni wachache wanaolijua, ni kwamba wanyama waliotajwa katika Biblia ambao kwa karne nyingi walikuwa wametoweka nao wamekuwa wakirejea," amesema Mwandishi Chris Mitchell, wa Shirika la habari la CW News. Amesema kuwa mwaka 1969 Mamlaka ya Utunzaji wa Maliasili ya Israeli, ilianza kuwaandalia wanyama hao mazingira ya kuwafaa kuishi, hususan katika maeneo yale waliyowahi kuishi hapo kale, jambo ambalo limeonyesha mafanikio makubwa. Mamlaka hiyo imeandaa miradi mikuu miwili ijulinayo kama 'Hai bar'. Wa kwanza uko kwenye Mlima wa Karmeli, katika mkoa wa Haifa, mahali ambako Nabii Eliya alishindana na miungu ya kipagani na wa pili katika eneo la Bonde la Arava karibu na Eilat. Miradi hii yote miwili ina kazi maalum ya kutetea na kulinda haki za wanyama ambao waliishi katika maeneo hayo kulingana na kumbukumbu za Biblia. Avinoam Luria, ni Mkurugenzi wa Hai Bar katika mlima wa Karmeli. Anasema, " Hai Bar kwa kweli ni ukanda wa Kibiblia wa wanyama ambao walikuwa wametoweka nchini katika miaka 200 iliyopita." Mamlaka ya Maliasili ya Israeli imesema inaona suala hilo kama Biblia kuishi kidhahiri kabisa miongoni mwao. Luria alisema, "Hii inaweza kuwa kutimia kwa unabii, kwa kuwa wanyama hawa nao hii ni nchi yao. Na haki yao ya kurejea hapa, naweza kusema ni sawa tu na ile tuliyo nayo sisi na sio pungufu ya hapo." Wanyama watajwao katika Biblia wanaokadiriwa kufikia 350 wamesharejea Israeli. Mingoni mwa viumbe vinavyorejeshwa Israeli ni ndege aina ya Tai, ambao hufananishwa na manabii wa Mungu kutokana na sifa yao ya kuona mbali kuliko viumbe wengine wote. Uri Beidats anayefanya kazi kama Mkurugenzi wa Israel Nature & Parks Authority aanasema, " (Mnyama aina ya) Ayala ni alama ya kabila la Naftali. Simba alikuwa alama ya kabila la Yuda, na nyoka alikuwa alama ya kabisa la la Dani, wakati mbwa-mwitu alikuwa alama ya kabila ya Benyamini na kadhalika." Baada ya kupoteza utaifa wao kwa karibu miaka 3000 iliyopita, Wayahudi walianza kurejea Mashariki ya Kati (Israeli) zaidi ya miaka 50 iliyopita ambapo mwaka 1948 Umoja wa Mataifa uliwatangazia taifa lao huru, na tangu wakati huo wamekuwa wakiendelea kurejea, kama ilivyotabiriwa katika Biblia. Wakati wa Yesu Wayahudi walikuwa chini ya ukoloni wa Warumi ambapo baadaye walisambaratishwa na adui zao na kutapakaa tena duniani kote, lakini jambo la ajabu ni kwamba katika kipindi chote cha miaka 3000 ya kupoteza utaifa wao bado wamehifadhi lugha yao na mila zao.

  Want to know God?

  mlima kilimanjaro

  picha ya mlima kilimanjaro kama uonekanavyo kwa upande wa kenya ktk hifadhi ya amboseli.hivi ndivyo ,kenya imekua ikinadi biashara ya utalii kupitia vyombo mbalimbali.

  title

  Click to add text, images, and other content

  videos mpya

  2152 views - 0 comments
  1869 views - 0 comments
  1789 views - 0 comments
  2461 views - 0 comments

  shuhuda

  • "Bi Getrude Hamphrey, amekaa ndani ya ndoa kwa miaka saba bila kupata mtoto, ?Nilidharauliwa na watoto wadogo, hata ndugu zangu wa karibu, wengi walinicheka na kuniona sifai, nil..."
   getrude humphrey
   aliyepata mtoto
  • "USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU UTANGULIZI: Ndugu yangu kuna shuhuda nyingi sana zinazoanguka duniani, lakini wachache wanaozingatia kwa vile watoaji si wa dini zao au si ..."
   nyisaki chaula
   USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU

  Recent Prayer Requests

  • http://www.gv88v4negblpz1452m97m6wjw5634m26s.org/

   HITAJI LA MAOMBI - Sifa na kuabudu tmhoxjqqjq http://www.gv88v4negblpz1452m97m6wjw5634m26s.org/ <a href="http://www.gv88v4negblpz1452m97m6wjw5634m26s.org/">atm...
  • maisha yangu

   naomba maombi yenu kuhusu mimi na familia yangu ,mungu atulinde siku zote za maisha yetu,kwani tuko kwenye majaribu mazito

  Recent Podcasts